Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 24,074
- 29,515
Kumbuka alichokisema jaji Warioba, bunduki na risasi kila mahali.Unasubiri washibe ?
Basi huja njaa
Kumbuka alichokisema jaji Warioba, bunduki na risasi kila mahali.Unasubiri washibe ?
Basi huja njaa
Inatawala kwa sababu sisi wananchi tunaendelea kutambua na kuheshimu mamlaka yake na kushirikiana nayo !Unajua kwamba Serikali haitawali kwa sababu tu ina polisi, mahakama, jeshi, fedha nk. Inatawala pia kwa sababu sisi wananchi tunaendelea kutambua na kuheshimu mamlaka yake na kushirikiana nayo.
Uhamasishaji wa uasi kwa wananchi wengine:hii inataka kufanana na lile zengwe la TL tutakinukishaKwa hiyo, kama serikali inakiuka kwa kiasi kikubwa masharti yaliyofanya mamlaka yake ikubalike, wananchi tunaweza kuanza kudai upya mamlaka yetu ya kisiasa kupitia umoja wa kiraia, NGO's, maandamano ya amani, kutoshirikiana na vitendo visivyo vya haki, habari huru na uhamasishaji wa uasi kwa wananchi wengine
asante mkuu 🙏Soma kitu kinaitwa social contract nafikiri utaelewa vizuri.
Nini kinafata sasa 🤔Kumbuka alichokisema jaji Warioba, bunduki na risasi kila mahali.
Kiukweli kabisa, nimeguswa na bandiko hili, wewe ShesRise_1 ni mzalendo wa kweli wa nchi hii!,Morning wana JF
Watanzania tumekuwa tukilalamika kila siku kuhusu uongozi na mambo mbalimbali ambayo hatupendezwi nayo
Tunashindwa kuungana?
Tunaogopa?
Hatuna imani kwamba tunaweza kubadilisha mambo?
Au bado tunasubiri mtu mwingine aje atufanyie?
ShesRise_1 ✋️
Yes, bila strong rebellion hakuna kitachobadilika, tutaendelea hivi hivi mpaka 2070 huko. Haki siku zote huwa haiombwi, inadaiwa. Na kumdai mtu ambaye hataki kukupa haki yako inahitaji mbinu za ziada kama hizo.Uhamasishaji wa uasi kwa wananchi wengine:hii inataka kufanana na lile zengwe la TL tutakinukisha
Conclusion kama hiyo ni useless kwenye harakati za ukombozi wa nchi. Wewe kama mwandishi wa habari una nafasi kubwa na nzuri sana kuchangia katika vuguvugu hilo la kudai mabadilikohatimaye nikafikia conclusion sisi Watanzania ni mazuzu!.
Wna nini cha maana acha zako , unadanganywa eti uchumi huku wanashikilia uchumi nchi nzima hwafiki hata asilimia 10 , wengine wanagombania mpaka ugali..Ukiona nchi wanaandamana kwa vitu vidogo na kufanya uharibifu basi ni hopeless , kenya kuna mgomo wa madaktari , juzi kulikuwa na mgomo wa wafanyakazi wa airport ...Nimeona hapo neno uchawa
Labda kama hufatilii mabandiko yangu mimi sina uchawa wa ki jinga kabisa
Ikipatikaka katiba mpya
Swala la muungano likaangaziwa
Mihimili yote ikafanya kazi kwa weredi bila kusomana
Malalamiko hayataisha kibinadamu ila yatapungua sana hata kwa asilimia 80
Hao Senegal na Kenya unaowatolea mifano huwezi kujifananisha nao kwa chochote
Kitu unachopaswa kujua saivi hata ukipika gizani tutawasha taa tutamulika
Hapo uliposema Rais kuwa ndiye mwenyekiti wa chama chake , nakuunga mkono ..Hizi siasa zingefutwa, kama wana akili kweli wajiingize kwenye ugunduzi ..Nchi kubwa mnaenda kuwapa kikundi cha watu , kinachojiita chama cha siasa ..Mwaka 2000 baada ya uchaguzi kukatokea machafuko makubwa sana Zanzibar, wananchi waligomea matokeo ambayo dhahìri kabisa Maalim Seif aliporwa ushindi
Yale maandamano yalifanya vikosi kutoka Tanganyika kupelekwa kutuliza ghasia ambazo ama kwa hakika watu wengi sana walipotezwa.
Toka 2000 mpaka leo wazanzibari wamekuwa wapole sana, hata wakiporwa ushindi wanakaa kimya.
Fast forward 2025 October, mambo yamekuwa kama kule unguja. Hii maana yake nini, Tanzania kama haitakuwa na wanasiasa wenye utashi wa kukaa mezani na kuweka mambo sawa, tutaongozwa kidikteta miaka mingi ijayo, nasema kidiktrta kwa sababu katiba ya 1977 ambayo kimsingi imezeeka, haiendani na maisha ya sasa, inakumbatiwa na watawala kwa sababu tu inawapa favours nyingi kuendelea kutawala.
Raisi ambaye ni mwenyekiti wa chama hawezi kuwa ndio anateua mwenyekiti wa INEC, wakurungenzi wa kusimamia uchaguzi, watendaji wa serikali za kata/mitaa/vijiji halafu useme kuna uchaguzi, hakuna fair grounds hata kidogo.
What to do, watch!!
Egypt chini ya Hosni Mubarak alikuwa na jeshi lenye nguvu na alius wengi, lakini wananchi walijitoa muhanga na Mubarak aliondoka. Na hapa ni kujitoa muhanga tu.Wananchi hatuna kitu wenzetu wana majeshi na wanayatumia.. unadhani nani atamfunga paka kengere
Hawawezi kukubali mabadiliko yoyote, katiba iliyopo inamfanya mwenyekiti wa chama ambaye ni raisi wa nchi na mgombea uraisi kuteua wasimamizi wa uchaguzi, yaani timu A inateua refa wa kuchezesha mechi ya Timu A vs Timu B. Hakuna faith grounds.Tutafanyaje na CCm hawataki mabadiliko.
Wewe unadhani tufanyeje, ccm imeshikilia kila kitu kuanzia madaraka mpaka majeshi, kama wao watataka mabadiliko ya kikatiba, mabadiliko ya kimfumo, itakuwa rahisi. Ila hawataki na hawatakubali kubadilisha chochote maana wanajua any changes and they're out.Umeongea vizuri na kwa mifano hai
Sasa tufanye nini ?
Sisi Watanzania ni mazuzu 🤔Kiukweli kabisa, nimeguswa na bandiko hili, wewe ShesRise_1 ni mzalendo wa kweli wa nchi hii!,
maswali kama haya yako, niliwahi kuyauliza humu,
hatimaye nikafikia conclusion sisi Watanzania ni mazuzu!. https://www.jamiiforums.com/threads...ehewe-kuandika-ukweli-au-ni-zuzu-tuu.2470629/
- https://www.jamiiforums.com/threads...-zero-nil-hamna-kitu-je-tutabadilika.2052027/
- Je, Wajua Japo Tanzania Ilipaswa Kutawaliwa na Ukuu wa Katiba, Lakini Inatawaliwa na Ukuu wa Chama?. Mbele ya Chama, Katiba si Lolote, si Chochote!
DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili
Mzee Pasco
Wote tukisema hivi itakuaje sasa ?Nasoma mawazo yenu maana hata nikichangia hamna kitakachobadilika.
Asante kwa maoniWna nini cha maana acha zako , unadanganywa eti uchumi huku wanashikilia uchumi nchi nzima hwafiki hata asilimia 10 , wengine wanagombania mpaka ugali..Ukiona nchi wanaandamana kwa vitu vidogo na kufanya uharibifu basi ni hopeless , kenya kuna mgomo wa madaktari , juzi kulikuwa na mgomo wa wafanyakazi wa airport ...
Hakuna kitakachobadilika hata siku moja ,nchi ifuate hali ya maisha ya wananchi sio kuongelea vitu vya kutoa kwenye vitabu.
Hii ndiyo kusema usiombe haki yako ila chukua haki yakoYeah, bila strong rebellion hakuna kitachobadilika, tutaendelea hivi hivi mpaka 2070 huko. Haki siku zote huwa haiombwi, inadaiwa. Na kumdai mtu ambaye hataki kukupa haki yako inahitaji mbinu za ziada kama hizo.
My friends, ladies and gentlemen,Morning wana JF
Watanzania tumekuwa tukilalamika kila siku kuhusu uongozi na mambo mbalimbali ambayo hatupendezwi nayo
1. Tumeongea sana tukiomba maboresho ya Katiba
2. Tumezungumza sana kuhusu kupitiwa upya kwa suala la Muungano
3. Tumezungumza kuhusu Mahakama na utendaji kazi wake
(Mpaka sasa tunaona mwenendo wa kesi ya mwenyekiti wa chadema TL inavyoenda huku watu wakiwa na mashaka makubwa )
Na mengine mengi sana
Lakini mpaka sasa hakuna matokeo chanya ya kutosha, licha ya kwamba tulipo leo sio tulipokuwa jana
Kuna mambo yamebadilika, lakini bado kuna mengi ambayo tumekuwa tukiyazungumza kwa miaka mingi bila kuona mabadiliko tunayoyatarajia
Tumeona nchi kadhaa zikifanya jitihada za pamoja
Wananchi wameungana, wameandamana na kudai mabadiliko na katika baadhi ya nchi hata jeshi liliishia kuingilia kati baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi
Hii mifano nimeweka hapa nimesoma huko mitandanoni
👇
Mfano, Philippines mwaka 1986, wananchi waliungana katika maandamano makubwa ya amani yaliyokuja kujulikana kama People Power Revolution, na hatimaye utawala wa Ferdinand Marcos ukaondoka
Tunisia mwaka 2011, wananchi waliingia barabarani kudai mabadiliko na maandamano yakawa makubwa kiasi cha kumfanya Rais Zine El Abidine Ben Ali kuondoka madarakani
Sudan mwaka 2019, wananchi waliandamana kwa miezi kadhaa wakidai mabadiliko, mpaka hatimaye Omar al-Bashir akaondolewa madarakani baada ya miaka takribani 30 ya utawala
Hapa kwetu tulijaribu pia
Kupaza sauti zetu tukiwa na madai mbali mbali
Lakini wote tunajua nini kilitokea October 29 💔
Na wote tunajua mtu anayekwenda kinyume na watawala au anayesema mambo fulani hadharani, mara nyingi kinachoweza kumpata
Ukiongea hadharani unatulizwa
Sasa tutaongea chumbani?
Kama hatuwezi kuongea hadharani, kama hatuwezi kuuliza maswali, kama hatuwezi kukosoa na kudai mabadiliko bila kuogopa, basi tutaikomboaje hii nchi?
Na ninaposema kuikomboa, simaanishi kwamba twende kwenye vurugu au kumwaga damu (nisinukuliwe vibaya)
Ninamaanisha taifa ambalo wananchi wawe waamuzi wa mwisho
Taifa ambalo mwananchi awe na uhuru wa kuzungumza, kuuliza, kukosoa, kuchagua na kushiriki katika kuamua mustakabali wa nchi yake
Kwa sababu sasa tumeongea sana
Tumeandika sana
Tumeomba sana
Tumeilalamikia serikali kwa mambo mengi sana
Lakini swali linabaki pale pale
Nini kifanyike ili tutoke kwenye kulalamika?
Kwa sababu sasa tutalalamika mpaka lini?
Je, tunahitaji nini kama wananchi ili sauti yetu iwe na nguvu na iweze kuleta matokeo?
Na kama nchi nyingine zimewahi kufikia hatua wananchi wakaungana na kudai mabadiliko mpaka yakatokea, sisi tatizo letu ni nini?
Tunashindwa kuungana?
Tunaogopa?
Hatuna imani kwamba tunaweza kubadilisha mambo?
Au bado tunasubiri mtu mwingine aje atufanyie?
ShesRise_1 ✋️