Tutalalamika mpaka lini?

Tutalalamika mpaka lini?

Wewe unadhani tufanyeje, ccm imeshikilia kila kitu kuanzia madaraka mpaka majeshi, kama wao watataka mabadiliko ya kikatiba, mabadiliko ya kimfumo, itakuwa rahisi. Ila hawataki na hawatakubali kubadilisha chochote maana wanajua any changes and they're out.

Mtu ambaye hataki make mezani muongee unadhani utatumia njia gani kuelewana nae, tell me!!
Kuna kitabu cha dini kinasema :

Usimnyime mtoto wako mapigo
maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa Utampiga kwa fimbo, na kumponya nafsi yake na kuzimu
 
Sisi Watanzania ni mazuzu 🤔
Mzee Pascal Mayalla wewe umeliona jua kabla yangu
Unaweza kua sawa na mzazi wangu au zaidi?
Nikuulize kwa upole je kuna dawa ya uzuzu?
Uzuzu ni kama ulivyo ujinga, ujinga ni kutokujua, ukielimishwa ukijulishwa ujinga unakutoka unakuwa mwerevu, sio mjinga tena.

Uzuzu ni hii hali ya kufanywa lolote huku wewe umetulia tuu kama zuzu, dawa ya uzuzu ni kuzinduka kwenye usingizi wa pono, ukifanyiwa jambo ambalo sio, unasimama imara na kusema loud and clear a Big No!, you can't do this to us!, sisi sio mazuzu!.

Hili la uzuzu, nimelizungumza hapa

Je Wajua Taifa Bila Mhimili wa 4 Huru na Imara ni Taifa Mfu?. Je Watanzania ni Mazuzu?. Gazeti la M/halisi Lisamehewe Kuandika Ukweli au ni Zuzu Tuu?

na hapa

Japo sio lazima kuhoji kila kitu kwa kuuliza maswali lakini mtu mwenye akili zake timamu ni lazima ajiulize. Ukimya wetu, msitufanye mazuzu kuna...

P
 
My friends, ladies and gentlemen,

binafsi nadhani wanachoweza kufanya hao waTanzania wachache sana wanaolalamika hasa kupitia mitandao ya kijamii ni kuungana kutukana, kuporomosha matusi na pengine kuwazomea watu wenye maoni tofauti na yao, wanaweza kuungana kushangilia vifo vya waja wa Allah wenye mtazamo tofauti na wao na sio zaidi ya hapo.

Malalamiko uliyoyaeleza hapo juu mengi yanaendelea kufanyiwa kazi na wawakilishi wa wananchi bungeni, lakini pia serikali sikivu ya CCM katika utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi, inayafanyia kazi masuala yote yanayozungumzwa mitandaoni ambayo kwakweli ni ya kawaida sana na yalielezwa hata kwenye kampeni za uchaguzi 2025.🐒
Mwenyekiti wa CCM alitoa ahadi kua swala la katiba lingeanzishiwa mchakato ndani ya siku 100 vipi mpaka sasa siku 100 moja bado?
 
Mwenyekiti wa CCM alitoa ahadi kua swala la katiba lingeanzishiwa mchakato ndani ya siku 100 vipi mpaka sasa siku 100 moja bado?
Nadhani ikiwa umefualilia kongamano la TCD linaloendelea jijini Dar Es Salaam, makamu mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Stephen Masatu Wasira ameeleza kwa kina zaidi kuhusu ahadi hiyo muhimu sana, ambayo kutokana na mazingira yaliyotokea ilikosa umuhimu wa kuzingatiwa na kutekelezwa au kufanyiwa kazi.

Nadhani hakuna hata mTanzania moja alielalamikia kuhusu hilo kwasababu kila mtu anajua hali ilivyo kua. Kuna vitu vingine ni lazima kua wangwana kidogo 🐒
 
Uzuzu ni kama ulivyo ujinga, ujinga ni kutokujua, ukielimishwa ukijulishwa ujinga unakutoka unakuwa mwerevu, sio mjinga tena.

Uzuzu ni hii hali ya kufanywa lolote huku wewe umetulia tuu kama zuzu, dawa ya uzuzu ni kuzinduka kwenye usingizi wa pono, ukifanyiwa jambo ambalo sio, unasimama imara na kusema loud and clear a Big No!, you can't do this to us!, sisi sio mazuzu!.

P
Kwa maana hiyo kuendelea kulialia na kutoa kamasi tunazidi kudhihirisha uzuzu wetu upo kwa viwango vya juu zaidi

Nimesema kwenye bandiko watu wamejaribu kuandamana ikashindika hiyo pia ilikua sehemu ya kuonesha kua watu wamechoka kuonekana mazuzu

Wewe mwenyewe unajua kilichotokea

Wakosoji wanaonekana kua na impact kwa jamii Unajua nini hua kina tokea

Sasa ili tusionekane mazuzu tufanyeje

NB: jitihada za mabadiliko zitachelewa kwa sababu unafiki umetamalaki
 
Nadhani ikiwa umefualilia kongamano la TCD linaloendelea jijini Dar Es Salaam, makamu mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Stephen Masatu Wasira ameeleza kwa kina zaidi kuhusu ahadi hiyo muhimu sana, ambayo kutokana na mazingira yaliyotokea ilikosa umuhimu wa kuzingatiwa na kutekelezwa au kufanyiwa kazi.

Nadhani hakuna hata mTanzania moja alielalamikia kuhusu hilo kwasababu kila mtu anajua hali ilivyo kua. Kuna vitu vingine ni lazima kua wangwana kidogo 🐒
Hali ilikuaje?
Nini kilisababisha hali ikawa hivyo?
Je mambo mengine yamesimama pia kutokana na hali hiyo au ni katiba tu?
 
Achaneni na hizo habari tafuteni hela na my enjoy maisha..katiba haikunyimi pombe haikunyimi kucheza haikunyimi mapenzi sasa ya nini uhangaike nayo kwani wewe ni mwanasiasa?
 
Ukikosoa unakuwa adui wa taifa.
Just imagine mkuu, na haitaishia hapo, ukiendelea kukosoa utatekwa, utafirwa, utatobolewa macho na kuuwawa. Ndio ujue hawa jamaa wamedhamiria kukaa madarakani.

Basi wangefanya maendeleo, wakawafikia wananchi, wakatatua kero, wakatumia rasilimali kwa faida ya wote. Ila wao wanajua lwa nini hasa wanang'ang'ania madaraka, wanajua.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom