U-SPIKA: Sitta, Chenge wapigwa panga CCM!

U-SPIKA: Sitta, Chenge wapigwa panga CCM!

Usilaani ili nawe usilaaniwe! Angaliwa mabaya unayowatakia yasikurudie wewe. Mungu akusamehe.

Kikwete na Serikali yake ni chaguo la Mungu na Watanzania.
Mungu hawezi kusikiliza dua mbaya dhidi yao.

Amini usiamini matokeo ni haya

TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU WA 2010REGIONAL # OF VOTERS VOTERS TO VOTE KIKWETE LIPUMBASLAARUNGWEPETERMUGAHYWA TOTAL WINNER BY REGIONALARUSHA 831,827.00 540,687.55 179,240.00 10,814.00 349,011.00 220.00 500.00 902.00 540,687.00 SLAA DAR ES SALAAM 1,786,290.00 1,161,088.50 464,435.40 104,497.97 580,544.25 3,000.00 5,500.00 3,110.00 1,161,087.62 SLAA DODOMA 1,032,372.00 671,041.80 416,045.92 26,841.67 221,443.79 2,000.00 2,000.00 2,710.00 671,041.38 KIKWETE IRINGA 921,054.00 598,685.10 239,474.04 11,973.70 341,250.51 1,986.00 2,100.00 1,900.00 598,684.25 SLAA KAGERA 1,155,770.00 751,250.50 308,012.71 7,512.51 428,212.79 2,000.00 2,512.00 3,000.00 751,250.00 SLAA KIGOMA 768,797.00 499,718.05 264,850.57 134,923.87 94,946.43 1,997.00 1,560.00 1,440.00 499,717.87 KIKWETE KILIMANJARO 912,542.00 593,152.30 166,082.64 5,931.52 415,206.61 1,930.00 2,000.00 2,001.00 593,151.78 SLAA LINDI 508,193.00 330,325.45 188,285.51 109,007.40 32,032.00 200.00 300.00 500.00 330,324.91 KIKWETE MANYARA 634,065.00 412,142.25 98,914.14 4,121.42 304,985.27 2,000.00 121.00 2,000.00 412,141.83 SLAA MARA 813,330.00 528,664.50 200,892.51 10,573.29 315,198.00 1,405.00 500.00 95.00 528,663.80 SLAA MBEYA 1,275,389.00 829,002.85 265,280.91 24,870.09 530,561.82 8,000.00 200.00 90.00 829,002.82 SLAA MOROGORO 1,122,583.00 729,678.95 496,181.69 145,935.79 80,264.68 500.00 600.00 6,196.00 729,678.16 KIKWETE MTWARA 731,444.00 475,438.60 247,228.07 180,666.67 38,035.09 8,500.00 750.00 258.00 475,437.83 KIKWETE MWANZA 1,659,641.00 1,078,766.65 409,931.33 21,575.33 636,472.32 2,000.00 787.00 8,000.00 1,078,765.98 SLAA PWANI 562,373.00 365,542.45 201,048.35 109,662.74 51,175.94 655.00 1,500.00 1,500.00 365,542.03 KIKWETE RUKWA 668,817.00 434,731.05 239,102.08 18,790.00 174,500.00 350.00 1,542.00 446.00 434,730.08 KIKWETE RUVUMA 710,579.00 461,876.35 318,694.68 25,454.00 116,727.00 245.00 500.00 255.00 461,875.68 KIKWETE SHINYANGA 1,650,632.00 1,072,910.80 343,331.46 25,450.00 697,392.02 1,200.00 1,450.00 4,087.00 1,072,910.48 SLAA SINGIDA 668,697.00 434,653.05 226,019.59 12,500.00 195,593.00 520.00 8.00 12.00 434,652.59 KIKWETE TABORA 1,000,091.00 650,059.15 273,024.84 162,514.79 213,519.00 250.00 700.00 50.00 650,058.63 KIKWETE TANGA 1,031,239.00 670,305.35 375,371.00 201,091.61 90,842.00 1,200.00 1,412.00 400.00 670,316.60 KIKWETE 20,445,725.00 13,289,721.25 5,921,447.41 1,354,708.36 5,907,913.52 40,158.00 26,542.00 38,952.00 13,289,721.29 %44.5610.1944.450.300.200.29 100.00 MIKOASLAA10KIKWETE11JUMLA
 
Baada ya kusikia kuwa CCM wamewachagua wakina mama watatu kuwania uspika, moja kwa moja hisia zilinipeleka kuamini kuwa Chenge hakuchukua fomu ya kugombea uspika kwa hiari yake. Alitumwa na chama chake kufanya hivyo. Lazima walikaa na kupanga mkakati huo.

Kila mtu mzima angeliweza kutambua kuwa kulikuwa na jambo; wakati Chenge alipokuwa akibweka katika vyombo vya habari wakati wa kutangaza nia ya kuwania uspika. Hakuwa yeye, bali ilikuwa ni nguvu iliyo ongea juu yake. Kwa kihaya nguvu hiyo inaitwa enchweke.

Kwa kuwa nia ya Chenge haikuwa kuwania uspika bali alitumika kama enchweke, ni dhahiri kuwa sasa Chenge ni mshindi na chama chake. Aliyeshindwa ni Sitta.

Sitta ataachwa hivi hivi. Lazima ataitwa na wazee na kumweleza kuwa ni mapenzi ya Mungu. Atapozwa kwa uwaziri. Na mkewe je?

Siasa, si hasa.
 
KWA MIMI NIJUAVYO ni kwamba bunge lilipitisha kujengwa kwa ofisi za wabunge kila jimbo(sio ofisi ya spika) na walianza na kujenga kwa ofisi ya SITA ,ila kwa kuwa ndio alikuwa spika basi kila mtu anaita ni ofisi ya spika,huu sio ukweli ni upotoshaji mkubwa kabisa.Hata takapo maliza ubunge wake hizo ofisi zitatumika kwa mbunge yeyote atakaye chaguliwa.Hizo ni ofisi za wabunge na zitajengwa kila jiombo Tanzania nzima,tujaribu kufuatialia ukweli sio kuwa washabiki tu wauongo..lol..:A S-baby:
SASA KAMA SITTA OUT, ITAKUWAJE KUHUSU LILE JENGO LA SPIKA LILILOZINDULIWA NA KIKWETE MWAKA HUU KULE URAMBO? JE MAKINDA AKIPITA NAYE ATAJENGA LA KWAKE KULE NJOMBE AU ATAKUA ANAKWENDA URAMBO? INA MAANA SERIKALI HAINA MIPANGO YA MUDA MREFU? NAOMBA YALE MAJIMBO YATAKAYOKUWA NA UCHAGUZI THIS WEEKEND WASIFANYE MAKOSA KUICHAGUA CCM.
attachment.php

:israel:
 
Wote ni majina ya siku nyingi sana: Anna Makinda, Anna Abdallah na Kate Kamba ni majina niliyoskia tangu miaka ya sabini.
Hivi Kate Kamba kafanya nini huo EALA?
Hivi Anna Abdallah ndiye mke wa Msekwa?
Hivi Anna Makinda ndiye aliyekuwa Naibu Spika wakati Sitta?
Mwalimu!
Kwani Sitta alikuwa wa leo?Pili Hao wote waharibifu wacha tu safari hii Bunge liongozwe na mwanamke naona aliyekuwa Naibu ana uzoefu wa miaka mitano iliyopita na hakuwa mbaya sana kwa kila alipoachiwa nafasi ya kuongoza vikao, cha msingi kama atakuwa alijifunza mengi yanayohusu kanuni za uendeshaji na sheria mbali mbali plus na kutokuwa na ugeni na uendeshaji mzima wa bunge na eneo la utendaji kazi yani kwenye Meza Kubwa au Spika Podium na kuwakabili waongeaji anaweza akafanya vyema.Cha msingi ajitahidi asiwe Partisan kwa sana na vile vile changamoto imeongezeka kwa bunge la safari hii kwani Idadi ya wabunge wa vyama vingine imeongozeka kwa zaidi ya asilimia mia moja anatakiwa alitambue hili na wengi wao naamini wataleta hoja zenye kuambatana na vthibitisho.Akilitambua hilo na akasimamia kanuni bila ya kupindisha ataweza tu.
 
Ofisi hiyo, ambayo ilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita, inaelezwa kuigharimu Serikali zaidi ya Sh milioni 500, kama zitajumlishwa gharama za ujenzi pamoja na samani (furniture) zilizomo ndani ya ofisi hiyo, maalumu kwa ajili ya mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki.

Haikuweza kufahamika ni kwanini Sitta, ambaye pia ni Spika wa Bunge linalomaliza muda wake, aliamua kujenga ofisi mpya wakati tayari anayo Ofisi ya Mbunge katika jengo la mkuu wa wilaya ya Urambo.

Rai limeelezwa kwamba kila mbunge, katika mwaka wa fedha wa 2009/2010, alitengewa Sh milioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mbunge jimboni kwake, lakini mbunge wa Urambo Mashariki yeye aliamua ajenge ofisi yenye hadhi ya nafasi yake ya Uspika.

Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya watu walioshuhudia hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo uliofanywa na Rais Kikwete wiki iliyopita, zinasema hata Rais alishitushwa na hadhi ya ofisi hiyo, kiasi cha kujikuta akitamka kwamba ‘kama kila mbunge atataka ajengewe ofisi ya kiwango hiki, basi wabunge wataifilisi nchi hii.'

Jengo la ofisi hiyo ya jimbo, mbali na kuwa na ofisi ya mbunge, inayo pia ofisi ya msaidizi wa mbunge, katibu muhtasi, watumishi wengine wasaidizi (technical staff), chumba maalumu cha watu mashuhuri (vip lounge) na ukumbi wa mikutano unaoweza kuwakusanya watu 30 wakiwa wamekaa kwenye viti.
 
Baada ya kusikia kuwa CCM wamewachagua wakina mama watatu kuwania uspika, moja kwa moja hisia zilinipeleka kuamini kuwa Chenge hakuchukua fomu ya kugombea uspika kwa hiari yake. Alitumwa na chama chake kufanya hivyo. Lazima walikaa na kupanga mkakati huo.

Kila mtu mzima angeliweza kutambua kuwa kulikuwa na jambo; wakati Chenge alipokuwa akibweka katika vyombo vya habari wakati wa kutangaza nia ya kuwania uspika. Hakuwa yeye, bali ilikuwa ni nguvu iliyo ongea juu yake. Kwa kihaya nguvu hiyo inaitwa enchweke.

Kwa kuwa nia ya Chenge haikuwa kuwania uspika bali alitumika kama enchweke, ni dhahiri kuwa sasa Chenge ni mshindi na chama chake. Aliyeshindwa ni Sitta.

Sitta ataachwa hivi hivi. Lazima ataitwa na wazee na kumweleza kuwa ni mapenzi ya Mungu. Atapozwa kwa uwaziri. Na mkewe je?

Siasa, si hasa.
Ugagura wako huenda ukatimia, ila hapo kwenye red inakuwa kama unajicontradict, au labda ni hiki kiswahili cha kihaya cha Enchweke!....sisi kwetu hiyo Enchweke tunaita "amakinga".
 
Chenge na Sitta sio basi tena yaani ndio saloon kwa kwenda mbele.:israel:
CCM imependekeza majina matatu kwa nafasi ya uspika yaani Kate Makamba, Ana Abdalah na Ana Makinda,

Ina maana Chenge na Sitta ndio basi?

source : Chanel Ten
 
Hii noma, bunge halitakuwa na raha tena kama Sitta sio spika
 
Huu ndiyo wakati muafaka kwa upinzani kama watajipanga vizuri safari hii Bunge linaweza ongozwa na spika toka upinzani.Wapinzani Fanyeni tathmini ya kina na wekeni mtu ambaye ana uwezo wa kukubalika na baadhi ya wabunge wa Chama tawala kwasababu kura ni siri wanaweza vuna Spika!Wapinzani chezeni karata yenu kuna uwezekano mkubwa tu!
 
Bingwa hesabu yako nimeipenda, assume wapinzani wote wamevote kwa Marando, sasa 2tafute posibility ya kupata 120 ndani ya ccm
1 Sitta
2 Mwakyembe
3

Ukweli ni kwamba nina imani kubwa na wabunge wazalendo wachache walioko ndani ya ccm hawataikubali hali hii na ndiyo maana hii hesabu inaleta maana zaidi na zaidi sana naona kama ccm inajichimbia kaburi maalum la kudumu kama watako spika wao ambao wanadai wanataka mwanamke basi wangetoa na tangazo hilo mapena kuwa wanataka spika mwanamke na siyo mwanamke na wakina sitta wasingejiingiza huko lakini hapa naona ubabaishaji mtupu na utapeli usio na kikomo wa Demokrasia
 
Ugagura wako huenda ukatimia, ila hapo kwenye red inakuwa kama unajicontradict, au labda ni hiki kiswahili cha kihaya cha Enchweke!....sisi kwetu hiyo Enchweke tunaita "amakinga".

Samahani Paka Shume. Nilimaanisha, hataachwa hivi hivi.
 
Mwakyembe, killango, manyanya, shelukindo (beatrice), sitta, lembeli, na wabunge wanaopinga ufisadi pamoja na wale wote wenye mapenzi mema tunawaomba muwape support wapinzani ili wakamate kiti hicho muhimu cha uspika kwa maendeleo ya taifa.
 
Samahani Paka Shume. Nilimaanisha, hataachwa hivi hivi.
disregard man...usijali
Najua Enchweke ("amakinga")ikikolea mwilini, ukiunganisha na hasira wanazotupandisha hawa mafisadi, lazima mtu unapoteza kidogo! ...ha..,haaa!:doh:
 
TUNATAKA spika wa kike.
wanataka wao au taifa ndilo linataka????
 
Mwakyembe, killango, manyanya, shelukindo (beatrice), sitta, lembeli, na wabunge wanaopinga ufisadi pamoja na wale wote wenye mapenzi mema tunawaomba muwape support wapinzani ili wakamate kiti hicho muhimu cha uspika kwa maendeleo ya taifa.
 
In my opinion i think the game plan was kumuondoa SITTA sababu alikuwa tishio ndio maana wakaamua kumuweka CHENGE ili aweze kuharibu mambo kwasababu chenge alikuwa anampiga vijembe sana sitta baada ya kuchukua fomu na ukiangalia vizuri ile kambi ya ambayo chenge pia yupo ilikuwa haimtaki sitta kwasababu alikuwa anaruhusu mijadala ambayo ilikuwa ni tishio kwao, na pia katibu mkuu wa CCM Makamba naye alikuwa hamtaki sitta kutokana na mwenendo wake wa kuliendesha Bunge ndio hapo ninapokuja kusema siku zote mtu MWADILIFU huwa CCM hawampendi kwasababu huwa anawavua nguo hadharani kwa namna moja au nyingine tunaona sasa kuwa yale makundi CCM bado yanaendelea kuwepo na mpasuko utazidi kuongezeka

Kutokana na hili swala kwasababu nina imani spika naye ana kambi yake inayompa sapoti, kazi ipo kwenye upigaji kura wa kumteua spika je kambi ya Spika watampa kura nani? Ingekuwa jambo zuri kama wangempa kura zao mpinzani anayegombea Uspika lakini sidhani hilo kama litawezekana ila kwa mtazamo wa juu juu naona kuelekea 2015 CCM watakuja kujutia kwa maamuzi wanayoyafanya sasa hivi sishangai pale CCM itakapokufa mikononi mwa Kikwete.
 
WanaJF,
Mama ANNA ABDALA ndiye speaker wetu kuanzia leo.

PM anabaki MIZENGO PINDA.

Mawaziri wengi mwaka huu ni kinamama tuu, wanaume imekula kwao.

MwanaJF Dodoma.
 
Hii noma, bunge halitakuwa na raha tena kama Sitta sio spika
Wacha aende tu,kwani kipindi cha uongozi wake pamoja na kusimamia baadhi ya hoja za upinzani bila ya kubana lkn kuna nyingi alizibania na zilikuwa na manufaa kwa Taifa.Kipindi cha Uongozi tumeshuhudia akikarabati nyumba ya spika kwa mabilioni ya fedha,ofisi ya spika jimboni kwake,magari ya kifahari yenye thamani kubwa,kwa kulinda kivuli chake ili asionekane anakula sana peke yake yaani apate wafuasi amepigania posho na mishahara ya wa bunge na wake kuongezwa maradufu bila ya kujali wananchi wanahali gani,kuongeza viinua mgongo vya wabunge maradufu,kubariki muswada wa kuongeza majimbo ujadiliwe na sambamba na ongezeko la viti maalum yaani bunge lilopita limetafuna fedha za walipa kodi sana na kwa msingi huo uliojengwa chini ya usimamizi wake hata bunge la safari litaendelea kuwagharimu walipa kodi kuagharimia wabunge wengi wa viti maalum na majimbo yaliyoongezwa hali ya kuwa nchi na wananchi wake waliowengi wanazama kwenye dimbwi la umasikini .Kubania mswada wa mapendekezo ya katiba mpya na hili ni kubwa zaidi kwani angalau kwa uwezo wake angeliruhusu kujadiliwa na kuamuliwa kwa kura lkn hakutaka hata lijadiliwe kwa msingi wa kulinda nafasi yake ya kupendekezwa tena kuwania Uspika(ubinafsi)Sasa wamemtosa ni bora angeitumia nafasi yake kwa mapana zaidi na kuruhusu demokrasia itawale mijadala ya bunge kwa kufuata kanuni zaidi na si mara nyingine kuzipindisha.Kwa kifupi hakuwa na huruma na watanzania ndiyo walewale tu.Mimi naamini Hoja zikiendelea kujengwa na kuwa na viambatanishi thibitisho kutoka kwa wabunge na kufuata kanuni na sheria za bunge ktk kuziwakilisha bado zitapasua mawimbi ya ubazazi na kusimama kama hoja hata spika awe nani hawezi kuzizuia au kuzibania.
 
Back
Top Bottom