Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba usipokee Maombi ya Watanzania ulete Mvua, bali acha Kwanza tufe ili Akili zitukae sawa na tuache kuwa Mazuzu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,798
2,000
Yaani tunaharibu wenyewe Mazingira kwa Uzuzu wetu huku wengine tukikataa Kupanda Miti mingi au hata Kuitunza tu ili ije itusaidie kwa Kivuli, Upepo na hata Mvua leo tunataka Kumhangaisha Mwenyezi Mungu mwenye Majukumu Mamilioni kidogo dhidi ya Watu na Mataifa mbalimbali atusamehe na atushushie Mvua.

Mwenyezi Mungu tafadhali KEROZENE nakuomba endelea tu na Majukumu yako na kamwe usihangaike na Sisi Watanzania bali acha Kwanza tupukutike kwa Kufa kwa Joto Kali na Njaa inayokuja labda ndipo Aklli zitatukaa vyema na tutabadilika.

Haingii Akilini Mataifa yenye shida ya Mvua kwa mfano Israel na Visiwa vya Shelisheli wamejijengea Nidhamu nzuri ya Kutunza Mazingira na hata Kuyavuna Maji kisha Kuyatunza kwa Matumizi ya Kipindi cha Ukame ili yawasaidie katika Kilimo na Matumizi mengine Muhimu ila kwa Watanzania yenye Misimu ya Kutosha ya Mvua tukimbwela mbwela tu na hali ikiwa mbaya ndiyo tunajifanya Kumkumbuka na Kumkimbilia Mwenyezi Mungu kwa Msaada wake.

Huu ni Unafiki na Upuuzi usiovumilika!
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
12,096
2,000
Hata kama tutakuwa makini kushinda umakini wa kufanya kazi kwa mchwa na nyuki kufikia kupanda MITI kona zote ila mwanadamu haimpasi kuacha KUOMBA.

Na Mungu Mwenyezi hachoki kuombwa na kusifiwa.

Mungu Mwenyezi huombwa nyakati zote kwenye SHIDA NA RAHA.

#Yetzer ha-tov
 

Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,404
2,000
Hautayaona unayoyatarajia ikiwa maombi yako yatakubaliwa, kwani utapata ulichokiomba.

Walakini kuna nafasi ya kutubu na kugeuka. Tubu ugeuke sasa kabla haujachelewa.
 

St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,668
2,000
Huyu jamaa apewe like za kutosha, akikutana na baba Jessica alete habari kama malaika nao wanafurahia huko au la.

Lunatic
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom