Uamuzi wa viongozi wa CHADEMA kutohudhuria tena mahakamani una tafsiri gani kisheria?

Jaji Mkuu ni mshikaji wake Jk; wakati akiwa UDSM sehemu ya mlimani, kitivo cha sheria alimbeba Riz1 - dogo alikwisha ramba ngoma kama nne za kumpelekea kwenye discontinue, na baadaye kumpa fadhila ya ujaji kabla ya kuwa jaji mkuu!
 
nchi ina taratibu zake na sheria, whether good or bad

CDM wanahitaji kuheshimu hayo, kwani ipo siku wanaweza kuwa madarakani na sijui wanatuonyesha nini kama wanashindwa kuheshimu msingi mmojawapo muhimu wa utawala... kwangu ni maamuzi ya kihuni

two wrongs wont make it right... never!!!

wanatufundisha nini?? kwamba kuna mahakama za watanzania na ni tofauti na za cdm??

maamuzi kama haya huwa yanatolewa na walevi wa pombe, na nikiwa serikali, nitaamuru washughulikiwe kwa mujibu wa sheria

Thanx mkuu acid.
umeeleza kitu cha maana sana ingawaje mleta mada sijui katoa wapi hii maneno.
Watu wanapenda tu kusikia vile wanapenda tu bila kujalisha umantiki wake, they dont like to think criticaly
 
naona mnatuchanganya mara walisema hawaendi mara walisema wanaenda vyote ni mkanganyiko!,ila nimesoma tanzania daima la leo kuna maelezo kuwa moja ya tamko lao ni kutaka kesi ifutwe bila masharti vinginevyo hawatahudhuria mahakamani na wapo tayari kukamatwa.

maoni yangu:
japokuwa suala ili limekaa kisiasa zaidi ni bora wahudhurie mahakamani kuliko kutokwenda,cdm wamekuwa wakihubiri amani ni bora kuitekeleza kivitendo kwani suala ili linaweza kuibua mgogoro mkubwa sana.
 
Serikali (Membe) imeshasema polisi walikosea kwa hiyo hata kukamatwa kwa viongozi wa CDM ni makosa hakuna mashtaka hapo yafutwe.

Membe alisema tamko hilo ni lake binafsi kwani mabalozi wamekuwa wakimsumbua atoe tamko la serikali.Amesema tamko la serikali litatolewa wiki hii.
Isitoshe, hata ktk tamko la Membe aliwalaumu Polisi si kwa kuvunja maandamano, bali kwa 'kutumia nguvu kupita kiasi' na 'kuvuka mipaka yao kisheria'.
Hiyo haisemi lolote juu ya mwenendo wa kesi.
 
which rule of law you guys are talking about?
There is no rule of law here, let me wait 2015 may be it will visit my beloved Tanzania!
 
hili la kutoenda mahakamani ndiyo nimeliona hapa lkn binafsi sikusikia kauli hii sana sana waliwaomba wananchi kufika siku ya kesi yao ambayo itakuwa tarehe 21-01.2011


Katika Tamko Na 4 kati ya 7 CHADEMA wanasema, na hapa nanukuu:
"Mashtaka ya uongo ya jinai yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA, wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote waliokumbwa na kumba kumba ya Jeshi la Polisi la Tanzania yafutwe bila masharti yoyote kwa sababu maandamano na mkutano wa hadhara uliozuiliwa yalikuwa halali kwa mujibu wa sheria husika za nchi yetu. Tunasisitiza katika jambo hili kwamba viongozi, wanachama na wafuasi wetu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka haya hawatahudhuria mahakamani tena kuhusiana kesi iliyofunguliwa dhidi yao hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani".

Mwisho wa kunukuu.
 
nchi ina taratibu zake na sheria, whether good or bad

CDM wanahitaji kuheshimu hayo, kwani ipo siku wanaweza kuwa madarakani na sijui wanatuonyesha nini kama wanashindwa kuheshimu msingi mmojawapo muhimu wa utawala... kwangu ni maamuzi ya kihuni

two wrongs wont make it right... never!!!

wanatufundisha nini?? kwamba kuna mahakama za watanzania na ni tofauti na za cdm??

maamuzi kama haya huwa yanatolewa na walevi wa pombe, na nikiwa serikali, nitaamuru washughulikiwe kwa mujibu wa sheria

Ndugu Acid,

Ulishawahi kuona wapi mahakama za tanzania zinatenda haki kwa wanyonge, ni juzi tu chenge anatozwa laki saba kwa hatia ya kuwaua watu wawili na kuendesha gari lisilo na bima. kama haitoshi tumeona kwa ditopile, Zombe, Mama wa mwanza aliyedhalilishwa mgodini etc hiyo ni mifano michache tu. kwa hiyo tusiiamini hizi mahakama kivile watapiga kesi dana dana hadi 2015 na kuwahukumu kipindi cha kura ya maoni.

Sisi tunawajua CCM vizuri, inakuwa polisi waliouwa watu wana randa randa mtaani hadi leo mtaani kama kweli mahakama ina nguvu. Kwani haioni kama wamevunja sheria.

Peoples power itafanya kazi kama vipi.
 
maamuzi kama haya huwa yanatolewa na walevi wa pombe, na nikiwa serikali, nitaamuru washughulikiwe kwa mujibu wa sheria

Na huu ni ulevi wa chimpum haswaa. Unaongeza maji moto tuuu
 
kwakweli mimi naona kesi hapo haipo, kwasababu hakuna kosa la kisheria serikali imejikanyaga yenyewe, na ukiangalia doc. utagundua serikali hususani polisi ndio wanapaswa kushitakiwa kwa kuua na kuumiza raia pasipo na hatia
 
Dhamira waliyo nayo viongozi wa chadema ni SAFI SANA; polisi kwa mda wamekuwa wakilalamikiwa na raia kubambikiza watu kesi, na safari hii ndivyo ilivyo fanyika. Hivyo wapambanai wetu wanaiambia polisi wakome. Pili mahakama imekuwa ikitumiwa vibaya na wanasiasa hasa katika masuala ya uchaguzi, matokeo ya uchaguzi yamekuwa yanapindishwa kwa kujua kuwa mtu akienda mahakamani kutafuta haki, kesi hiyo itapigwa dana dana mpaka kipindi cha uongozi kiishe, ccm ilitegemea mambo yatakuwa hivyo kwenye ili suala la umeya wa Arusha, lakini chadema ikasema no way safari hii itatumika peoples power; hata kwa swali hili, mahakama ikikubali kutumiwa kisiasa sana sana itawafutia mzamana, ili waendelee kusikiliza kesi yao wakiwa mabusu. Hivi hilo likitokea Arusha kutakalika; hasa ikiwekewa maanani ya kuwa waarifu halisi katika sakata hili hawajakamatwa.
 
Why are we speculating???

Hivi CDM wanavyojulikana kwa kutokurupuka huku wakiwa na wanasheria nguli, mnadhani haya maswali mnayojiuliza hapa hawayajui???

Mnadhani hawana majibu yake???

Tusubiri tar 21.01.2011 ndipo hii thread iletwe kwa sasa tunaweza tukapoteza nguvu bure.

Je mnakumbuka ngunguri mmoja wa CUF alivyowabeza CDM baada ya maandamano ya Buguruni??? Alisema "CUF ndo dume, kama CDM wanaume waingie barabarani tuone maana wao siku zote nyuma ya keyboard tu" Leo ataongea nini huyu mtu??

Lets not rush to blind conclusions!!!!!!
 
Si vizuri kukurupuka na kuweka uzushi hapa JF kama ulihudhuria mkutano wa NMC jana, Mkt Mbowe alisema kuwa tarehe 21 ndio kesi yao itatajwa na kuwauliza wadau kama watakuwepo mahakamani kuwaunga mkono, kauli ambayo ilioungwa mkono na mkutano wote. Kama hukuwepo ktk mkutano wa NMC na umesikia toka kwa source nyingine na siyo toka kwa aliyezungumza basi fanya utafiti tena.

Gazetí la mwanachi limeandika Chadema awatokwenda mahakamani, katika madai ya katiba mpya chadema jambo kubwa katika katiba wanataka matokeo ya kura za urais yapingwe mahakami, sasa kama leo Chadema wameweka bayana awatokwenda mahakamani katika sakata la vurugu zilizotekea wakati polisi wakivunja maandamano kisha kuuwa watu watatu pamoja na polisi, Membe kasema polisi walitumia nguvu lakini Membe ana nguvu zaidi ya mahakama?
 
Si vizuri kukurupuka na kuweka uzushi hapa JF kama ulihudhuria mkutano wa NMC jana, Mkt Mbowe alisema kuwa tarehe 21 ndio kesi yao itatajwa na kuwauliza wadau kama watakuwepo mahakamani kuwaunga mkono, kauli ambayo ilioungwa mkono na mkutano wote. Kama hukuwepo ktk mkutano wa NMC na umesikia toka kwa source nyingine na siyo toka kwa aliyezungumza basi fanya utafiti tena.

Kwenye Tamko la Chadema kwenye gazeti la Tanzania Daima Uk18-19 katika uk. 19 kwenye kichwa cha habari HAKI LAZIMA ITENDEKE ARUSHA, katika aya ya 7 mistari 5 ya mwisho inasomeka hivi, na hapa nanukuu, "Tunasisitiza katika jambo hili kwamba viongozi na wanachama na wafuasi wetu wote, waliokamatwa na kufunguliwa mashitaka haya hawatahudhuria mahakamani tena kuhusiana na kesi iliyofunguliwa dhidi yao hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani" mwisho wa kunukuu

tafsiri yangu ni kuwa utekelezaji wa tamko hili hasa kifungu nilicho nukuu hapo juu kitahold true baada ya kuhudhuria mahakamani tar 21/1/2011. kwani waliokuwa NMC waliambiwa wajumuike nao mahakamani siku ya kutajwa kwa kesi!
 
Gosbergudlucky acha kupotosha umma kwa kusema viongozi wamesema hawatahudhuria mahakamani,huo ni uongo walichosema ni kwamba tarehe 21 wananchi wajitokeze kwa wingi mahakami wakati kesi itakapotajwa,cdm wana ushahidi wa maandishi wa kuruhusiwa kuandamana na kufanya mkutano,so hamna wasi qwasi wa kutendewa haki,ushindi upo wazi kabisa,ila walisema polisi waache kuwabambikia watu kesi,eg kuna vijana walishikwa kwenye maandamano kisha polisi kuwafungulia kesi ya jinai,ndicho cdm wanachopinga,
 
Ndugu zangu wanaJF,
Kwenye tamko lake kuhusu mauaji yaliyofanywa na jeshi la polisi jijini arusha, chadema inaonyesha kuwa mkutano waliofanya ulikuwa halali kwa mujibu wa katiba ya nchi na kwa hiyo kukamatwa kwao na kusomewa mashtaka mahakamani ilikuwa ni uonevu mkubwa. Kutokana na hilo, chama kimeamua kuwa viongozi wake hawatahudhuria tena mahakamani. Jamani hapo ndipo penye swali langu. Hivi uamuzi huo wa cdm una implication gani kisheria?? Hofu yangu ni kuwa isije ikawa ndiyo chanzo cha matatizo mengine.

haya yote ni ya kwako sidhani kama tamko la chadema limeelezea viongozi wake kutokuhudhuria mahakamani viongozi wa chadema watahudhuria mahakamani kwani ni wapenda amani na wanaofuata sheria upotoshaji wa habari nadhani ndio unaotupelekea kujadili jambo ambalo halipo na halitakuwepo!
 
kwa vile mashitaka yao ni ya jinai na wako nje kwa dhamana, hatari iliyopo ni dhamana kufutwa kama masharti yake yataonekana mahakamani kuwa yamekiukwa na hivyo wote kukamatwa tena na kurudishwa rumande...... na wao katika tamko lao naoma wameishalifahamu hilo na wamesema wako tayari........ so i can see that everything is properly culculated na hii ni siasa, kazi iliyopo ni washitaki wao nao ku-culculate the implication ya kuendelea na masitaka dhidi yao ama la, kama wataendelea na mshitaka dhidi yao, hakuna mwanya wa kuepuka kufutiwa dhamana kama kweli watatekeleza azma yao hiyo....................

in my opinion, chandema wanashinikiza kitu amabacho ni obvious kitatokea, yaani kufutiwa mashtaka, labda wanataka tu kuongeza shinikizo la kufutiwa haraka...............serikali kwa kufahamu hisia za jamii na jumuia ya kimataifa, haitakuwa tayari kufanya kosa kama la kuwakamata tena, arusha yaweza kulipuka upya na hata nchi nzima yaweza kulipuka kwa maandamano kuprotest hilo na hata jumuiya ya kimataifa yaweza kuiweka nchi yetu kundi moja na ivry coast............... so i believe, in the end serikali itakuja kiutu uzima na viable solution............

Ubarikiwe kwa maelezo mazuri. Nimekuelewa vizuri sana.
 
Ndugu Acid,

Ulishawahi kuona wapi mahakama za tanzania zinatenda haki kwa wanyonge, ni juzi tu chenge anatozwa laki saba kwa hatia ya kuwaua watu wawili na kuendesha gari lisilo na bima. kama haitoshi tumeona kwa ditopile, Zombe, Mama wa mwanza aliyedhalilishwa mgodini etc hiyo ni mifano michache tu. kwa hiyo tusiiamini hizi mahakama kivile watapiga kesi dana dana hadi 2015 na kuwahukumu kipindi cha kura ya maoni.

Sisi tunawajua CCM vizuri, inakuwa polisi waliouwa watu wana randa randa mtaani hadi leo mtaani kama kweli mahakama ina nguvu. Kwani haioni kama wamevunja sheria.

Peoples power itafanya kazi kama vipi.

Mkuu ni kweli kwamba haki haipatikani kirahisi na kwa haki kwenye nchi hii.

Hawa viongozi wa CDM ni public figure na watu wengi tuko nyuma yao kutaka kujifunza mengi.
Kwa uamuzi huu wa kutokwenda sio sahihi na mimi ningewashauri wakae chini waamue tena upya na kukubali kwenda mahakamani.
Haki hata kama itakiukwa hakuna mtu ambae hatajua.

Wao waende halafu haki ikiukwe ndipo JK na timu yake watakapojua kuwa hii nchi watu tumechoka

Viongozi wa CDM wasirekebishe kosa kwa kosa
 
Kwani hukumu ya chenge imeahirishwa mara ngapi kwa kuwa hakuwepo Dsm eti mara alikuwa msibani huko unyantuzuni ,mara alikuwa mgonjwa ughaibuni,na hakuna hatua yeyote Mahakama za kifisadi zilichukua kumbana Chenge leo mnaleta wasi wasi kwa kuwa sisi ni CHADEMA?Mahakamani hatuji na mkitaka mje kutushika muone shabashiiiiiiiiiiiiiiiiiiii;;;
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom