Uamuzi wa viongozi wa CHADEMA kutohudhuria tena mahakamani una tafsiri gani kisheria?

wasiwasi wangu ni kuwa mbali na yaliyotokea arusha, ccm inataka kuonyesha kuwa upinzani ni vurugu kama jinsi ambavyo wamekuwa wakiropoka wao wapo tayari kuona hata watu wanakufa ili kukamilisha malengo yao ya kisiasa kisha kuanza kunyooshea kidole wengine,mfano angalia ya arusha licha ya uzembe wao bado wanadiriki kufungua mdomo kutetea mauaji!la kushangaza licha ya kuwa hakuna hata taasisi moja isiyo ya kiserikali na watu wenye uelewa kuwaunga mkono bado wamesimamia kuwa kama cdm wasingekaidi amri ya polisi yasingetokea!

la kujiuliza ni kwamba kwanini wao watumie polisi kuua demokrasia?,ni kwanini polisi ikitumika vibaya bado tu watu watii?

Kishe,
Nafikiri nafikiri tunazungumza lugha moja sasa. Ni vyema ccm wakaendelea kuonekana wajinga. Serikali yao kupitia waziri Mende ... oops ... Membe, ndio wametamka kuwa Polisi walikurupuka. Na kama ni hivyo basi wafute kesi. Kama watu wao ndio waliokurupuka kwa nini mtu mwingine aendelee kufuatilia kesi hewa?
 
Mkuu Crashwise...
Hii ni mpya kwangu!.

Huyu Gosbertgoodluck kapata wapi ya kugomea mahakama?

Jana Mbowe aliwaomba wana-Arusha wote wajitokeze tarehe 21/01/11 bila kukosa kwenye mahakama...ili tuone ni nani kati ya ccm na peoples power mwenye nguvu!..
Hii habari ni ya kutunga, na hatujaelewa ina maana gani kwa jamii!

Nimesikia kwenye mojawapo ya redio zetu. Inawezekana habari hiyo ilichakachuliwa kukidhi matakwa ya sisiem.
 
Najaribu kuangalia from another angle kwamba chombo kilichowaita wajibu mashtaka siyo jeshi la polisi bali ni mahakama ambayo ni mojawapo ya mihimili mikuu ya nchi. Sasa kutohudhuria mahakamani maana yake ni kuwa wanaigomea mahakama. Je, hiyo inakubalika?? Kwa nini wasiendelee kuhudhuria ili haki itendeke then hukumu ikitolewa ndipo wawasilishe kwenye mahakama hiyo hiyo madai ya hasara watakayoipata in whatever form? Wasiwasi wangu ni cdm wasije wakapoteza credibility yao kwa wasomi na wanazuoni.

Mahakama haikuwaita, wameperekwa mahakamani na Polisi kwa niaba ya Jamhuri; Mahakama ni third part inasikiliza mashtaka kama yalivyoletwa na Jamhuri (Serikali) dhidi ya Washtakiwa; sijui katika kuamua kutokwenda madhara gani watapata ila rejea kuwa kuna-washeria waliobobea kesi za jinai pale chadema kama wakina Marando, Tundu et al sijui kama wameamua kwa hasira au wameangalia kiundani!;

Ila Ninachoona mimi hata wakishiriki bado kuna tatizo maana katika kesi za Tanzania hakuna msingi halisi wa haki, maana Mchunguzi ni Polisi na Muendesha mashtaka kwa niaba ya DPP ni Polisi hao hao na katika hili la Viongozi wetu ni tata zaidi maana Polisi sasa wana sura nne, MOJA: Ndio walalamika number moja au shahidi namba moja kwa lugha ya Ki_mahakama kwa maana wao ndio watakao toa ushahidi wa uhalali au uharamu wa maandamano ya Jan 5 kwa maana ya kuwepo au kutokuwepo kwa kibali; PILI: wao ndio Wa-endesha mashtaka kwani niaba ya DPP juu ya kesi hiyo; TATU: wao ndio wachunguzi wa tukio kwamba watajichunguza vipi kutoa majibu labla kuwa kesi haina ukweli iwapo hilo ndio jibu sahihi! NNE: Ni sura yao ya nje ya Upolisi yaani walinzi wa raia na mali zao (au amani ya ndani ya nchni) hapo kuna tatizo kubwa.

Mi nadhani kama POLISI yetu ingekuwa ni Jeshi la wasomi, ambalo viongozi wake wanafanyakazi kwa utashi wa ELIMU na uelewa sio umimi na nafasi za kupewa kama za zawadi wasinge ua watu kama ni kweli maandamano haya kuwa na kibali, hapo ndipo kesi yao ingeonekana ni ya maana na ina nguvu ya kisomi zaidi sio misuri na siasa Uchwara za kutumwa na wanasiasa waliokwisha kufa kimawazo na kiroho; wangewakamata vingozi CDM baada ya maandamano hata siku moja baadae na kuwapereka mahakamani kwa kesi kama hiyo lakini sio kwenda kuvamia raia kama unavamia IDD-AMINI alafu una-justify uvamizi huo na neno dogo sana kukosa kibali what is kibali just a peace of paper inyosahiniwa na mjinga mmoja RPC ambaye hata Form hana, ndio wafanye vita? hapo msingi wa kesi yao hamna tena. Tena na kwambia huyo siMWEMA ni mjinga sana toka akiwa RCO wa DSM uwezo wake ni mdogo sana ila sasa serikali za dhuruma vyeo wanapewa Mbumbumbu ili wawatume kama matahira we unadhani mtu mwenye uwezo mkubwa aliye elimika na Msomi angelikubali kutumwa akaue watanzania wenzake akubali thubutu, angemwambia Mkuu sahamani sana kama kuna kosa nitalishughulikia kwa mujibu wa sheria, sio ndio Mkuu ni uwe wangapi? hili waogope kabisa PUMBAFU Tutampereka THE HUGE Nalifanyia kazi kwa sasa.
 
Asante sana mkuu kwa muda wako. Umetuelimisha wengi. Nakubaliana na hoja yako kwamba viongozi wetu wana hulka mbaya ya kuteua watu wasio na uwezo wa kushika nafasi nyeti ili wawatumie kwenye mambo yao binafsi. Said Mwema ambaye pia shemeji yake jk, ni mmojawapo wa waliofaidika na hulka hiyo chafu.
 
gosbertgoodluck;
Hilo la ushemeji wa KJ na Si-Mwema la ukweli? Hebu tupe kidogo. Kama ni hivyo basi hatuna serikali.
 
Back
Top Bottom