RRONDO
Platinum Member
- Jan 3, 2010
- 60,420
- 139,278
Wana JF natumaini wengi wenu mkinunua magari yaliyotumika huwa mnakimbilia yaliyotembea km chache. Kiukweli na kwa akili ya kawaida hili ni jambo sahihi kabisa kwa mnunuzi wa magari yaliyotumika.
Kwa kujua hili wauzaji wa magri mengi yaliyotumika wamekuwa na tabia ya kurudisha km nyuma. Wengi wetu walikuwa wakiamini 'digital' odometer haziwezi kuchezewa na kurudishwa nyuma,hilo ni kosa kubwa sana. Digital odometer zinaweza kuchezewa sana.
Ili kurudisha nyuma km kwenye odometer ya digital unahitaji laptop na software tu kazi ambayo inachukua chini ya nusu saa. Kuna rafiki yangu aliwahi kuwa na toyota cresta km 33,000 mimi nikamwambia hii gari ina miaka 10 sasa km 33,000 ina maana kwa mwaka hii gari ilikuwa inatembea km 3000 tu! nikamwambia hii wameishusha na kweli baada ya muda mfupi ile gari ilipofika 33999 badala ya kuingia 34000 ikaruka mpaka 44,000km ndipo aliponipigia simu na kuamini hio odometer ilichezewa!
Mimi binafsi gari ya miaka 8-10 ukiniambia ina km 30,000-40,000 sinunui niko radhi ninunue yenye km 100,000 ambazo naamini kwa muda huo gari hio inastahili kufikisha. Hivi kweli mtu akae na gari kwa miaka 10 au zaidi asifikishe hata km 80,000 ina maana kanunua gari ya nini??
Kwa wenzetu japan au uk na nchi nyingine tununuapo magari hawanunui vitu bila kuhitaji. Mtu hawezi kununua gari kwa $30,000 halafu aendeshe km 300 kwa mwezi[3600km kwa mwaka appr 40,000 kwa miaka 10] kama mtu hana matumizi ya gari sana mara nyingi wanatumia public transport ambayo inaaminika na haisumbui kabisa.
Kuna aina ya gari ambazo zinaweza kuendeshwa mara moja kwa wiki au hata mara moja kwa mwezi. Gari kama ferrari,buggati,rolls royce etc ni magari ambayo watu wananunua kama 'toys' tu au status symbol lakini magari yetu mengi ya kawaida ni kwa ajili ya mizunguko ya kila siku. Pia magari machache yanayomilikiwa na wazee yanaweza kuwa na km chache lakini huwezi jua lipi ni lipi labda ununue mwenyewe kutoka kwa huyo mzee na sio kuagiza kama tufanyavyo.
Ushauri wangu,tununuapo magari tuangalie lina miaka mingapi halafu tuipe average kama 7000km kwa mwaka tuone kama hio km waliyokwambia na average km kwa mwaka ni 'realistic'? Ukiona gari ya mwaka 2003 ina km 30000 nakushauri achana nayo kuna kitu hapo sio bure. Magari mengi wanayotengeza UK wakati yakiwa mapya wanatoa warranty ya miaka 3 na miles 60,000[approx 100,000km]!!! Haina maana kwamba kwa miaka mitatu liwe limetembea hizo km ila linaweza kutembea hizo kwa miaka 3 au 10!
Kwa uzoefu wangu wa magari kutoka UK, ukinunua used car ulizia SERVICE HISTORY ya gari husika,ni kijitabu kinachorekodi service kila baada ya miles/muda fulani na matengenezo mengine yote ya gari husika tangu inanunuliwa mpaka inakufikia. Kwenye service history utaona umri wa gari kulingana na tarehe ilizofanyiwa service kwa interval fulani kutegemea na gari.
Pia unaweza na unatakiwa upewe M.O.T certificates ya gari ilio hai na za zamani[tanzania imezoeleka kwa jina ka VOSA].Kila mwaka gari zenye zaidi ya miaka mitatu huwa zinafanyiwa ukaguzi wa kila kitu ndio unapata m.o.t certificate ambamo utaona tarehe ukaguzi wa kwanza hadi wa mwisho wakati unalinunua gari.
Nawasilisha.
CC: OLESAIDIMU Kaizer @CYBERTEQ Chacha Kisiri MANI ChelseaBlue