Fahamu jinsi ya kupata gari unalotaka

Fahamu jinsi ya kupata gari unalotaka

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,191
Reaction score
2,880
1. Fanya utafiti mdogo juu ya gari unalolitaka: Uliza ujue gari unalolitaka linauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.
2. Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.
3 Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua, hata kama una ujuzi(idea) na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.
5. Epuka gari lililopigwa rangi:bila ubora Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.japo kuna wakati mwingine ni muhimu gari ipigwe rangi ili kuleta mvuto

6. Epuka gari lililooshwa engine: Ukikagua gari ukiona limeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi magari yanaoshwa engine kuficha 'leakage', yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.

7. Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini, chochote kinachogonga kuwa makini, usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha? Ingawa yapo matatizo
Madogo.
 

Attachments

  • FB_IMG_1793185425650.jpg
    FB_IMG_1793185425650.jpg
    61.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom