Tutalalamika mpaka lini?

Tutalalamika mpaka lini?

Au we mwenzetu mtt wa mkubwa
Au unaishi abroad?😃
Mada km hizi kuandika sio mchezo
Imebidi nicheke 😁
Nikujibu sasa 👇
1 Hapana mimi sio mtoto wa mkubwa

2 naishi Tanzania Dar es Salaam

3 Mada kama hizi wataandika kina nani?

NB : Mada yangu ni ya kujadili na watanzania wenzangu haina uchochezi wa aina yoyote

Sisi kama Watanzania kujadili mstakabali wa taifa imekua jinai?
 
Maandamano hapo tanzania yataleta vifo wanao shkilia madaraka wamesha lewa.

Wataishia kuua raia kama 2025 .

Huyo mama na serikali yake hawana huruma hata chembe.
 
Morning wana JF

Watanzania tumekuwa tukilalamika kila siku kuhusu uongozi na mambo mbalimbali ambayo hatupendezwi nayo

1. Tumeongea sana tukiomba maboresho ya Katiba

2. Tumezungumza sana kuhusu kupitiwa upya kwa suala la Muungano

3. Tumezungumza kuhusu Mahakama na utendaji kazi wake

(Mpaka sasa tunaona mwenendo wa kesi ya mwenyekiti wa chadema TL inavyoenda huku watu wakiwa na mashaka makubwa )

Na mengine mengi sana

Lakini mpaka sasa hakuna matokeo chanya ya kutosha, licha ya kwamba tulipo leo sio tulipokuwa jana
Kuna mambo yamebadilika, lakini bado kuna mengi ambayo tumekuwa tukiyazungumza kwa miaka mingi bila kuona mabadiliko tunayoyatarajia

Tumeona nchi kadhaa zikifanya jitihada za pamoja
Wananchi wameungana, wameandamana na kudai mabadiliko na katika baadhi ya nchi hata jeshi liliishia kuingilia kati baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi

Hii mifano nimeweka hapa nimesoma huko mitandanoni
👇
Mfano, Philippines mwaka 1986, wananchi waliungana katika maandamano makubwa ya amani yaliyokuja kujulikana kama People Power Revolution, na hatimaye utawala wa Ferdinand Marcos ukaondoka

Tunisia mwaka 2011, wananchi waliingia barabarani kudai mabadiliko na maandamano yakawa makubwa kiasi cha kumfanya Rais Zine El Abidine Ben Ali kuondoka madarakani

Sudan mwaka 2019, wananchi waliandamana kwa miezi kadhaa wakidai mabadiliko, mpaka hatimaye Omar al-Bashir akaondolewa madarakani baada ya miaka takribani 30 ya utawala

Hapa kwetu tulijaribu pia
Kupaza sauti zetu tukiwa na madai mbali mbali

Lakini wote tunajua nini kilitokea October 29 💔

Na wote tunajua mtu anayekwenda kinyume na watawala au anayesema mambo fulani hadharani, mara nyingi kinachoweza kumpata

Ukiongea hadharani unatulizwa

Sasa tutaongea chumbani?

Kama hatuwezi kuongea hadharani, kama hatuwezi kuuliza maswali, kama hatuwezi kukosoa na kudai mabadiliko bila kuogopa, basi tutaikomboaje hii nchi?

Na ninaposema kuikomboa, simaanishi kwamba twende kwenye vurugu au kumwaga damu (nisinukuliwe vibaya)

Ninamaanisha taifa ambalo wananchi wawe waamuzi wa mwisho
Taifa ambalo mwananchi awe na uhuru wa kuzungumza, kuuliza, kukosoa, kuchagua na kushiriki katika kuamua mustakabali wa nchi yake

Kwa sababu sasa tumeongea sana

Tumeandika sana

Tumeomba sana

Tumeilalamikia serikali kwa mambo mengi sana

Lakini swali linabaki pale pale

Nini kifanyike ili tutoke kwenye kulalamika?

Kwa sababu sasa tutalalamika mpaka lini?

Je, tunahitaji nini kama wananchi ili sauti yetu iwe na nguvu na iweze kuleta matokeo?

Na kama nchi nyingine zimewahi kufikia hatua wananchi wakaungana na kudai mabadiliko mpaka yakatokea, sisi tatizo letu ni nini?

Tunashindwa kuungana?

Tunaogopa?

Hatuna imani kwamba tunaweza kubadilisha mambo?

Au bado tunasubiri mtu mwingine aje atufanyie?

ShesRise_1 ✋️
Taifa limefika pabaya sana..
Kilichobaki ni nature kutake its course...
I tell u.
Either CCM ing'atuke au pachafuke milele.
Tizameni comments za Wtanzanzania kwa msiba huko ZNZ....
NI HATARI MNOO...
 
Kila nikipitia hii thread napata wasiwasi mkubwa sana siku moja hichi ndicho kinacho enda kutokea hapo nchini. ShesRise_1 soma hii

 
Kila nikipitia hii thread napata wasiwasi mkubwa sana siku moja hichi ndicho kinacho enda kutokea hapo nchini.

Inafikirisha sana mkuu 🤔
 
Imebidi nicheke 😁
Nikujibu sasa 👇
1 Hapana mimi sio mtoto wa mkubwa

2 naishi Tanzania Dar es Salaam

3 Mada kama hizi wataandika kina nani?

NB : Mada yangu ni ya kujadili na watanzania wenzangu haina uchochezi wa aina yoyote

Sisi kama Watanzania kujadili mstakabali wa taifa imekua jinai?
😀😀
Sawa mkuu
 
Nadhani swali la msingi sio "kwa nini Watanzania hawajaleta mabadiliko makubwa?" Bali "ni mazingira gani hufanya mabadiliko yatokee?"

Mifano uliyoitoa ya nchi kama

Philippines (1986),Sudan (2019), na Tunisia (2011).

Kwa kuongezea nchi za South Korea mwaka 1987 yalitokea maandamano ya amani yalichangia kurejesha uchaguzi wa moja kwa moja wa rais

Nchini Indonesia ulitokea mgogoro wa uchumi, maandamano ya wanafunzi na shinikizo la Wananchi vikachangia kuondoka kwa Suharto.

Zambia (1991): shinikizo la wananchi na vyama vya upinzani likaishia kwenye uchaguzi uliobadilisha uongozi.

Kwa Tanzania, mazingira hali ni tofauti. Kuna mjadala mkubwa kuhusu Katiba, mfumo wa uchaguzi, uhuru wa kisiasa na mwenendo wa baadhi ya kesi zenye maslahi ya umma, ikiwemo ya Tundu Lissu.

Watu wengi wanaona bado kuna nafasi ya maboresho, na wapo wanaohisi kasi ya mabadiliko haitoshi (hasa mitandaoni)

Pamoja na yote yanayoendelea na yaliyotokea October 29 2025 bado tatizo linaweza kuwa kuendea kutokana hofu ya athari za kisiasa kwa baadhi ya watu, kutokuwepo kwa mwafaka mpana juu ya ajenda moja ( Hili Chadema wamelizungumzia mara nyingi sana)

Tatizo jingine ni imani tofauti kuhusu njia bora ya kufikia mabadiliko. (CCM wamekuwa waongo kukubali mabadiliko na imefikia hatua Chadema wameamua kulipeleka hilo jambo kwa Wananchi, Wananchi nao hawajui wasimamie upande upi.

Mabadiliko ya kudumu mara nyingi hutokea pale ambapo wananchi wanaendelea kushiriki kwa njia za amani na za kisheria zikiwemokupiga kura, kufuatilia uwajibikaji, kushiriki mijadala ya sera, kuelimishana na kuunga mkono taasisi zinazofanya kazi ndani ya sheria.

Nguvu ya sauti ya wananchi huongezeka zaidi inapokuwa ya pamoja, yenye nidhamu na inayolenga suluhisho, sio vurugu.

Bado Watanzania hatujui tupo katika njia ipi. Na Mabadiliko kila nchi hutokea kwa njia tofauti. La msingi Watawala wajifunze kupitia historia za mabadiliko kutoka nchi mbalimbali.
Nimeipenda hii
 
Ni kutokujua tu nature ya binadamu na kupuuza somo la historia.

Asili ya binadamu ukimkandamiza lazima ataretaliate, historia inaonesha dunia imepata kuongozwa na wababe na mwishowe walianguka. Haitakuwa tofauti kwa CCM.

Kwa kilichotokea october 29, watu wamerudi kwenye drawing board, tujipe muda.
✍️✍️
 
Kitu ambacho tunawaomba watawala ni kuwasikiliza wananchi, mtu anapokwambia mathalani unanuka mdomo,hapo hutakiwi kumchukia bali unatakiwa kumshukuru kwakuwa katika wengi amejaribu kukwambia ukweli ili usizidi kufedheheka na kadhia hiyo

Nadhani ifike kipindi serikali na wananchi tuwe kitu kimoja,na siri kubwa ni kusikilizana tu,Serikali isikilize wananchi na wananchi waisikilze serikali,hapo tutafikia kwenye Tanzania tunayo itaka

Bado hatuja chelewa
 
Kitu ambacho tunawaomba watawala ni kuwasikiliza wananchi, mtu anapokwambia mathalani unanuka mdomo,hapo hutakiwi kumchukia bali unatakiwa kumshukuru kwakuwa katika wengi amejaribu kukwambia ukweli ili usizidi kufedheheka na kadhia hiyo

Nadhani ifike kipindi serikali na wananchi tuwe kitu kimoja,na siri kubwa ni kusikilizana tu,Serikali isikilize wananchi na wananchi waisikilze serikali,hapo tutafikia kwenye Tanzania tunayo itaka

Bado hatuja Chelsea
Muda tunao bado hatujachelewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom