allow cp
JF-Expert Member
- Aug 15, 2026
- 747
- 2,408
Mfano nilioupenda ni wa Tunisia hapo , Mmachinga alikufa kishujaa sana yuleHiyo mifano niliyoweka hapo huoni ni wananchi waliamua ?
Wananchi tumebaki kumuachia Mungu atende muujiza.. na ndio maana unaona wengi wanashangilia kifo cha kiongozi.. hii yote ni kutafuta comfort 🥹So sad
Basi tukae na tuangalie tusibiri muujiza
Nimeona hapo neno uchawaIli kufanikiwa lazima mambo hayo yawe ni mahitaji ya wananchi sio wanasiasa , kufanikiwa ngumu kama mtabaki na mambo ya kufuatilia mijadala ya demokrasia..Wananchi ndiyo wenye nchi sio viongozi , viongozi wanataka kula kodi za wananchi yaani wanasiasa wote , kila shughuli ya kisiasa basi wanatafuna kodi zetu .
Mngeacchana na uchawa siasa ndipo tukaungana ila kama mmebaki kushikilia siasa zile zile za kiafrika mtaisha ..Mfano hapo kenya , kenya wana katiba mpya ,wanpokezana madaraka ila maandamano kila siku .
Twende kule senegal , juzi wameandamana kisa maisha magumu baada ya kumuingiza mpinzani .Ombi langu tusije kuingia sehemu ambayo itakuwa majuto zaidi , harakati za wanasiasa ni drama wote ni wazee wa bahasha .Unatkiwa ujue kwamba unachotaka kina impacts za moja kwa moja na unachofikiria , usije kufikiria kwamba kuna mwanasiasa ataingia na watu watakuwa wanapata pesa kirahisi bila yaa kufanya kazi .
Elimu za darasani hazileta ukombozi ,usidanganywe demokrasia italeta maendeleo , fanya tathmini zenu kwa sababu mpaka leo hamjui tatizo liko wapi .
AiseeeMfano nilioupenda ni wa Tunisia hapo , Mmachinga alikufa kishujaa sana yule
Hakika ni kutafuta comfort ambayo inadumu kiduchu kabla ya kuyeyukaWananchi tumebaki kumuachia Mungu atende muujiza.. na ndio maana unaona wengi wanashangilia kifo cha kiongozi.. hii yote ni kutafuta comfort 🥹
Huyo Tareeq Mohamed Bouaziz aisee ni moja ya watu ambao ni mashujaa wangu, nitachangia hii mada naendelea kufikiriAiseee
Ngoja tuendelee kusubiri on target japo dakika ni za lala salama.Hakika ni kutafuta comfort ambayo inadumu kiduchu kabla ya kuyeyuka
Tutafanyaje na CCm hawataki mabadiliko.Mwaka 2000 baada ya uchaguzi kukatokea machafuko makubwa sana Zanzibar, wananchi waligomea matokeo ambayo dhahìri kabisa Maalim Seif aliporwa ushindi
Yale maandamano yalifanya vikosi kutoka Tanganyika kupelekwa kutuliza ghasia ambazo ama kwa hakika watu wengi sana walipotezwa.
Toka 2000 mpaka leo wazanzibari wamekuwa wapole sana, hata wakiporwa ushindi wanakaa kimya.
Fast forward 2025 October, mambo yamekuwa kama kule unguja. Hii maana yake nini, Tanzania kama haitakuwa na wanasiasa wenye utashi wa kukaa mezani na kuweka mambo sawa, tutaongozwa kidikteta miaka mingi ijayo, nasema kidiktrta kwa sababu katiba ya 1977 ambayo kimsingi imezeeka, haiendani na maisha ya sasa, inakumbatiwa na watawala kwa sababu tu inawapa favours nyingi kuendelea kutawala.
Raisi ambaye ni mwenyekiti wa chama hawezi kuwa ndio anateua mwenyekiti wa INEC, wakurungenzi wa kusimamia uchaguzi, watendaji wa serikali za kata/mitaa/vijiji halafu useme kuna uchaguzi, hakuna fair grounds hata kidogo.
What to do, watch!!
People make history and history make people. Don't stress, watu wachache tu ndio huamsha , huchochea au huleta mabadiliko katika nyakati zisizotarajiwa kabisa na kutengeneza historia yao na ya jamii zao.Morning wana JF
Watanzania tumekuwa tukilalamika kila siku kuhusu uongozi na mambo mbalimbali ambayo hatupendezwi nayo
1. Tumeongea sana tukiomba maboresho ya Katiba
2. Tumezungumza sana kuhusu kupitiwa upya kwa suala la Muungano
3. Tumezungumza kuhusu Mahakama na utendaji kazi wake
(Mpaka sasa tunaona mwenendo wa kesi ya mwenyekiti wa chadema TL inavyoenda huku watu wakiwa na mashaka makubwa )
Na mengine mengi sana
Lakini mpaka sasa hakuna matokeo chanya ya kutosha, licha ya kwamba tulipo leo sio tulipokuwa jana
Kuna mambo yamebadilika, lakini bado kuna mengi ambayo tumekuwa tukiyazungumza kwa miaka mingi bila kuona mabadiliko tunayoyatarajia
Tumeona nchi kadhaa zikifanya jitihada za pamoja
Wananchi wameungana, wameandamana na kudai mabadiliko na katika baadhi ya nchi hata jeshi liliishia kuingilia kati baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi
Hii mifano nimeweka hapa nimesoma huko mitandanoni
👇
Mfano, Philippines mwaka 1986, wananchi waliungana katika maandamano makubwa ya amani yaliyokuja kujulikana kama People Power Revolution, na hatimaye utawala wa Ferdinand Marcos ukaondoka
Tunisia mwaka 2011, wananchi waliingia barabarani kudai mabadiliko na maandamano yakawa makubwa kiasi cha kumfanya Rais Zine El Abidine Ben Ali kuondoka madarakani
Sudan mwaka 2019, wananchi waliandamana kwa miezi kadhaa wakidai mabadiliko, mpaka hatimaye Omar al-Bashir akaondolewa madarakani baada ya miaka takribani 30 ya utawala
Hapa kwetu tulijaribu pia
Kupaza sauti zetu tukiwa na madai mbali mbali
Lakini wote tunajua nini kilitokea October 29 💔
Na wote tunajua mtu anayekwenda kinyume na watawala au anayesema mambo fulani hadharani, mara nyingi kinachoweza kumpata
Ukiongea hadharani unatulizwa
Sasa tutaongea chumbani?
Kama hatuwezi kuongea hadharani, kama hatuwezi kuuliza maswali, kama hatuwezi kukosoa na kudai mabadiliko bila kuogopa, basi tutaikomboaje hii nchi?
Na ninaposema kuikomboa, simaanishi kwamba twende kwenye vurugu au kumwaga damu (nisinukuliwe vibaya)
Ninamaanisha taifa ambalo wananchi wawe waamuzi wa mwisho
Taifa ambalo mwananchi awe na uhuru wa kuzungumza, kuuliza, kukosoa, kuchagua na kushiriki katika kuamua mustakabali wa nchi yake
Kwa sababu sasa tumeongea sana
Tumeandika sana
Tumeomba sana
Tumeilalamikia serikali kwa mambo mengi sana
Lakini swali linabaki pale pale
Nini kifanyike ili tutoke kwenye kulalamika?
Kwa sababu sasa tutalalamika mpaka lini?
Je, tunahitaji nini kama wananchi ili sauti yetu iwe na nguvu na iweze kuleta matokeo?
Na kama nchi nyingine zimewahi kufikia hatua wananchi wakaungana na kudai mabadiliko mpaka yakatokea, sisi tatizo letu ni nini?
Tunashindwa kuungana?
Tunaogopa?
Hatuna imani kwamba tunaweza kubadilisha mambo?
Au bado tunasubiri mtu mwingine aje atufanyie?
ShesRise_1 ✋️
Siku wenyenchi wakishiba watatuachia makombo.Morning wana JF

Unajua kwamba Serikali haitawali kwa sababu tu ina polisi, mahakama, jeshi, fedha nk. Inatawala pia kwa sababu sisi wananchi tunaendelea kutambua na kuheshimu mamlaka yake na kushirikiana nayo.Hili linawezekana vipi
Kwa mazingira yaliyopo na namna watu wamevunjika moyo kwa lile la mo 29
Hao wanaoteka na kuua wenzao kwanini tusiwateke na sisi?Tunaogopa kutekwa na kuuawa.
Umeongea vizuri na kwa mifano haiMwaka 2000 baada ya uchaguzi kukatokea machafuko makubwa sana Zanzibar, wananchi waligomea matokeo ambayo dhahìri kabisa Maalim Seif aliporwa ushindi
Yale maandamano yalifanya vikosi kutoka Tanganyika kupelekwa kutuliza ghasia ambazo ama kwa hakika watu wengi sana walipotezwa.
Toka 2000 mpaka leo wazanzibari wamekuwa wapole sana, hata wakiporwa ushindi wanakaa kimya.
Fast forward 2025 October, mambo yamekuwa kama kule unguja. Hii maana yake nini, Tanzania kama haitakuwa na wanasiasa wenye utashi wa kukaa mezani na kuweka mambo sawa, tutaongozwa kidikteta miaka mingi ijayo, nasema kidiktrta kwa sababu katiba ya 1977 ambayo kimsingi imezeeka, haiendani na maisha ya sasa, inakumbatiwa na watawala kwa sababu tu inawapa favours nyingi kuendelea kutawala.
Raisi ambaye ni mwenyekiti wa chama hawezi kuwa ndio anateua mwenyekiti wa INEC, wakurungenzi wa kusimamia uchaguzi, watendaji wa serikali za kata/mitaa/vijiji halafu useme kuna uchaguzi, hakuna fair grounds hata kidogo.
What to do, watch!!
Karibu mkuu uchangieHuyo Tareeq Mohamed Bouaziz aisee ni moja ya watu ambao ni mashujaa wangu, nitachangia hii mada naendelea kufikiri
Sawa mkuuNgoja tuendelee kusubiri on target japo dakika ni za lala salama.
Sawa mkuu muda utasemaPeople make history and history make people. Don't stress, watu wachache tu ndio huamsha , huchochea au huleta mabadiliko katika nyakati zisizotarajiwa kabisa na kutengeneza historia yao na ya jamii zao.
Unasubiri washibe ?Siku wenyenchi wakishiba watatuachia makombo.