Tusidanganywe na Magari Yenye Km Chache

Tusidanganywe na Magari Yenye Km Chache

Kuna jamaa alishaanzishaga uzi jinsi ya kujua umri wa gari lako kwa kusoma chasis #.
 
Tukiamini kuwa watu wote si waaminifu tutamwona mtoa mada kama yuko sahihi. Lakini kiuhalisia gari ya miaka kumi inaweza kuwa na KM 60,000. Mimi gari yangu nafanya Service kila baada ya Kilometer 3,000 na kwa mwaka nafanya service mara mbili which means natumia km 6,000 kwa mwaka, sasa kwa nini miaka kumi ukatae kuwa na km 60,000?

Shida zetu zinatufanya tutende dhambi kwa kuwawazia mabaya wenzetu, kuna familia zina gari ya Baba, ya mama na ya kuwahudumia watoto shule; sasa hilo la shule kwa miaka kumi litafikisha 60,000km kama shule ziko karibu?

sijasema kuwa watu wote si waaminifu. kama unafanya 6000km kwa mwezi hizo ni 72,000km kwa mwaka. kama umesoma kiumakini kuna sehemu nimetoa average ya 7000km kwa mwaka ambayo haina tofauti sana na gari yako. nilichosema mimi ni gari ya miaka 10 iwe na km 30,000.....its too good to be true....ninavyoona mimi labda hio gari ilikuwa ya mzee/mstaafu ambacho wewe mnunuzi huwezi kujua unless umenunua personally kwa huyo mtu.
 
Hii ilinitokea mwaka 2011 nilinunua Carina ya 2001 ikiwa na Km 39000 baada ya kutembea Km 100 yenyewe inaonesha nimetembea Km 1,000 ndipo nilipogundua kwamba imechezewa..! Tuwe makini jamani

haya mambo yapo...tuwe makini tusidanganywe na low milage vehicles....washajua ugonjwa wetu hivyo wanatupiga huko huko.
 
Niliwahi kushawishika kufanya hivyo kipindi nataka kuuza gari langu. Ila baada ya kusoma Biblia nikagundua kuwa Mwenyezi Mungu amekataza 'vipimo vya udanganyifu'. Nikaghairi zoezi hili la kupunguza mileage!

je unafikiri ni wangapi walikuwa na mawazo kama wewe Biblia ikawazuia?? wachache sana,wengi wanazichakachua.
 
Kweli ujanja si kwa mama ntilie tu kuweka amira
wana jf natumaini wengi wenu mkinunua magari yaliyotumika huwa mnakimbilia yaliyotembea km chache. Kiukweli na kwa akili ya kawaida hili ni jambo sahihi kabisa kwa mnunuzi wa magari yaliyotumika.

Kwa kujua hili wauzaji wa magri mengi yaliyotumika wamekuwa na tabia ya kurudisha km nyuma. Wengi wetu walikuwa wakiamini 'digital' odometer haziwezi kuchezewa na kurudishwa nyuma,hilo ni kosa kubwa sana. Digital odometer zinaweza kuchezewa sana.

Ili kurudisha nyuma km kwenye odometer ya digital unahitaji laptop na software tu kazi ambayo inachukua chini ya nusu saa. Kuna rafiki yangu aliwahi kuwa na toyota cresta km 33,000 mimi nikamwambia hii gari ina miaka 10 sasa km 33,000 ina maana kwa mwaka hii gari ilikuwa inatembea km 3000 tu! Nikamwambia hii wameishusha na kweli baada ya muda mfupi ile gari ilipofika 33999 badala ya kuingia 34000 ikaruka mpaka 44,000km ndipo aliponipigia simu na kuamini hio odometer ilichezewa!

Mimi binafsi gari ya miaka 8-10 ukiniambia ina km 30,000-40,000 sinunui niko radhi ninunue yenye km 100,000 ambazo naamini kwa muda huo gari hio inastahili kufikisha. Hivi kweli mtu akae na gari kwa miaka 10 au zaidi asifikishe hata km 80,000 ina maana kanunua gari ya nini??

Kwa wenzetu japan au uk na nchi nyingine tununuapo magari hawanunui vitu bila kuhitaji. Mtu hawezi kununua gari kwa $30,000 halafu aendeshe km 300 kwa mwezi[3600km kwa mwaka appr 40,000 kwa miaka 10] kama mtu hana matumizi ya gari sana mara nyingi wanatumia public transport ambayo inaaminika na haisumbui kabisa.

Kuna aina ya gari ambazo zinaweza kuendeshwa mara moja kwa wiki au hata mara moja kwa mwezi. Gari kama ferrari,buggati,rolls royce etc ni magari ambayo watu wananunua kama 'toys' tu au status symbol lakini magari yetu mengi ya kawaida ni kwa ajili ya mizunguko ya kila siku. Pia magari machache yanayomilikiwa na wazee yanaweza kuwa na km chache lakini huwezi jua lipi ni lipi labda ununue mwenyewe kutoka kwa huyo mzee na sio kuagiza kama tufanyavyo.

Ushauri wangu,tununuapo magari tuangalie lina miaka mingapi halafu tuipe average kama 7000km kwa mwaka tuone kama hio km waliyokwambia na average km kwa mwaka ni 'realistic'? Ukiona gari ya mwaka 2003 ina km 30000 nakushauri achana nayo kuna kitu hapo sio bure. Magari mengi wanayotengeza uk wakati yakiwa mapya wanatoa warranty ya miaka 3 na miles 60,000[approx 100,000km]!!! Haina maana kwamba kwa miaka mitatu liwe limetembea hizo km ila linaweza kutembea hizo kwa miaka 3 au 10!

Kwa uzoefu wangu wa magari kutoka uk, ukinunua used car ulizia service history ya gari husika,ni kijitabu kinachorekodi service kila baada ya miles/muda fulani na matengenezo mengine yote ya gari husika tangu inanunuliwa mpaka inakufikia. Kwenye service history utaona umri wa gari kulingana na tarehe ilizofanyiwa service kwa interval fulani kutegemea na gari.

Pia unaweza na unatakiwa upewe m.o.t certificates ya gari ilio hai na za zamani[tanzania imezoeleka kwa jina ka vosa].kila mwaka gari zenye zaidi ya miaka mitatu huwa zinafanyiwa ukaguzi wa kila kitu ndio unapata m.o.t certificate ambamo utaona tarehe ukaguzi wa kwanza hadi wa mwisho wakati unalinunua gari.

Nawasilisha.

Cc: olesaidimu kaizer @cyberteq chacha kisiri mani chelseablue
 
kuna siku nilikuwa naangali TOP GEAR presented by JEREMY CLARKSON,JAMES MAY NA R. HAMMOND....siku hio walikuwa wanazungumzia used cars, wakazungumzia jinsi mercedes benz s class yenye 60,000miles[about 100,000km] ilivyo cheap to buy. kilichonigusa ni kauli ya Jeremy Clarkson kuwa kwa gari kama hii merc s class 60,000miles[100,000km] ni sawa sawa na mcheza mpira kamaliza kufanya warm ndio anaingia mpirani kupambana.

Point yangu hapa tusiogope sana tukiona gari ina km 100,000. Itunze inavyotakiwa service kwa muda unaotakiwa na hio gari itagonga hadi 200,000km. Nishawahi kukodi gx110 ya tours in km 230,000 na nilienda nayo dar-iringa bila kupata issue yoyote ile.
 
Wana JF natumaini wengi wenu mkinunua magari yaliyotumika huwa mnakimbilia yaliyotembea km chache. Kiukweli na kwa akili ya kawaida hili ni jambo sahihi kabisa kwa mnunuzi wa magari yaliyotumika.

Kwa kujua hili wauzaji wa magri mengi yaliyotumika wamekuwa na tabia ya kurudisha km nyuma. Wengi wetu walikuwa wakiamini 'digital' odometer haziwezi kuchezewa na kurudishwa nyuma,hilo ni kosa kubwa sana. Digital odometer zinaweza kuchezewa sana.

Ili kurudisha nyuma km kwenye odometer ya digital unahitaji laptop na software tu kazi ambayo inachukua chini ya nusu saa. Kuna rafiki yangu aliwahi kuwa na toyota cresta km 33,000 mimi nikamwambia hii gari ina miaka 10 sasa km 33,000 ina maana kwa mwaka hii gari ilikuwa inatembea km 3000 tu! nikamwambia hii wameishusha na kweli baada ya muda mfupi ile gari ilipofika 33999 badala ya kuingia 34000 ikaruka mpaka 44,000km ndipo aliponipigia simu na kuamini hio odometer ilichezewa!

Mimi binafsi gari ya miaka 8-10 ukiniambia ina km 30,000-40,000 sinunui niko radhi ninunue yenye km 100,000 ambazo naamini kwa muda huo gari hio inastahili kufikisha. Hivi kweli mtu akae na gari kwa miaka 10 au zaidi asifikishe hata km 80,000 ina maana kanunua gari ya nini??

Kwa wenzetu japan au uk na nchi nyingine tununuapo magari hawanunui vitu bila kuhitaji. Mtu hawezi kununua gari kwa $30,000 halafu aendeshe km 300 kwa mwezi[3600km kwa mwaka appr 40,000 kwa miaka 10] kama mtu hana matumizi ya gari sana mara nyingi wanatumia public transport ambayo inaaminika na haisumbui kabisa.

Kuna aina ya gari ambazo zinaweza kuendeshwa mara moja kwa wiki au hata mara moja kwa mwezi. Gari kama ferrari,buggati,rolls royce etc ni magari ambayo watu wananunua kama 'toys' tu au status symbol lakini magari yetu mengi ya kawaida ni kwa ajili ya mizunguko ya kila siku. Pia magari machache yanayomilikiwa na wazee yanaweza kuwa na km chache lakini huwezi jua lipi ni lipi labda ununue mwenyewe kutoka kwa huyo mzee na sio kuagiza kama tufanyavyo.

Ushauri wangu,tununuapo magari tuangalie lina miaka mingapi halafu tuipe average kama 7000km kwa mwaka tuone kama hio km waliyokwambia na average km kwa mwaka ni 'realistic'? Ukiona gari ya mwaka 2003 ina km 30000 nakushauri achana nayo kuna kitu hapo sio bure. Magari mengi wanayotengeza UK wakati yakiwa mapya wanatoa warranty ya miaka 3 na miles 60,000[approx 100,000km]!!! Haina maana kwamba kwa miaka mitatu liwe limetembea hizo km ila linaweza kutembea hizo kwa miaka 3 au 10!

Kwa uzoefu wangu wa magari kutoka UK, ukinunua used car ulizia SERVICE HISTORY ya gari husika,ni kijitabu kinachorekodi service kila baada ya miles/muda fulani na matengenezo mengine yote ya gari husika tangu inanunuliwa mpaka inakufikia. Kwenye service history utaona umri wa gari kulingana na tarehe ilizofanyiwa service kwa interval fulani kutegemea na gari.

Pia unaweza na unatakiwa upewe M.O.T certificates ya gari ilio hai na za zamani[tanzania imezoeleka kwa jina ka VOSA].Kila mwaka gari zenye zaidi ya miaka mitatu huwa zinafanyiwa ukaguzi wa kila kitu ndio unapata m.o.t certificate ambamo utaona tarehe ukaguzi wa kwanza hadi wa mwisho wakati unalinunua gari.

Nawasilisha.

CC: OLESAIDIMU Kaizer @CYBERTEQ Chacha Kisiri MANI ChelseaBlue

thanks kwa taarifa ndugu
 
Yaani acha tu. Hapo bado hujaenda kufanya service ukawekewa oil ya "kutengenezwa"

oil ya kutengenezewa,unawaambia wabadili air filter wanapiga upepo wanarudisha ya zamani! utajijua mwenyewe mbele ya safari.....kwenye gari yangu nishaacha ubosi, nasimamia mwenyewe.
 
Wengne wanauza baada ya kupata ajari

kuuza baada ya ajali sio kosa. nilishawahi kufanya hii biashara UK. uk magari yaliyopata ajali huwa yanapewa categories A,B,C,D,X

A-HALIFAI KABISA...kisheria huruhusiwi kuliuza mengi ni yale yaliyoungua moto au yalijaa maji kwenye mafuriko
B-HALIFAI KABISA...kisheria huwezi kuuza mengi yamegongwa hadi kupinda chasis
C-YANATENGENEZEKA....unaruhusiwa kulitengeneza na kuuza lakini lazima lifanyiwe VOSA VIC inspection
D-YANATENGENEZEKA...unaruhusiwa kuuza haya ni yale yamegongwa kidogo sana labda limevunjika taa au limebonya mlango
X-hayana ubovu kabisa...haya ni yale yaliibiwa mwenye nalo akalipwa bima baadae likapatikana.

Hayo yote niliyoorodheshwa uamuzi unatolewa na wataalam wa bima.
 
RRONDO.nimekusoma kaka..safi sana

Will be back..
 
Last edited by a moderator:
Mi pia nilikuwa nafikiri kuwa labda tukichukua average Kwamba Huyu mtu ana drive maximum of 30km per day. Maana yake kwa siku 365 yaani mwaka inakuwa ni (30km*365=10950km per year) so for 10 yrs inakuwa ni 109500 km which I think inaweza kuwa na ukweli assuming na yeye gari aliinunua ikiwa mpya 0km. So Kama gari ni 10 yrs and over at least iwe na not less than 100,000km.


Sent from my iPad using JamiiForums

Mmmmh, kwa hiyo sie tulionunua yenye 60k tumeliwa, Lol.


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Back
Top Bottom