Tutalalamika mpaka lini?

Tutalalamika mpaka lini?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
18,787
Reaction score
44,084
Morning wana JF

Watanzania tumekuwa tukilalamika kila siku kuhusu uongozi na mambo mbalimbali ambayo hatupendezwi nayo

1. Tumeongea sana tukiomba maboresho ya Katiba

2. Tumezungumza sana kuhusu kupitiwa upya kwa suala la Muungano

3. Tumezungumza kuhusu Mahakama na utendaji kazi wake

(Mpaka sasa tunaona mwenendo wa kesi ya mwenyekiti wa chadema TL inavyoenda huku watu wakiwa na mashaka makubwa )

Na mengine mengi sana

Lakini mpaka sasa hakuna matokeo chanya ya kutosha, licha ya kwamba tulipo leo sio tulipokuwa jana
Kuna mambo yamebadilika, lakini bado kuna mengi ambayo tumekuwa tukiyazungumza kwa miaka mingi bila kuona mabadiliko tunayoyatarajia

Tumeona nchi kadhaa zikifanya jitihada za pamoja
Wananchi wameungana, wameandamana na kudai mabadiliko na katika baadhi ya nchi hata jeshi liliishia kuingilia kati baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi

Hii mifano nimeweka hapa nimesoma huko mitandanoni
👇
Mfano, Philippines mwaka 1986, wananchi waliungana katika maandamano makubwa ya amani yaliyokuja kujulikana kama People Power Revolution, na hatimaye utawala wa Ferdinand Marcos ukaondoka

Tunisia mwaka 2011, wananchi waliingia barabarani kudai mabadiliko na maandamano yakawa makubwa kiasi cha kumfanya Rais Zine El Abidine Ben Ali kuondoka madarakani

Sudan mwaka 2019, wananchi waliandamana kwa miezi kadhaa wakidai mabadiliko, mpaka hatimaye Omar al-Bashir akaondolewa madarakani baada ya miaka takribani 30 ya utawala

Hapa kwetu tulijaribu pia
Kupaza sauti zetu tukiwa na madai mbali mbali

Lakini wote tunajua nini kilitokea October 29 💔

Na wote tunajua mtu anayekwenda kinyume na watawala au anayesema mambo fulani hadharani, mara nyingi kinachoweza kumpata

Ukiongea hadharani unatulizwa

Sasa tutaongea chumbani?

Kama hatuwezi kuongea hadharani, kama hatuwezi kuuliza maswali, kama hatuwezi kukosoa na kudai mabadiliko bila kuogopa, basi tutaikomboaje hii nchi?

Na ninaposema kuikomboa, simaanishi kwamba twende kwenye vurugu au kumwaga damu (nisinukuliwe vibaya)

Ninamaanisha taifa ambalo wananchi wawe waamuzi wa mwisho
Taifa ambalo mwananchi awe na uhuru wa kuzungumza, kuuliza, kukosoa, kuchagua na kushiriki katika kuamua mustakabali wa nchi yake

Kwa sababu sasa tumeongea sana

Tumeandika sana

Tumeomba sana

Tumeilalamikia serikali kwa mambo mengi sana

Lakini swali linabaki pale pale

Nini kifanyike ili tutoke kwenye kulalamika?

Kwa sababu sasa tutalalamika mpaka lini?

Je, tunahitaji nini kama wananchi ili sauti yetu iwe na nguvu na iweze kuleta matokeo?

Na kama nchi nyingine zimewahi kufikia hatua wananchi wakaungana na kudai mabadiliko mpaka yakatokea, sisi tatizo letu ni nini?

Tunashindwa kuungana?

Tunaogopa?

Hatuna imani kwamba tunaweza kubadilisha mambo?

Au bado tunasubiri mtu mwingine aje atufanyie?

ShesRise_1 ✋️
 
Tunaelewa kabisa kwamba yote tuliyofanya hayatafua dafu sababu serikali imeshaamua kuwa ya kidikteta.. kwahiyo hata tuseme mazuri au mabaya hakuna wanachosikiliza na sababu kuu wanajua hakuna tutakachofanya.. coz watz ni waoga by nature
Maneno yako ni mtu aliekata tamaa kabisa 😢
Hakuna option nyingine hebu tujadili jamani
 
If the government fails to protect rights or becomes tyrannical, we citizens have the right to resist, potentially by force.
And in this case violence is morally justified since it is a last resort, proportional, and aimed at restoring justice.
 
Maneno yako ni mtu aliekata tamaa kabisa 😢
Hakuna option nyingine hebu tujadili jamani

Maneno yako ni mtu aliekata tamaa kabisa 😢
Hakuna option nyingine hebu tujadili jamani
Wananchi hatuna kitu wenzetu wana majeshi na wanayatumia.. unadhani nani atamfunga paka kengere
 
Ili kufanikiwa lazima mambo hayo yawe ni mahitaji ya wananchi sio wanasiasa , kufanikiwa ngumu kama mtabaki na mambo ya kufuatilia mijadala ya demokrasia..Wananchi ndiyo wenye nchi sio viongozi , viongozi wanataka kula kodi za wananchi yaani wanasiasa wote , kila shughuli ya kisiasa basi wanatafuna kodi zetu .

Mngeacchana na uchawa siasa ndipo tukaungana ila kama mmebaki kushikilia siasa zile zile za kiafrika mtaisha ..Mfano hapo kenya , kenya wana katiba mpya ,wanpokezana madaraka ila maandamano kila siku .


Twende kule senegal , juzi wameandamana kisa maisha magumu baada ya kumuingiza mpinzani .Ombi langu tusije kuingia sehemu ambayo itakuwa majuto zaidi , harakati za wanasiasa ni drama wote ni wazee wa bahasha .Unatkiwa ujue kwamba unachotaka kina impacts za moja kwa moja na unachofikiria , usije kufikiria kwamba kuna mwanasiasa ataingia na watu watakuwa wanapata pesa kirahisi bila yaa kufanya kazi .

Elimu za darasani hazileta ukombozi ,usidanganywe demokrasia italeta maendeleo , fanya tathmini zenu kwa sababu mpaka leo hamjui tatizo liko wapi .
 
If the government fails to protect rights or becomes tyrannical, we citizens have the right to resist, potentially by force.
And in this case violence is morally justified since it is a last resort, proportional, and aimed at restoring justice.

Hili linawezekana vipi
Kwa mazingira yaliyopo na namna watu wamevunjika moyo kwa lile la mo 29
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom