TIQO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 13,786
- 2,104
kwahio uko salama zaidi kununua gari lenye km 100,000 kuliko lenye km 30,000 wakati yote yana miaka 10!!
Sasa tutakuwa tunawachezea huko kwenye 100,000km
kwahio uko salama zaidi kununua gari lenye km 100,000 kuliko lenye km 30,000 wakati yote yana miaka 10!!
ha ha ha ha yaani unaonyesha jinsi gani mnavyowaumiza wanaoabudu km chache kwenye odometer!!! mimi huwa sitishwi na km gari nzuri nikiiona nakuisikia naijua....uje na gari yako ya 2003 ina km 40,000 tena ushaitumia bongo wala siiangalii nakuaga tu.
Sasa tutakuwa tunawachezea huko kwenye 100,000km
Kuna wengine wananunua herufi. Kwa mfano herufi C ndo inayonunuiwa kwa sasa, zile B na A watu wanasema ya zamani, wakati facts ni kuwa namba ya usajili pekee si kigezo
Kwa mwendo huu gari likiwa na 40,000 za kweli tutalichezea zifike 100,000 ili liuzike!
Kuna mdau mkubwa wa magari humu anaitwa CYBERTEQ sijamuona humu....hii mada anaweza kuwa na mchango mkubwa sana.
Mkuu hii mbona tulishazungumzia humu kitambo!..nimeiona hii thread nikapita tu, lakini kwa vile umenikurupua mkuu ni kwamba, wauzaji wa magari hasa Tanzania ni watu wajanja sana na wanajua kusoma alama za nyakati, wanajua kucheza na akili za watu. Kuna wakati watu walikuwa wanaangalia sana registration number, kuna wakati watu walikuwa wanaangalia body condition kudetermine gari imetumika kiasi gani, wajanja wakawa wanapiga rangi "mkono mmoja" huwez kugundua, hilo la milage ndiyo kabisa watu wameshaacha kuchezea odo zamani hiyo ilishapitwa na wakati! hakuna wakati ulio mgumu kwa watu wenye showroom kama huu, watu wengi wanaagiza magari wenyewe, biashara imeshahamia kwenye magari "mapya zaidi"! Kifupi ni kwamba, kwa magari ya kutoka nje, kama umenunua kwenye kampuni kubwa ukiona milage ndogo usiogope nunua, hawana huo muda wa kubadili odo, wao wanauza kwa kadri walivyonunua, higher mileage cars na zenye dents na scratchs mnadani bei ziko chini sana, hiyo migari mizee wao wananunua bei za kutupa!Ni mara chache sana gari ya kutoka nje ukafanyiwa udanganyifu kama umenunua kutoka kwenye kampuni kubwa,japo inaweza kutokea bahati mbaya ukapata gari mbovu, hiyo ni bahati mbaya tu. Cha msingi angalia aina ya gari unayonunua, angalia ni model gani, ya mwaka gani, kama ni mzoefu kila gari unajua madhaifu yake, hicho ndicho cha kuchunguza, waliowahi kununua RAV4 za miaka fulani kutoka UK wananielewa.
Uzi huu kwakweli umenifungua macho, kila nikifanya kautafiti mtandaoni nitafute usafiri gani, moja ya vigezo ni km kuwa chini ya laki 1, lkn model ya gari husika ni ya 2002-03. Sasa nitaanza kuangalia ya kati ya km laki hadi laki na nusu. Shukrani mleta mada.
Kuna mdau mkubwa wa magari humu anaitwa CYBERTEQ sijamuona humu....hii mada anaweza kuwa na mchango mkubwa sana.
Hizi ndio mambo ambazo zinanifanya nisijilaumu kupoteza muda kupita hapa JF.Huu uzi upo vizuri.Mkuu natumaini upo UK au una uzoefu na ununuzi wa gari za UK.Naomba unisaidie haya maswala mawili
1. Hivi kwa returning citizen ambao huwa wanapewa exemption nasikia kuna kadi ya gari huwa wanaibadilisha ili ionekane gari amekuwa analitumia kipindi yupo kwenye nchi husika.Embu nipe nondo kuhusu hili swala,ni kitu gani huwa wanacheza nacho?
2. Ukiachia ebay na autotrader ni mtandao gani naweza kupata gari kwa bei zetu za kimasikini? Au hata kama kuna mnada unaoujua au watu unaowajua ndani na nje ya London pia itasaidia
aisee na mimi nazungumzia hayo magari ya nje wala sio ndani ya tanzania....huu mchezo wa kuchezea odometer umeanzia nje hapa tz wamejifunzia hao wa nje....nishashuhudia magari kadhaa ya watu ninaowajua wamenunua makampuni makubwa ya nje zimechezewa odometer.
Mkuu Cyberteq kampuni kama beforward may be au autorec do you think kweli hawana mchezo huu wa kubadili mileage.