Tusidanganywe na Magari Yenye Km Chache

Tusidanganywe na Magari Yenye Km Chache

PRONDO umesema kweli lakin pale kwenye matumizi ya gar umesahau kitu. Kwa wenzetu Japan gar ni bei rahisi mno na weng humiliki gar 2 mpka 3 sasa mtu mwenye gar zaid ya mbili obvious hawez itumikisha sana gar moja ndio maana km 30,000 au 40,000 zinawezekana.. Mimi nilikaa Slough nje kdgo ya London kwa kweli alikuwepo bwana mmoja mpemba pale ana Car wash akaja nyanganywa na Waganda flani ivi uyu mpemba ilikua huitaji kumoa pound 60 akufanyie hilo gumashi yeye hata 30 au 40 anakufutia km zinarudi utakazo. Km gauge sio conclusive kbsa!

mkuu kwa mtu wa kawaida kumiliki gari mbili nchi zilizoendelea ni mzigo sana....wewe uko slough unajua mzigo wa gari mbili kwa mtu mmoja...insurance,road tax,service za nini wakati unaendesha gari moja...kumbuka nimesema mtu wa kawaida...na watu wa kawaida ndio wamiliki wa hizi mark2,mark x etc.....
 
labda zamani, siyo sasa, they are simply too big for that!

lakini mkuu be foward ni moja ya kampuni zinaleta magari mengi yenye matatizo tz....niliagiza rav 4 ya 2006 mwaka jana ikaja ina gonga chini balaa nilibadili hadi mikono ya steering ndio ikatulia...pia niliagiza pajero ya 2003 ilisumbua gearbox baada ya mwezi tu! pamoja na kuwa kampuni kubwa hai-guarantee kuwa reliable na sio siri magari mengine nimenunua kwao yako vizuri tu.
 
mkuu kwa mtu wa kawaida kumiliki gari mbili nchi zilizoendelea ni mzigo sana....wewe uko slough unajua mzigo wa gari mbili kwa mtu mmoja...insurance,road tax,service za nini wakati unaendesha gari moja...kumbuka nimesema mtu wa kawaida...na watu wa kawaida ndio wamiliki wa hizi mark2,mark x etc.....

kwa maoni yangu hao watu wa daraja hilo wako busy sana mkuu, wanafanya kazi masaa mengi, either wanaendesha baiskeli, au wanatumia usafiri wa jumuiya ili kkuwahi kazini na kupunguza gharama za mafuta.
 
lakini mkuu be foward ni moja ya kampuni zinaleta magari mengi yenye matatizo tz....niliagiza rav 4 ya 2006 mwaka jana ikaja ina gonga chini balaa nilibadili hadi mikono ya steering ndio ikatulia...pia niliagiza pajero ya 2003 ilisumbua gearbox baada ya mwezi tu! pamoja na kuwa kampuni kubwa hai-guarantee kuwa reliable na sio siri magari mengine nimenunua kwao yako vizuri tu.

basi una bahati mbaya mkuu, mimi nimefanya nao biashara magari mengi mno na sijawahi kupata gari mbovu zaid ya usumbufu mara chache sana gari kuchelewa. btw, hata gari mpya unaweza kununua ikakuzingua ndani ya mwezi mmoja, sema mpya hauumii kwa sababu muuzaji anakuwa nyuma yako.
 
kwa maoni yangu hao watu wa daraja hilo wako busy sana mkuu, wanafanya kazi masaa mengi, either wanaendesha baiskeli, au wanatumia usafiri wa jumuiya ili kkuwahi kazini na kupunguza gharama za mafuta.

aisee tafsiri yangu mtu wa kawaida kwa nchi zilizoendelea anaweza kumiliki gari....baiskeli au usafiri wa umma hata david cameron anatumia.
 
kabisa....utakuta mtu unamwambia nauza gari anauliza namba gani C?? ukimwambia B hataki, wakati hizo gari C ni ya mwaka 2003 na B ni ya mwaka 2006!!! ONLY IN TZ where an old car gets newer registration than the latest car!!!

Ukiingiza gari UK leo kutoka Japan kama ni ya mwaka 2003 itapewa registration ya mwaka 2003!!!

Mkuu hebu fafanua hapo kwenye namba C n B umenichanganya kidogo
 
Unapoagiza gari online si linakua na mwaka wake wa kutengenezwa..!! Na unapolileta hapa nchini si itabidi lifanyiwe registration..??
Sasa utakuta mtu kaagiza gari toka Japan mfano ya mwaka 2006 halafu ikaja hapa ikakuta registration bado zinacheza kwenye B halaf mwngne akaagiza la mwaka 2003 akakutana na Registration imeshasogea kwenye C... sasa kasumba ya wabongo sisi tunaangalia registartion kudetermine upya wa gari na wala sio ile Manufacturer serial.. Ukiangalia vzur hapo hilo la C ni la zaman kuliko hilo la B ndicho alichomaanisha mtaalam pale juu. So utauziwa gari lenye registartion ya C chakavu kuliko lenye registration ya B only bcoz sisi wabongo tunaangalia registration namba kama kigezo cha gari mpya...!!!
 
Nimekuelewa kaka nadhani hili ni tatizo la kimfumo zaidi Tra wanatakiwa waige mifumo kutoka nchi zenye mafanikio zaidi katika haya mambo
 
vipi kama utapewa iyo m.o. t na service history na vikasupport iyo km 40,000? bado hutanunua.?

Kuna kununua kwa bei ya km 40,000 na kwa bei ya km 3,000. Kwa hiyo point ya kuhakikisha km bado ni muhimu kwa km zozote, kwa sababu km zinaeleza jinsi gari lilivyotumika na bei gani itakuwa nzuri, kwa watu wanaopenda uhakiki na urari mzuri.

Mimi mwenyewe nilikuwa sielewi sana watu wanaonunua magari brand new, nikifikiri wanachezea fedha, kwani kuna magari yaliyotumika mazuri tu.

Nikaja kufanya mahesabu ya kuangalia tofauti za gari jipya na lililotumika kidogo (ambalo linaweza kuwa limetumika sana na kuuzwa kama limetumika kidogo kwa kubadilishwa km) nikaona mara nyingi kama unaenda kwa dealer anayeeleweka tofauti inaweza kuwa si kubwa sana, kutegemea na gari. Hivyo wengine huona ni bora wanunue gari jipya na kulipa an extra $ 5,000 -7,000 or so kuliko kununua gari lililotumika halafu ukakuta limetumika zaidi ya lilivyonadiwa.

Of course, "tofauti si kubwa sana" is a relative term. Kwa hiyo tofauti ninayosema si kubwa sana, mwingine atapata gari analolitaka hapohapo.

Lakini, kama unaweza kumudu kununua gari jipya nalo ni jambo la kufikiria. Utaondoa habari nzima ya kubashiri gari limetembea kiasi gani. Ila kiujumla magari ya miundo mipya huwa na bima ya juu zaidi ya yale ya zamani, kwa hiyo hilo nalo halikosi ubaya wake.
 
RRONDO nimeona huu uzi kaka na nimekuwa nikijiuliza sana haya maswali kuwa inakuwaje kwa muda na mileage za chini!!!!????

Thanx sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
RRONDO nimeona huu uzi kaka na nimekuwa nikijiuliza sana haya maswali kuwa inakuwaje kwa muda na mileage za chini!!!!????

Thanx sana mkuu

tatizo letu kubwa bajeti. mtu ana bajeti ya kutosha gari ya 2003/4 lakini anataka liwe na km chache. sasa wauzaji wanashindwa kuuza hayo magari maanake kiukweli kwa umri huo yanakuwa na 100,000+ km ndio inabidi wayachezee yaonekane yana 30,000 au 40,000 ili wasipoteze wateja wao.

kama watu wanataka low milage wajitahidi wapunguze umri wa gari waanzie 2007/8/9 hapo utapata 40,000km au 50,000km ya ukweli.
 
Kuna kununua kwa bei ya km 40,000 na kwa bei ya km 3,000. Kwa hiyo point ya kuhakikisha km bado ni muhimu kwa km zozote, kwa sababu km zinaeleza jinsi gari lilivyotumika na bei gani itakuwa nzuri, kwa watu wanaopenda uhakiki na urari mzuri.

Mimi mwenyewe nilikuwa sielewi sana watu wanaonunua magari brand new, nikifikiri wanachezea fedha, kwani kuna magari yaliyotumika mazuri tu.

Nikaja kufanya mahesabu ya kuangalia tofauti za gari jipya na lililotumika kidogo (ambalo linaweza kuwa limetumika sana na kuuzwa kama limetumika kidogo kwa kubadilishwa km) nikaona mara nyingi kama unaenda kwa dealer anayeeleweka tofauti inaweza kuwa si kubwa sana, kutegemea na gari. Hivyo wengine huona ni bora wanunue gari jipya na kulipa an extra $ 5,000 -7,000 or so kuliko kununua gari lililotumika halafu ukakuta limetumika zaidi ya lilivyonadiwa.

Of course, "tofauti si kubwa sana" is a relative term. Kwa hiyo tofauti ninayosema si kubwa sana, mwingine atapata gari analolitaka hapohapo.

Lakini, kama unaweza kumudu kununua gari jipya nalo ni jambo la kufikiria. Utaondoa habari nzima ya kubashiri gari limetembea kiasi gani. Ila kiujumla magari ya miundo mipya huwa na bima ya juu zaidi ya yale ya zamani, kwa hiyo hilo nalo halikosi ubaya wake.

maelezo mazuri mkuu.
 
For sure Broda,hata mie nilinunua yenye kilometer 114,000 ,2001 Model
 
Kweli kabisa, Wakati mwingine hata japan wanakuwa hawaelezi ukweli. Magari mengine yanakufa odometer yakiwa na kilometer 70,000 inawekwa mpya inaanza kusoma 0 inatumika miaka michache unauzwa ikisoma 30,000 kumbe tayari hapa ina imeshapiga kilometer 100,000. ni watu wachache sana wenye uelewa huu wa kutojali odometer, unakuta gari inasoma kilometer chache ila imechoka mbaya kutu kila kona.
ushauri wangu ukinunua gari kama hizi angalia km zake zikupe average kama 7000km per year.....gari ya 2003 ikiwa na km 30,000 ikimbie kabisa
 
Tukiamini kuwa watu wote si waaminifu tutamwona mtoa mada kama yuko sahihi. Lakini kiuhalisia gari ya miaka kumi inaweza kuwa na KM 60,000. Mimi gari yangu nafanya Service kila baada ya Kilometer 3,000 na kwa mwaka nafanya service mara mbili which means natumia km 6,000 kwa mwaka, sasa kwa nini miaka kumi ukatae kuwa na km 60,000?

Shida zetu zinatufanya tutende dhambi kwa kuwawazia mabaya wenzetu, kuna familia zina gari ya Baba, ya mama na ya kuwahudumia watoto shule; sasa hilo la shule kwa miaka kumi litafikisha 60,000km kama shule ziko karibu?
 
Hii ilinitokea mwaka 2011 nilinunua Carina ya 2001 ikiwa na Km 39000 baada ya kutembea Km 100 yenyewe inaonesha nimetembea Km 1,000 ndipo nilipogundua kwamba imechezewa..! Tuwe makini jamani
 
Mimi huwa naangalia kitu roho inapenda kwanza, inakuja accident history then mwaka ulotengenezwa.

Mengine mbwembwe tu
 
Niliwahi kushawishika kufanya hivyo kipindi nataka kuuza gari langu. Ila baada ya kusoma Biblia nikagundua kuwa Mwenyezi Mungu amekataza 'vipimo vya udanganyifu'. Nikaghairi zoezi hili la kupunguza mileage!
 
huu uzi ni mzuri sana, tunapata somo zuri mno, asante jamii forum
 
Back
Top Bottom