Tusidanganywe na Magari Yenye Km Chache

Tusidanganywe na Magari Yenye Km Chache

Naweza kupingana na wewe kwa namna fulani. Hayo magari mengi tunayonunua huya yanakuwa yanauzwa kwa muda mrefu sana ndo maana wakati mwingine unakuta hadi tairi zimeoza kwa ajili ya kutotembea muda mrefu. Ukikuta gari ya 2003 in km 40000 ukute imeanza kuuzwa toka mwaka 2006. Na kwa calculation zako za km 7000 kwa mwaka ina maana ni magari ya 2009 na kuendelea ndo yatakuwa below 40,000km. na kwa hali ya mtanzania wa kawaida kununua gari ya 2009 ni ndoto.

nani atakuwekea korokoro la 2003 kuanzia 2006 hadi 2014!!! kama haliuziki wana scrap wanaenda kutengenezea mafriji!!!
 
Naweza kupingana na wewe kwa namna fulani. Hayo magari mengi tunayonunua huya yanakuwa yanauzwa kwa muda mrefu sana ndo maana wakati mwingine unakuta hadi tairi zimeoza kwa ajili ya kutotembea muda mrefu. Ukikuta gari ya 2003 in km 40000 ukute imeanza kuuzwa toka mwaka 2006. Na kwa calculation zako za km 7000 kwa mwaka ina maana ni magari ya 2009 na kuendelea ndo yatakuwa below 40,000km. na kwa hali ya mtanzania wa kawaida kununua gari ya 2009 ni ndoto.

hii sio sheria.....nishaona gari za 2010/11/12 zina km 100,000!!! ni matumizi tu...kuna watu wanafanyakazi [mfano] morogoro kazi dar kila siku anakwenda na kurudi na company car,au ni engineer anazunguka from city to city everyday anabadili gari mpya kila mwaka na ukiona km zake utakimbia....kama unataka gari nzuri nunua latest usinunue gari ya zamani [miaka 15] then ujipe moyo ina km chache,hicho ni chuma chakavu tu.
 
Niliwahi kushawishika kufanya hivyo kipindi nataka kuuza gari langu. Ila baada ya kusoma Biblia nikagundua kuwa Mwenyezi Mungu amekataza 'vipimo vya udanganyifu'. Nikaghairi zoezi hili la kupunguza mileage!

Well said mkuu
 
hii sio sheria.....nishaona gari za 2010/11/12 zina km 100,000!!! ni matumizi tu...kuna watu wanafanyakazi [mfano] morogoro kazi dar kila siku anakwenda na kurudi na company car,au ni engineer anazunguka from city to city everyday anabadili gari mpya kila mwaka na ukiona km zake utakimbia....kama unataka gari nzuri nunua latest usinunue gari ya zamani [miaka 15] then ujipe moyo ina km chache,hicho ni chuma chakavu tu.
Ok siwezzi kupingana na wewe maana experience yako iko kwenye gari ndogo ila magari ya mizigo na tipper tanzania 90% ni za chini ya mwaka 2002 na we ndo unaita chuma chakavu wenzako ndo wanatajarikia humo.
 
kutajirikia kwenye hayo magari hakuyafanyi yasiwe old bangers!! ndio maana malori kila siku yanasababisha ajali....TAMAA MBELE MAUTI NYUMA.....kupenda kwako utajiri unaua wengine....na hamna sehemu niliyokataza mtu kununua gari ya zamani...NIMETOA ANGALIZO TU MAGARI MENGI YA ZAMANI WANARUDISHA KM NYUMA ILI KUVUTIA WATU KAMA WEWE AMBAE HATA KAMA UNAONA KUTU UNANUNUA KWA ROHO NYEUPE KISA UMEONESHWA 32,000KM GARI YA 1999!
 
No research no right to speak According to report ya mwaka 2007 ya SUMATRA 76.4 % ya ajali zinasababishwa na human factor not mechanical or road factor. Na wajapan wana JAAI inspection ambayo inafanyika kwenye gari na likifeli halisafirishwi wanakutafutia jingine. (Myself ishanitokea twice). we ita machuma lakini ni bora ninunue Landcruiser ya mwaka 2002 kwa 20m kuliko Vits ya mwaka 2013 kwa 20m. Hayo ni maoni yangu.
 
kama hizo research zenu zingekuwa na maana tusingekuwa hapa leo.....SUMATRA unayozungumzia ni hii ya pale aga khan au INDONESIA?? btw nimesema malori yanasababisha ajali SIO KWAMBA % KUBWA YA AJALI TZ NI ZA MALORI! wewe ndio wale gari ya juu ndio ya maana hata ikiwa ya mwaka 1980!
 
Wakuu hebu nishaurini, nataka kununua gari kutoka tradecarview lakini kila invoice waliyonitumia iki expire na gari nalo linashuka mileage. Mwanzoni niliona ikiwa 133,000 sasa hivi ipo 42,000. Hili sio wanataka kunibambikia?
 
Wana JF natumaini wengi wenu mkinunua magari yaliyotumika huwa mnakimbilia yaliyotembea km chache. Kiukweli na kwa akili ya kawaida hili ni jambo sahihi kabisa kwa mnunuzi wa magari yaliyotumika.

Kwa kujua hili wauzaji wa magri mengi yaliyotumika wamekuwa na tabia ya kurudisha km nyuma. Wengi wetu walikuwa wakiamini 'digital' odometer haziwezi kuchezewa na kurudishwa nyuma,hilo ni kosa kubwa sana. Digital odometer zinaweza kuchezewa sana.

Ili kurudisha nyuma km kwenye odometer ya digital unahitaji laptop na software tu kazi ambayo inachukua chini ya nusu saa. Kuna rafiki yangu aliwahi kuwa na toyota cresta km 33,000 mimi nikamwambia hii gari ina miaka 10 sasa km 33,000 ina maana kwa mwaka hii gari ilikuwa inatembea km 3000 tu! nikamwambia hii wameishusha na kweli baada ya muda mfupi ile gari ilipofika 33999 badala ya kuingia 34000 ikaruka mpaka 44,000km ndipo aliponipigia simu na kuamini hio odometer ilichezewa!

Mimi binafsi gari ya miaka 8-10 ukiniambia ina km 30,000-40,000 sinunui niko radhi ninunue yenye km 100,000 ambazo naamini kwa muda huo gari hio inastahili kufikisha. Hivi kweli mtu akae na gari kwa miaka 10 au zaidi asifikishe hata km 80,000 ina maana kanunua gari ya nini??

Kwa wenzetu japan au uk na nchi nyingine tununuapo magari hawanunui vitu bila kuhitaji. Mtu hawezi kununua gari kwa $30,000 halafu aendeshe km 300 kwa mwezi[3600km kwa mwaka appr 40,000 kwa miaka 10] kama mtu hana matumizi ya gari sana mara nyingi wanatumia public transport ambayo inaaminika na haisumbui kabisa.

Kuna aina ya gari ambazo zinaweza kuendeshwa mara moja kwa wiki au hata mara moja kwa mwezi. Gari kama ferrari,buggati,rolls royce etc ni magari ambayo watu wananunua kama 'toys' tu au status symbol lakini magari yetu mengi ya kawaida ni kwa ajili ya mizunguko ya kila siku. Pia magari machache yanayomilikiwa na wazee yanaweza kuwa na km chache lakini huwezi jua lipi ni lipi labda ununue mwenyewe kutoka kwa huyo mzee na sio kuagiza kama tufanyavyo.

Ushauri wangu,tununuapo magari tuangalie lina miaka mingapi halafu tuipe average kama 7000km kwa mwaka tuone kama hio km waliyokwambia na average km kwa mwaka ni 'realistic'? Ukiona gari ya mwaka 2003 ina km 30000 nakushauri achana nayo kuna kitu hapo sio bure. Magari mengi wanayotengeza UK wakati yakiwa mapya wanatoa warranty ya miaka 3 na miles 60,000[approx 100,000km]!!! Haina maana kwamba kwa miaka mitatu liwe limetembea hizo km ila linaweza kutembea hizo kwa miaka 3 au 10!

Kwa uzoefu wangu wa magari kutoka UK, ukinunua used car ulizia SERVICE HISTORY ya gari husika,ni kijitabu kinachorekodi service kila baada ya miles/muda fulani na matengenezo mengine yote ya gari husika tangu inanunuliwa mpaka inakufikia. Kwenye service history utaona umri wa gari kulingana na tarehe ilizofanyiwa service kwa interval fulani kutegemea na gari.

Pia unaweza na unatakiwa upewe M.O.T certificates ya gari ilio hai na za zamani[tanzania imezoeleka kwa jina ka VOSA].Kila mwaka gari zenye zaidi ya miaka mitatu huwa zinafanyiwa ukaguzi wa kila kitu ndio unapata m.o.t certificate ambamo utaona tarehe ukaguzi wa kwanza hadi wa mwisho wakati unalinunua gari.

Nawasilisha.

CC: OLESAIDIMU Kaizer @CYBERTEQ Chacha Kisiri MANI ChelseaBlue

umezungumza kitu cha kweli sababu mimi,diagnostic tool yangu ninayotumia ina uwezo wa kucorrect mileage kwenye odometer na ninapata wateja wengi sana wa huduma hiyo
 
Back
Top Bottom