Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Mleta maada umedhirihisha kwamba wewe ni Inzi kweli.

Inzi hatofautishi pilau na kinyesi. Nina imani umenielewa. Hivi ubobezi unamlinganisha na nani?

Kwenye kambi ya Nyumbu kuna wa kumlinganisha naye?

Unaleta mambo ya ku publish academic articles hadi unaongelea impact factor ya journal. Hivi unafikiri mambo hayo ni relevant kwenye jukwaa hili.

Wewe binafsi umewahi kutoa article kwenye jarida hata kama halina hiyo impact factor?

Hivi unajua mbinu zinazotumiwa na majarida kupata impact factor kubwa?

Hata PhD thesis unadai haijawa cited. Labda ungesoma na kusema haina jipya. Labda supervisors wake na examination team waliona inafaa kuwa PhD.

Mimi nikisoma post ya mtu lazima niangalie Avatar na Signature yake. Hapo napata mengi kama ya kwako.
Kwenye ubobezi hakuna kulinganishana, maana hata juha ukimlinganisha na juha mwenzie anaweza kupatikana "mbobezi". Kwa maana hiyo vigezo vya mtu vinapimwa kwa kuangalia yeye tu.

Na usimshambulie aliyeleta mada. Kwanza hujui kama anayo machapisho au hana, na hata kama hana..kwani kuna aliyemwita mbobezi?
 
Mleta maada mwenyewe ameishajibu hoja zangu. Ingekuwa vyame kabla ya kumaliza viroba vyako, ukasoma alivyonijibu. Kikubwa naelewa hujui hata maana ya Impact Factor. Usidhani ni jina la mtaa.

Kuna options mbili tu. Ama kumlinganisha na mgombea wa UKAWA au watangulizi wake katika kazi hiyo.
 
Mkuu,
Hongera sana kwa uchambuzi wa hali ya juu kuhusu Dr. Tulia. Ni wachache sana humu watakaoelewa nini ulichojaribu kuweka wazi, kwani wengi hawataki kusikia madhaifu ya mtu wao. Hongera tena kwa uchambuzi makini.
Amejitahidi sana, tena sana. Kwa kweli ameandika uzi kitafiti. Bahati mbaya wengi humu hawana uwezo wa kuelewa mambo ya kitafiti, na wengine hata wenye uwezo huo wana mahaba na chama chetu hivyo wamegeuka kuwa vipofu na viziwi.

Kwa wengine, kufika chuo kikuu wanaona tayari mtu kabobea, achilia mbali kufundisha huko. kifupi Tanzania tuna tatizo kubwa nalo ni kuwa wafinyu wa kuelewa mambo in both global and specicic contexts
 
Narudia tena Dr Tulia hayupo
pale by coincidence, amewekwa na system kwa manufaa ya system
Waliomuweka ndio wanajua anafaa

Ahaaa...nashukuru umekiri hilo. Na ndo maana sisi wengine tunaona kabisa hafai kwani hana tajiriba yoyote ile ya kiutendaji kumfanya awe naibu spika.

Hata uwezo wake wa kujieleza ni pedestrian. Anajiumauma tu. Kaulizwa maswali na hakujibu. Spika akamnusuru.

She is a pawn.
 
Mleta maada mwenyewe ameishajibu hoja zangu. Ingekuwa vyame kabla ya kumaliza viroba vyako, ukasoma alivyonijibu. Kikubwa naelewa hujui hata maana ya Impact Factor. Usidhani ni jina la mtaa.

Kuna options mbili tu. Ama kumlinganisha na mgombea wa UKAWA au watangulizi wake katika kazi hiyo.

Una papara tu ya kuandika. Tulia uandike vizuri.

Wewe na mimi hatujuani. Kama wewe vyako ni viroba kila siku usidhani kila mtu ndivyo alivyo.

Na kama unafikiri wewe ndiye mjuaji wa mambo basi umepotea. Kama unafikiri impact factor unaijua peke yako umepotea pia. Naweza kuwa na machapisho mengi tu kwenye majarida yenye impact factor kubwa, ndogo na mengine yasiyokuwa na impact factor, ila hii siyo issue kwa sasa. Hilo haliondoi uhalisia wa hoja ya mleta uzi, na huwezi kufuta uzito wake kwa hoja za kilevi kama zako.

Ungekuwa na akili timamu japo kidogo ungeligundua kuwa mleta uzi hajajikita kwenye kumlinganisha na waliokuwa wanashindana naye. Na hoja yake haikujikita kwenye ushindani wa nafasi ya uspika au unaibu spika. Maana hata kama ungelinganisha "mataahira" wawili kama wewe, angepetikana "mbobezi"

Ila sina sababu ya kujisumbua. Watu wa aina yako tunao wengi sana nchi hii. Ndio hao hao "wabobezi" waliolifikisha taifa hili kwenye viwango hivi vya aibu kutokana na ubobezi wa kubebana kwa faida binafsi.
 
Hii ndio Jamii forum sasa......makada wa vyama mkae pembeni jmn.....
Hongera sana kwa ndugu NZI. Nina imani nia ya huu uchambuzi si kumponda mtu bali kujua ukweli wa kile kinachohubiriwa.
 
Bachelor's degree - Shahada ya kwanza
Master degree - Shahada ya Uzamili
PhD - Shahada ya Uzamivu..
Alitunukiwa Shahada ya Kuzama Ndani kabisa katika Masuala ya Sheria hizo....
Kuzama katika sheria hadi Kutambuliwa na mabingwa wa Sheria ndio UBOBEZI Wenyewe.
Hata bila kupitia transcripts na machapisho na mambo mengine.. Kwa Kiswahili Uzamivu ndio Ubobezi.

Ndivyo na mimi nimekuwa najua hivyo siku zote, sasa jamaa miwivu imemniga huko anakuja na maandishi lukuki humu huyu si mbobezi.
 
Ah post nzuri ,af kasema yy haoni huo ubobezi,,nafkiri kwa post hii,,na mm nitapata wasi wasi juu ya ubobezi huo ambao ndugu zetu wamemtunuku
 
Ahaaa...nashukuru umekiri hilo. Na ndo maana sisi wengine tunaona kabisa hafai kwani hana tajiriba yoyote ile ya kiutendaji kumfanya awe naibu spika.

Hata uwezo wake wa kujieleza ni pedestrian. Anajiumauma tu. Kaulizwa maswali na hakujibu. Spika akamnusuru.

She is a pawn.

Kwakutumia the so called "ubobezi" amepewa kiti ili kuzima hoja za wapinzani pale watakapotaka kutumia kanuni ili kupenyeza hoja flani
 
Ile ya mita 200 ilikuwa lazima ashinde. Yaani ile hata kama wakili wa serikali ningekuwa mimi nisiyejua hata Law 101, yaani hata definition ya neno "law" sijui, bado tu ningeshinda. Maana ile kesi ilikuwa ni lazima serikali ishinde.

ndio kashinda sasa... credibility ya ushindi ni kitu kingine
 
Ahaaa...nashukuru umekiri hilo. Na ndo maana sisi wengine tunaona kabisa hafai kwani hana tajiriba yoyote ile ya kiutendaji kumfanya awe naibu spika.

Hata uwezo wake wa kujieleza ni pedestrian. Anajiumauma tu. Kaulizwa maswali na hakujibu. Spika akamnusuru.

She is a pawn.

Nikubaliane na wewe kutokukubaliana kwetu
Kweli tumemkosa mtu mwenye tajiriba Magdalena Sakaya na wabunge kutukamchagua mbumbumbu Dr Tulia
 
Eboo! Kumbe unakubaliana na tunaosema kuwa kabebwa. Sasa mbona unabisha?

Mkuu Dr Tulia hajabebwa bali ameteuliwa na "system" husika kama vile alivyowekwa Magufuli kugombea Urais au Lowassa kugombea kupitia Ukawa
 
Ndiyo tatizo la kuingia kwenye siasa, unachambuliwa kisiasa. Nafikiri ili kuthibitisha ubobezi wake wa fani hiyo tungeelezwa siyo tu machapisho bali na kesi au changamoto alizosimamia na kuleta mabadiliko. Hii ya mita 200 inayosemwa siyo kipimo sahihi kwa sababu ilikuwa na mashinikizo ya kisiasa na kiusalama.
 
Bwana Paulo, naona ni aidha hunielewi au hutaki kunielewa.

Wapi nimesema Tulia hana sifa ya kugombea nafasi ya NS? Nionyeshe mahala niliposema hilo.

Shida yangu ni yeye mwenyewe Tulia na watu wa CCM kum-label Tulia kama mbobezi katika sheria. Na imekuwa hivyo kutokana na watu kuuliza juu ya utaratibu uliotumika wa bidada Tulia kujitokeza kugombea nafasi hiyo. Naamini unafahamu jinsi alivyokuwa fast tracked kutoka naibu mwanasheria mkuu wa serikali, mgombea nafasi ya spika, mteuliwa wa nafasi ya ubunge, mgombea nafasi ya naibu spika hadi kuwa naibu spika. Sasa katika ku-justify hiyo fast tracking ndiyo kigezo cha 'ubobezi' wa Tulia katika sheria kikaanza kuzungumzwa. Narudia tena, nilichofanya ni kupinga upotoshaji huo. Sasa kama hana kigezo, kwanini alikuwa fast tracked hivyo? Ana nini cha ziada kuliko wengine wote? Hapa ndipo inapokuwa rahisi kuhitimisha kuwa ni mbeleko. Na kama walivyosema wadau humu, pengine kawekwa kwa lengo maalumu ili kukidhi matakwa ya waliom-fast track.

Ni kweli ni mtazamo wangu. Lakini mtazamo huu haujatokea tu hewani, nimeujenga kwa hoja nilizozieleza na ushahidi niliouweka. Katika dunia ya kisomi, ukitaka kuonyesha mtazamo wangu haupo sawa, unaupinga kwa hoja zenye ushahidi. Sijaona unafanya hivyo zaidi ya kuongea kwa nadharia na hisia tu.

Mkuu nimekuelewa sana na nimekubaliana na wewe kwamba kwa mujibu wa vigezo vyako Dr Tulia sio mbobezi

Kusema Dr Tulia amebebwa ni sawa na kusema hana sifa na hakustahili kuwa pale

Ukawa walifanya michakato yao wakaja na jina Sakaya
CCM wakafanya yao wakaja ma Dr Tulia
Kura zikapigwa Dr Tulia kashinda
Sasa kubebwa kwake kuko wapi?( labda kama tuhame mada na kuongelea utumishi na uanachama)

Mantiki ya hoja yako ilikua ni mbobezi au sio mbobezi!!!!?
Lakini sasa imegeuka imekua amebebwa, haya ni maoni yako tu na huna hoja yoyote kama mwingine anvyoweza kudai Sakaya kabebwa sababu hana ubobezi
 
Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

8.jpg

Chanzo: CCM Blog: DK TULIA ACKSON NDIE NAIBU SPIKA WA BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Salaam,

Jana Tanzania iliweza kupata Naibu Spika wa Bunge la 11. Ni Tulia Ackson, aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ya JMT, mjumbe wa Bunge Maalumu la kutunga Katiba, na Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pamoja na hizo nafasi ambazo alikuwa nazo awali, 'sifa' kubwa ambayo Tulia Ackson amekuwa akitajwa kuwa nayo ni ubobezi katika sheria.

Gazeti la Habari Leo limeandika, "Dk Tulia anakuwa Naibu Spika wa kwanza katika siku za karibuni, asiye Mbunge wa Jimbo, lakini akiwa amebobea katika sheria." Mawaziri- Majaliwa muadilifu, hana makuu

Likaendelea, "Alikuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba na ni mtaalamu katika sheria za hifadhi za jamii, kazi, uhifadhi wanyamapori, udhamini, sheria ya usimamizi wa mirathi, ufadhili miradi na madini.
"http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/3727-mawaziri-majaliwa-muadilifu-hana-makuu

Na mengi ya kufafanana na sifa hiyo yamesemwa na watu hapa JF.

Sasa kwa minajili ya kutaka kufahamu ubobezi wake katika sheria (naomba kusema wazi kuwa mimi siyo mtaalamu wa sheria, na nilikuwa simfahamu Tulia Ackson. Ila napenda kujifunza nini watu walio wabobezi katika fani fulani wanafanya), nikaamua kufanya 'utafiti' kidogo. Lengo kuu la 'utafiti' huu usio rasmi ilikuwa ni kuangalia mchango wake kama Mhadhiri wa Sheria katika fani ya Sheria. Ninaposema mchango wake katika fani ya Sheria, ninamaanisha kuangalia machapisho yake katika majarida ya kitaifa na kimataifa katika fani ya Sheria. Katika akademia, ubobezi wa mtu utokana na nini alichochapisha, wapi alipochapisha (ikimaanisha viwango vya majarida husika katika fani), na watu wangapi wamesoma na kwa muhimu sana, kuyanukuu machapisho yake.

Ni rahisi sana kufahamu ubobezi wa mtu katika fani kwa sasa. Njia rahisi ni ya kutumia Google Scholar, kama injini ya kutafutia machapisho ya mtu fulani na kuangalia 'ubobezi' wake. Lakini, hii itategemeana kama mtu huyo ana akaunti katika Google Scholar. Kama hana, kuna vyanzo vingine maarufu kama, Researchgate na Academia.edu.

Kwa hiyo nilianza kwa kuandika jina "Tulia Ackson' katika Google Scholar, kwa bahati mbaya Tulia Ackson hana akaunti katika Google Scholar. Lakini machapisho yake yaliweza kujitokeza, ambapo niliweza kuona jumla ya machapisho 8 aliyoandika Tulia Ackson. Katika machapisho hayo 8, Google Scholar ilinionyesha idadi ya machapisho yaliyoweza kunukuu machapisho ya Tulia Ackson. Hapa chini naorodhesha machapisho hayo, na kuweka idadi ya nukuu za machapisho.

1. "Disability benefits and workers with HIV/AIDS: Coverage issues and challenges in the United Republic of Tanzania" - hili alichapisha katika jarida liitwalo International Social Security Review, mwaka 2008.
Linapatikana hapa: Disability benefits and workers with HIV/AIDS: Coverage issues and challenges in the United Republic of Tanzania - Ackson - 2008 - International Social Security Review - Wiley Online Library

Na toka mwaka huu, Google Scholar inaonyesha kuwa chapisho hili limenukuliwa mara moja tu. Na aliyelinukuu ni Abdallah Possi katika tasnifu yake ya shahada ya uzamivu mwaka 2014. Inapatikana hapa: www.opus4.kobv.de/opus4-fau/frontdoor/deliver/index/docId/5940/file/THESIS_Possi.pdf

2. "Justiciability of Socio-economic Rights in Tanzania" - hili amelichapisha katika jarida liitwalo, African Journal of International and Comparative Law, mwaka 2015. Linapatikana hapa: An Error Occurred Setting Your User Cookie

Mpaka natumia Google Scholar muda mfupi uliopita, chapisho hili lilikuwa halijanukuliwa.

3. "Social Security Fragmentation in Tanzania: The Challenge of Governance" - hili aliliandika akiwa mwanafunzi wa shahada ya uzamivu pale Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika ya Kusini, mwaka 2008. Linapatikana hapa: http://www.idll.uct.ac.za/usr/idll/resources/monographs/IDL_monograph_2008-1.pdf

Aliliandika kama Monograph iliyotakana na tasnifu yake ya shahada ya uzamivu. Nalo toka mwaka huo, alijawahi kunukuliwa kwa mujibu ya Google Scholar.

4. "The role of the law of regional organisations in reforms of social protection systems: portability of social security benefits in the East African Community" - hili alichapisha kama sehemu ya kitabu kiitwacho, "Social Protection in Developing Countries: Reforming Systems" kilichoandikwa mwaka 2013. Kurasa za awali za kitabu hiki zinapitkana hapa: http://samples.sainsburysebooks.co.uk/9781136178511_sample_493868.pdf

Kwa mujibu wa Google Scholar, hili chapisho nalo halijaweza kunukuliwa na mtu yeyote.

5. ?Access to social services for non-citizens and the portability of social benefits in Tanzania? - hili nalo aliandika kama sehemu ya kitabu kiitwacho, "Access to Social Services for Non-citizens and the Portability of Social Benefits within the Southern African Development Community", kilichoandikwa mwaka 2011. Linapatikana hapa: https://www.uj.ac.za/EN/Faculties/l...uments/Access to social services.pdf#page=139

Kwa mara nyingine tena, Google Scholar inaonyesha kuwa andiko hili halijapata kunukukuliwa.

6. "Social Security Law and Policy reform in Tanzania with reflections on the South African Experience" - hili ndilo tasnifu ya shahada yake ya uzamivu aliyoipata pale UCT, mwaka 2007. Linapatikana hapa: https://open.uct.ac.za/handle/11427/4615

Nalo toka 2007, kwa mujibu wa Google Scholar, halijawahi kunukuliwa.

7. "Extension of social security coverage to the rural population in Tanzania: lessons from India and Iran" - hili alichapisha katika jarida liitwalo, Journal of African and International Law, mwaka 2009. Linapatikana hapa: AfricaBib | Extension of social security coverage to the rural population in Tanzania: lessons from India and Iran

Kwa mara nyingine, Google Scholar inaonyesha kwamba andiko hili halijawahi kunukuliwa.

8. "The New Employment and Labour Relations Law in Tanzania: An Analysis of Labour Legislation in Tanzania" - hili ameandika pamoja na B. Rutinwa na E. Kakula pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 2012. Lakini katika Google Scholar haitoi 'link' ya kuelekea andiko hili, wala ni wapi limechapishwa. Ingawa nalo halijawahi kunukuliwa.

Hivyo basi, katika maandiko yake hayo 8, Tulia Ackson, aliyekuwa Mhadhiri wa Sheria na anayesemwa kuwa mbobezi wa sheria, kaweza kunukuliwa mara 1 tu. Na aliyemnukuu ni mtanzania aliyekuwa akisoma shahada ya uzamivu katika sheria.

Sikuridhika sana na majibu ya Google Scholar. Nikaamua nihamishie utafutaji Researchgate, ambayo katika siku za hivi karibuni watu wengi katika akademia wameonekana kupenda kuwa na akaunti huko. Kule nilimpata Tulia Ackson na rekodi zake. Mwangalie hapa: https://www.researchgate.net/profile/Tulia_Ackson

Rekodi zake katika Researchgate zinaonyesha kuwa: ana jumla ya machapisho 8, ambayo kwa ujumla wake yamesomwa mara 33 (ilikuwa mara 32, ikaongezeka 1 baada ya mimi kufungua andiko lake moja) na kunukuliwa mara sifuri.

Sikuridhika sana. Nikasema, pengine yale majarida ambayo alichapisha maandiko yake ni ya viwango vya juu sana katika fani ya Sheria. Kwa maana katika ulimwengu wa akademia, wapi unachapisha maandiko yako ina nafasi kubwa sana ya kuonyesha 'ubobezi' katika fani. Unaweza kuwa na machapisho machache sana, lakini katika majarida ya viwango vya juu sana, na ukaonekana 'mbobezi' sana kupita yule aliye na machapisho mengi katika majarida ya viwango vya chini. Sasa katika 'utafiti' wangu huu, inaonyesha Tulia amekwishachapisha katika majarida haya: Journal of African and International Law, African Journal of International and Comparative Law, na International Social Security Review.

Nikaamua kwenda mbele zaidi kufuatilia kwa undani majarida hayo. Pengine nidokeze kidogo jambo hili: katika akademia ubora wa majarida utokana na kitu kinachoitwa 'impact factor', kwa tafsiri isiyo rasmi ni athari (katika taaluma sana sana) ya jarida katika fani husika. Na hii 'impact factor' utokana na wastani ambapo chapisho katika jarida hilo unukuliwa kwa mwaka. Kwa hiyo kama jarida lina 'impacts factor' ya 4, inamaanisha kwamba kwa wastani, machapisho katika jarida hilo unukuliwa mara 4 na machapisho mengine.

Sasa, jarida la Journal of African and International Law, tovuti yake ni hii: Law Journals: Submissions and Ranking, ingawa hii siyo tovuti rasmi, ila ni tovuti inayoonyesha 'link' kwenda kwenye tovuti ya jarida hilo. Kwa mshangao mkubwa, nimejaribu mara nyingi kufungua 'homepage' (http://aicil.or.tz/law-journal/) ya jarida hilo, na kushindwa mara zote. Anuani ya ofisi zake zinaonyesha zipo Songea, Tanzania, katika taasisi iitwayo, 'African Institute for Comparative and International Law'. Jarida halina 'impact factor' na kwa kweli inavyoonekana, ni jarida la viwango vya chini sana. Kwani hata katika Google Scholar, upatikanaji wa jarida hili, ni wa mashaka, ukitoa chapisho ambalo Tulia analo katika jarida hili.

African Journal of International and Comparative Law, jarida hili utolewa na 'Edinburgh University Press', Scotland. Ingawa nalo halina 'impact factor', lakini angalau linaonekana kuwa la kuaminika kiasi.

International Social Security Review, jarida hili uchapishwa na "International Social Security Association" kupitia Wiley Publishing. Ingawa nalo halina 'impact factor', lakini pia linaonyesha kuwa la kuaminika kiasi.

Kwa hiyo, pamoja na majarida hayo machache, Tulia hajaweza kuchapisha katika majarida yenye viwango vya juu katika fani ya sheria. Majarida ya viwango vya juu katika sheria ni yepi? Angalia hapa kupata list ya majarida ya fani ya sheria: http://about.jcr.incites.thomsonreuters.com/full-titles-2015.pdf

Kwa upande mwingine, kitu ambacho kinajidhiirisha katika rekodi yake ni kwamba, Tulia Ackson anaonyesha kuwa na 'utaalamu' katika sheria za hifadhi ya jamii. Na wala siyo mtaalamu wa sheria za uhifadhi wanyamapori, udhamini, sheria ya usimamizi wa mirathi, na ufadhili miradi na madini kama gazeti la Habari Leo linavyotaka kuniaminisha. Rekodi yake inaonyesha hivyo, wala siyo mimi ninayesema hivyo.

Kwa kifupi, 'utafiti' wangu usio rasmi umenifanya nijiulize maswali ya kile kinachoitwa ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson. Labda kama kuna viashiria vingine (ambavyo mimi sivifahamu) katika ulimwengu wa akademia ambavyo umfanya mtu aitwe mbobezi katika fani yake. Lakini kama viashiria vinavyotumika kwa sasa: idadi ya machapisho, wapi yamechapishwa (hapa naongelea kuchapishwa katika majarida yenye viwango vinavyotambulika katika fani husika), na mara ngapi yamenukuliwa katika machapisho ya watu wengine, hakika bado sijaona ubobezi wa Tulia Ackson katika fani ya Sheria.

Kwa hiyo, ningependa kuuliza, upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa?

Asante kwa ufafanuzi wako mkuu. Maana tumedanganywa na kuaminishwa mengi mno kuhusu huyo mdasa
 
Bachelor's degree - Shahada ya kwanza
Master degree - Shahada ya Uzamili
PhD - Shahada ya Uzamivu..
Alitunukiwa Shahada ya Kuzama Ndani kabisa katika Masuala ya Sheria hizo....

Sawa. Nifanye kukubaliana nawe. Kwa hiyo Tulia Ackson ndiyo wa kwanza kutunukiwa hizo shahada? Ni kipi cha kipekee katika 'ubobezi' wake kushinda wengine kiasi cha kupelekea awe fast tracked kwa mwendo ule? Kumbuka justification ya fast tracking ni kwamba yeye ni mbobezi, wa kipekee na muhimu sana kuwa naibu spika mwenye ubobezi wa sheria. Kwa maana kama huo uzamaji wa ndani unaousema, si Tulia peke yake alionao hapa Tanzania.

Kuzama katika sheria hadi Kutambuliwa na mabingwa wa Sheria ndio UBOBEZI Wenyewe.

Ebu thibitisha hili. Usiseme mambo nadharia tu. Thibitisha hao mabingwa wa sheria waliomtambua Tulia. Lete profiles zao tuweze kuona huo ubingwa wao katika sheria.

Anyway, pengine kukusaidia tu, kutambuliwa na bingwa wa fani fulani hakukufanyi uwe mbobezi kwenye fani husika. Wanafunzi wa shahada ya uzamivu waliosimamiwa na Einstein, baadhi yao hawakupata kuwa wabobezi kwa kuwa walitambuliwa na Einstein. Issa Shivji, bingwa na nguli wa sheria hapa nchini, kasimamia wanafunzi wengi tu katika shahada ya uzamivu, lakini wengine hawajaweza kuwa wabobezi.

Hata bila kupitia transcripts na machapisho na mambo mengine.. Kwa Kiswahili Uzamivu ndio Ubobezi.

Kwa hili sikubaliani nawe. Labda ni kigezo ambacho umekitunga wewe katika ulimwengu wako wa akademia. Lakini, katika ulimwengu wa akademia ninaoufahamu, kupingana na vigezo vya ubobezi katika fani kama nilivyoelezea, ni sawa na kupigana na ukuta. Kuwa na shahada ya uzamivu pekee hakukufanyi uwe mbobezi kwenye fani yako ndugu. Ushajiuliza kwanini kwenye akademia kuwa na shahada ya uzamivu pekee hakukuhakikishii ajira ya kudumu? Kwanini kuna masharti ya kuandika machapisho kwa viwango ambavyo vimewekwa ili uweze kudumu katika akademia?

Eti "kwa kiswahili uzamivu ndio ubobezi". Mbona uzamivu tayari ni neno la Kiswahili?
 
Mkuu Dr Tulia hajabebwa bali ameteuliwa na "system" husika kama vile alivyowekwa Magufuli kugombea Urais au Lowassa kugombea kupitia Ukawa

Kumbe Magufuli aliwekwa? Nilidhani alishinda kwenye uchaguzi wa ndani ya CCM?? Anyway, hilo si la muhimu.

Tatizo lako Bwana Paulo unakwepa hoja yangu ya msingi juu ya hicho unachokiongelea. Nimekuuliza kwanini alikuwa fast tracked? Nini cha kipekee sana juu yake katika fani ya sheria?

Napenda nifahamu merits alizonazo Tulia Ackson zaidi ya wengine, zilizopelekea yeye 'ateuliwe' na 'system'. Otherwise labda unataka kusema wateuzi hawakuzingatia merits kama kigezo. Na kama ndivyo, sielewi kwanini unabisha kuwa hiyo inamaanisha kubebwa. Kubebwa nikimaanisha hana merits zilizo-justify fast tracking na maneno ya Tulia na CCM kusema ni mbobezi wa sheria.

Pengine niendane na ulichosema juu ya 'kuteuliwa' kwa Magufuli na 'system'. Sababu zilizotolewa ni msafi, hana makundi na mchapakazi. Hizi ndizo zilikuwa merits zake juu ya wagombea wengine.

Sasa with all people in the field of law Tanzania, Tulia ana merits zipi juu yao? Maana nimeshaonyesha kuwa kama kigezo ni ubobezi kwenye sheria, basi yeye hana. Tafadhali bwana Paulo, mbona hili swali unalikimbia? Nimekwambia nitajie ili uni-prove wrong kwamba hajabebwa.
 
Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

8.jpg

Chanzo: CCM Blog: DK TULIA ACKSON NDIE NAIBU SPIKA WA BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Salaam,

Jana Tanzania iliweza kupata Naibu Spika wa Bunge la 11. Ni Tulia Ackson, aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ya JMT, mjumbe wa Bunge Maalumu la kutunga Katiba, na Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pamoja na hizo nafasi ambazo alikuwa nazo awali, 'sifa' kubwa ambayo Tulia Ackson amekuwa akitajwa kuwa nayo ni ubobezi katika sheria.

Gazeti la Habari Leo limeandika, "Dk Tulia anakuwa Naibu Spika wa kwanza katika siku za karibuni, asiye Mbunge wa Jimbo, lakini akiwa amebobea katika sheria." Mawaziri- Majaliwa muadilifu, hana makuu

Likaendelea, "Alikuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba na ni mtaalamu katika sheria za hifadhi za jamii, kazi, uhifadhi wanyamapori, udhamini, sheria ya usimamizi wa mirathi, ufadhili miradi na madini.
"http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/3727-mawaziri-majaliwa-muadilifu-hana-makuu

Na mengi ya kufafanana na sifa hiyo yamesemwa na watu hapa JF.

Sasa kwa minajili ya kutaka kufahamu ubobezi wake katika sheria (naomba kusema wazi kuwa mimi siyo mtaalamu wa sheria, na nilikuwa simfahamu Tulia Ackson. Ila napenda kujifunza nini watu walio wabobezi katika fani fulani wanafanya), nikaamua kufanya 'utafiti' kidogo. Lengo kuu la 'utafiti' huu usio rasmi ilikuwa ni kuangalia mchango wake kama Mhadhiri wa Sheria katika fani ya Sheria. Ninaposema mchango wake katika fani ya Sheria, ninamaanisha kuangalia machapisho yake katika majarida ya kitaifa na kimataifa katika fani ya Sheria. Katika akademia, ubobezi wa mtu utokana na nini alichochapisha, wapi alipochapisha (ikimaanisha viwango vya majarida husika katika fani), na watu wangapi wamesoma na kwa muhimu sana, kuyanukuu machapisho yake.

Ni rahisi sana kufahamu ubobezi wa mtu katika fani kwa sasa. Njia rahisi ni ya kutumia Google Scholar, kama injini ya kutafutia machapisho ya mtu fulani na kuangalia 'ubobezi' wake. Lakini, hii itategemeana kama mtu huyo ana akaunti katika Google Scholar. Kama hana, kuna vyanzo vingine maarufu kama, Researchgate na Academia.edu.

Kwa hiyo nilianza kwa kuandika jina "Tulia Ackson' katika Google Scholar, kwa bahati mbaya Tulia Ackson hana akaunti katika Google Scholar. Lakini machapisho yake yaliweza kujitokeza, ambapo niliweza kuona jumla ya machapisho 8 aliyoandika Tulia Ackson. Katika machapisho hayo 8, Google Scholar ilinionyesha idadi ya machapisho yaliyoweza kunukuu machapisho ya Tulia Ackson. Hapa chini naorodhesha machapisho hayo, na kuweka idadi ya nukuu za machapisho.

1. "Disability benefits and workers with HIV/AIDS: Coverage issues and challenges in the United Republic of Tanzania" - hili alichapisha katika jarida liitwalo International Social Security Review, mwaka 2008.
Linapatikana hapa: Disability benefits and workers with HIV/AIDS: Coverage issues and challenges in the United Republic of Tanzania - Ackson - 2008 - International Social Security Review - Wiley Online Library

Na toka mwaka huu, Google Scholar inaonyesha kuwa chapisho hili limenukuliwa mara moja tu. Na aliyelinukuu ni Abdallah Possi katika tasnifu yake ya shahada ya uzamivu mwaka 2014. Inapatikana hapa: www.opus4.kobv.de/opus4-fau/frontdoor/deliver/index/docId/5940/file/THESIS_Possi.pdf

2. "Justiciability of Socio-economic Rights in Tanzania" - hili amelichapisha katika jarida liitwalo, African Journal of International and Comparative Law, mwaka 2015. Linapatikana hapa: An Error Occurred Setting Your User Cookie

Mpaka natumia Google Scholar muda mfupi uliopita, chapisho hili lilikuwa halijanukuliwa.

3. "Social Security Fragmentation in Tanzania: The Challenge of Governance" - hili aliliandika akiwa mwanafunzi wa shahada ya uzamivu pale Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika ya Kusini, mwaka 2008. Linapatikana hapa: http://www.idll.uct.ac.za/usr/idll/resources/monographs/IDL_monograph_2008-1.pdf

Aliliandika kama Monograph iliyotakana na tasnifu yake ya shahada ya uzamivu. Nalo toka mwaka huo, alijawahi kunukuliwa kwa mujibu ya Google Scholar.

4. "The role of the law of regional organisations in reforms of social protection systems: portability of social security benefits in the East African Community" - hili alichapisha kama sehemu ya kitabu kiitwacho, "Social Protection in Developing Countries: Reforming Systems" kilichoandikwa mwaka 2013. Kurasa za awali za kitabu hiki zinapitkana hapa: http://samples.sainsburysebooks.co.uk/9781136178511_sample_493868.pdf

Kwa mujibu wa Google Scholar, hili chapisho nalo halijaweza kunukuliwa na mtu yeyote.

5. ?Access to social services for non-citizens and the portability of social benefits in Tanzania? - hili nalo aliandika kama sehemu ya kitabu kiitwacho, "Access to Social Services for Non-citizens and the Portability of Social Benefits within the Southern African Development Community", kilichoandikwa mwaka 2011. Linapatikana hapa: https://www.uj.ac.za/EN/Faculties/l...uments/Access to social services.pdf#page=139

Kwa mara nyingine tena, Google Scholar inaonyesha kuwa andiko hili halijapata kunukukuliwa.

6. "Social Security Law and Policy reform in Tanzania with reflections on the South African Experience" - hili ndilo tasnifu ya shahada yake ya uzamivu aliyoipata pale UCT, mwaka 2007. Linapatikana hapa: https://open.uct.ac.za/handle/11427/4615

Nalo toka 2007, kwa mujibu wa Google Scholar, halijawahi kunukuliwa.

7. "Extension of social security coverage to the rural population in Tanzania: lessons from India and Iran" - hili alichapisha katika jarida liitwalo, Journal of African and International Law, mwaka 2009. Linapatikana hapa: AfricaBib | Extension of social security coverage to the rural population in Tanzania: lessons from India and Iran

Kwa mara nyingine, Google Scholar inaonyesha kwamba andiko hili halijawahi kunukuliwa.

8. "The New Employment and Labour Relations Law in Tanzania: An Analysis of Labour Legislation in Tanzania" - hili ameandika pamoja na B. Rutinwa na E. Kakula pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 2012. Lakini katika Google Scholar haitoi 'link' ya kuelekea andiko hili, wala ni wapi limechapishwa. Ingawa nalo halijawahi kunukuliwa.

Hivyo basi, katika maandiko yake hayo 8, Tulia Ackson, aliyekuwa Mhadhiri wa Sheria na anayesemwa kuwa mbobezi wa sheria, kaweza kunukuliwa mara 1 tu. Na aliyemnukuu ni mtanzania aliyekuwa akisoma shahada ya uzamivu katika sheria.

Sikuridhika sana na majibu ya Google Scholar. Nikaamua nihamishie utafutaji Researchgate, ambayo katika siku za hivi karibuni watu wengi katika akademia wameonekana kupenda kuwa na akaunti huko. Kule nilimpata Tulia Ackson na rekodi zake. Mwangalie hapa: https://www.researchgate.net/profile/Tulia_Ackson

Rekodi zake katika Researchgate zinaonyesha kuwa: ana jumla ya machapisho 8, ambayo kwa ujumla wake yamesomwa mara 33 (ilikuwa mara 32, ikaongezeka 1 baada ya mimi kufungua andiko lake moja) na kunukuliwa mara sifuri.

Sikuridhika sana. Nikasema, pengine yale majarida ambayo alichapisha maandiko yake ni ya viwango vya juu sana katika fani ya Sheria. Kwa maana katika ulimwengu wa akademia, wapi unachapisha maandiko yako ina nafasi kubwa sana ya kuonyesha 'ubobezi' katika fani. Unaweza kuwa na machapisho machache sana, lakini katika majarida ya viwango vya juu sana, na ukaonekana 'mbobezi' sana kupita yule aliye na machapisho mengi katika majarida ya viwango vya chini. Sasa katika 'utafiti' wangu huu, inaonyesha Tulia amekwishachapisha katika majarida haya: Journal of African and International Law, African Journal of International and Comparative Law, na International Social Security Review.

Nikaamua kwenda mbele zaidi kufuatilia kwa undani majarida hayo. Pengine nidokeze kidogo jambo hili: katika akademia ubora wa majarida utokana na kitu kinachoitwa 'impact factor', kwa tafsiri isiyo rasmi ni athari (katika taaluma sana sana) ya jarida katika fani husika. Na hii 'impact factor' utokana na wastani ambapo chapisho katika jarida hilo unukuliwa kwa mwaka. Kwa hiyo kama jarida lina 'impacts factor' ya 4, inamaanisha kwamba kwa wastani, machapisho katika jarida hilo unukuliwa mara 4 na machapisho mengine.

Sasa, jarida la Journal of African and International Law, tovuti yake ni hii: Law Journals: Submissions and Ranking, ingawa hii siyo tovuti rasmi, ila ni tovuti inayoonyesha 'link' kwenda kwenye tovuti ya jarida hilo. Kwa mshangao mkubwa, nimejaribu mara nyingi kufungua 'homepage' (http://aicil.or.tz/law-journal/) ya jarida hilo, na kushindwa mara zote. Anuani ya ofisi zake zinaonyesha zipo Songea, Tanzania, katika taasisi iitwayo, 'African Institute for Comparative and International Law'. Jarida halina 'impact factor' na kwa kweli inavyoonekana, ni jarida la viwango vya chini sana. Kwani hata katika Google Scholar, upatikanaji wa jarida hili, ni wa mashaka, ukitoa chapisho ambalo Tulia analo katika jarida hili.

African Journal of International and Comparative Law, jarida hili utolewa na 'Edinburgh University Press', Scotland. Ingawa nalo halina 'impact factor', lakini angalau linaonekana kuwa la kuaminika kiasi.

International Social Security Review, jarida hili uchapishwa na "International Social Security Association" kupitia Wiley Publishing. Ingawa nalo halina 'impact factor', lakini pia linaonyesha kuwa la kuaminika kiasi.

Kwa hiyo, pamoja na majarida hayo machache, Tulia hajaweza kuchapisha katika majarida yenye viwango vya juu katika fani ya sheria. Majarida ya viwango vya juu katika sheria ni yepi? Angalia hapa kupata list ya majarida ya fani ya sheria: http://about.jcr.incites.thomsonreuters.com/full-titles-2015.pdf

Kwa upande mwingine, kitu ambacho kinajidhiirisha katika rekodi yake ni kwamba, Tulia Ackson anaonyesha kuwa na 'utaalamu' katika sheria za hifadhi ya jamii. Na wala siyo mtaalamu wa sheria za uhifadhi wanyamapori, udhamini, sheria ya usimamizi wa mirathi, na ufadhili miradi na madini kama gazeti la Habari Leo linavyotaka kuniaminisha. Rekodi yake inaonyesha hivyo, wala siyo mimi ninayesema hivyo.

Kwa kifupi, 'utafiti' wangu usio rasmi umenifanya nijiulize maswali ya kile kinachoitwa ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson. Labda kama kuna viashiria vingine (ambavyo mimi sivifahamu) katika ulimwengu wa akademia ambavyo umfanya mtu aitwe mbobezi katika fani yake. Lakini kama viashiria vinavyotumika kwa sasa: idadi ya machapisho, wapi yamechapishwa (hapa naongelea kuchapishwa katika majarida yenye viwango vinavyotambulika katika fani husika), na mara ngapi yamenukuliwa katika machapisho ya watu wengine, hakika bado sijaona ubobezi wa Tulia Ackson katika fani ya Sheria.

Kwa hiyo, ningependa kuuliza, upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa?
Kinachoonekana ni wivu tuu unakusumbua huna lolote. Wewe umeandika machapisho mangapi?
 
Back
Top Bottom