Tahadhari kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa

Ninja

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
361
Reaction score
726
Barua yangu kwa No 1 haikuzingatiwa, nasikitika sana, ona sasa yanayoendelea!, na sasa nakuja kwenu KAMATI na taarifa kutoka kwa ULIMWENGU usioonekana.

Sote tunatamani kuwa maovu yote yaliyotokea Tanganyika (Tanzania Bara) yasitokee tena kamwe. Tunatamani mambo yarudi kama zamani.

Kwenye ulimwengu usioonekana kuna taarifa tuliyonayo na pia mmoja wenu anajua ni kwamba tarehe 9 sio tu kwamba yatafanyika maandamano makubwa, lakini kuna wauaji waliopandikizwa na wanamtandao kwa lengo la kufanya mauaji makubwa zaidi dhidi ya watanganyika na hasa vijana wa kikristo. ( kwa lengo maalum)

Kuna watanganyika watajibu kwa kuua wazanzibari walioko Tanganyika. Kuna waislamu watajibu kwa kuua wakristo. Kuna makanisa na misikiti itachomwa moto.

Kuna wahuni wataona fursa na kuanza kuua ovyo, kubaka, kupora mali za watu na wahuni hao watatoka kila kona kuanzia uraiani, majeshini, magerezani na kila kona.

Kule Zanzibar watanganyika watasakwa wauawe na wao wataanza kujitetea.

Kuna kikao kiliwahi kufanyika hapo awali ndani ya nchi A cha lengo la kuidhoofisha nchi ili kupora rasilimali.

Kuna nchi B na nchi C zitaingia kwa haraka Tanganyika na makomando wasio na sare ili kuua askari polisi kwa niaba ya raia lakini kwa lengo la kuharibu uimara wa ulinzi wa Taifa.

Jeshi litagawanyika kabisa. Kuna vikosi vya anga vya nchi jirani bila kujitambulisha vitaingia na kuharibu maeneo yote nyeti ikiwemo Ikulu za Dar na Dodoma, miradi yote mikubwa n.k. Silaha kinga tulizonunua wakati ule wa Col J hazitafanya kazi kuzuia.

Watanzania watatamani kukimbilia Sudan maana itakuwa ni bora kuliko yanayokwenda kutokea wiki chache zijazo.

Watakaoathirika kwa kiasi kikubwa sana ni watoto, wanawake, walemavu, wagonjwa na wanyonge wengine. Wengi watakimbia nchi. Wanaume wengi watauawa na wakati mwingine bila hata hatia.

Hakuna atakayekuwa salama, iwe komando au raia, mkristo au muislamu, mnyonge au mbabe, mbunge au mpiga debe.

Ziko nchi za karibu na za mbali zimejipanga kutumia hilo kama fursa kwao.

Wahuni watapanga kukimbilia nchi A na familia zao kama walivyoahidiwa lakini baadhi yao na hasa namba 1 na watu wake wa karibu hawataweza na watakamatwa na wakora na kufanyiwa ukatili utakaoweka rekodi ya kidunia tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Kuna watu wa karibu sana na namba 1, anawaamini sana. WATAMGEUKA kwa kiwango cha nyota saba.

Lengo la nchi A ni kushirikiana na nchi X na mpinzani wake nchi Y ili Tanzania ikishakuwa tepetepe kuliko DRC na Sudan basi wafanye kuchota rasilimali kama kulamba asali kwa kijiko.

Wakati huo majeshi yatakuwa yamedhoofishwa na mgawanyiko mkubwa na hivyo kundi kubwa litageuka kuwa waasi kwa maslahi ya taifa na lingine kwa maslahi binafsi.

Kuepuka haya yote, NINI KIFANYIKE!?

1. TUBUNI. Hapa muwaulize masheikh(sio maseikh ubwabwa) na wachungaji (sio kina Mwampesa) ili mjue kutubu maana yake ni nini.
2. Maamuzi magumu kwamba bora kuiokoa Tanzania kuliko kung'ang'ania madaraka..( Rais Ally Hassan Mwinyi aliwahi kufanya jambo la kishujaa enzi akiwa waziri wa mambo ya ndani)
3. Kuacha mara moja kuwachukulia watanzania wote kwa ujumla wao kama watoto wadogo wa kudanganywa na peremende. Eti maridhiano, tuache huo ugoro.
4. Humprey Polepole, Tundu Lissu, Mdude Nyagali, wote waliobambikiwa kesi za uhaini, wote waliobambikiwa kesi za kisiasa.. waachiwe MARA MOJA.
5. Madai ya Gen Z kwenye barua yao na madai ya raia wengineo yatekelezwe, ikiwemo katiba mpya, uchaguzi urudiwe, fidia kwa wahanga wa mauaji na madhara mengineyo katika uchaguzi haramu wa 29 Oktoba, pamoja na uwajibishwaji na uwajibikaji wa wahusika wote.
6. Serikali ya mpito inahitajika haraka kuongoza mapambano ya kulikomboa taifa, serikali ambayo itaaminiwa na wananchi wote. Hii iliyojipa madaraka haiaminiki.
7. Lengo liwe moja kwa pande zote. KULIKOMBOA TAIFA. Na sio kuonyeshana ubabe.

Je tunataka kuokoa taifa letu au tunataka kufa na vyeo vyetu na sifa zetu na viburi vyetu na kuifuta kabisa Tanzania kwenye uso wa ramani ya dunia?

TAFADHALI KAMATI, 9D Tuiepuke kwa gharama yeyote. Kuua raia, kuwatisha, kubambika kesi, kuteka wapinzani na yanayofanana na hayo ni kuongezea petroli kwenye moto wa 9D.

Nimeyaona hayo kwenye ulimwengu usioonekana. SIYAPENDI, SIYATAKI, SIYASHABIKII. Ningeweza kuyazuia ningeyazuia. NIMEYALETA KWENU kwa kuwa HILI NI LENU.
 
Itategemeana na uimara wa nchi kutokuingilika kwa maadui wa nje. Nchi ni kubwa hii na ina utajiri mwingi, kuna viinchi jirani ni vikora, vinatamani Tanzania iwe kama congo na sudani ili viingie kwa urahisi kujichukulia rasimali bwerere.
 
Mkianza kupigana wenyewewe kwa wenyewe ulinzi wa mipaka ya nchi unakuwa dhaifu, mara rwanda na uganda wanaingia na kuteka kagera, kigoma, mwanza, geita hadi shinyanga, upande ule malawi analichukua eneo lote la ziwa nyasa. kule kusini wale wahuni wa delgado wanaichukua mtwara mpaka lindi, kenya nao wanajichukulia kilimanjaro. Masultani nayo yanaibuka yakichuka tanga, dar hadi mafia, kwa hali hii nchi itakuwa imesambaratika kizembe kama hatua madhubuti hazitachukuliwa kuilinda nchi kikamilifu
 
Tumeonya sana humu watu viongozi hawaskii kwasababu JWTZ na Tiss wameamua kulinda kikundi cha wahuni aliosema Polepole waendelee kutafuna ngoja watoto wa watu unawaita wahalifu kwa kudai haki zao wakati nyie watoto wanatembelea kila aina ya gari ya kifahari JWTZ na Tiss wanapambana kulinda Uozo wa kikundi cha watu baada ya Nchi na wananchi
 
Itategemeana na uimara wa nchi kutokuingilika kwa maadui wa nje. Nchi ni kubwa hii na ina utajiri mwingi, kuna viinchi jirani ni vikora, vinatamani Tanzania iwe kama congo na sudani ili viingie kwa urahisi kujichukulia rasimali bwerere.
Nchi ikikosa umoja na mshikamano ukubwa wake hausaidii kitu, inaingilika kirahisi na yeyote. Ndiyo sababu Rwanda na udogo wake inajichotea raslimali ndani ya DRC kama shambani kwa Bibi yao
 
yote haya ya nini, Watu wamalizane na Samia tu basi patatulia tulii
Barua yangu kwa No 1 haikuzingatiwa, nasikitika sana, ona sasa yanayoendelea!, na sasa nakuja kwenu KAMATI na taarifa kutoka kwa ULIMWENGU usioonekana.

Sote tunatamani kuwa maovu yote yaliyotokea Tanganyika (Tanzania Bara) yasitokee tena kamwe. Tunatamani mambo yarudi kama zamani.

Kwenye ulimwengu usioonekana kuna taarifa tuliyonayo na pia mmoja wenu anajua ni kwamba tarehe 9 sio tu kwamba yatafanyika maandamano makubwa, lakini kuna wauaji waliopandikizwa na wanamtandao kwa lengo la kufanya mauaji makubwa zaidi dhidi ya watanganyika na hasa vijana wa kikristo. ( kwa lengo maalum)

Kuna watanganyika watajibu kwa kuua wazanzibari walioko Tanganyika. Kuna waislamu watajibu kwa kuua wakristo. Kuna makanisa na misikiti itachomwa moto.

Kuna wahuni wataona fursa na kuanza kuua ovyo, kubaka, kupora mali za watu na wahuni hao watatoka kila kona kuanzia uraiani, majeshini, magerezani na kila kona.

Kule Zanzibar watanganyika watasakwa wauawe na wao wataanza kujitetea.

Kuna kikao kiliwahi kufanyika hapo awali ndani ya nchi A cha lengo la kuidhoofisha nchi ili kupora rasilimali.

Kuna nchi B na nchi C zitaingia kwa haraka Tanganyika na makomando wasio na sare ili kuua askari polisi kwa niaba ya raia lakini kwa lengo la kuharibu uimara wa ulinzi wa Taifa.

Jeshi litagawanyika kabisa. Kuna vikosi vya anga vya nchi jirani bila kujitambulisha vitaingia na kuharibu maeneo yote nyeti ikiwemo Ikulu za Dar na Dodoma, miradi yote mikubwa n.k. Silaha kinga tulizonunua wakati ule wa Col J hazitafanya kazi kuzuia.

Watanzania watatamani kukimbilia Sudan maana itakuwa ni bora kuliko yanayokwenda kutokea wiki chache zijazo.

Watakaoathirika kwa kiasi kikubwa sana ni watoto, wanawake, walemavu, wagonjwa na wanyonge wengine. Wengi watakimbia nchi. Wanaume wengi watauawa na wakati mwingine bila hata hatia.

Hakuna atakayekuwa salama, iwe komando au raia, mkristo au muislamu, mnyonge au mbabe, mbunge au mpiga debe.

Ziko nchi za karibu na za mbali zimejipanga kutumia hilo kama fursa kwao.

Wahuni watapanga kukimbilia nchi A na familia zao kama walivyoahidiwa lakini baadhi yao na hasa namba 1 na watu wake wa karibu hawataweza na watakamatwa na wakora na kufanyiwa ukatili utakaoweka rekodi ya kidunia tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Kuna watu wa karibu sana na namba 1, anawaamini sana. WATAMGEUKA kwa kiwango cha nyota saba.

Lengo la nchi A ni kushirikiana na nchi X na mpinzani wake nchi Y ili Tanzania ikishakuwa tepetepe kuliko DRC na Sudan basi wafanye kuchota rasilimali kama kulamba asali kwa kijiko.

Wakati huo majeshi yatakuwa yamedhoofishwa na mgawanyiko mkubwa na hivyo kundi kubwa litageuka kuwa waasi kwa maslahi ya taifa na lingine kwa maslahi binafsi.

Kuepuka haya yote, NINI KIFANYIKE!?

1. TUBUNI. Hapa muwaulize masheikh(sio maseikh ubwabwa) na wachungaji (sio kina Mwampesa) ili mjue kutubu maana yake ni nini.
2. Maamuzi magumu kwamba bora kuiokoa Tanzania kuliko kung'ang'ania madaraka..( Rais Ally Hassan Mwinyi aliwahi kufanya jambo la kishujaa enzi akiwa waziri wa mambo ya ndani)
3. Kuacha mara moja kuwachukulia watanzania wote kwa ujumla wao kama watoto wadogo wa kudanganywa na peremende. Eti maridhiano, tuache huo ugoro.
4. Humprey Polepole, Tundu Lissu, Mdude Nyagali, wote waliobambikiwa kesi za uhaini, wote waliobambikiwa kesi za kisiasa.. waachiwe MARA MOJA.
5. Madai ya Gen Z kwenye barua yao na madai ya raia wengineo yatekelezwe, ikiwemo katiba mpya, uchaguzi urudiwe, fidia kwa wahanga wa mauaji na madhara mengineyo katika uchaguzi haramu wa 29 Oktoba, pamoja na uwajibishwaji na uwajibikaji wa wahusika wote.
6. Serikali ya mpito inahitajika haraka kuongoza mapambano ya kulikomboa taifa, serikali ambayo itaaminiwa na wananchi wote. Hii iliyojipa madaraka haiaminiki.
7. Lengo liwe moja kwa pande zote. KULIKOMBOA TAIFA. Na sio kuonyeshana ubabe.

Je tunataka kuokoa taifa letu au tunataka kufa na vyeo vyetu na sifa zetu na viburi vyetu na kuifuta kabisa Tanzania kwenye uso wa ramani ya dunia?

TAFADHALI KAMATI, 9D Tuiepuke kwa gharama yeyote. Kuua raia, kuwatisha, kubambika kesi, kuteka wapinzani na yanayofanana na hayo ni kuongezea petroli kwenye moto wa 9D.

Nimeyaona hayo kwenye ulimwengu usioonekana. SIYAPENDI, SIYATAKI, SIYASHABIKII. Ningeweza kuyazuia ningeyazuia. NIMEYALETA KWENU kwa kuwa HILI NI LENU.
!
 
Back
Top Bottom