econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 23,946
- 37,232
Selective prosecution ni Nini?
Ni hali ambapo mamlaka ya mashitaka, kama DPP, wanaamua kumshitaki mtu mmoja lakini wakaacha watu wengine waliotenda kosa hilo bila mashitaka. Kwa maneno mengine: sheria inatumika kwa kubagua watu, si kwa usawa kwa wote. Kwa maana nyingine wewe umechaguliwa kushitakiwa wakati wengine waliotenda kosa lile lile hawakushitakiwa.
Selective prosecution inakuja pale ambapo uamuzi wa kukushitaki ulitokana na sababu zisizofaa kisheria. Mfano: rangi yako, dini, kabila, maoni ya kisiasa, au kulipiza kisasi.
Kwa Tanzania serikali yetu imeonesha wazi kwamba imejikita kwenye selective prosecution , hasa kwenye makosa ya uchochezi.
Kwa mfano Kuna kauli mbaya na za kiuchochezi zinatolewa na viongozi wa CCM au wanachama wa CCM au mashabiki wa CCM ila hakuna hatua zinachukuliwa.
Kwa mfano, Kauli ya shehe Mawinda mnamo Julai 2025 ya kwamba Tundu Lissu afanyiwe chochote kwenye mwili wake. Kwa maana nyingine Shehe Mawinda akitaka Lissu auawe. Mpaka Leo hakuna chombo chochote kilichomhoji Wala kumfungulia kesi ya uchochezi. Sababu kubwa ni kwamba yeye ni shabiki wa CCM.
Kauli nyingine ni ya Kiongozi wa UVCCM bwana Faris Burhani alitoa kauli ya kwamba watu wanaoikosoa serikali mitandaoni wakipotea Polisi wasiwatafute. Hii kauli ni ya uchochezi mkubwa sana, ila hakuna hatua yoyote ya kimashtaka aliochukuliwa bwana Burhani.
Huko nyuma aliyekuwa Katibu mwenezi wa CCM Amos Makalla alitoa kauli ya kwamba michango ya CHADEMA ipo kwa ajili ya kueneza virusi vya ebola na corona, ila hakuna aliyemgusa.
Huko nyuma pia aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa bwana Kenani Kihongozi aliwahi kutoa kauli ya kwamba Zitto kabwe akirudi nchini auawe kabisa. Hakuna chombo cha serikali kilichomchukulia hatua baadala yake akapewa cheo cha ukuu wa wilaya kule Arusha.
Hivi karibuni ametokea shehe anaitwa mwaipopo yeye kadai kabisa kwamba ana kundi la mbwa mwitu ambalo lipo kwa ajili ya kudhibiti maandamano ya tarehe 7/7/2026. Shehe huyu Wala hajaguswa na mtu yeyote Wala kuhojiwa. Hii kauli ni mbaya sana na inaweza kuchochea fujo za kidini au kisiasa.
Nihitimishe kwa kusema ya kwamba, kama serikali imeamua kushughulika na kosa la uchochezi, basi ishughulike na wote sio kubagua nani ashtakiwe na nani asishtakiwe. Na kama inabagua, basi iseme wazi kwamba kosa la uchochezi ni kwa ajili ya wapinzani pekee ili ijulikane hadharani.