Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,551
Wanabodi,



Mimi mwanahabari wako, Paskali Mayalla, leo asubuhi, kama kawaida ya kila Jumamosi asubuhi, huwa nashiriki kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa live na Star TV kutokea Mwanza, kikiongozwa na Nguli Dotto Emmanuel Bulendu na huku Dar huwa niko mimi tukikuchambulia kilicho tawala vyombo vya habari kwa wiki nzima.

Kwa wiki ya 3 mfululizo, tangu Bunge la Bajeti limeanza, ikitarajiwa media itatawaliwa na habari za Bunge, habari za maambukizi ya ugonjwa wa Corona yameendelea kutawala vichwa vya habari vya TV, Redio, Magazeti na mitandao ya kijamii.

Katika kuangazia wajibu wa vyombo vya habari kwenye janga la maambukizi ya ugonjwa wa Corona tutajidili, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?.

Andamana nami katika mjadala huu elimishi.

1. Hatua ya Kwanza ni kukuelimisha media ni nini na kazi za media.
Media ni vyombo vya habari vinavyotumika katika upashanaji habari. Vyombo hivi vimegawanyika katika makundi makuu mawili, ambazo ni
1. Traditional Formal Mass Media, vyombo rasmi vya habari ambavyo ni Redio, TV na Magazeti, na uhabarishaji hufanywa na waandishi wa habari waliosomea yaani professionals.
2. Kufuatia maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia na utandawazi, kumeibuka modern media ambazo ni online media, na social media zikiwemo Blogs, Online Forums, Facebook, Instagram, Twitter, YouTube, WhatsApp groups etc, ambapo every Tom, Dick and Harry ni mwandishi wa habari, hii inaitwa citizens journalism.

2. Kazi za Media
Traditional media ilikuwa na kazi kuu tatu
1. Kuhabarisha Jamii
2. Kuelimisha Jamii
3. Kuburudisha Jamii
Kwa modern Media zimeongezeka
4. Watchdogs of the society, Ku act as 4th Estate

1.Jukumu la 1 la Uhabarishaji.
Kwenye jukumu kuu la kwanza la media kwenye uhabarishaji, Media imetimiza jukumu lake kikamilifu na nimepongeza hatua ya serikali kuweka list ya wazungumzaji rasmi 5 wa Corona kitaifa ambao ni
  1. Rais wa JMT
  2. M/Rais
  3. Waziri Mkuu
  4. Waziri wa Afya
  5. Msemaji Mkuu wa serikali.
Nikasema hatua hii ni mzuri ili taifa lipate taarifa moja iliyonyooka, kama kila mtu ataachwa ajisemee itakuwa chaos, utaratibu huu unaitwa restrictive media reporting na hutumika hata wakati wa vita.
  1. Information is a two way traffic, serikali inatoa tuu taarifa, media ilikuwa ina wajibu wa kufikisha taarifa za serikali kwa umma, lakini hakuna utaratibu wowote wa serikali kupokea mrejesho hao wananchi wanaopelekewa taarifa na maelekezo ya serikali jee wanasemaje?. Wanatekeleza?, Wananawa kwa maji tiririka?. Wanafanya social distancing?. Kwenye eneo hili, media hatujatimiza wajibu wetu kikamilifu.
  2. Kazi ya hao wazungumzaji wanne ni kutoa update ya Corona. Kwenye eneo hili la media kutoa taarifa za serikali za Corona, media tumetimiza wajibu wetu kikamilifu kabisa na tunastahili pongezi za dhati.
  3. Lakini ukweli Corona ni zaidi ya updates, kila vizara, kila idara, kila Taasisi itakuwa affected na Corona hivyo mawaziri wengine na wakuu wengine wote wana wajibu wa kuizungumzia Corona haswa how to mitigate the after effects, huko sio kutoa update huko ni kuisaidia serikali na Watanzania jinsi ya kukabiliana na madhara ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Corona. Kwenye eneo hili la kutoa taarifa nyingine zozote kuhusu madhara ya Corona kwa sekta nyingine zote. Hivyo katika eneo hili linalotwa mitigating the corona virus after effects, serikali yetu ni myopic!, haioni mbali!, mwisho wa uoni wa serikali yetu katika hili janga la corona, ni kwenye just the short term effects, kuzuia isisambae, na ku deal na ugonjwa na wagonjwa only, lakini hakuna popote mid terms madhara ya corona yanazungumza, na madhara makubwa kabisa ya corona ni long term effects ambazo hazizungumzwi kabisa, but they start to bite, hata sisi media ambao hatujatimiza kabisa wajibu wetu kikamilifu, tunajifanya ni mabubu, lakini long time effects za corona, zitakapoanza kututandika kwa ku destabilize uchumi wa nchi, na sisi media tutakuwa severely and serious hit kwa watu kukosa kazi na media kufungwa, muda huo ukifika, ndio kuna watu watajifanya kushangaa as if, hawakujua!.
  4. Watoa taarifa wa serikali wanaisoma taarifa ya maandishi na kuwasomea media hakuna any room kwa media yoyote kuuliza kupata ufafanuzi, matokeo yake media kazi yake ni kulishwa tuu habari, spoon fed, na media kazi yake ni kumeza tuu hizo, habari, hukuna kuzichakata, hakuna news analysis, hakuna news relevance alimradi Msemaji ni serikali na serikali imesema.
2. Jukumu la Pili la Uelimishaji Jamii
Hili pia media imejitahidi ila bado, Watanzania wanahabarishwa vizuri kuhusu Corona lakini kazi ya uelimishaji bado inafanywa kwa kiwango cha chini, hivyo kuna watu wananawa kwa maji tiririka kwasababu ni lazima, lakini kwenye social distancing bado, misongamano bado ipo kila mahali.
Zaidi ya kuripoti zile updates za Corona, hakuna TV yoyote, redio yoyote, au magazeti yenye dedicated Program kuhusu uelimishaji umma wa Corona zaidi ya yale matangazo ya Corona.
Hivyo kwenye jukumu la media za Tanzania katika uelimishaji umma kuhusu Corona bado sana.

Kwa vile Corona haina dawa, Watanzania walipaswa waelimishwe hao wagonjwa huko kwenye vituo walikotengwa wanafanywa nini hadi wengine wanapona kabisa na kuruhusiwa ili wenye uwezo wawatibie watu watu kwa kuzua na sio kusubiri watu waugue wazidiwe wakarudikane kusubiria... wakati watu wangeelimishwa huduma ya kwanza ingeanzia nyumbani.

There's a lot of education inputs kutoka nje kuliko kutoka ndani. Serikali imetoa list ya wataalamu official watakao elimisha kuhusu Corona, sijabahatika kuona hata kipindi kimoja cha wataalamu hao!.

Vituo vya Redio na TV vitenge dedicated Program za uelimishaji umma kuhusu Corona. Hao wataalamu wawe pro active kwenda kwenye media kuelimisha umma na sio kuwa reactive kusubiria majanga yatokee na ndipo wao wajitokeze kufafanua madhara ya majanga, wana kuna fursa ya kuzuia majanga kwa uelemishaji umma!.

The regulator, TCRA, atoe muongozo kwa vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii kuandaa vipindi elimishi kuhusu Corona

Wakati Wazungu wamehangaika kutafuta tiba, sisi tungewatumia wataalamu wetu wote kuanzia madaktari, tiba mbadaka, tiba asili, ma sangoma, waganga hadi Babu wa Samunge kukijaribishia kikombe.

Hao wachungaji wenye uwezo wa nguvu za uponyaji, waruhusiwe mahospitalini ili tushuhudie uwezo wa nguvu zao na sio kuwakamua masikini Watanzania kwa kusingizio cha kufanya miujiza, Wachungaji wenye uwezo wa kuponya kwa miujiza wajitokeze kuonyesha uwezo wao na serikali iwaruhusu, kama alivyojitokeza Askofu Gwajima, aruhusiwe tuone uwezo wake na miujiza ya Mungu katika uponyaji.

Unapo deal na gonjwa ambalo halina tiba na kuna wagonjwa wamezidiwa mahututi na hatimaye watakufa tuu, what is wrong to turn them into Guinea pigs and test them, we may save them, hata kama kwa kuwajaribishia hizo tiba mbadala na bado wakafa, let it be, at least tumejaribu, hata tusinge jaribu, they were going to die tuu anyway. Let's try to do anything something kuliko doing nothing.

3. Jukumu la 3 la Media ya Tanzania Kubudisha Jamii
Kazi ya tatu ya media ni kuburudisha jamii. Kwenye eneo hili pia media ya Tanzania haijatimiza wajibu wake kikamilifu.
Kwa vile Corona ni janga, na kufuatia kilichotokea Wuhan, Italy, UK na US, Corona imetisha na kuogofya, media nazo zikalipokea hivyo hivyo. Shujaa wa eneo hili ni rais Magufuli aliposema tusitishane, ka Corona ni ka ugonjwa kadogo tuu, tena sio kirusi ni shetani disguise as kirusi, tukamkabidhi kwa Mungu kiboko ya shetani!.
Pamoja na mabalaa yote ya janga la Corona, pia kuna mazuri ya Corona, kuna positives za Corona zilipaswa kuangaliwa. Mwana FA na meneja wa Diamond, Salaa did. Kuna watu wanapona wanaruhusiwa. Media ilipaswa kuwatafuta madaktari waliofanya miujiza tufanye human interest stories za mazuri ya Corona. Kuna watu wamepiga pesa kwa kuziangazia fursa za Corona, hata Diamond alichofanya akiwa quarantine ni jambo zuri, tusiizungumze Corona kwa ubaya tuu, tuizungumze kwa wema. Italy Wazee ni wengi mno na wanaishi sana, hivyo Corona ni kama mkombozi fulani kwa blessing in disguise kwa mifuko ya hifadhi za jamii kwa..., ame fykelea...

Sisi baadhi ya familia, baba na mama ni working class, familia yangu nina watoto 9, wamepishana miaka 2, the oldest ni 24, 22, 20, hawa wako vyuo. Then kuna 18, 16 na 14 wako sekondari, kisha kuna 12, 10 na 8 wako primary. Ukiondoa Christmas Day, there is no any other time watoto wote wako nyumbani. Kwenye Corona wote wamerudi home, baba ni mwandishi wa habari wa mikutano, warsha, seminar, makongamano na events, zimesimamishwa, niko home. Wife ni mfanyabiashara wa safari za nje, zimesimamishwa!, nyumbani kuna Dada wa jikoni, dada wa usafi, kaka wa garden, feeding a family of 15 is not a joke. Ukishinda nyumbani na watoto ndipo unagundua kiukweli hawa wadada wa kazi, walipaswa kulipwa vizuri!.

Hivyo Corona has lots and lots of human interest stories na sio habari tuu za ku stigimize kwa idadi inaongezeka, lakini wanaopona hatuwazungumzii. Kutembelea kambi za quarantine na ku file stories about life in quarantine zitakuwa very interesting stories.

4. Jukumu la 4 la media ya Tanzania as a Watchdogs of the Society kwe janga la Corona
Kazi ya Watchdogs ni wale mbwa wanaofanya kazi ya ulinzi, kazi yao ni kubweka tuu ili kumjulisha mwenye nyumba something is not right.

Hawa mbwa pia wapo mbwa wa aina 3,
1. Sheppards Dogs habweki ana ng'ata.
2. Barking Dogs kazi yake ni kubweka tuu ila hang'ati!
3. Lap Dogs kazi yake ni kuchezesha mkia na kukamba lamba, habweki wala hang'ati!.

Kwenye janga hili la Corona, the Tanzania media has failed this nation katika role ya Watchdogs.
Toka Corona inaanza kule Wuhan ije December 2019 tungekuwa na serious media, tungeanza kubweka ili kuiandaa serikali yetu for preparedness kwa Corona, angalieni China ilipolipuka tuu Wuhan, mpaka imedhibitiwa haikufika Beijing na wala haikuingia Japan.

Tanzania ndio nyumba yetu, baba mwenye nyumba ni rais wetu na serikali yake, wao wako ndani wamelala, sisi media ndio mbwa ambao tuko macho tunalinda nyumba. Corona ndio mwizi anayekuja kutuibia nyumbani kwetu.

Media ya Tanzania ingekuwa ni Sheppard dog, ingefanya kazi kama gazeti la The Washington Post wakati wa kashfa ya Watergate, naomba tukiri udhaifu kwenye complex issue kama hii ya Corona, media zote za Tanzania hakuna hata moja yenye uwezo kuajiri ma medical journalist wa kuandika story za kina kuhusu Corona ambazo zingeisaidia serikali yetu. Angalieni CNN na Dr. Sunjay Gupta.
Hivyo media ya Tanzania kwenye kuisaidia serikali kwenye hili la Corona ni zero. Naamini kuna madaktari wazuri tuu ambao wanaopenda kuwa watu wa media kama alivyo Dr. Maro kwa Clouds.

Tukija yule mbwa wa pili wa barking Dogs, kiukweli mainstream media pia has failed this nation on this role. Kazi hapa ni kubweka tuu ili kumuamsha mwenye nyumba.

Media ambayo imelitenda hili ni JF pekee.
Pale rais wa nchi anaposema ka Corona ni ka ugonjwa kadogo tuu na serious media ambayo ni barking Dogs zilipaswa zibwekwe.

Rais Magufuli na serikali yake walipaswa wasaidiwe na media kwa kuwaonyesha good practices elsewhere ambazo zimesaidia.

Rais Magufuli aliporuhusu mikusanyiko ya nyumba za ibada, serious media ilipaswa i bweke kwa kuonyesha kama Roma wenyewe kwenye Ukatoliki wamefunga makanisa, Saudi Arabia wenye Uislamu wamefunga misikiti who are we?. Media tulipaswa kuwaumbua viongozi wa dini wanaohemea sadaka hata kwa kuhatarisha maisha ya watu!.

Hapa Tanzania tulipaswa kuwa na strong independent media yenye uwezo wa kumweleza rais Magufuli na serikali yake kuwa baadhi ya hatua anazosita kuchukua ikiwemo kuendelea kuruhusu mikusanyiko ya nyumba za ibada is wrong. Media ionyeshe jinsi Mungu alivyo Omnipresent yuko popote na mikusanyiko ya nyumba za ibada sio miongoni mwa mikusanyiko muhimu. Kwenye hili angalau sisi jf tulisema.

Kwenye hili media ya Tanzania ni just lap Dogs!. Kazi ya mainstream media zetu haswa za electronics ni kuchezesha tuu mkia na kulamba lamba kila kinachofanywa na serikali, hakuna analysis, hakuna critics na mwendo wa kusifu tuu na kupiga makofi.

Mimi kwenye Programs yangu hii ya Jicho Letu, angalau tumemuita Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile, maswali yalikuwa mengi muda ulikuwa mfupi ila naomba kukiri udhaifu hata mimi pia ni Lap dog tuu, kwasababu the right to information act inataka tuwaandikie maswali tuwape rasmi lazima maswali yote yangejibiwa.

Hata hivyo bado nina mshukuru Dr. Abbas for being available twice at my disposal tukashindwa sisi. Kwa upande wa Dr. Ndugulile kiukweli nilimbwekea ila naye yuko fit sana kukwepa mishale. Hata yeye namshukuru na ni mwana jf mwenzetu ila...

Kitendo cha media ya Tanzania kukubali kuwa lapdog hivyo kushindwa kuitumia position yetu as Mhimili, the 4th Estate or The 4th protocol to mitigate short time, midium term na long term effects za corona, sio tuu kutapelekea media kudhaurika, kama the Washington Post limewahi kumchoropoa rais fulani Ikulu, media ya Tanzania ingeonyesha uwezo huo kwa kuisaidia serikali kuiambia mipango yake haitekelezeki na kuonyesha matokeo ya serikali kutokusikiliza ni nini, halafu serikali kweli ikadharau na sasa tunaelekea kwenye hicho media ilichokisema. Kikitokea cha kutokea, ambacho kama serikali ingeshauriwa na kusikiliza, tusinge fika huku tunakokwenda kifika, serikali kama hii ingekuja kuwarudia wananchi na kuwaeleza nini?.

Kwa sasa ninapoandika hapa, kwa sababu corona ndio kwanza iko kwenye mlipuko, madhara halisi ya corona, hayataonekana sasa au leo, bali yanakuja huko mbele kwa uchumi kuporomoka, biashara kufungwa kwa kushindwa kujiendesha, na watu kupunguzwa kazi kwa makampuni kushindwa kulipa mishahara!. Muda huu ukifika, ndipo mtaishangaa media ikianza kufungua bakuli lake na kuanza kulia kuwa inaumia!.

Media has failed this nation!. Hatukutimiza wajibu wetu kikamilifu and when that time comes, we'll pay our consequences by paying the price kwa kutokutimiza wajibu kwetu.

Asanteni

Paskali
 
The media has been muzzled by the myopic government, how then can the same media be efficient?. If you are not permitted to report who is suffering from or died of covid 19, then you are only remaining with one task of singing the government's favourite songs. The media is not free, therefore we shouldn't blame it.
 
Kama mpo live kwahiyo tufanyeje sie? Endeleeni kujifanya mnachambua kumbe mnajikita kusifia mfalme juha kwa maombi.Waandishi wa Tanzania mmejaa ubahaluli tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usiweke mwamvuli wa fikra zako wa watu wote!

Jisemee kwa nafsi yako! Sema UFANYAJE sio useme TUFANYAJE!

Mleta mada hajakulazimisha kuangalia hicho kipindi!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hili swali halikuulizwa jana, pia kwenye media tofauti ?, na Kesho pia tutauliza hiki hiki kwenye media nyingine ?

Je hamjapata jibu tu kwamba mnafanya kazi au hamfanyi, ili muanze kufanyia kazi mnayoambiwa au bado mnatafuta data ?

Kwa sasa mnachofanya ni kureport kile wizara inachosema hamuendi deeply wengine wanasema nini au hata ku-challenge au kuongeza au kupunguza kinachosemwa..., nadhani kama hamna uhuru basi sio vibaya endeleeni kutuburudisha kwa kutupa burudani huku mkisubiri taarifa ikitoka ili mtuhabarishe....
 
...hii tabia ya kuanza hiki kipindi nilifikiri itakuwa imeisha nilivyosikia Dotto na Mayalla mtakuwa mnakiendesha ila kumbe nilikuwa najidanfanya...Leo kimeanza SAA 2 juu ya alama wakati ratiba inasema kitaanza SAA 1:30 asubuhi....tabia ya hovyo sana hii
...inaonyesha kutojioganaizi kwa wahusika-..lifanyieni kazi hilo kwanza.
...otherwise-tuna imani kubwa na Dotto na Pasko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mayalla

Naomba ukirekodi kipindi chote halafu ukiweke kwenye Youtube chaneli yako ili nikiangalie baadaye.

Natanguliza shukrani zangu!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wanabodi,



Tuko Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Bado Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?.

Karibu

Paskali

Haitimizi waandishi wa media zote wanashindwa kuuliza je hadi sasa tumeshapima watu wangapi? Na je kati ya hawa wagonjwa waliothibitika wanatokea maeneo gani specific mana ukisema Dsm au mwanza ni kubwa sana tufanye kama Zanzibar wanavyotoa detailed report hivyo media utekeleze majukumu yake kusaidia jamii
 
Wanabodi,



Tuko Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Bado Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?.

Karibu

Paskali


Nimependa hapo uliposema utatoa ushauri jinsi ya kuiboresha Star TV. Ila hiyo TBC unayoisifia ni kama unalazimisha kutakatisha Kaniki.

Hilo la katiba Magufuli halitaki maana sio mtu anayetii katiba, na wala hana uwezo wowote wa kuileta maana haimlipi.
 
Nimependa hapo uliposema utatoa ushauri jinsi ya kuiboresha Star TV. Ila hiyo TBC unayoisifia ni kama unalazimisha kutakatisha Kaniki.

Hilo la katiba Magufuli halitaki maana sio mtu anayetii katiba, na wala hana uwezo wowote wa kuileta maana haimlipi.
Alafu umealikwa na star tv,hao TBC unaitangaza kwenye Tv nyingine ili iweje,hata kama unatafuta uteuzi ,umepitiliza,kwani wateule wote huwa wanalamba viatu vya wakubwa ndipo wanapata nafasi?
 
Masuala nyeti kama haya yalikuwa yakitokea panakuwepo na waandishi wa habari wenye upeo wa ziada, wanaenda mbali zaidi kufanya uchunguzi wao, wajue idadi ya walioambukizwa, waliopona, na vifo vipo vingapi, hii ingesaidia kuuaminisha umma kama mapambano yanayoendelea yanafanikiwa au hapana.

Matokeo yake utawala huu umewafunga midomo wote hao, mnataka wote wafanye kazi moja ya kusifia tu, ndio maana jana Waziri wa Afya akasema sasa ataanza kuripoti ukweli, kumbe hiyo kazi ilitakiwa iwe inafanywa na waandishi wanaojielewa, wamewafunga midomo, wakatulisha habari za uongo mpaka wamechoka wenyewe.

Sasa unaposema kama media inatimiza wajibu wake naona hiyo media imelazimishwa kutimiza huo wajibu kwa upande mmoja tu, ule wa kusifia, vinginevyo wakae kimya kama wana maoni tofauti, huu ndio unaoitwa "uzalendo wetu" wa siku hizi.

Wengi wameamua kuchagua njia ya pili kukaa kimya, kwasababu kwa wengine ni sawa na kuwatusi kuwalazimisha wafikirie kwa upeo mdogo kwenye jambo wanaloona wanaweza kwenda mbali zaidi, ila wanaogopa kuwakasirisha watawala kwa mawazo na maoni yao watakayotoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,



Tuko Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Bado Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?.

Karibu

Paskali

Hili ndiyo zao la kukataza ama kuwaadhibu waandishi wa habari wanao andika habari za kiuchunguzi na zinginezo kwa kuwabambikizia kesi za uhujumu uchumi. Swali fikirishi je hawa waandishi wa habari hawana kumbukumbu? kwa matukio km haya 'most of them are demoralized already'
 
Nilichoambulia cha maana:
Pascal: nyumba za ibada zifungwe kama ni sadaka iwekwe namba ya Mpesa kila nyumba ya ibada waumini wasali nyumbani kwao.

Gwangwai: kwa kuwa habari za kiuchunguzi juu ya covid zinahatarisha maisha, basi habari picha juu ya yanayoendelea kwenye jamii inaweza kuifikirisha Serikal mf.mbanano, kutovaa barakoa, UVCCM kuzifanya wanatoa elimu wakati wao hawajajikinga, watoto kuwatoroka wazazi na kujikusanya mtaani n.k
 
Back
Top Bottom