Mfamaji
JF-Expert Member
- Nov 6, 2007
- 6,631
- 1,926
MF,
Sidhani kama huyo jamaa anaweza kusema hayo mambo ukikutanana nae uso kwa uso.
Unajua nina nadharia moja kwamba kitu chochote kile unpopular kinachosemwa kwenye anonymous forum kama hii kina faida yake fulani -hata uendawazimu.
Kwanza, inasadia kuleta upande mwingine wa shilingi uwe considered, ambao unaweza kuwa mzuri lakini ukiusema hadharani utapigwa mawe kama walivyotaka kumfanyia Galileo Galilei.
Na kama huo upande mwingine wa shilingi ni utumbo kabisa kabisa, bado inasaidia kujua watu wanafikiri nini. Kwa mfano, kuna wakati ukisoma posti fulani fulani hapa unaona hisia hisia za kikabila kabila na kidini dini, ambazo watu wasingeweza kuzisema hadharani. Inasaidia kujua Watanzania wenzako wanafikiri nini kisiri siri - hata vioja.
Sasa huo hapo juu - bunge lisiwe transparent - ni moja kituko ambacho sijawahi kukisikia maishani. Kusema machache!
Na huyo aliyeamuru TV zisionyeshe ni mwenda wazimu zaidi maana kisiri siri anafikiri WTz bado ni makenge kama enzi zao