Tutaachana lini na lugha ya kiingereza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by mtafungwa, Mar 5, 2012.

 1. m

  mtafungwa Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote napenda kuwasalimuni ninyi nyote katika jukwaa hili.

  Lugha ya kiingereza ni ngumu kwa wengi wetu lakini bado serikali inasisitiza kwamba iendelee kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Wakati huohuo lugha ya Kiswahili imekukuwa/kuzwa na kufikia kiwango ambacho kinafaa na kutosha kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Kwa nini tusiachane na kiingereza na badala yake tutumie Kiswahili chetu ktk taasisi zetu za elimu? Kwa nini lugha ya kiingereza isibaki tu kama somo la kawaida mashuleni na vyuoni? Maoni yenu tafadhali.

  Shukrani za awali.
   
 2. Nelsweeter

  Nelsweeter Senior Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa karne hii ya utandawazi kama hujui Kiingereza chimba shimo jifukie, maana your negligible in this world. Alie juu ya mti mfutate huko huko. Wewe subiri chini tu, utakuwa unakota maganda watu wanakula maembe dodo juu ya mti.
   
 3. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unfortunately, mpaka tuitwe tumeendelea.

  Institute za higher learning zote bado zinatumia kiingereza. Anza wewe kutunga vitabu vya curriculum kiswahili na tutabadili tabia ya kutumia Kiingereza.

  Lakini ni vizuri kukumbusha umma kuwa bado tu watumwa wa ki fikra.
   
 4. B

  Benaire JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa tumeshachelewa na mfumo huu umeshaota mizizi...cha msingi kama zilivyo english medium,shule za serikali nazo ziwe hivyo kitaaluma...halafu kiswahili kiwe somo la lazima kuanzia msingi mpaka chuo!
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Tukiacha kiingereza tutaongea lugha gani?
   
 6. m

  mtafungwa Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona lugha ya kiswahili tunayo? Halafu kuna lugha nyingine nyingi kibao!
   
 7. m

  mtafungwa Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani maana yangu ilikuwa tusifundishie kiingereza...lakini twaweza kujifunza tu lugha hii ya kuazima...
   
 8. m

  mtafungwa Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini unaweza kula dodo juu ya mti baada ya kuukwea huo mti kwa kutumia kiswahili...Jamani mbona sieleweki?
   
 9. m

  mtafungwa Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini unaweza kula dodo juu ya mti baada ya kuukwea huo mti kwa kutumia kiswahili...Jamani mbona sieleweki?
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kingereza kigumu kinoma aisee coz misingi hatuna ndio maana kinatupiga chenga sana,big up ally kiba ulipohojiwa na spora ulitelemsha kishwahili,kina kanumba igeni mfano huo,kama haujui kingereza ukihojiwa we jibu kishwahili tu na hao wanaokuaji wataweka subtitle tu.
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,462
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Tuna dini mbili..........lugha mbili....serikali mbili.......:lol::eyebrows::embarassed2:
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Waingereza lazima watakuwa wanajivuna sana! Na hata wakituona sisi duni wanastahili kabisa kutuona hivyo.
   
 13. m

  mtafungwa Member

  #13
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli. Unajua lugha ni ufunguo wa utambuzi na maarifa. Ukiijua vizuri na kuitumia vizuri utafikiri kwa ufasaha, utapanga mambo kiufasaha, utajiangalia mwenyewe nafsini kwa ufanisi zaidi na kujikuza kiufahamu na kisaikolojia. Utayachambua mambo kisawasawa. Your mind becomes clearer. Maana yake ni kwamba unakuwa na power. Pia unakuwa ni mtu wa kujiamini. Waingereza wanajua sana suala hili. Ukijiamini ukatumia lugha yako kwa shughuli zako muhimu kama elimu kama wanavyofanya nchi nyingine huru, unakuwa na nguvu na mwingereza hawezi kukushika tena kwa kutumia lugha yake. Kwa ujumla unapotumia lugha ya watu wengine unakuwa si mtu wa kujiamini unapohsiana nao k.m kibiashara. Maana yake unakuwa huna power na inakuwa rahisi kutawalika na kubakia kuwa tegemezi siku zote. Kiingereza twaweza kujifunza kwani imekuwa pia lugha ya kimataifa...ila isitutawale. Tujikite zaidi kwenye Kiswahili na tukitumie kama ufunguo wetu wa kufungulia makabati ya ufahamu na maarifa. Pia tueneze Kiswahili kwa wengine pia duniani na tujivune nacho hasa.
   
 14. m

  m'monga JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Rugha ndio nguvu ya elimu nchi Zetu za Africa bado hazija pata uhuru wa serekali kujiendesha zenyewe ndiomana Rugha Zetu zimegandamizwa Rugha ni utawala na ki ukweli bado tuna tawaliwa na nchi za ulaya na marekani(wazungu)kuna rugha ya Afrikanse south Africa ina tumika kwa sector zote na elimu yoyote ya juu kwa sababu
  Niya wazungu.Afrikanse ina mchanganiko wa English,France,PortUguese,Dutch,.kikubwa ni serekali zetu ziwe huru ki uchumi na sheria ndio tutafanikiwa kutumiya rugha zetu Za Africa kwa elimu ya juu
   
 15. m

  mtafungwa Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya yote ni kweli. Nina mfano mmoja kuhusiana na hicho ulichokisema. Miaka ya nyuma nchi ya Finland ilitawaliwa kwa karne zaidi ya nne na waswidi, halafu tena kwa karibu karne moja ilitawaliwa na warusi. Walirithi kiswidi na kwa kiasi fulani, kirusi, yakiwa ni matokeo ya kutawaliwa. Lakini walipopata uhuru wao mwaka 1917 waliamua kuachana na lugha hizo na kuiendeleza lugha yao ambayo ilikuwa imedharauliwa na wakoloni. They were very serious. Waliendeleza lugha yao licha ya kudharauliwa, kwa sababu walitaka kuwa huru kweli kweli ili waiendeleze nchi yao pasipo miingiliano mingi toka kwa watawala wao. Leo hii lugha ya kifini ni moja kati ya lugha zinazoheshimika sana ulimwenguni. Ingawa lugha ya kiswidi ipo, inazungumzwa na watu wachache sana (asilimia tano hivi). Lugha inayotawala ni kifini. Finland imeendelezwa na wafini wenyewe hadi kufikia hatua za kushangaza dunia. Hutasikia mfini akijiita mzungu, hata lugha yao haina uhusiano na lugha kama kiingereza, kifaransa, kispanish, kirusi, nk. It is unique, somewhat, sounding like an african language. Mtanzania, wewe amua kuikuza na kuitumia lugha yako ya kiswahili katika maendeleo yako ya kila siku halafu utaona nchi inavyopaa kimaendeleo. Uelewa utaongezeka haraka, ubunifu wa mambo ya kisayansi, kiteknolojia, nk. utaongezeka kwa kasi kubwa, hali ya kujiamini itaongezeka sana, wengine duniani wataishangaa Tanzania jinsi inavyopaa kimaendeleo. Tumia lugha za kigeni kwa ajili ya mawasiliano nao tu, vinginevyo, tumia lugha yako. jifunze lugha mbalimbali za kimataifa ili kujua kinachoendelea duniani na kuwasiliana na watu duniani, lakini tumia lugha yako ukiwa ndani ya nchi yako na katika shughuli zako za ndania. Wageni uwafundishe Kiswahili ili waongee Kiswahili wanapokuwa nchini kwako. Eneza lugha yako mahali popote duniani ili lugha hii ifahamike na wengi. Unajua Kiswahili kinapendwa sana na watu wa nje kuliko wenye mali yao? Hii ni aibu kubwa. Nawasilisha.
   
 16. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Usemayo si kweli kabisaa. Kwa mfano kuna mataifa kibao ya ulaya ambayo hayatumii kiingereza kama lugha ya kwanza na bado yameendelea. Wadenish, wafaransa, wajerumani, wafinish, waspenish n.k. Vile vile ukiangalia wachina, wajapan hata wakorea kiingereza chao ni taabu sana lakini wameendelea. Hii kasumba ya kuabudu kiingereza ni kwa sababu tulitawaliwa na hao kwa hiyo bado haijatutoka. Sawa, ufahamu wa kiingereza ni vizuri lakini kusema eti kama hujui kiingereza chimba shimo jifukie, hapo unavuka mipaka!
   
 17. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Aisee m'monga ingawa nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja, hebu niruhusu kusahihisha maneno flani katika mchango wako:

  1. rugha = lugha
  2. serekali = serikali
  3. ndiomana = ndio maana
  4. rugha ya Afrikanse = lugha ya Afrikaans
  5. mchanganiko = mchanganyiko
  6. kutumiya = kutumia

  Mshairi Shaaban Robert katika shairi lake maarufu la Titi la Mama aliandika ifuatavyo:

  Titi la mama li tamu
  Hata likiwa la mbwa
  Kiswahili naazimu
  Sifayo iliyofumbwa
  Na kwa wasio kufahamu
  Niimbe ilivyo kubwa
  Toka kama mlizamu
  Funika palipozibwa

  Lugha yangu ya utoto
  Hadi sasa nimekua
  Tangu ulimi mzito
  Na sasa kusema najua
  Ni sawa na manukato
  Moyoni mwangu na pua
  Pori bahari na mto
  Napita nikitumia

  Titile mama li tamu
  Jingine haliishi hamu.


  Shaaban Bin Robert (1 January 1909 – 22 June 1962)
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2012
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ni uchaguzi wako ndugu muuliza swali.
  Una hiari kukataa kutumia hiyo lugha na kung'ang'ana na kiswahili.
  Hebu komaa na kiswahili tu halafu uje hapa utupe matokeo.
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwi kwi kwi, teh teh teh.
   
 20. m

  mtafungwa Member

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  If you're a government or some sort of supreme leader, one way to sustain power is to control your people's minds by controlling the education you make available to them. To control that education, do so by controlling the language used in providing education. A country full of ignorant and confused people is easier to govern than one with a population that is fully aware of what the government is up to. Sorry! This is supposed to be top secret.
   
Loading...