Serikali, CCM na Polisi wanapaswa kujiuliza kwa nini wananchi wakiona askari polisi anashambuliwa hawatoi msaada?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Juzi hapa kulikuwa na tukia la askari Polisi mkuu wa kituo cha polisi Mwanakwerekwe, Zanzibar, akishambuliwa hadharani, na wananchi wakishangilia japo waliona askari alikuwa amezidiwa (angalia picha hapa chini).

1707285687407.png

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharib, amewalalamikia wananchi kwamba walishuhudia tukio hilo lakini hawakutoa msaada wowote, na hata wengine walishangilia kuona mkuu wa polisi huyo akipewa kipigo.

Sasa hili ni jambo la kufikirisha sana. Si mara ya kwanza kunapotokea polisi kuuwawa au kushambuliwa wananchi wanashangilia au kutoa kauli za kejeli zinazoonyesha hawasikitishwi na kufa au kushambuliwa kwa polisi.

Tunajua si kitendo cha uungwana kushangilia kifo cha binadamu, lakini ni CCM na Polisi wenyewe wamesababisha hili. Wamejitakia wenyewe. Ni ujumbe tosha kabisa kwa serikali kwamba wananchi hawawaoni tena askari kama wapo kwa jukumu la kuwatumikia wananchi, bali kuwatumikia "mabwana" wao wa utawala wa CCM dhidi ya wananchi.

Polisi siku zote wamekuwa wakifanya kazi kwa kujipendekeza kwa utawala wa CCM, bila kufuata miongozo ya kazi zao. Polisi hawafanyi kazi tena kwa mujibu wa kanuni za polisi bali kwa maagizo toka juu, hata wakijua kwamba hayo maagizo toka juu yanakiuka haki za wananchi. Imefikia mahali wananchi wanaona kuwa askari polisi ni namna fulani ya utumwa kwa serikali ya CCM, kama kupewa "limbwata" hivi na chama tawala. Polisi wamepewa jina la PoliCCM.

Tumeshuhudia mara nyingi sana hata wanapoagizwa kuwakamata watu wa vyama vya upinzani, polisi wengine huomba msamaha kwamba wameamriwa toka juu na wanafanya hivyo si kwa utashi wao au kwa kuwa kuna sheria zimevunjwa. Kuna tetesi polisi hata wameambiwa watunge kesi za uongo dhidi ya watu, kuwabambikia kesi, na wanafanya hivyo bila kusita.

Tumefikia mahali watu mitaani wanasema mie nikikuta polisi anashambuliwa na mnyama au watu siwezi kabisa kumsaidia, kwa sababu polisi nao wamekuwa kama wanyama. Wengine wanasema siwezi hata siku moja kumpangisha polisi nyumba yangu. Wengine wanasema mwanangu akichumbiwa na polisi namkana. Haya ndio yaliyotokea Zanzibari. Wananchi wamefikia kutukana na kuwaita Polisi mbwa wa CCM. Kwa nini?

Sasa polisi ifikie mahali mjiulize, huu ndio uhusiano mnaotaka kujenga na wananchi, wa kuchukiwa kiasi cha wananchi kushangilia vifo vyenu? Mnafikiri ni nini kimewafikisha wananchi mahali hapo?

Endeleeni kujipendekeza kwa utawala wa CCM, na kadiri mnavyofanya hivyo mjue mnazidi kuharibu uhusiano wenu na wananchi. Mambo huwa yanabadilika. Kuna siku hao mnaojipendekeza kwao hawatakuwapo na mtabaki na aibu na fedheha kubwa. Na fedheha hii wenzenu wanaipata hata sasa hivi pale wanapostaafu na kurudi mitaani kwa wananchi. Wanaona aibu hata kujumuika na watu wa kawaida.
 
Inakuwaje wafuasi wa mnyazimungu wakishangilia kuona mtu akipigwa? Ningetegemea kwa imani yao ya dini ya haki. Zanzibar ingekuwa ni sehemu ya mfano wa amani na upendo na ni sehemu salama pa kuishi😁😁😁😁😁😁
 
Inafikia mahali maudhi yanazidi na utu na hekima vinatoweka
 
Unapokuwa ni mwananchi, unakutana na vitu kama hivi, halafu baada ya muda fulani ukasikia kuna polisi amekufa, ni wazi utashangilia. Psychologically unachukulia kuwa polisi aliekufa ni mojawapo ya waliompiga huyu bwana

1707299543936.png
 
Mod wamebadili title yangu na kuondoa maneno kuhusu wananchi kushangilia wakisikia polisi amekufa. Kulikuwa hakuna haja ya kufanya hivyo kama JF ni platform tunapodiriki kuongea ukweli kama ulivyo. Mnaficha nini? Huo ndio ukweli. Hata humu ndani kuna threads zinazotoa taarifa kuhusu polisi kufa, baadhi ya wachangiaji huonyesha kufurahishwa na hayo matukio. Labda ndugu zao waliwahi kuuwawa mikononi mwa polisi
 
Juzi hapa kulikuwa na tukia la askari Polisi mkuu wa kituo cha polisi Mwanakwerekwe, Zanzibar, akishambuliwa hadharani, na wananchi wakishangilia japo waliona askari alikuwa amezidiwa (angalia picha hapa chini).

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharib, amewalalamikia wananchi kwamba walishuhudia tukio hilo lakini hawakutoa msaada wowote, na hata wengine walishangilia kuona mkuu wa polisi huyo akipewa kipigo.

Sasa hili ni jambo la kufikirisha sana. Si mara ya kwanza kunapotokea polisi kuuwawa au kushambuliwa wananchi wanashangilia au kutoa kauli za kejeli zinazoonyesha hawasikitishwi na kufa au kushambuliwa kwa polisi.

Tunajua si kitendo cha uungwana kushangilia kifo cha binadamu, lakini ni CCM na Polisi wenyewe wamesababisha hili. Wamejitakia wenyewe. Ni ujumbe tosha kabisa kwa serikali kwamba wananchi hawawaoni tena askari kama wapo kwa jukumu la kuwatumikia wananchi, bali kuwatumikia "mabwana" wao wa utawala wa CCM dhidi ya wananchi.

Polisi siku zote wamekuwa wakifanya kazi kwa kujipendekeza kwa utawala wa CCM, bila kufuata miongozo ya kazi zao. Polisi hawafanyi kazi tena kwa mujibu wa kanuni za polisi bali kwa maagizo toka juu, hata wakijua kwamba hayo maagizo toka juu yanakiuka haki za wananchi. Imefikia mahali wananchi wanaona kuwa askari polisi ni namna fulani ya utumwa kwa serikali ya CCM, kama kupewa "limbwata" hivi na chama tawala. Polisi wamepewa jina la PoliCCM.

Tumeshuhudia mara nyingi sana hata wanapoagizwa kuwakamata watu wa vyama vya upinzani, polisi wengine huomba msamaha kwamba wameamriwa toka juu na wanafanya hivyo si kwa utashi wao au kwa kuwa kuna sheria zimevunjwa. Kuna tetesi polisi hata wameambiwa watunge kesi za uongo dhidi ya watu, kuwabambikia kesi, na wanafanya hivyo bila kusita.

Tumefikia mahali watu mitaani wanasema mie nikikuta polisi anashambuliwa na mnyama au watu siwezi kabisa kumsaidia, kwa sababu polisi nao wamekuwa kama wanyama. Wengine wanasema siwezi hata siku moja kumpangisha polisi nyumba yangu. Wengine wanasema mwanangu akichumbiwa na polisi namkana. Haya ndio yaliyotokea Zanzibari. Wananchi wamefikia kutukana na kuwaita Polisi mbwa wa CCM. Kwa nini?

Sasa polisi ifikie mahali mjiulize, huu ndio uhusiano mnaotaka kujenga na wananchi, wa kuchukiwa kiasi cha wananchi kushangilia vifo vyenu? Mnafikiri ni nini kimewafikisha wananchi mahali hapo?

Endeleeni kujipendekeza kwa utawala wa CCM, na kadiri mnavyofanya hivyo mjue mnazidi kuharibu uhusiano wenu na wananchi. Mambo huwa yanabadilika. Kuna siku hao mnaojipendekeza kwao hawatakuwapo na mtabaki na aibu na fedheha kubwa. Na fedheha hii wenzenu wanaipata hata sasa hivi pale wanapostaafu na kurudi mitaani kwa wananchi. Wanaona aibu hata kujumuika na watu wa kawaida.
Jamaa alitaka na kubaka, mbona suruali ameteremsha adi boxer chafu linaonekana?

Na pembeni yao kuna vimiminika vya rangi ya hudhurungi, je jamaa alijikojolea?
 
Huenda ikawa. Nikimwangalia huyo polisi yupo kwa namna ambayo amekata tamaa kabisa ya kuishi. Na jamaa angekuwa na kitu cha ncha kali huyo polisi angekuwa six feet under sasa hivi.
 
πŸ˜‰πŸ™‚πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
Polisi bila uniform ni waoga sana, usiwaone hivyo. Wana nguvu wakiwa pamoja na wakiwa na uniform. Kuna mmoja nilimwambia ukweli. Mie ni Mtanzania na naiheshimu sana uniform yako. Sasa kama wewe ni mwanaume kweli njoo siku moja bila hiyo uniform tukutane kama raia nikuonyeshe kazi. Nakupa wiki mbili za kujiandaa, kula na mayai kabisa, halafu njoo nikuonyeshe kazi! Aliishia kujisemesha semesha tu.
 
Juzi hapa kulikuwa na tukia la askari Polisi mkuu wa kituo cha polisi Mwanakwerekwe, Zanzibar, akishambuliwa hadharani, na wananchi wakishangilia japo waliona askari alikuwa amezidiwa (angalia picha hapa chini).

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharib, amewalalamikia wananchi kwamba walishuhudia tukio hilo lakini hawakutoa msaada wowote, na hata wengine walishangilia kuona mkuu wa polisi huyo akipewa kipigo.

Sasa hili ni jambo la kufikirisha sana. Si mara ya kwanza kunapotokea polisi kuuwawa au kushambuliwa wananchi wanashangilia au kutoa kauli za kejeli zinazoonyesha hawasikitishwi na kufa au kushambuliwa kwa polisi.

Tunajua si kitendo cha uungwana kushangilia kifo cha binadamu, lakini ni CCM na Polisi wenyewe wamesababisha hili. Wamejitakia wenyewe. Ni ujumbe tosha kabisa kwa serikali kwamba wananchi hawawaoni tena askari kama wapo kwa jukumu la kuwatumikia wananchi, bali kuwatumikia "mabwana" wao wa utawala wa CCM dhidi ya wananchi.

Polisi siku zote wamekuwa wakifanya kazi kwa kujipendekeza kwa utawala wa CCM, bila kufuata miongozo ya kazi zao. Polisi hawafanyi kazi tena kwa mujibu wa kanuni za polisi bali kwa maagizo toka juu, hata wakijua kwamba hayo maagizo toka juu yanakiuka haki za wananchi. Imefikia mahali wananchi wanaona kuwa askari polisi ni namna fulani ya utumwa kwa serikali ya CCM, kama kupewa "limbwata" hivi na chama tawala. Polisi wamepewa jina la PoliCCM.

Tumeshuhudia mara nyingi sana hata wanapoagizwa kuwakamata watu wa vyama vya upinzani, polisi wengine huomba msamaha kwamba wameamriwa toka juu na wanafanya hivyo si kwa utashi wao au kwa kuwa kuna sheria zimevunjwa. Kuna tetesi polisi hata wameambiwa watunge kesi za uongo dhidi ya watu, kuwabambikia kesi, na wanafanya hivyo bila kusita.

Tumefikia mahali watu mitaani wanasema mie nikikuta polisi anashambuliwa na mnyama au watu siwezi kabisa kumsaidia, kwa sababu polisi nao wamekuwa kama wanyama. Wengine wanasema siwezi hata siku moja kumpangisha polisi nyumba yangu. Wengine wanasema mwanangu akichumbiwa na polisi namkana. Haya ndio yaliyotokea Zanzibari. Wananchi wamefikia kutukana na kuwaita Polisi mbwa wa CCM. Kwa nini?

Sasa polisi ifikie mahali mjiulize, huu ndio uhusiano mnaotaka kujenga na wananchi, wa kuchukiwa kiasi cha wananchi kushangilia vifo vyenu? Mnafikiri ni nini kimewafikisha wananchi mahali hapo?

Endeleeni kujipendekeza kwa utawala wa CCM, na kadiri mnavyofanya hivyo mjue mnazidi kuharibu uhusiano wenu na wananchi. Mambo huwa yanabadilika. Kuna siku hao mnaojipendekeza kwao hawatakuwapo na mtabaki na aibu na fedheha kubwa. Na fedheha hii wenzenu wanaipata hata sasa hivi pale wanapostaafu na kurudi mitaani kwa wananchi. Wanaona aibu hata kujumuika na watu wa kawaida.
Wanatakiwa kusaidiwa na waliofaidika na wizi wao wa kura
 
Hao vilaza na wapumbavu walio pata zero kidato Cha Nne hakuna wanalo jua,zaidi ya kutumia nguvu hata sehemu ya kutumia akili.

Police ndo majambazi na wanyang'anyi wakubwa.
 
Fideo ipo wapi namimi nishangilie πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hao vilaza na wapumbavu walio pata zero kidato Cha Nne hakuna wanalo jua,zaidi ya kutumia nguvu hata sehemu ya kutumia akili.

Police ndo majambazi na wanyang'anyi wakubwa.
Ila sasa, utaona hata hao viongozi wa Polisi ambao unakuta wana degree za sheria, ukiangalia mambo wanayofanya au kusema ni kama hawana kitu kichwani. Kuna wakati mie nilidokeza kwamba huenda ile harufu mbaya vituo vya polisi inaharibu uwezo wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom