Uamuzi wa viongozi wa CHADEMA kutohudhuria tena mahakamani una tafsiri gani kisheria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uamuzi wa viongozi wa CHADEMA kutohudhuria tena mahakamani una tafsiri gani kisheria?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 13, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaJF,
  Kwenye tamko lake kuhusu mauaji yaliyofanywa na jeshi la polisi jijini arusha, chadema inaonyesha kuwa mkutano waliofanya ulikuwa halali kwa mujibu wa katiba ya nchi na kwa hiyo kukamatwa kwao na kusomewa mashtaka mahakamani ilikuwa ni uonevu mkubwa. Kutokana na hilo, chama kimeamua kuwa viongozi wake hawatahudhuria tena mahakamani. Jamani hapo ndipo penye swali langu. Hivi uamuzi huo wa cdm una implication gani kisheria?? Hofu yangu ni kuwa isije ikawa ndiyo chanzo cha matatizo mengine.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  tuseme kushitakiwa kwao ni majungu na fitna za kisiasa.

  unadhani watatendewa haki?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,420
  Trophy Points: 280
  na kama wanataka mabalaa watoe warrant ya kuwashika leeeeee!! hapo baba watakuwa wanachokoza nyuki
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Najaribu kuangalia from another angle kwamba chombo kilichowaita wajibu mashtaka siyo jeshi la polisi bali ni mahakama ambayo ni mojawapo ya mihimili mikuu ya nchi. Sasa kutohudhuria mahakamani maana yake ni kuwa wanaigomea mahakama. Je, hiyo inakubalika?? Kwa nini wasiendelee kuhudhuria ili haki itendeke then hukumu ikitolewa ndipo wawasilishe kwenye mahakama hiyo hiyo madai ya hasara watakayoipata in whatever form? Wasiwasi wangu ni cdm wasije wakapoteza credibility yao kwa wasomi na wanazuoni.
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Serikali (Membe) imeshasema polisi walikosea kwa hiyo hata kukamatwa kwa viongozi wa CDM ni makosa hakuna mashtaka hapo yafutwe.
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  In short it is a planned move hata yale maandamano yalikuwa planned watu walikuwa wanasema kama unavyosema wewe watapoteza credibility lakini leo ni tofauti. Kwanza haki unayosema itolewe na nani mahakama ya Makamba? you must be joking.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  akibanwa(membe) na mahakama utasikia akisema 'yalikuwa ni maoni yangu binafsi'
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Yes, nikifikiria credibility ya mahakama zetu, napata kizunguzungu. Ngoja tusikie maoni ya wataalam wengine. My opinion is that cdm should at no time lose its high credibility before the public. Ninafurahi ninapoona katika kila issue/game, sisiem ndiyo inakuwa guilty, kama ilivyotokea arusha.
   
 9. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NINADHANI KWA SUALA LA KUTOKUHUDHURIA MAHAKAMANI WAMEKOSEA. NI VIZURI WAKAHUDHURIA MAHAKAMANI ILI KULINDA HESHIMA YA MAHAKAMA. KWA KUWA CHADEMA NI CHAMA MAKINI, Watu wengi watapenda kuiga mfano wao. IT IS HIGHLY IMPORTANT THAT THEY SHOW THEIR RESPECT TO THE RULE OF LAW.
   
 10. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kwa vile mashitaka yao ni ya jinai na wako nje kwa dhamana, hatari iliyopo ni dhamana kufutwa kama masharti yake yataonekana mahakamani kuwa yamekiukwa na hivyo wote kukamatwa tena na kurudishwa rumande...... na wao katika tamko lao naoma wameishalifahamu hilo na wamesema wako tayari........ so i can see that everything is properly culculated na hii ni siasa, kazi iliyopo ni washitaki wao nao ku-culculate the implication ya kuendelea na masitaka dhidi yao ama la, kama wataendelea na mshitaka dhidi yao, hakuna mwanya wa kuepuka kufutiwa dhamana kama kweli watatekeleza azma yao hiyo....................

  in my opinion, chandema wanashinikiza kitu amabacho ni obvious kitatokea, yaani kufutiwa mashtaka, labda wanataka tu kuongeza shinikizo la kufutiwa haraka...............serikali kwa kufahamu hisia za jamii na jumuia ya kimataifa, haitakuwa tayari kufanya kosa kama la kuwakamata tena, arusha yaweza kulipuka upya na hata nchi nzima yaweza kulipuka kwa maandamano kuprotest hilo na hata jumuiya ya kimataifa yaweza kuiweka nchi yetu kundi moja na ivry coast............... so i believe, in the end serikali itakuja kiutu uzima na viable solution............
   
 11. n

  niweze JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanini Viongozi CDM Waende Mahakamani? How About Waliopigwa Risasi na Kufa Nao Tuwalete Mahakamani? How About Waliowapiga Risasi Je, Hukumu na Sheria Zao Ziko Wapi? How About JK na Wote Waliohusika Kutoa Orders za Mauaji Wanafikishwa Mahakamani Lini? Hili Swali Hapa Juu Linauliza Only Viongozi wa CDM, Sheria Ipi Walivunja na Hatari Gani Waliisababishia Mkoa wa Arusha na Taifa? "Katiba Hii ya Sasa Haina Meno na Hatutaifuata Kamwe Mpaka Katiba Mpya Ipite?" Wananchi Tusikubali Kamwe Kunyamazishwa na Sera na Taratibu Mpya za CCM.
   
 12. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Kama wanataka kutawala nchi hii lazima waonyeshe wanavyojua utawala wa sheria, na kuufuata.

  Innocent until proven guilt, na hii inapatikana mahakamani, haiwezekani wakamua wenyewe kuwa innocent. Tutaamua.
   
 13. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  CDM ndo waliomba kupelekwa mahakamani ili sheria ifuatwe. walitaka kuwatema kikudakuda huku weshawadharirisha.
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Naomba niwajibu nyote kwa pamoja kama ifuatavyo.........nafikiri implications mnazofikiria tayari wenyewe wanazijua angalieni kwenye bold.

   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hili la kutoenda mahakamani ndiyo nimeliona hapa lkn binafsi sikusikia kauli hii sana sana waliwaomba wananchi kufika siku ya kesi yao ambayo itakuwa tarehe 21-01.2011
   
 16. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nilikuwepo uwanjani, nilisikia kwa masikio yangu. Chadema waliagiza polisi wafute kesi mahakamani bila masharti yoyote kwa kuwa serikali na jamii ya kimataifa imeshakubali kuwa ni polisi ndio waliokosea. Lakini Mbowe aliwaomba wakazi wote wa arusha kuhudhuria mahakamani siku ya kesi iwapo polisi watakuwa hawajafuta kesi.

  hivi huwa kuna adhabu kwa mtu anayeanzisha uzushi na kuna ushahidi kuwa ananzisha uzushi?
   
 17. Q

  Quick Senior Member

  #17
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Remember,there is no strict separation of power btn the Executive and Judiciary,thats y rule of Law ni mchanga wa macho
   
 18. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Si vizuri kukurupuka na kuweka uzushi hapa JF kama ulihudhuria mkutano wa NMC jana, Mkt Mbowe alisema kuwa tarehe 21 ndio kesi yao itatajwa na kuwauliza wadau kama watakuwepo mahakamani kuwaunga mkono, kauli ambayo ilioungwa mkono na mkutano wote. Kama hukuwepo ktk mkutano wa NMC na umesikia toka kwa source nyingine na siyo toka kwa aliyezungumza basi fanya utafiti tena.
   
 19. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ...mahakama itumie maamuzi ya busara,,,,ikijidai kuwa sheria ni msumeno itakula kwao manake its obvious kwamba kukamatwa kwa viongozi wa chadema na mauaji yaliyofanyika yalikuwa ni utekelezaji wa "amri ya mtu fulani".
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nchi ina taratibu zake na sheria, whether good or bad

  CDM wanahitaji kuheshimu hayo, kwani ipo siku wanaweza kuwa madarakani na sijui wanatuonyesha nini kama wanashindwa kuheshimu msingi mmojawapo muhimu wa utawala... kwangu ni maamuzi ya kihuni

  two wrongs wont make it right... never!!!

  wanatufundisha nini?? kwamba kuna mahakama za watanzania na ni tofauti na za cdm??

  maamuzi kama haya huwa yanatolewa na walevi wa pombe, na nikiwa serikali, nitaamuru washughulikiwe kwa mujibu wa sheria
   
Loading...