U-SPIKA: Sitta, Chenge wapigwa panga CCM!

U-SPIKA: Sitta, Chenge wapigwa panga CCM!

WanaJF,
Mama ANNA ABDALA ndiye speaker wetu kuanzia leo.

PM anabaki MIZENGO PINDA.

Mawaziri wengi mwaka huu ni kinamama tuu, wanaume imekula kwao.

MwanaJF Dodoma.

Hiyo inaitwa comeback ya kipekee kwa mzee Msekwa, manake mke wake akiwa spika, is as good as yeye ndiye spika. Mzee yule bifu lake haliishi, toka Six amtoe kwenye ugali wake amekuwa na bifu naye si mchezo, loh this peole can kill kwa ajili ya madaraka. Naona aliona opportunity akamtonya mkewe achukue fomu, kweli viongozi hawa uchwara wa bongo ni tishio kwa mustakabali wa taifa letu. I am so suprised Six hakuona siasa za maji taka zikija, amekaa hadi zikamzoa na kumtupa kwenye dimbwi la mavi, sasa ananuka na aibu imempaa. Six, you should learn kusoma alama za nyakati. Hata ukipewa uwaziri, huna jina kama ulilokuwa nalo la uspika, ni kuwa umetupwa pwaaa, loh, labda uwe PM, which i rearely doubt it

Ulisema Mrema kafulia, that is politics, leo uko juu kesho uko chini unavaa raba kama mrema, nadhani na wewe unaelekea kufulia
 
Succession battle ya 2015 imeanza vibaya kwa CCM maana kila mpiga kura mwenye upeo japo mdogo atajua CCM inataka viongozi wa aina gani. Kujaribu kuiziba mdomo kambi ya upinzani kwa kumtosa Sitta hakutasaidia. Wapiga kura tutawahukuma tena 2015.
 
Sijamuelewa makamba anataka mh. spika mwanamke ili iweje sasa
anataka kutekeleza nini tena kwa huyo mwanamke mwenye ufahamu
zaidi naomba atueleze hapa
 
Inasemekana Kuwa Muheshimiwa Samwel Sitta alikuwa anatetea Kwenye ukweli hata kama ukweli huo unakighalimu chama,, na hii imedhihilika katika Bunge lililo pita pale kwenye Interest nyingi za Nchi Speakre Sitta alikuwa anaelekezea Interest hizo Pahala husika, kitu ambacho kimekighalimu chama kiasi cha Majibu yake tume yaona Term hii..
Sasa kilichotokea sasa ni kumuondoa hata kwenye kinyang'anyiro hicho ili Jina lake lisije kutoka kwenye kura za Bungeni ambazo Wabunge pinzani walijiandaa kumpigia Muaminifu kwa taifa Muheshimiwa Samwel Sita...

Kuhusu chenge tunajua Fika yeye ndiye aliye sign Katiba yetu Yenye matatizo lukuki, na ndiye aliyekuwa na kashifa nyingi sana ambazo alilighalimu Taifa kwa uzembe wake na kujisahau kwake katika Uongozi,, sasa anataka kukiongoza chombo Nyeti kama Bunge ili kujitahidi kuficha mauchafu yake aliyo yafanya Ui9ngereza inasema Tuhuma Za Rada hazijaisha kwahiyo si muda muhafaka kuanza kumsafisha Bwana Chenge..

Kwasababu hiyoBasi wameamua Kuwatoa wote wawili huku ikisemekana kuwa Chenge na Muheshimiwa Sitta ni mahasimu wa sikunyingi kwasababu Sitta akiwa speakrer aliwahikutoa maamuzi yaliyo mghalim Chenge kipindi cha Bunge lililopuita,,

So kwamimi naweza kusema kisasi pia kimekingwa...
 
Hii ni Mungu ameleta, njia ipo wazi kwa upinzani kuchukua kiti cha spika. Ni kuomba wabunge wote wenye mapenzi mema na nchi hii wanaomwogopa Mungu na wanaotaka maendeleo ya kweli kuungana bila kujali itikadi zao na kuhakikisha spika wa upinzani anapita Chonde chonde tuangalie majaliwa ya kizazi kinachokuja. By the way upinzani umemchagua nani?
 
Tumeona CCM wakibebana katika ngazi za uraisi, kwa maana kuwa mtu akiingia lazima amalize vipindi vyake viwili (labda adondoshwe na upinzani). Wao wamesema kuwa ni 'utamaduni' wa chama.

Katika uspika, utamaduni huu umekuwa mkubwa zaidi kwani kwa maspika wawili wa mwanzo (Mkwawa na Msekwa), wote waliachwa hadi kustaafu (ingawa msekwa alitaka kufuta azma yake ya kustaafu, hadi akastaafishwa na wabunge kwa kura). Lakini kwa Sitta hali ni ya kushangaza kwani ameongoza bunge kwa kipindi kimoja tu, gafla CCM wanakuja na 'idea' ya bunge (mhimili mmoja wa dola), uongozwe na mwanamke.

Hivi kama ni suala la mhimili kuongozwa na mwanamke, mbona uraisi ndio ungekuwa mzuri? Au basi mahakama.. ingeshindikana nini raisi kuteua mwanamke, tena tukijua kuwa jaji mkuu aliyepo sasa amebakiza mda mfupi tu astaafu?

Lengo ni mhimili kuongozwa na mwanamke, au lengo ni matakwa ya uraisi kubaki mikononi mwa 'watu fulani' hapo 2015?
 
Chenge alijiuzulu kutokana na habari zilizoandikwa na vyombo vya habari kuhusiana na ununuzi wa radar, Bunge halikuhusika kwa Chenge kujiuzuli.
 
SERIKALI ya Uingereza imetoa tamko kuhusu taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) ya kumsafisha aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, ikieleza kuwa kwa sasa si sahihi kufanyia hitimisho suala lolote linalomhusu mtu aliyehojiwa kuhusika na sakata la rada.

Taarifa hiyo imesema suala la kufungwa mjadala wa shauri hilo litajulikana mara Mahakama ya Uingereza itakapolifunga na si mtu ye yote, kwa kuwa mpaka sasa halijafikishwa katika mahakama hiyo.

Sehemu ya taarifa hiyo ilieleza: "Kwa hatua ya sasa kesi inayoihusisha BAE na kile
ilichokifanya na Tanzania bado haijafika mahakamani nchini Uingereza.

Hivyo si sawa kufanya au kufikia hitimisho iwe ni kwa ye yote aliyehojiwa kuhusika katika shauri hilo kwa namna yoyote."
Source: Habali Leo
 
Mwakyembe, killango, manyanya, shelukindo (beatrice), sitta, lembeli, na wabunge wanaopinga ufisadi pamoja na wale wote wenye mapenzi mema tunawaomba muwape support wapinzani ili wakamate kiti hicho muhimu cha uspika kwa maendeleo ya taifa.
tuwatafute wahesabuji kura tuwashawishi na si wapiga kura kwani anayeleta ushindi ni muhesabukura na si mpigakura
 
Siku ya kufa nyani matawi yote huteleza. sisiem ikaribia kifo chake na hakuna wa kukizuia
 
Chenge alijiuzulu kutokana na habari zilizoandikwa na vyombo vya habari kuhusiana na ununuzi wa radar, Bunge halikuhusika kwa Chenge kujiuzuli.

haupo siriasi unaposema bunge halikuhusika na kujiuzuru kwa chenge! Mi ninavyojua kashfa kuhusu manunuzi ya rada yalitolewa bungeni na mh. mzalendo Dr Slaa. Sasa unaposema bunge halihusiki sijakuelewa.:nono::nono:
 
Nahisi Chenge hakunuia kuupata Uspika, bali ilikua kuzuga, ili Sitta atakapomwagwa attention iwe kwingine. Na kauli kwamba ni wakati sasa kiongozi wa mhimili mmoja (Bunge - na Uspika) awe mwanamke - nahisi kuna kitu kinapandikizwa, ambacho wanaona wakiweka mwanamke itakua ngumu kwetu kutanabahi... NAHISI, Sijui na wewe?
 
Inawezekana ni nafasi nzuri kwa upinzani lakini itategemea na nani atasimamishwa>
Sina uhakika sana na Mabere Marando kama anauzika.
 
HIVI JANA MLIONA MATANGAZO YA MAPENDEKEZO YA CCM KWENYE USPIKA.MAKAMBA ALIVYO SEMA KUNA WATU WATATU YEYE AKAONYESHA VIDOLE VI NNE.....mzee kashachoka inabidi astafu tu
 
SPIKA wa Bunge, Samwel Sitta ameshikiwa bango na wapinzani wake wa kisiasa wakishinikiza afukuzwe katika chama kutokana na msimamo wake wa "kujenga Bunge lenye kasi viwango."
Taarifa kutoka ndani ya vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mijini Dodoma, zinasema baadhi ya wajumbe walishinikiza Sitta aachie ngazi kwa madai kwamba amekuwa akitumia Bunge kama silaha ya kupambana na wenzake katika chama na serikali.
Kikubwa ambacho kimemjengea Sitta maandui ni ujasiri wake katika kusimamia suala la kashfa ya Richmond. Kingine kinachohusishwa ni maamuzi yake kuhusu Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba katika malalamiko yake dhidi ya mbunge wa CHADEMA, Halima Mdee.
Hata hivyo, ukichunguza kwa makini mwenendo wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, haraka utabaini kuwa Sitta ndiye mtetezi mkuu wa serikali. Anaweza kunyongwa na wana-CCM kwa kuwa siyo wepesi wa kung'amua.
Spika hauyuko bungeni peke yake. Pamoja na kuwepo wabunge wengi wa CCM ambacho ni chama chake, kuna Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Kikao cha Bunge cha CCM na kamati za kisekta.
Source: Manahalisi

hay ni mambo ya msingi ya kuyaangalia, Na CCM wamemtooa kwasababu hiyo Mh. Sitta lakini sisi tulikuwa tuna muhitaji bado
 
Anna Abdallah tena jamani? Hivi hakuna wanawake wengine wenye uwezo CCM? Mumewe si alishakuwa spika bado familia haijatosheka?Betri ikiisha nguvu hata uianike juani haitodumu kwa kweli...dawa ni kununua nyingine tu
 
Sasa sisi wanaccm tunataka katibu mkuu wa chama chetu awe mwanamke, pia tunataka waziri mkuu awe mwanamke.
 
CCM contains its own seeds of destruction, haya ni maandalizi ya mazishi ya CCM, Jeneza na mwili viko tayari
 
Back
Top Bottom