Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
Hiyo redio ifungwe mara moja. Yakitokea yale ya Rwanda itabidi wenye redio wapelekwe ICC
Hiyo redio haiwezi kufungwa kwa sababu ina baraka za serikali iliyo madarakani na ccm kwa ajili ya malengo binafsi ya muda mfupi. Hata hivyo watambue kabisa kwamba mwisho wake kutakuwa na majuto makubwa sana.
 
Kwa iyo Mr.Green guard inabidi husiadhimishe sherehe ya kumbukumbu ya baba wa taifa bali anzisheni siku yenu maalumu ya kumuenzi mama wa taifa (Bibi Titi Mohamed) kama hao jamaa wa Radio Iman wanavyoshauri.

Mr Daudi Masaburi.
Hakuna mama wa taifa wala baba wa taifa
 
Sitajaribu na wala sitafanya makosa kusikiliza hii radio,ni kati ya radio za ajabu sijapata ona.........Uislamu ni dini moja safi sana,ila kuna watu wachache au taasisi chache wanaitumia vibaya including Bakwata,CCM na Radio kama hizi...

ka ukijua mkuu kuna bakwacha na bakwata sasa basi wanaopindisha uislamu na kuingia kwenye siasa ni bakwacha na sio bakwata..
 
Hawa wanaosema waislam ndio waliopigania huru leo wanaweza kutudhiilishia kama Tanganyika iliwai kuwa nchi ya Kiislam?Watu walishiriki kama watu wa Tanganyika wazalendo na siyo waislam.

Hilo ndilo la msingi, sidhani kama Uislam ndio uliwafanya waingie katika harakati za ukombozi. Ni UZALENDO wa kutaka UHURU wa MTANGANYIKA.
 
kwan Nyerere ni nani? ndo Mungu wenu Watanzania? Mnamuenz kwa nana gan? ndo maana mnapata malaana kwa kuenzi na kusujudia Mifupa. yeye ndo chanzo chawa washenzi waliopo madarakani. Nyerere amewaacìa nini had mnajidai kumkumbuka sana? Muogopeni Mungu nyie watanganyika.

Wewe unaeneza chuki na ubaguzi unapaswa kumuogopa nani?
 
yale yale ya kale. tuna kazi kweli kama dini ndiyo kigezo cha mawazo yenye mantiki basi tumetawaliwa hadi ndani ya viini vya fikra zetu. Waarabu walioleta dini kwa kunyanyasa na kuwafanya waafrika watumwa leo ndiyo mabwana wakubwa katika kuharibu asili yetu kwa dini yao? wakoloni walioleta ukristo kwa kutunyanyasa na kututumikisha na kutuibia raslimali zetu leo twawapigia magoti kwa kivuli cha dini yao. HIVI TUMELOGWA. tunaacha kujadili mfumuko wa bei unafanya maisha kuwa magumu kwa watanzania, tunajadili udini? tunahoji uhuru kwa dini? Kama tunataka MAMA wa Taifa, tulete mjadala wa babu wa taifa, bibi wa taifa, kaka wa taifa, dada wa taifa, shangazi wa taifa, mjomba wa taifa; the list is endless. Kuna mantiki hapo. Tuzungumze hatima ya Tanzania na siyo mijadala ya ulinganifu wa hovyo wa ubora wa waislamu na wakristo kwa Tanzania. BABA wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliliona hilo mapema akasema kwa sauti kubwa SERIKALI YA TANZANIA HAINA DINI. Leo kuna wajinga wachache wanataka kuturudisha kwenye udini. Mungu awatoe katika uso wa TANZANIA WOTE WENYE MITIZAMO YA KIDINI YENYE LENGO LA KULIGAWA TAIFA LA KIPEKEE DUNIANI-TANZANIA
 
Eti uhuru uliletwa na waislamu, wamesahau kwamba walianzisha AMNUT ili uhuru uchelewe mpaka wapate elimu
 
why always this radio think negative..what was the mission and vission of this radio?
 
Hawa radio imani ni wa chochezi sana.radio hii isipofungwa au kupewa onyo kali itavuruga nchi hii.
 
Serikali iwaangalie sn, hawa jamaa wanasema kwa kwa muislamu kumuenzi nyerere ni haramu

Kama Redio Imani na wachangiaji wao wanapaswa kuangaliwa basi JF na wachangiaji wana magwanda ndio wanaopaswa kuangaliwa na kuchungwa zaidi endapo taifa hili tungependa lisiingie matatani!!
 
Ni kweli hao jamaa wa radio iman wanachosema ni kweli kabisa.
Nyerere akuleta uhuru Tanzania

Mie nnachowashauri waislamu wenzangu ni kuwa tujitahidi sana kusoma shule, na katika kusoma huko tuanze kwanza na elimu za msingi, sekondari na kisa chuo, tusianze na chuo tukiwa bado watoto tukikua tutakuwa na gap kubwa sana ya uelewa.
 
Kuna mdaharo unaendelea kwenye hii radio wao wanasema uhuru wa tz uliletwa na waislamu na si nyerere, wanadai haina maana ya kumbuka mwalimu wakati historia imepotoshwa, wanasema nyerere alijikita ktk kujenga makanisa na sio misikiti, wanauliza kwa ni kuna baba wa taifa hakuna mama wa taifa? Wanasema labda kwa vile ni mwislamu bibi titi mohamed. Mimi hii radio siielewi hembu wadau leteni maoni yenu hapa, kama una redio wasikilize mada inaendelea.
Sasa wewe ndugu yangu inakuaje unatuletea vipindi vya madrasa kwenye JUKWAA LA SIASA???
 
Hii redio kama itaachwa iendelee kwa namna hii itaipeleka nchi pabaya sana,inaupotoshaji mkubwa sana, kama Serikali ilifanikiwa kuifungia HAKI ELIMU kwa kutoka katika misingi yake, ni kwanini isifanye hivyo kwa hii redio? Je kama redia za kikristo ambazo ni nyingi sana, zikiamua kujibu mapigo tutafika wapi? KEMEA UDINI, KEMEA MAFISADI.
 
Mie nnachowashauri waislamu wenzangu ni kuwa tujitahidi sana kusoma shule, na katika kusoma huko tuanze kwanza na elimu za msingi, sekondari na kisa chuo, tusianze na chuo tukiwa bado watoto tukikua tutakuwa na gap kubwa sana ya uelewa.

Ushauri mzuri!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom