Kiswahili kuthaminiwa kwako ndiyo uhuru wetu

huria

Member
Dec 11, 2018
27
79
Jikite kwenye dhana ambayo inajieleza hapo juu
Hakuna ukoloni mbaya kama ukoloni wa ki-utamaduni.

Tunajiita watanzania na lugha yetu ya taifa ni kiswahili, ni lugha ambayo imewaunganisha watanzania na kujiona wamoja

Halafu ...

Tunategemea lugha za nchi nyingine hasa (kiingereza) kama lugha ambayo inatuvusha kwenye nchi ya ahadi.

Kwenye elimu.

Maada ambazo leo nyingi zinafundisha shule ya msingi hata kwenye masomo ya sayansi zimeshushwa kutoka sekondari na walimu hao hao ambao walifeli kuyasoma kwa kiingereza ndio hao hao wanawafundisha wanafunzi hao kwa kutumia lugha ya kiswahili na matokeo yanaonekana kuliko huko sekondari.

Nini kifanyike...
1. Kwanza kabisa masomo ya sekondari kama vile somo la biology, chemistry, na fizikia yafundishwe kuanzia darasa la tatu tena kwa lugha ya kiswahili kama linavyofundishwa somo la sayansi na teknolojia.

2. Shule zote zitumie lugha ya kiswahili hadi vyuo vikuu, lugha ya kiingereza au kiarabu au kifaransa au kichina zifundishwe kama somo tu la lugha.

3. Taaluma zote nchi zikiwemo mahakama,vyuo vikuu,mikataba ya kitaifa na kimataifa, makongamano ya kitaifa na kimataifa ambayo yanafanyika nchini kwa maslahi ya watanzania lazima yafanyike kwa lugha ya kiswahili.

3. Lugha za kigeni zipigwe marufuku kutumika kama yanagusa maslahi ya umma.

4. Masomo ya sekondari yafanane na masomo ya shule ya msingi, mwanafunzi wa darasa la tatu ajue maana na misingi ya fizikia, chemia au biolojia tangia akiwa mdogo ili kuweza kujenga msingi sahihi kwa masomo hayo ya sayansi.

5. Masomo hayo watayasoma tokea darasa la tatu hadi kidato cha pili ambapo mwanafunzi atafanya maamuzi wakati anaingia kidato cha tatu kuchagua mchepuo ambao yeye anaupenda.

6. Vyombo vya habari kama vile magazeti, redio, runinga, vipeperushi, kutumia lugha fasaha ya kiswahili ikiwemo misamiati sahihi bila kuingiza maneno kutoka mitaani.(sheria iwepo).

7. Tufundishe watoto wetu ambo ndio kizazi cha kesho kupenda vya nyumbani.

Tuanze kwanza kwa kuipenda lugha yetu baadae tutajenga uzalendo kwa wananchi kupenda vya nyumbani
 
Back
Top Bottom