Jamani Someni historia vizuri. Waafrika wenyewe walijihusisha na biashara ya utumwa kwa kuwakamata wenzao na kuwauza. Wakina Mirambo na wengineo ndio walikua wahusika wakuu kuliko waarabu.
Hakuna ushahidi unaoonesha kuwa waarabu walivamia vijiji na kuwakamata watu kwa nguvu. Ni waafrika wenyewe ndio walifanya kazi hiyo. Kwa hiyo madai yaanze kwa waafrika wenyewe.
Waarabu walifika Tanzania au Afrika mashariki kabla ya wabantu na walileta maendeleo ya kwanza hapa , watu kutumia kalamu na karatasi na watu kujifundisha kuandika na kusoma kwa maandishi ya kiarabu , biashara baina ya makabila , Kufungua biashara na nchi mbali mbali , Kuifungua Afrika kwa walimwengu wa magharibi, Umeme ,Tram ( treni ndogo ya mjini ), maji ya mifereji, posta, telegraph - zanzibar chini ya waarabu ilikua ni katika nchi za kwanza za Afrika kufanya hivi vitu - hayo ni maendeleo.
Waarabu walishikiana na waafrika kupambana na ukoloni katili wa kijerumani na katika vita ya majimaji. Baadhi ya waarabu wanatambulika kuwa ni mashujaa wa taifa - kama Bushiri.
Yaliopita si ndwele tugange yaliyopo na yajayo