Kweli kabisa Mkuu. Kama nchi, tumeshindwa kabisa kuwapima wasomi wetu kwa utendaji na uzalishaji badala yake tunawapima kwa vyeti na GPAs. Tunashindwa kujua kuwa hivyo vipimo tunavyotumia havina tija kama haviwezi kubadilishwa na kuwa products. Ndiyo maana watu wanahangaika kutafuta vyeti hata kwa njia haramu!
Bwana Paulo, mbona hili nimelisema vizuri tu katika posts zangu zote? Wewe endelea kudhani tu, wakati jambo lipo wazi.
Ni kweli. Napinga upotoshwaji unaofanywa na watu wa CCM katika kumjengea Tulia taswira ya 'ubobezi' wa kisheria. Jambo ambalo kwa masikitiko makubwa Tulia mwenyewe 'amemezeshwa' na kusema kuwa yeye ni 'mbobezi' kikazi katika kutafsiri kanuni za Bunge, sheria za nchi na Katiba, kinyume na 'CV yake inavyoonesha. Nimeweka msisitizo kwenye neno kikazi, ili kuonyesha ni kwanini nimeamua kumchunguza kwenye engo ya akademia.
Kulikuwa hakuna haja ya CCM kutengeneza hype juu ya bidada Tulia. Kwanini tu wasingesema huyu bidada ni msomi wa sheria tu. Lakini kwa kutaka kutuaminisha kuwa ni 'mbobezi', kwamba ni bora kuliko wengine, hapo ndipo mantiki yangu ya kusema kabebwa inapokuja. Hata ukitumia literal translation ya kubebwa, utapata mantiki yangu; yaani CCM kwa kutumia kigezo cha 'ubobezi' wakaamua kumbeba Tulia juu ya wengine. Hili ndilo ninalolipinga, kwani hana sifa hiyo ya ubobezi hata punje.
Hakustahili kupata nafasi kama kigezo ambacho CCM walikitumia ni ubobezi kwenye sheria.
Narudia tena kusema, kwa kuwa CCM wanataka kutuaminisha kuwa Tulia Ackson ni mbobezi katika fani ya sheria, in fact, hata bidada mwenyewe kasema alipokuwa akijieleza Bungeni, na kwa vile nimeonyesha Tulia hana ubobezi wowote katika fani ya sheria ki-akademia (kikazi kama alivyosema mwenyewe), basi hitimisho ni rahisi tu Bwana Paulo, kabebwa. Hili wala huhitaji kuumiza kichwa kulifikia.
Kama siyo kweli kabebwa kwa kutumia kigezo cha ubobezi, basi jibu swali langu. Maana hadi sasa unakwenda na kurudi, lakini hujajibu swali langu la msingi: upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa? Jibu hili ni kuni-prove wrong kwa kuonyesha kuwa halistahili kupata nafasi kwa kigezo cha ubobezi katika taaluma ya sheria. It is that simple Paul.
Hili nakubaliana nawe. Lakini tafadhali usitake kuchanganya mambo. Hapa ninachoongelea ni ubobezi wa Tulia katika taaluma ya sheria, kama alivyosema yeye (kwamba ni mbobezi kikazi kwa miaka 14) na kama wanavyosema watu wa CCM. Kama alivyosema mkuu Dark City, usichanganye ubobezi wa mwanataaluma na practitioner. Haya ni maeneo mawili tofauti. Kwa sababu tukienda kwa vigezo vya ubobezi kwenye practice, Tulia hawezi kushindana hata na Sakaya, Makinda wala Ndugai. Wapo miles ahead of her.
Kuhusu vigezo vya nafasi ya Naibu Spika: ukiangalia kifungu cha 85 (vifungu vidogo vya 1 na 2) cha Katiba yetu, utaona kabisa zaidi ya kusema kuwa NS atachaguliwa miongoni mwa wabunge, na hatopaswa kuwa waziri, naibu waziri au mtu mwingine mwenye madaraka yoyote kama itakavyotajwa na sheria za Bunge, hakuna vigezo vingine zaidi ya hivi. Hivyo basi, hii inadhiirisha ni jinsi gani CCM wasivyofahamu hata Katiba ya nchi hii. Kulikuwa hakuna haja ya kutengeneza hype juu ya 'ubobezi' na upekee wa Tulia Ackson katika sheria ili ku-justify ugombeaji wake wa nafasi ya NS. Lakini kwa sababu ya mbeleko, utengenezwaji wa hype ulikuwa haepukiki. Nilichofanya ni kupinga upotoshaji huo na kuonyesha kuwa bidada Tulia siyo mbobezi katika sheria kama anavyodai na CCM wanavyotuaminisha. Nimetumia tu uhuru wangu kutenganisha ukweli na uongo; ili ukweli ubaki kuwa ukweli, na uongo uendelee kuwa uongo.
Sasa jibu swali langu: upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa?
Narudia tena Dr Tulia hayupoHuyo hafai kabisa kuwa naibu spika. Wingi wa CCM tu ndo umembeba. Na kwa jinsi tu mambo yalivyo unfold inaonyesha wazi kuwa kuna mtu au watu wenye nguvu nyuma yake.
Yes katiba inasema kutakua na naibu spika, haikutoka from no where!!!!Kwani huyo dokta wako kapata unaibu spika kwa sababu katiba inasema? Katiba inasema nini?
Really!!?Na wewe kama hupendezwi na kutopendezwa kwangu basi hilo ni tatizo lako na lako binafsi.
Labda tu niseme tunaweza kukubaliana Dr Tulia sio mbobezi kwa vigezo ulivyotaja lakini pia haimuondolei sifa ya kuwa mgombea wa uspika na wala haileti tafsiri ya kubebwa unayojaribu kuitengeneza
Bali huo ni mtazamo wako wa kubebwa
Mkuu, moja ya masuluhisho ambayo naamini yanaweza kufanikiwa ni kuwa na performance-based contracts kwenye sekta ya umma. Mtu unaajiriwa, lakini unapewa performance indicators (kwa ajili ya ku-screen utendaji na ufanisi wako) ambazo unapaswa kuzifikia na kuzitimiza katika kipindi fulani. Usipofikia na kutimiza hizo indicators, kazi huna; wala hupaswi kufukuzwa, unajiuzulu mwenyewe tu. Hili litawachuja wasomi makanjanja; kwani kama hastahili (kutokana na kujipa sifa zisizo zake), basi hataweza kuperform. Nchi zilizoendelea wanatumia huu utaratibu. Na pia ni utaratibu ambao unatumika kwenye akademia. Ndiyo maana kuna ule usemi you either publish or you perish. Machapisho ndiyo indicators za ufanisi katika akademia. Usipofikia malengo, kazi hauna. Sasa sielewi kwanini kusiwe na utaratibu kama huu kwenye sekta zingine za umma.
Leo hii Rais kawateua waziri mkuu na mwanasheria mkuu. Lakini ukiuliza nini ni vipimo vya utendaji na ufanisi katika majukumu waliyopewa, hutopata majibu. Yaani mambo ni kujiendea tu bila utaratibu wowote. Halafu hapo utegemee kupata matokeo tofauti. Yaani watumishi hawa wanapewa dhamana bila kupewa targets na namna ambavyo wanapaswa kufanya (hapa ndipo performance indicators zinaingia) hili wazifikie hizo targets. Inasikitisha sana mkuu.
Bwana Paulo, naona ni aidha hunielewi au hutaki kunielewa.
Wapi nimesema Tulia hana sifa ya kugombea nafasi ya NS? Nionyeshe mahala niliposema hilo.
Shida yangu ni yeye mwenyewe Tulia na watu wa CCM kum-label Tulia kama mbobezi katika sheria. Na imekuwa hivyo kutokana na watu kuuliza juu ya utaratibu uliotumika wa bidada Tulia kujitokeza kugombea nafasi hiyo. Naamini unafahamu jinsi alivyokuwa fast tracked kutoka naibu mwanasheria mkuu wa serikali, mgombea nafasi ya spika, mteuliwa wa nafasi ya ubunge, mgombea nafasi ya naibu spika hadi kuwa naibu spika. Sasa katika ku-justify hiyo fast tracking ndiyo kigezo cha 'ubobezi' wa Tulia katika sheria kikaanza kuzungumzwa. Narudia tena, nilichofanya ni kupinga upotoshaji huo. Sasa kama hana kigezo, kwanini alikuwa fast tracked hivyo? Ana nini cha ziada kuliko wengine wote? Hapa ndipo inapokuwa rahisi kuhitimisha kuwa ni mbeleko. Na kama walivyosema wadau humu, pengine kawekwa kwa lengo maalumu ili kukidhi matakwa ya waliom-fast track.
Ni kweli ni mtazamo wangu. Lakini mtazamo huu haujatokea tu hewani, nimeujenga kwa hoja nilizozieleza na ushahidi niliouweka. Katika dunia ya kisomi, ukitaka kuonyesha mtazamo wangu haupo sawa, unaupinga kwa hoja zenye ushahidi. Sijaona unafanya hivyo zaidi ya kuongea kwa nadharia na hisia tu.
Bachelor's degree - Shahada ya kwanza
Master degree - Shahada ya Uzamili
PhD - Shahada ya Uzamivu..
Alitunukiwa Shahada ya Kuzama Ndani kabisa katika Masuala ya Sheria hizo....
Kuzama katika sheria hadi Kutambuliwa na mabingwa wa Sheria ndio UBOBEZI Wenyewe.
Hata bila kupitia transcripts na machapisho na mambo mengine.. Kwa Kiswahili Uzamivu ndio Ubobezi.
Na postdoctoral training tutaziitaje? Mentors wenye uzoefu wa kucoach wahitimu wa ngazi zote ikiwemo uzamivu tutawaitaje?
Nahisi Kama Tanzania tumetengeneza vigezo vyetu vya taaluma
Humu jf kuna watu wachokozi kweli!.
Nzi
unapoteza muda wako
article ndeefu kisa unataka kum dis mtu?
unafahamu journals ngapi dunia hii?
unafikiri waalimu wa UDSM ni vilaza? ulizia mkuu
suppose sio au hana elimu au hana ubobezi, unachotaka kusema nini hasa
Ni naibu spika, wewe haujawa, ni PhD holder wewe hauna,ni notable figure wewe ni NZI TU
Ile ya mita 200 ilikuwa lazima ashinde. Yaani ile hata kama wakili wa serikali ningekuwa mimi nisiyejua hata Law 101, yaani hata definition ya neno "law" sijui, bado tu ningeshinda. Maana ile kesi ilikuwa ni lazima serikali ishinde.Yes,
Ile ya mita 200
Kwanza kabla ya kuanza kuelezea machapisho ya Dk. Tulia Ackson ulipaswa utueleze neno ubobezi kwako lina maana gani na kitu gani kinafanya binadamu akaitwa mbobezi katika sheria.
Jenga kwanza msingi wa hoja yako kabla ya kuanza kuelezea unachotaka kukichambua.