Uamuzi wa kuacha kazi baada ya mapato ya biashara kuzidi mshahara

Rurakha

Senior Member
Oct 20, 2019
121
209
Habari zenu wadau mimi ni muajiriwa sekta binafsi
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita nilikuwa najishughulisha na ujasiriamali mambo yalikuwa magum sana sikua na mtaji wa kutosha kuhimili soko na ushindani na ilifika wakati hata kodi ilisumbua
Namshukuru mungu nilipata ajira kwa mkataba wa miaka miwili

Nilifanya kazi na kujibana huku kiasi kilichopatikana nikiwekeza katika biashara yangu

Hatimae baada ya mwaka mmoja biashara ikakua ikawa na uwezo wa kunipa faida mpaka ya 2m kwa mwezi na mshahara wangu ni 900k kwa mwezi

Sasa kazini naona mambo haendi vizuri kama mnavyojua kwa wahindi sasa ninafikiria kuacha na nikomae na biashara zangu je uamuzi wangu ni sahihi
Naomba ushauri kwani hata boss wangu hatuelewani
 
Piga kazi hadi mkataba wako utakapo isha kwani hutapungukiwa jambo. Kwanini? Kwasababu hujafanya utafiti na kupata majibu kuwa kuacha kwako kazi kutasababisha vipi faida ipande kutoka 2M kwenda labda 2.9M kwenye biashara yako
 
Hongera sana kwa kufanikiwa kukuza biashara na kuingiza faida ya 2m. Hapo kuna maswali makuu 2 ya kujiuliza.

1. Una savings kiasi gani? Kiusalama ni vema uwe na saving ya kutosha angalau miezi 6 ya matumizi yako wewe kama wewe. Hii itasaidia usianze kula zaidi pesa ya biashara pale utapoacha kazi. Na itakupa muda zaidi kujenga biashara yako bila kuhitaji kutoa pesa yake.

2. Una mpango gani baada ya kuacha kazi? Tengeneza malengo ya biashara kutokana na free time zaidi utayoipata kwa kuacha kazi. Mfano kukuza faida kutoka 2m mpaka 4m. Ama kuongeza bidhaa kutoka 2 hadi 6 na vitu kama hivi. Hii itakuwa na tija zaidi kuliko kuacha kazi na kutobadilisha mwenendo wa biashara.
 
Ni vizuri hii nguvu unayowapa Wahindi kwa 0.9 uiweke kwako lakini katika hii faida ya 2.m jilipe mshahara let say 0.7 nyingine uweke.
Asiweke bali aendelee kuizungusha kulingana na muelekeo na mahitaji wa biashara/huduma anayoifanya maana kwa maelezo yake ni kama inakwenda vizuri.
 
Biashara bila supporting ni swala la muda tu kabla haijakumbwa na dhoruba itakayohitaji utoe pesa kuiponya. Kimbembe ni ukiwa huna hizo pesa maana kazi utakuwa huna ya kukupa hio laki 9 ya kuiboost. Itakufia mkononi na kukuacha na stress mbaya mno!

Ili biashara ijiendeshe yenyewe “Business entity concept” ni lazma uwe una kipato extra tofauti na biashara husika ama uwe na biashara 3 au zaidi zinazokwenda vizuri ili zibebane.
 
Je umemsoma hapa👇

Wakati wowote anaweza zushiwa swala, ili afukuzwe kazi, Hivyo ni vyema kwake akajiongeza, Na kuchukua hatua mapema zaidi.
Kukurupuka kuacha ghafla sio sahihi kwa upande wangu, ni bora zaidi ajikite zaidi katika kujiboresha kikazi ili apate hela zaidi maana anaweza kuwa na tamaa au shauku, what if biashara ikawa mbovu na mtaji ukaisha?
 
Biashara bila supporting ni swala la muda tu kabla haijakumbwa na dhoruba itakayohitaji utoe pesa kuiponya. Kimbembe ni ukiwa huna hizo pesa maana kazi utakuwa huna ya kukupa hio laki 9 ya kuiboost.

Ili biashara ijiendeshe yenyewe “Business entity concept” ni lazma uwe una kipato extra tofauti na biashara husika ama uwe na biashara 3 au zaidi zinazokwenda vizuri ili zibebane.
supported
 
Habari zenu wadau mimi ni muajiriwa sekta binafsi
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita nilikuwa najishughulisha na ujasiriamali mambo yalikuwa magum sana sikua na mtaji wa kutosha kuhimili soko na ushindani na ilifika wakati hata kodi ilisumbua
Namshukuru mungu nilipata ajira kwa mkataba wa miaka miwili

Nilifanya kazi na kujibana huku kiasi kilichopatikana nikiwekeza katika biashara yangu

Hatimae baada ya mwaka mmoja biashara ikakua ikawa na uwezo wa kunipa faida mpaka ya 2m kwa mwezi na mshahara wangu ni 900k kwa mwezi

Sasa kazini naona mambo haendi vizuri kama mnavyojua kwa wahindi sasa ninafikiria kuacha na nikomae na biashara zangu je uamuzi wangu ni sahihi
Naomba ushauri kwani hata boss wangu hatuelewani
Kwamba 2M inakufanya ufikirie kuacha kazi?Hio 2M NI YA MUDA GANI?Je kazi inaathiri uwezekano wa wewe kusimamia vizuri na kuzalisha angalau 20M kwa mwezi.Katika ulimwengu wa ujasiriamali 2M Sio pesa ya kukufanya uache kazi ispokuwa tu iwapo kazi inaathiri uwezo wako wa kutengeneza pesa nyingi zaidi.Ila kama unaweza kutengeneza 2m na kazi ukaendelea kufanya nafikri inaongeza productivity maana sasa pato lako lina 2.9M
 
Kuna vingi vya kujifunza katika biashara bado mapema sana.
 
Kwa maelezo yako haya ni ngumu kupata ushauri unaoeleweka badala yake utapata ushauri wa watu waliojawa uoga wa maisha na wanaoamini katika kutumwa......

Wewe ndio unaefahamu jahazi la maisha yako linavyoenda na likoelekea....... fanya maamuzi kulingana na mipango yako na kwa kuzingatia mwenendo mzima wa maisha yako.......
 
Back
Top Bottom