Nikipewa Kusahihisha Mitihani ya Wanafunzi wa Darasa la Saba nchini Watakaofaulu ni Wawili tu Wengine Watafeli tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,865
Kwa jinsi Wanafunzi wa Shule za Msingi ( hasa Darasa la Saba ) walivyo na Nidhamu mbaya katika Jamii zetu huku Wengi wao wakiwa hawana Akili Vichwani huwa nashangaa kuona kila mwaka katika Kutangazwa kwa Matokeo yao Kitaifa Wanaofaulu ni Wote / 99.9%

Duniani kote haiwezekani sehemu ambayo inahusisha Ushindani ( tena kama huu wa Kitaaluma ) Wote mkafaulu vyema kwani Wapumbavu ( Wanaofeli ) lazima wawepo ili Kuonyesha utofauti wa Kiubinadamu.

Kuna aliyekuwa Mkuu Mmoja wa Majeshi nchini Tanzania ( Namhifadhi Jina ) huyu GENTAMYCINE nilimpenda baada ya Siku Moja Kukataa kwenda Kufunga Zoezi Moja la Kijeshi alipokuta Walionza Kozi walikuwa ni 300 na Waliohitimu nao walikuwa ni hao hao 300.

Aliwaambia tu Wakufunzi kuwa Wao ni Goi Goi na kwamba hiyo Kozi ilikuwa ni ya Kilele Mama na kwamba alichojua Yeye alitegemea kusikia katika hao Wahitimu wa Kijeshi 300 basi angalau hata angesikia 50 Walikufa kwa Mafunzo, 75 Walivunjika Viungo vyao mbalimbali na 25 wamekuwa Matahaira wa Kudumu na 150 tu ndiyo Wameiva Kijeshi na kuwa tayari Kuipigania na Kuilinda nchi dhidi ya Adui / Maadui.

Kila mwaka tunatangaziwa tu kuwa Wanafunzi wa Darasa la la Saba waliofanya Mitihani ni 200,000 halafu Matokeo yao yakitoka tunaambiwa Waliofaulu ni 199,999 ( 99% ) na kwamba aliyefeli ni Mmoja tu.

Elimu niliyoiheshimu na Kuipenda ya Tanzania ni ile yetu ya miaka ya 60, 70, 80 na kidogo 90 mwanzoni ambako Mzazi na Familia ikisikia Umefaulu Darasa la Saba hufurahia, humshukuru Mwenyezi Mungu na hata Kukufanyia Sherehe Kubwa kwani waliokuwa Wakifaulu walikuwa ni Vichwa Kweli ( Intelligent ) Kitaaluma na siyo Wasio na Akili ( Mazuzu ) Walioko sasa.

Nakumbuka baada ya Kufaulu Darasa la Saba miaka ya early 90 Marehemu Babu yangu ( yetu ) Mpendwa Mzaa Mama ( ambaye ndiyo alikuwa Mwafrika wa Kwanza chini ya Wakoloni Waingereza kuwa Mkufunzi wa iliyokuwa IDM Mkoani Morogoro ) Mimi na Mdogo wangu wa Damu hapa JamiiForums aitwae steveachi alipendelea Mjukuu wake 'Chautundu' na aliyenipenda balaa GENTAMYCINE nikasome Forest Hill Secondary Morogoro ( ambayo Kipindi hiko ) ndiyo ilikuwa Shule nzuri Kitaaluma kwa Elimu ya Upili ( Secondary ) na ilikuwa inagombewa na kila Mzazi na kupata hapo nafasi ilikuwa ni Mbinde kwani ilikuwa inapokea Vichwa tupu.

Nakumbuka tuliofanya Mtihani wa Kujiunga nayo ( kupata Nafasi Forrest Hill Secondary ) tulikuwa Jumla ya Wanafunzi Elfu Tatu ( 3000 ) na Waliokuwa Wakitakiwa walikuwa ni Wanafunzi 300 tu ambapo Matokeo yalipotoka GENTAMYCINE nikawa ni miongoni mwa Waliotusua ( Waliofaulu ) na nakumbuka Marehemu Babu na Bibi yangu walinipongeza hadi Kunichinjia Kuku Nyumbani Kwake ( Kwao ) Saba Saba Mkoani Morogoro huku Marehemu Mjomba wangu Mpendwa Ian akininunulia Zawadi ya Mpira kwani alikitambua mapema sana Kipaji changu kingine Tukuka nilichokuwa nacho cha Kucheza Mpira.

Kama tu 90% ya Wanafunzi wa Darasa la Saba wa miaka ya sasa akina GENTAMYCINE kutwa tunapishana nao katika Vilinge vya Kubeti, Maskani za Kuvuta Bangu, Wengine Majumbani mwao wakiwa ni Vibaka watupu kwa Wavulana huku Wasichana wao muda wote tu ni Kutumika na Wazazi wao ( hasa akina Mama ) kwa Kujiuza ( Miili yao ) kwa Kubanduliwa na Wababa au Vijana ili wapate Hela ya Ugali na Mboga kwa Siku huo muda wa Wao Kusoma kwa Bidii na Kufaulu vyema hivi kila mwaka wanautoa wapi?

Hongereni mno Serikali ya Tanzania chini ya CCM kwa Makusudi kabisa kuichezea iliyokuwa Elimu nzuri ya Tanzania Kipindi cha Nyerere, Mwinyi na Mkapa na sasa kuifanya iwe rahisi na nyepesi ili iweze Kutengeneza Kizazi cha Wapumbavu wengi na Kazi ya Kuwatawala na Kuwapeleka mtakavyo isiwe na Miba wala Magugu huku 99% ya Watoto wenu ( zenu ) wakisoma Shule za maana, wakipata Elimu ya uhakika ambayo itaendelea kuwafanya miaka ya baadae waje Kuwarithi Nyadhifa zenu ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) kama inavyoonekana sasa.

Na GENTAMYCINE nimeyaandika haya yote kwa Uchungu na Hisia Kali kwakuwa nami ni Mdau mkubwa wa Elimu na pia ni Mtafiti Huru ( wa Kujitegemea ) wa Masuala ya Kijamii na Masuala Mtambuka ya Kitaifa na Kidunia na nayaona mengi mno hivyo ukiona Naumia juu ya Jambo ( Suala ) fulani jua ( jueni ) namaanisha.

Hakuna Elimu kwa sasa Tanzania Ok?
 
Naungana na serekali kufungia matokeo baadhi ya shule serekali ipo sahihi kabisa uhuni wa shule za binafsi haukubaliki kabisa, maana haiwezekani ndani ya darasa moja, swali la kwanza wanafunzi wote wajaze B, swali la pili wanafunzi wote wajaze C swali la tatu darasa ZIMA wakose, swali la nne wanafunzi wote wapate, alkadhalika hivyo hivyo kwa maswali yote 25. This is evils.
 
Mentality uliyonayo ni ya zamani.Zama zimebadilika.Hata Jeshi mafunzo niyakisasa sio kuvunja tofali.Drones na akili ndio inaitajika Dunia ya Leo sio nguvu na ugumu.
Hata kama kisasa Mzee hakuna training ya kijeshi iliyo serious kabisa muanze 300 mmalize 300 utakuta unfit wapo, utakuta wenye nidhamu mbaya wapo, waliopoteza uhai wapo sawa sawa na huko katika elimu asilimia ya ufaulu ni 99.9 nenda kafanye tafiti uone vituko vyake kiukweli hatuko serious kabisa na elimu.
 
Kwa jinsi Wanafunzi wa Shule za Msingi ( hasa Darasa la Saba ) walivyo na Nidhamu mbaya katika Jamii zetu huku Wengi wao wakiwa hawana Akili Vichwani huwa nashangaa kuona kila mwaka katika Kutangazwa kwa Matokeo yao Kitaifa Wanaofaulu ni Wote / 99.9%
Nikweli kabisa unachosema ila pia kumbuka zamani hakukua na shule nyingi za secondary ukilinganisha na sasa,leo hii kila kata ina secondary na madarasa yanajengwa mengi tu je unafikiri kama wanafunzi watawekewa ufaulu kama ule wa zamani madarasa yatakaa wakina nani?
 
Katika hili nakuunga mkono mleta Uzi, leo saa mbovu imeonyesha majira sahihi.........haya matokeo yamekaa kisiasa zaidi bila kuwa na uhalisia,kuna utafiti mmoja nilihusika ni kweli hawa secondary ni mizigo kwa waalimu.

Genta ajengewe sanamu Wizara ya Elimu Kwa hii hoja yake
 
Kwa jinsi Wanafunzi wa Shule za Msingi ( hasa Darasa la Saba ) walivyo na Nidhamu mbaya katika Jamii zetu huku Wengi wao wakiwa hawana Akili Vichwani huwa nashangaa kuona kila mwaka katika Kutangazwa kwa Matokeo yao Kitaifa Wanaofaulu ni Wote / 99.9%
Siku hizi sio tuu la saba.. na form four nayo ufaulu kama wotee.. poor country
 
Ni jambo la kushangaz kam utawapima watu 100 uje na matokeo kuwa watu 99 wote wamehitimu vzr hasa kizazi hiki cha nyoka,
 
Matokeo yake unakutana na mtoto wa form 4 hajui hata mto Ruvuma upo upande gani wa nchi.

Pathetic
 
Hata kama kisasa Mzee hakuna training ya kijeshi iliyo serious kabisa muanze 300 mmalize 300 utakuta unfit wapo, utakuta wenye nidhamu mbaya wapo, waliopoteza uhai wapo sawa sawa na huko katika elimu asilimia ya ufaulu ni 99.9 nenda kafanye tafiti uone vituko vyake kiukweli hatuko serious kabisa na elimu.
Nadhani siku hizi wameanza kuwa serious; hivi majuzi tumesikia huko Singida baadhi ya vijana waligundulika ni mashoga, walitimuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom