GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,646
- 109,031
Pamoja na huu Unyonge ( Umasikini ) wangu mkubwa na wa Kutukuka nilionao GENTAMYCINE kitu pekee ambacho namshukuru Mwenyezi Mungu ( Allah ) ni Kwanza Kunilinda Kiafya kwa Kutougua hovyo na Kubwa zaidi 'Kunibariki' na Damu ya Group O+ ambayo ni Kinga tosha Kwangu ( Kwetu ) katika kupata Changamoto mbalimbali za Kiafya.
Wanaonizunguka hadi Marafiki walianza kwa Kuugua sana Macho ila Mimi sikuugua. Kisha hao hao wanaonizuguka wakaanza tena Kuugua Mafua, Homa na Vifua hadi muda huu naandika huu Uzi lakini Mimi nipo vyema tu Kiafya hadi sasa Wananishangaa na kudhani Mimi ni Mchawi ( Kikagula ) wakati hata 'Kuroga' kwenyewe tu sijui.
Kama kawaida yangu GENTAMYCINE ya kupenda Kudadisi mambo ili Kujitajirisha zaidi Kimaarifa ikanilazimu niende Kuonana na Madaktari Bingwa Wawili Mmoja ni wa Hospitali ya Kimedani ( Kijeshi ) Mwenge na mwingine ni wa Hospitali ya Wazandiki ( Kinjagu ) Makumbusho ambapo Wote walinipa majibu yanayokaribiana Kimaelezo.
"GENTAMYCINE Kisayansi Watu wenye Damu ya Group O+ huwa hawaugui hovyo Magonjwa mbalimbali na hata kupata UKIMWI vile vile huwa ni ngumu kwani huwa ni Watu wenye Kinga Kali katika Miili yao halafu huwa siyo wengi hali inayopelekea hata Damu kuwa nadra kupatikana katika Benki zetu za Damu na hata ukiikuta huwa ni ya Gharama sana" walisema Madaktari Bingwa hawa.
Naomba ieleweke wazi hapa kuwa siyo kwamba nimeanzisha Uzi huu Kuwananga ( Kuwasiliba ) wale msio na Damu ya Group O+ au Kujivunia ( Kujimwambafai ) la hasha bali nimeandika hili ili kama Mwanadamu mwenye Imani ya Kiroho niweze kutoa Shukran zangu za dhati Kwake Baba Muumba kwa Kuniumba hivi kwani kwa huu Ufukara ( Umasikini ) wangu mkubwa na Ulionikomaa mpaka Kunizoea GENTAMYCINE najiuliza kama ningekuwa Naugua haya Magonjwa mbalimbali leo ningekuwaje au ningejitibu vipi wakati Hela sina au ningekuwa Mgeni wa nani kusudi niweze Kupona.
Ewe Mwenyezi Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo kupitia kwa Mwanao Yesu Kristo wa Nazareth Mimi GENTAMYCINE sina cha Kukupa au Kukurejeshea au Kukulipa kwa hizi Baraka na Neema zako za 'Kiafya' Kwangu ila nitaendelea Kulitaja Jina lako na Kukushukuru kila Uchao kwani unaniepusha na mengi ya Kidunia na Kikubwa nakuomba tu Usiniache bali endelea Kunikumbatia na Kunibariki zaidi niumalize mwaka huu 2021 salama na niingie mwaka 2022 nikiwa na Mafuriko ya Mafanikio na unifungulie Milango mingi ya Ustawi wa Maisha yangu Amina ( Amen )
Wenye Group O+ nyote Hongereni mno.