Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?

You want me to trust myself?? What a joke pal? Its not obligatory to agree with me.....let us agree to disagree over this!

If you don't want to trust yourself, how could I trust you? You've got to transform Africa into something more than USA in terms of everything...another joke?
 
Kwani mzee wa kumanufactures more teachers na lwaiganani mzee wa children don't listen their teachers because of hungry wansemaje katika hili?
 
If you don't want to trust yourself, how could I trust you? You've got to transform Africa into something more than USA in terms of everything...another joke?
This aint no a joke but something fussy and capricious! If i wil think like you then none of us will be thinking!
 
Nani alikwambia tunataka tuachane na Kiingereza? wewe usiyetaka kukijuwa achana nacho, wengine ndio kwanza tunajifunza lugha za tano na sita.
 
Nani alikwambia tunataka tuachane na Kiingereza? wewe usiyetaka kukijuwa achana nacho, wengine ndio kwanza tunajifunza lugha za tano na sita.
Teh teh teh...wel said mkuu! Also if he/she cant stand the heat let him be out of the kitchen!!
 
This aint no a joke but something fussy and capricious! If i wil think like you then none of us will be thinking!

Ok. but sorry if I've hurt you. I didn't mean it. Let's get back to the real issue, if you still wish. I'll try to behave this time.
 
Kiswahili katika masomo ya sayansi bado hakina maneno ya kutosha ... mfano katika baologia kuna kitu "NEGATIVE FEED BACK MECHANISMS & POSITIVE FEED BACK MECHANISMS " utayasema vipi kwa kiswahili...

Nchi yetu ni changa tunahitaji kujifunza kiingereza ili kujua mambo ya kimaendeleo wenzetu waliyo yaficha ndani ya lugha zao
 
Nani alikwambia tunataka tuachane na Kiingereza? wewe usiyetaka kukijuwa achana nacho, wengine ndio kwanza tunajifunza lugha za tano na sita.

ha ha haaa h hu huuu! Weye kazi yako kuchochea mambo tu...wala huchangii hoja...kumbe wee mjanja kiasi hicho! Hebu niandikie kaparagraph kamoja tu kwa king'eng'e halafu ndio tujue kwelikweli kwamba eh mwenzetu kakumbatia king'eng'e wala haachani nacho...yeye na hicho kinanihii ni pete na kidole jamani...ah! Dunia hii...sijui tutafika...
 
Kiswahili katika masomo ya sayansi bado hakina maneno ya kutosha ... mfano katika baologia kuna kitu "NEGATIVE FEED BACK MECHANISMS & POSITIVE FEED BACK MECHANISMS " utayasema vipi kwa kiswahili...

Nchi yetu ni changa tunahitaji kujifunza kiingereza ili kujua mambo ya kimaendeleo wenzetu waliyo yaficha ndani ya lugha zao

Kuhusu hayo maneno, lazima tafsiri yake kwa kiswahili ipo...ukipata muda jaribu kawaone Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) pale mlimani chuo kikuu cha Dar es Salaam. Ni kweli. Lugha za kigeni zinaweza kuficha maneno fulani ya kitaaluma. Lakini taasisi kama TATAKI ina jukumu la kuyatafuta maneno hayo na kutafsiri kwa lugha ya kiswahili na kueneza kwa watumiaji.

Kwa vile maneno mengi ya kitaalam aidha yamefichwa kwenye kiingereza au lugha za zamani kama kilatini na kigiriki, basi umuhimu wa kuyajua hayo upo kabisa, na kuyatafsiri maneno hayo ndiyo jambo linalotakiwa kufanywa na ni jambo la kawaida duniani. Kwa mfano nchi zote za ulaya isipokuwa waingereza zinatumia lugha zao. Hata waingereza wanatumia kiingereza ambayo ni lugha yao. Kwa hiyo katika kila nchi kuna taasisi kama TATAKI ambazo hutafsiri maneno ya kitaaluma toka kiingereza kwenda kwenye lugha zao. Kwa mfano pale Finland utasikia maneno kama kommunikaatio (communication), biologia (biology), kemia (chemistry), filosofia (philosophy) nk. na hutamkwa jinsi yanavyoandikwa. Maneno haya si ya kifini kwa asili ila yametafsiriwa toka kiingereza na lugha za zamani. Wafini wapo makini sana na suala hili la lugha...likitokea neno geni mara moja wataalam wanakaa kikao kujadili jinsi ya kulitafsiri kwenda kifini na kusambaza "innovation" hiyo haraka kwa watumiaji. Kwa hiyo kilichofichama ktk lugha nyingine hufichuliwa kwa namna hiyo.

Halafu pia Tanzania ni ya zamani kuliko, kwa mfano marekani (ukiondoa uwepo wa wahindi wekundu)...nafikiri marekani wana umri kama miaka miambili hivi...sisi na kiswahili chetu tumekuwepo toka zamani sana. Nasikia karne ya pili waarabu waliofika ukanda wetu walifundishwa kiswahili na wenyeji wa pwani. karne ya nane ndiyo kabisaa kiswahili kilikuwa kimekuwa zaidi kwa sababu ya uhusiano wa kibiashara na waarabu hasa wa persia. Ni kweli Tanzania kama taifa la kisasa bado changa lakini watu wenyewe ni wakongwe sana. Kwa hiyo hoja ya uchanga kilugha siikubali.

Mwisho, kujifunza kiingereza ni lazima kwa kila msomi na ni muhimu kwa mwananchi wa kawaida. Ikiwezekana tujifunze hata lugha nyingine za kimataifa kama kichina au kiarabu. Lakini ninachoona ni kitu muhimu sana ni matumizi ya lugha yetu katika mafunzo na elimu ktk ngazi zote za elimu...yaani, kwa mfano, tujifunze baiolojia kwa kiswahili toka ngazi ya msingi hadi chuo kikuu, huku tukijifunza lugha za kigeni kama masomo ya lazima toka msingi hadi sekondari au vyuo kabisa. Kwa maneno mengine, tufanye kama wenzetu wajerumani, wafaransa, waswidi, wafini, wadanish, waisrael, na wengineo wengi wanavyofanya. Kwa kufanya hivyo, kasi ya uelewa itaongezeka na ujuzi wa lugha za kigeni utaongezeka maana wanaofundisha lugha hizo watatakiwa kuwa na taaluma ya kutosha ktk lugha hizo.
 
Lugha ya kiswahili,huko mitaani,inakua kwa kasi sana lakini katika kilinge cha Elimu sidhani kama inakua wa kasi hiyohiyo.

Si kweli kwamba Lugha ya kiswahili imekua kiasi cha kuweza kufaa kuwa lugha ya kufundishia sekondari na vyuo vikuu, hata kama kuna anaye amini imekua kiasi hicho vitabu viko wapi?

Sijaona mwalimu akifundisha Biology chemistry au physics kwa kiswahili.

Hesabu ya Culculas,linear algebra au Differential equation itafundishwa vipi kwa kiswahili? Msamiati upo??

Neno base, coefficient au hata constant kiswahili ni nini?

Ili Kiswahili kiweze kutumika darasani hadi evel ya University zinahitajika juhudi za makusudi kama kuchukua msamiati toka Kilatini kihindi na Kiarabu.
Maneno karibu yote ya English asili yake ni Kilatini na baadhi ni ya Kiarabu na kihindi.

English pamoja na lugha kadhaa Ulaya ni lugha asilia zenye uwezo wa kuelezea kwa ufasaha ujanja karibu wote uliopo hapa duniani.

Ila kama tunataka tu kuwa na elimu ya kibabaishaji na pengine ya mahudhurio ni kweli tunaweza anza fundisha kwa kutumia kiswahili hadi University.

Tatizo kubwa ni; Watu wengi Tanzania wanadhani wakipewa mtihani wa kiswahili watapata 100%. Ukweli ni kwamba kiswahili kama lugha ni ngumu kujifunza na kuongea kwa ufasaha.

Awali ya yote napenda kuwasalimuni ninyi nyote katika jukwaa hili.

Lugha ya kiingereza ni ngumu kwa wengi wetu lakini bado serikali inasisitiza kwamba iendelee kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Wakati huohuo lugha ya Kiswahili imekukuwa/kuzwa na kufikia kiwango ambacho kinafaa na kutosha kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Kwa nini tusiachane na kiingereza na badala yake tutumie Kiswahili chetu ktk taasisi zetu za elimu? Kwa nini lugha ya kiingereza isibaki tu kama somo la kawaida mashuleni na vyuoni? Maoni yenu tafadhali.

Shukrani za awali.
 
One language dies in every 14 days.

Last edited by a moderator:

Kiswahili ni kigumu kwa sababu hakijaanza kupewa uzito unaostahili. Serikali haijaanza kufanya hivyo. Walimu shuleni hawajaandaliwa kufundisha kwa kiswahili hayo masomo ya science kwa sababu hawajawezeshwa kufanya hivyo...ni jambo la kisera na mwamko. Ndiyo maana tunalijadili hapa. Tunataka serikali itambue umuhimu wa lugha hii na ianze kujenga mazingira yanayohitajika.

Pia napinga kwamba kiingereza na lugha nyingine ulaya ni lugha asilia...lugha hizo zinahistoria ndefu ya ukuaji...historia yake inaanzia hapahapa africa...hata taaluma ya kuandika ilianza africa (e.g., Nubia ambayo sasa ni Sudan). Wazungu wa kale walipata maarifa mbalimbali kuhusiana na lugha na taaluma nyingine toka kwetu...(soma "the Black Athena" na vitabu vingine vya historia ya ulimwengu). Kwa ujumla asili ya taaluma zote zilizopo duniani ni africa. Hata ushirikina ulianzia kwetu.

Kwa mfano historia inatuambia kwamba watu walishaanza kutumia hisabati ktk maisha yao zaidi ya miaka 30 000 iliyopita huko maeneo ya Kongo na kusini mwa afrika. Wazungu na waarabu wameendeleza tu na kuzifanya taaluma zile ziwe za kisasa na bora zaidi.

Huyu hapa pia anakubaliana na mimi hasa kuhusu eneo la sahara:

"African literacy began in the Sahara over 5000 years ago (Winters 1971, 1981a,1983). This earliest form of writing was a syllabic system that included hundreds of phonetic signs, which over time was shortened to between 22 and 30 key signs. This civilization was later spread to the rest of the world, including the Arab and European worlds"
Pia soma hii text

"The original inhabitants of the Sahara were not Berbers or Indo-Europeans (Winters 1985b). This was the ancient homeland of black African people (Anselin 1989, p.16, 1992; Winters 1981,1985b,1989, 1991,1994). The inhabitants of this area lived and created innovations around and after 4000 B.C. We call these people the Proto-Saharans (Winters 1985b, 1991)".

Kwa hiyo ustaarabu wa wazungu umeanza juzijuzi tu. Msemo usemao "Usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe" una maana kubwa. Lakini ukijitambua umelala na umechoka kulala basi hunabudi kuanza kuamka.

Kwa kifupi maarifa mengi yamejificha kwenye lugha zetu za asili...na kwa sisi wenyewe na akili zetu, ila haujatambua vya kutosha...sawa ni vizuri kujua lugha nyingine ili uazime maarifa toka kwa wengine, lakini kumbuka kwamba chanzo cha maarifa ni ubunifu unaotokana na lugha unayoielewa sana...Hapo unaweza kuunda misingi mipya ya fizikia, kwa mfano, na kutunza ktk maandishi kwa kutumia lugha yako. Wengine wakitaka kujua ni lazima wajifunze kiswahili...that's how it started in europe.

Sasa unasema kiswahili kigumu, je kiingereza je? Kumbuka kwamba: Nasisitiza kwamba tujifunze lugha nyingine kama kiingereza tena kwa bidii...lakini jambo la msingi ni kuikubali na kuitumia kikamilifu lugha yetu ktk elimu. Jukumu la serikali nikuhakikisha kiswahili kinatumika kama lugha ya kufundishia. Mbona you can innovate using any language you know best...unaweza kubuni mashine hata kwa kutumia kimakonde. Wazungu wanabuni na kuhifadhi maarifa yao ktk lugha yao. Maana yake ni kwamba mimi naweza kufanya hivyo hivyo kwa kutumia lugha yangu...

Nakubali kabisa unaposema kwamba

"Ili Kiswahili kiweze kutumika darasani hadi evel ya University zinahitajika juhudi za makusudi kama kuchukua msamiati toka Kilatini kihindi na Kiarabu. Maneno karibu yote ya English asili yake ni Kilatini na baadhi ni ya Kiarabu na kihindi.
"

Na hivyo ndivyo wanavyofanya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) pale chuo kikuu cha Dar es Salaam. Tatizo ni kwamba support ya serikali ni haba hasa kisera na pesa.

Pia angalia video ambayo imekuwa posted na EMT hapo juu...kwa ujumla unaweza kupata taaluma ktk lugha yoyote unayomudu zaidi, si kiingereza tu.
 
Awali ya yote napenda kuwasalimuni ninyi nyote katika jukwaa hili.

Lugha ya kiingereza ni ngumu kwa wengi wetu lakini bado serikali inasisitiza kwamba iendelee kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Wakati huohuo lugha ya Kiswahili imekukuwa/kuzwa na kufikia kiwango ambacho kinafaa na kutosha kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Kwa nini tusiachane na kiingereza na badala yake tutumie Kiswahili chetu ktk taasisi zetu za elimu? Kwa nini lugha ya kiingereza isibaki tu kama somo la kawaida mashuleni na vyuoni? Maoni yenu tafadhali.

Shukrani za awali.
kweli hili linahitaji mjadala wa kina
 
Tusidanganyane!Tumechelewa,na hivyo,hatuna budi kujibidiisha katika lugha hii ya kigeni.

Sasa unaposema tumechelewa, nini kimetuchelewesha? Jibu lipo: Kilichotuchelewesha ni mambo mengi, moja wapo ni kutokuwa makini na sera yetu ya lugha ktk elimu yetu. Lakini tambua kwamba sera ya lugha ktk nchi yoyote ile huwa ndyo kiini (bila shaka kuna viini vingine...lakini tujikite kwenye hiki kwanza.Ndiyo maana hata upige kelele au ulalamike kwamba elimu imeshuka, kama hujazingatia kiini hiki cha lugha huwezi kufaulu, hata kama viini vingine viko sawasawa, yaani vitu kama kama ubora wa vitabu, walimu, mabweni, na uwekezaji zaidi kifedha. Lakini hivi navyo ni muhimu na ni lazima vifanywe. Lakini vifanywe kwa masharti kwamba kiini hiki cha sera ya lugha na utekelezaji wake murwa kimefanyiwa kazi...or else, tutabaki kuchelewa tu. Kiingereza kama lugha ya kufundishia imetufikisha hapa tulipo. Nimekutana na walimu kadhaa shule za sekondari na nimeshuhudia jinsi wanavyodharau kiingereza pamoja na watumiaji wa lugha hiyo...sababu ni kwamba wao (si wote) kiingereza kinawashinda...ukiingia huko darasani utashangaa kwa nini ulizaliwa, maana badala ya kujifunza mada, wanafunzi wengi wanachanganyikiwa. Kwani pia huwaoni wanafunzi wanavyoshindwa kuelewa masomo yao vyuo vikuu na badala yake wanakariri...ukiangalia karatasi za mitihani unaona hakuna cohesion...si wote lakini wengi wao wapo hapo...usipoelewa somo maana yake hujapata maarifa...hata kama unaweza kuandika makarasi kibao na kupata A kwa kumwaga yale uliyokariri. Language is an issue greater than the way it looks like. At the end of the day, you can't even write a letter to your pal, hata kama una shahada ya mlimani. Let's face it!

Tujitahidi kujifunza kiingereza na lugha nyingine za kimataifa kwani zinamanufaa kwetu na kwa wengine, lakini jambo la msingi ni kwamba elimu ya kiuhakika inaweza kufundishwa na ikaeleweka kwa kutumia lugha ambayo aidha inafahamika vizuri sana na wale wanaojifunza au wanaofundisha, au inawezekekana kujifunza lugha hiyo haraka sana na kuanza kuitumia ktk elimu. Lugha hiyo wala si kiingereza, bali ni Kiswahili. Watu wajifunze lugha nyingine za kigeni kwa ukamilifu wake wote lakini wapewe elimu kwa lugha yao ya kiswahili...Tukifanya hivyo, utaona jinsi kasi ya maendeleo katika nyanja zote (sayansi, teknolojia, sanaa, uvumbuzi, ubunifu, dini, maisha kwa ujumla) itakavyojitokeza...sababu ni kwamba hali ya kujiamini itaongezeka sambamba na kasi ya kujitambua, umakini ktk fikra utaongezeka...unajua watu wakishakumbatia lugha yao wataithamini maana wanaona manufaa yake...kinachofuata ni kueneza lugha hiyo nje ya nchi...there are lots of other psychological outcomes as well. Mtanzania atajisikia anajukumu kubwa la kueneza lugha yake na ustaarabu unaoambatana na lugha hiyo...atapenda wengine wafaidike na lugha hiyo kama yeye mwenyewe alivyofaidika nayo...act now and I promise, you'll never regret! Let the government and everyone take this issue seriously and liberate Tanzania.
 
One language dies in every 14 days.

Ahsante sana EMT kwa video yako. Inaelimisha vizuri...nakumbuka mwaka 2000 nilitakiwa kufanya mtihani wa TOEFL ili nikifaulu niweze kuruhusiwa kuendelea na masomo nje ya nchi...Ingawa nilifanya, nilijisikia kuwa walikuwa hawajaridhika na shahada yangu ya kwanza ambamo somo kuu (major subject) lilikuwa lugha za nje ikiwa ni pamoja na kiingereza. Sasa lazima ifike wakati ambapo mwanafunzi anayetaka kuja kusoma hapa Tanzania afanye na kufaulu mtihani maalum wa kiswahili ambao tutauita Mtihani wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni (MKILUKI) ambao utaweza kufanywa popote duniani ambako kiswahili ni lugha ya kigeni. Let's have that test please...Kwa hiyo lazima mwanafunzi huyo au mgeni anayetafuta fursa ya kazi Tanzania afanye na kufaulu MKILUKI.
 
Last edited by a moderator:
kila jambo linawakati wake, hivyo suala hili nalo litafika wakati watu hawataambiwa ila kwa vitendo vyao wataacha kukitumia hicho kiingereza.:bump2:
 
kila jambo linawakati wake, hivyo suala hili nalo litafika wakati watu hawataambiwa ila kwa vitendo vyao wataacha kukitumia hicho kiingereza.:bump2:

Ndugu yangu, kuna mambo ambayo hubadilika yenyewe kwa sababu ya nguvu ya wakati. Kwa mfano mabadiliko ya tabiajua. Lakini hili la lugha za duniani linahitaji sana nguvu ya mtu au taasisi--bila shaka wakati unaweza kuwa msindikizaji mzuri. Tukiuachia wakati uamue basi mabadiliko hayatatokea. Ni lazima sisi watanzania tutafakari, tuamue na tutekeleze, na hatimaye tuyafaidi matunda yake. Watanzania ni waafrika, lakini ni waafrika wa pekee sana (unique) duniani. Tunahitaji kuuimarisha upekee huu kwa njia ya kuimarisha na kutumia chombo muhimu hiki cha maendeleo na ustaarabu, yaani lugha yetu. Bila shaka hatuna budi pia kujifunza kwa bidii lugha nyinginezo. Hata hivyo, lugha ya kujifunzia ni lazima iwe ni lugha tunayoweza kujifunza haraka sana au ni lugha ambayo tunaimudu vizuri tayari--lugha hiyo si kiingereza wala kifaransa bali ni Kiswahili.
 
Anayesema tutakosa ajira katika soko la EA anakosea. Ajira zipo hapa hapa, na sisi kwa kile tunachokijua tukitumie kulinda ajira nchini, kwa mfano tukisema mtu toka nje hawezi kuajiriwa mpaka awe anafahamu kiswahili kwa usahihi kwa kuandika na kusoma, wangapi toka nje wataajiriwa hapa nchini? Halafu tujiulize ni watu wangapi hapa nchini wanatumia ligha za kigeni katika shughuli zao za kila siku?? Je ni watanzania wangapi wanafanya biashara zao na nchi nyingine??Tayari wenzetu wa Kongo, Burundi, Rwanda wanasisitiza kutumika kwa kiswahili ili waweze kufanya biashara zao kwa umakini kokote katika EA sie tunang'ang'ania Kiingereza.Hapa nilipo nimeshika dawa inaitwa MUCOLYN. Ndani kuna karatasi ya maelezo imeandikwa kwa Kiingereza na nadhani na Kifaransa. Dawa hii imetengenezwa na SHELYS PHARMACEUTICALS LTD DSM. nina imani soko kubwa la dawa hii liko hapa hapa Tanzania, najiuliza hizi lugha zilizotumika humu zimemlenga mtumiaji gani?? Ziko dawa toka China wameanza kuandika maelezo kwa Kiswahili wao wanajua mlengwa wao ni Mswahili. Sie tunag'ang'ania Kiingereza. Wakati huo huo Microsoft/Google wameingia katika matumizi ya Kiswahili sisi wenyewe ndio hao tunaotoa kipaumbele kenye Kiingereza. Tuendelee na mjadala lakini nadhani huu ni wakati mwafaka kutumia Kiswahili katika nyanja zote. Waanze viongozi wetu, utakuta Rais mzima katika dhifa ya kitaifa anaongea Kiingereza, kwa nini asitumie Kiswahili halafu awepo Mkalimani atafsiri? Kuna maana gani kutuonyesha shughuli hizo "live" hii ni aibu.
 
Mzeelapa, kweli inaelekea tumelala usingizi mkali...wanajaribu kutuamsha lakini wapi...tupo fofofo. Kwa kuongezea kidogo hayo uliyoyasema, waKongo wanapenda sana kusikiliza idhaa zetu za kiswahili. Pia wageni wengi wanaofika Tanzania, hata kwa utalii tu, wanatamani kujifunza Kiswahili haraka ili watumie lugha hiyo wakiwa hapa na pia wajisikie wapo ndani ya utamaduni mwingine. Hivyo, lazima ziwepo shule maalumu kwa ajili ya kuwafundisha wageni kiswahili pamoja na utamaduni wetu kabla hawajaanza kufanya kazi nchini. Wafanye mitihani na kufaulu na kupewa vyeti maalum vikiwa kama kigezo mojawapo kwa mgeni kuweza kufanya kazi...Kwa ujumla Mzeelapa, suala hili ni muhim sana maana, kama unavyosema, linahusisha mambo mengi, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa ajira zetu na shughuli za kibiashara....
 
Back
Top Bottom