Ubaguzi: Mkuu wa Wilaya akataa kuzindua mashindano ya mpira kisa jezi kufanana na bendera ya CHADEMA

Hapo ndipo Tanzania tumefikia, na mwelekeo ndio huo huo maana huenda Boss ndio anataka hivyo na anapenda hivyo, ni kubaguana tu kwa kwenda mbele...

Yaani ukihusishwa na CHADEMA tu basi utakiona cha mtema kuni. Kuanzia rangi, msimamo, biashara, kauli, kabila, ukanda nk.

Ninaichukia Tz ya sasa.
 
Kwakweli hicho ni kitendo kibaya sana ,sasa tytaanza kubaguana kwa mavazi kweli? Kweli nimeamini.Kauli ya mwalimu nyerere kuwa dhambi ya ubaguzi nisawa na kula nyama ya mtu, tunakoelekea mpaka vinywaji au mavazi ya kaki yatapigwa marufuku
 
Mkuu wa Wilaya ya Njombe amegoma kushiriki shughuli za uzinduzi wa jezi ya timu ya mpira wa miguu ya Wilaya ya Njombe iliyofuzu kucheza Ligi Kuu ya VodaCom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018, akidai bendera ya timu hiyo inafanana na ile ya CHADEMA.
View attachment 544650 View attachment 544651
Hatunaga Jipya kwani tumeshaondolewa ufahamu hivi bila kuhudhuria utapata wapi mtu wa kumbadiliisha itikadi aliyinayo itikadi ni ushawishi

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
wanatekeleza matakwa ya baba yao hivyo ndo vitu wanavyoambiwa kupambana na upinzani
 
Anajua PM juzi alihutubia wananchi Mtama huku kukiwa na wanachadema kibao na magwanda yao mbele kabisa?

I wish vyeo vya ukuu wa wilaya na mkoa vifutiliwe mbali maana wanamwaibisha sana mkuu wa nchi.

 
Wana mtia aibu aliyewachagua.
Magufuli kachagua watu wa ajabu sana

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
Kwani aliyewateua mwenyewe yukoje? Mbona mimi naona wanareflect mteuzi wao. Anayoyasema na kuyatenda husikii na huyaoni? Anataka aongee yeye tu na chama chake tu wengine wote wakae kimya hadi 2020 vinginevyo ni saa 48

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom