Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!

Status
Not open for further replies.

Pundit

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2007
Messages
3,740
Points
1,225

Pundit

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2007
3,740 1,225
MKJJ did Nyerere plagiarize that (as often, like you are doing now, albeit paraphrasing)or was that an original? It is one of those unverifiable nuggets that pass for truism.

Mwingine anaweza kusema dhambi ya kutokuwa discriminate haikomi, ukiwa mtu wa loose balls utakwenda na loose ball lolote even to your own demise.
 

Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2006
Messages
1,329
Points
0

Chuma

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2006
1,329 0
NASHAURI WANAOENEZA CHUKI ZA DINI WAACHE...ila hilo laekea kuwa gumu...ikiwa wakristo wanaona kila Zuri la waislam lisifanyike....Hoja za Makadhi na wengine...atlast Nyerere ndio atakaebeba dhambi ya HUU UDINI unaonuka Tanzania...waislam hawakumwangalia yeye kwa jicho la DINI yake...waliangalia Ukombozi wa NCHI...waislam waliweza kuwasimanga waislam wenzao waliokuwa wakitaka kumbagua Nyerere kwa DINI yake...Shekhe Suleiman TAKADIR ilibidi asizikwe na waislam wenzake na kuimbiwa Nyimbo "Selemean Mtaka DINI"...hawa waislam walifanya on Favor ya UTANGANYIKA.....soon after UHURU Nyerere alipopata MAMLAKA akatia KITANZINI maendeleo ya waislam...
 

Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2006
Messages
1,329
Points
0

Chuma

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2006
1,329 0
JokaKUU watu hawana chuki na UKILIMANJARO...na wengine tumeoa HUKO...Hili la ukabila mnalo au wanalo wenzetu wa K'njaro...na wao ndio wamekuwa wakiyafilisi mashirika ya Umma au Taassis za Umma wanazosimamia kwa kutaka utajir wa HARAKA...
 

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,777
Points
1,195

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,777 1,195
Jamani lisemwalo lipo kama halipo basi li njiani lina kuja!!! Tutafunika weeeeee but kuna siku litaripuka, japo maombi yangu dhaifu kwa maulana ni hili lisitufike kamwe!
 

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
17,559
Points
2,000

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
17,559 2,000
Chuma,

..kama Kilimanjaro wana ukabila inakuwaje wengi wenu mkaoa na kuolewa huko?

..yako mashirika mengi yameuawa na mameneja wanaotoka sehemu nyingine zaidi ya Kilimanjaro.

..miaka ya 1990 tulikuwa na mgogoro mkubwa na wafadhili kwasababu ya rushwa na kutokukusanya kodi. waziri wa fedha,katibu mkuu,mkurugenzi mkuu wa customs, wote hawakuwa wenyeji wa kilimanjaro.

..sikatai kwamba kuna baadhi ya wananchi wa Kilimanjaro wamehusika na hile au lile hapa Tanzania. Kinachonishtua ni kwamba kelele na hasira zinakuwa kubwa zaidi pale mkosaji anapokuwa mwenyeji wa Kilimanjaro.
 

Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2006
Messages
1,329
Points
0

Chuma

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2006
1,329 0
JOKAKUU pls usije ukawala watu....
Yapasa uelewe Watanzania wengi hawana misingi ya ukabila hasa linapokuja suala la ndoa. Zipo baadhi ya Familia ambazo hutoa msisitizo lazima uoe au uolewe na HOME BOY...
Pia si wote wa Kilimanjaro wana UKABILA wengine wamestaarabika Waendelee kuwa HIVYO...Nawe Hili walijua...Tena mmefikia pabaya ikiwa MKO Nje ya Kilimanjaro mtakwenda mtaweka Mbele Kilimanajro na mkiwa ndani wenyewe kwa wenyewe mnaleteana U-Majimbo..aha yule mmeru..yule mkibosho ohh yule hivi..nafsi yako kama MK basi siri yako....
Kilimanjaro ni case study, lkn yapo makabila like wahaya, wanyaksusa...baadhi ya Iringa ambao kwa namna moja au ingine wanaona watu wanaofaa kufanya nao kazi basi ni kabila hilo. na Hapa nakusudia % wise. Wapo wengi ambao wamestaarabika baada ya kukaa ktk Jamii mseto na zile attitude za U-mkoa zimepungua au kuondoka kabisa..
 

Bin Maryam

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2007
Messages
685
Points
0

Bin Maryam

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2007
685 0
Ni kweli kuwa mambo mengi kenya yanafanyika kwa kuangalia majina na sehemu ya kuzaliwa kama ilivyo kawaida ya nchi nyingi za Afrika. Hili la uchaguzi unaokwisha ambao umeleta mzee kikongwe mwingine madarakani (miaka 76) na kinachoendelea sasa hivi ni lazima kifundishe mataifa mengine.

Kama vile kenya kulivyo na ukabila, siku za karibuni mambo mengi tanzania yanaangaliwa kwa misingi ya kidini. Majina ya watu (ya kiarabu VS ya kikristo) yanatumika sana siku hizi katika mambo mengi tu Tanzania. Nilisikitika sana kuambiwa kuwa hata mashuleni siku hizi chaguzi za viongozi wa wanafunzi pia ni kwa misingi ya kidini!

Badala ya kukaa tunatoa macho kuwapondea wakenya kwa kile ambacho kimefanyika, ni vyema sasa Tanzania pia tukaacha haya ya udini ambayo sasa hata yanagawanya waislam (shia dhidi ya sunni) na wakristo ( walokole dhidi ya wasiookoka).

Tusipoacha hili, tusubiri tena vizazi vingine vitatu ili kupata maendeleo yale tunayopigania kwa mama yetu afrika.
Maendeleo ya Tanzania au Kenya hayakwamishwi na ukabila au udini. Naomba uwe unafikiri unapoandika vitu na usichulie migogoro midogo midogo ya kidini au kikabila kama ndio chanzo cha matatizo ya maendeleo yetu.

Mtu katoka India anakuja Tanzania akiwa na rangi na dini tofauti na anaweza kufanya biashara za maendeleo.

Mzawa pamoja na kuelewa mazingira yako bado unangojea vizazi vingine vitatu. Huu ni UTUMBO USIOKUBALIKA.
 

Choveki

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2006
Messages
449
Points
195

Choveki

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2006
449 195
mzee naomba kujiondoa katika kundi hilo...simo na wala sitarajiii
Game Theory;
Tafadhali rejea ule msemo wa kiswahili; "hujafa hujaumbika!" au wa kiingereza usemao "never say never!" huwezi kukanusha hivyo kwani wewe bado u hai, na hujamaliza kuandika kurasa za maisha yako! Huwezi kujua ati, na kuna leo na kesho.

Tukirudi kwenye mada, ni kweli Kenya kuna ukabila wa nguvu, ila udini wao ndo wala usisemi, Waislamu huko wala hawapumui, na hayo niliambiwa na rafiki yangu wa karibu saana ambaye ni Mkikuyu. Alisema safari yake ya kwanza kwenda Tz, alishangaa kuona kusivyokuwa na ubaguzi wa aina yeyote, na ameahidi atahamia na Tz moja kwa moja kwa sababu hizo.

Tz, ndo tunaelekea huko huko mara nyingi nawaambia watu kuwa matunda ya hizi seminari (dini zote) zinazoota kama uyoga na bila mfumo au mwongozo maalum toka serikalini tutayavuna baadaye miaka ijayo, nyie ngojeni tu, naombea tu kijiwe hiki kuwa bado kiwepo ili niaambie "I told you so".

Mifano ya TRA, "Mwakabima", na kule kitengo cha Kompyuta mlimani, au kule Commerce na Management ni vielelezo vichache tu ambavyo vinatuonesha tuendako. Ila watakaoshinda kwa wingi ni hili kabila na dini mpya ambayo ina mlango na mfumo wa watoto wa wakubwa kama kule BOT! Yaani kama una jina fulani tu regardless dini au kabila lako wewe utapeta tu.
 

Choveki

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2006
Messages
449
Points
195

Choveki

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2006
449 195
Aisee nipo interested kitengo cha computa mlimani kimefanyeje? UKABILA au UDINI? na Commerce na Management...?
Kitengo cha kompyuta kama hutoki mkoa fulani (sachi JF utaona hiyo topiki) wala usihangaike kuomba kazi hapo, tetesi za karibu ni kuwa hata lugha izungumzwayo humo mara nyingi si kiswahili!, Kule Commerce na Managememt kwenyewe ni battle field sasa hivi kati ya makabila mawili, zamani kama sikosei kulikuwa kama TRA tu.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
1.
Kama vile kenya kulivyo na ukabila,
Hawa wa-Kenya nimesema toka jana, kwamba ukweli wanasikitisha sana kwa sababu hii ya ukabila kwao imekuwa ni tatizo kubwa sana ambalo haliwezi kutatulika, that by it self I find it to be insane, siku moja nilihudhuria party nyumbani kwa balozi wa Kenya, I mean total insanity, kwenye party hiyo hiyo moja, ghorofa la juu kuna party ya wa-Kikuyu, na Basement kuna party ya Wa-Jaluo, lakini ni the same party ya balozi wao ambaye ni Mkikuyu, party nzima hakugusa chini kwa wa-Jaluo, at one point nikaamuuliza exactly what was going on? Akacheka tu na kusema hii mambo ya Kenya,

Mpaka leo asubuhi, wamekufa wananchi 125, swali ni for what? Ungetegemea jibu liwe kubakwa kwa Demokrasia, Yes in one way, then comes ukabila and you are lost, maana too many explainations, maana now you have to go kuanzia kwenye foundations za hivi vyama, ambako utakuta too much ishus ambazo hazihusiani kabisa na siasa wala Demokrasia, bali ukabila,

According to the dataz, investment kubwa za Wazungu zipo hasa Nairobi, na hao wawekezaji ndio haa wenye upperhand kwenye ku-influence matokeo ya uchaguzi hasa wa rais, nasikia kabla hata uchaguzi haujafanyika wa-Kikuyu, walishapanga plan A, and B, moja ya kujaribu kushinda kwa kura, na nyingine waliyoitumia jana baada ya kushindwa kura, huku Jeshi na GSU wakiwaonya tume ya uchaguzi kuwa wako tayari kwenda msituni iwapo Kibaki angeshindwa, Mwenyekiti wa tume akawakimbia waandishi chumba kimoja na kukimbilia chumba kingine na kutangaza kuwa Kibaki ndiye mshindi, the next thing US imeitambua serikali ya Kibaki, a big joke!

Kibaki na Odinga, one time walikuwa patners for Ikulu kwenye NARCO, upinzani bongo tuliwakumbatia sana hawa jamaa, lakini the minute tu walipopata power, Odinga akaja bongo na kuzungumza na waandishi pale Maelezo, akasema tena bila aibu kuwa NARCO have nothing to do na upinzani wa Tanzania kwa sababu wao sasa NARCO ni watawala kama CCM, kwa hiyo wako samba samba na CCM not upinzani. Now Odinga anajua fika kuwa njia zote walizozitumia kuingia Ikulu hazikuwa safi, na in one way or another kulikuwa pia na mkono wa Moi, kwenye kuwasaidia, sasa this time arround exactly alitegemea nini kitafanyika tofauti? Hizi political affiliations za dakika za mwisho kabla ya uchaguzi ili kukimbilia Ikulu tu zinaweza vipi kuzaa matunda mema kwa taifa?

Ukweli ni kwamba ishu kama hizi zinatukumbusha moja ya political legacy na ustaarabu wa Mwalimu, kutoruhusu huu upuuuzi bongo, I mean hawa ni watu gani ambao mpaka leo 2007, bado hawawezi kuachana na mizizi ya ukabila? Leo ukienda Nairobi, ni kawaida kusikia wananchi wakiongea kwa lugha zao, hebu jaribu kuongea kwa nguvu lugha yako Dar, uone wananchi watakvyokushangaa, halafu sio wa-Kenya tu, hata wa-Rundi, wa-Zaire, wa-Burundi ni ujinga ule ule tu, sasa kweli eti tunaungana nao kwenye EAC hawa? Wanaotuburuza huko EAC na hawa watu wa kuja kweli wanahitaji kutueleza kwa kirefu kulikoni hasa?


2.
siku za karibuni mambo mengi tanzania yanaangaliwa kwa misingi ya kidini. Majina ya watu (ya kiarabu VS ya kikristo) yanatumika sana siku hizi katika mambo mengi tu Tanzania.
Kwa kweli in general siamini kuwa hii sasa hivi ni ishu kubwa sana bongo, au kwamba tmefikia hatua mbaya sana mpaka ya kupewa our national attention, sasa inaonekana kuwa tuna un-written rule kama taifa ya kupokezana urais kati ya wa-Kristo na wa-Islam, sasa kuna the obvious kuwa rais akiwa dini flani lazima atachagua viongozi wengi wa kumsaidia kutoka dini yake na hata kabila lake, in Mwalimu case aliwatumia sana watu wa kabila lake kwenye nafasi muhimu, Mwinyi aliwatumia watu wa dini yake, Muungwana, ninaweza kusema kuwa angalau amekuwa fair somehow, ingawa onetime na yeye alianza kutumbukia kwenye dini lakini nfikri makelele yalimshitua na akaacha kama sio kupunguza,

Lakini kama kuna dataz ziwekwe tujue ukweli, lakini binafsi bado siwezi kumhukumu Muungwana, kwenye hili na sina uhakika kama bongo tunaelekea au tuko kwenye hali mbaya na hili, kwa kweli labda zitolewe more evidence, maana ya hawa wa-Kenya bado hatujafikia wakuu tena tumshukuru Mungu kwa hili.

Ahsante Wakuu.
 

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Messages
8,570
Points
0

Game Theory

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2006
8,570 0
Game Theory;
Tafadhali rejea ule msemo wa kiswahili; "hujafa hujaumbika!" au wa kiingereza usemao "never say never!" huwezi kukanusha hivyo kwani wewe bado u hai, na hujamaliza kuandika kurasa za maisha yako! Huwezi kujua ati, na kuna leo na kesho.

hizo ni assumptions tuuu

mimi kuoa huko juu hakutowezekana. Kwanza siwezi safari za kupanda Treni na pili kusema ukweli i dont find ma sista wa huko juu kama wanavutia kwangu

ndio wengi wasomi etc etc lakini there is more to mwanamke zaidi ya kuwa na degree tatu
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Quote:-

Moi kuwasaidia NARC waishinde KANU ya project yake na Uhuru Kenyatta?

Mkuu seriously, naomba nikuulize kweli unaamini kuwa Moi alitaka kuwaachia KANU power, leave alone kumuachia Uhuru Kenyatta?

Then how come this time amemsaidia adui wake wa NARC Kibaki?
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,159
Points
1,250

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,159 1,250

hizo ni assumptions tuuu

mimi kuoa huko juu hakutowezekana. Kwanza siwezi safari za kupanda Treni na pili kusema ukweli i dont find ma sista wa huko juu kama wanavutia kwangu

ndio wengi wasomi etc etc lakini there is more to mwanamke zaidi ya kuwa na degree tatu

game theory nishajua unachokitafuta, ambacho zaidi ya mwanamke.

karibu nyumbani zenji ujiopolee watoto wa pwani, uandaliwe vikuba vya athumini na udi wa maridi na machopo chopo ya kila aina.

karibu zenji kama ushaoa ukitaka kuongeza karibu na kama unataka kuoa the first hand ndio utastarehe
 

Kithuku

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2006
Messages
1,397
Points
1,250

Kithuku

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2006
1,397 1,250
Tanzania hakuna udini serikalini, hizo ni conspiracy theories tu za watu wa makundi fulani wanapoona matokeo wasiyoyapenda, hasa hasa ni za watu wachache nje ya serikali wenye udini. Mkapa alishutumiwa kuwapendelea wakristo kwenye utawala wake, mimi sikuona upendeleo wowote alioufanya, mwenye ushahidi aweke hapa. Sasa hivi kuna watu wanamtuhumu Kikwete kuwa anawapendelea waislamu katika utawala wake, sijaona upendeleo wowote alioufanya hadi sasa, mwenye ushahidi pia anakaribishwa. Namaanisha ushahidi, si maneno ya umbea ya kudai eti nasikia hivi nasikia vile!

Huo ukabila nimeuona kiasi fulani kwa makabila machache, na sasa hivi unajengeka kwa kasi mijini, hasa vyuoni na kwenye mashirika ya umma. Siku moja nilikaribishwa kwenye shughuli ya chama cha watu wa kabila fulani pale chuoni mlimani Dar, walikuwa wamealika pia vigogo wa kabila hilo kutoka universities na mashirika mbalimbali. Katika kutaja mafanikio yao, vigogo hao walikuwa wanakitaarifu chama hicho cha wanafunzi idadi ya "homeboys" waliokwisha kuwasaidia kuingia kwenye maofisi yao, na kuwahimiza kuhusu nafasi nyingine zilizoko wazichangamkie. Sasa hii ndio nepotism, maana asiyekuwepo kwenye shughuli hii atapata taarifa ya nafasi hizi zikiwa zimeshajazwa na watu wenye "sifa", maana kinachoangaliwa hapo ni cheti ambacho wote waliowahishiwa taarifa wan sifa hiyo.

Ila kwa wachagga nina maoni tofauti kuhusu jinsi wanavyoweza kumudu ukabila. Miaka 10 niliyoishi kwa wachagga, nilijifunza kuwa wachagga kama kabila hawana uwezo wala organization ya kusimama pamoja kupambana na hayo makabila mengine kama suala ni ukabila. Wao ni opportunists, wana-pair na yeyote atakayewawezesha kupata hela (awe mhindi, mwarabu,yeyote yule), na wanamtema yeyote asiyewasaidia kwenye hela hata kama ni mchagga mwenzao. Wenyewe kwa wenyewe hawana solidarity yoyote, hata wakianzisha vyama vyao vya kusaidiana kikabila huwa haimei. Kwanza kabila lenyewe la "wachagga" halipo, kuna vikabila vidogovidogo ambavyo kwa pamoja wanajiita wachaga, lakini kimsingi ni tofauti sana. Wapo wauru, wamachame, wakibosho, warombo, wavunjo, wakilema, nk, na wote hawa kila mmoja anamdharau mwenzie vibaya sana na hawawezi kufanya kitu cha solidarity kamwe. Wanaweza tu kufanya partnership ya biashara, ambayo pia wangeweza kufanya na mtu yeyote, lakini undugu hakuna! Katika shule moja niliyofundisha kulikuwa na Headmaster akiitwa Mushi (wenyewe tulimwita Mzee Mushi), basi alikuwa na tuhuma kibao, na aliyekuwa kinara wa kusukuma mbele hizi tuhuma alikuwa mchaga (sasa huyu simtaji). Siku moja nikawa interested nikamwuliza mbona unamwandama sana ndugu yako? Akanijibu "wewe, ndugu yangu gani, acha kabisa! Huyu ni mmachame ati, mmachame si mtu!". Duh, niliishiwa nguvu, nilitegemea anijibu kuwa labda hawezi kuficha uovu kwa kisingizio cha undugu, kumbe yeye anapambana na "mmachame"! Kwa hiyo hawa wanaojiita wachaga, ubaguzi wao ni katika level ambayo ni below uchaga, ambayo kitaifa madhara yake kisiasa siyaoni. Ni ma-opportunists tu kama wahindi, wanafuata pale penye maslahi ya kiuchumi kwanza (ndio maana mzee Mkapa alipochangisha yale mamilioni ya "kukomboa" majimbo ya Kilimanjaro, aliyarejesha yote CCM isipokuwa lile moja alilokuwa anamlazimishia shemeji yake, CCM wenyewe wakaamua kumpiga chini na kumpa Ndesamburo. Na bado hapo kuna "money factor" ya Ndesamburo ambaye pia ni "mzima" idara hiyo).

Kama kuna mchaga wa kuyapinga niliyosema ajitokeze, nasisitiza siwashambulii wajameni, ni wajomba wa baba yangu nawaheshimu, lakini hayo ndiyo ninayoyajua kwa undani kuwahusu. Wao ni pesa mbele, dini na kabila baadae.

Nahitimisha kusema kuwa udini Tanzania kuna kikundi cha watu wachache wanaopenda kuonesha dunia kuwa upo wakati kimsingi haupo, na kimegawanyika vikundi vidogo viwili. Akiwa rais mkristo, kile kimoja kinaamka na kudai waislamu wanaonewa, kingine kinalala. Akichaguliwa rais mwislamu, kile kingine kinaibuka kichinichini na kudai anapendelea waislamu. Labda siku tukipata asiye na dini kabisa tutaona watasemaje. Na tena kigezo chao cha kulalamika upendeleo ni kuangalia majina ya wateuliwa, ambayo wameyaweka katika makundi ya majina ya kikristo na kiislamu. Mimi siamini kuwa majina kama hayo yapo. Hivi majina John au Mary ni ya dini gani? Maana Yesu Kristo alipozaliwa alikuta tayari kuna watu wanaitwa hivyo, kwa hiyo ukristo uliyakuta hayo majina yapo. Ni ya kikristo hayo? Kwa msingi upi? Na Mihayo ni jina la dini gani? Si la kikristo kwa nini? Maana wamishenari walipokuja kutuhubiria walikuta tayari tunaitwa majina haya, kama Yesu alivyowakuta wao na majina yao. Sasa sie huku tuna matatizo, tukiona jina Gunda Mihayo, tunasema la kisukuma, lakini Mary John ati ni la kikristo, mbona ni la kizungu tu? Maftaha ni jina la kiislamu? Si la kiarabu? Na Ufunguo je, haliwezi kuwa jina la kiislamu? Au hili litaitwa la "kiswahili"? Nahisi pia tukianza kuwapa wanetu majina ya asili kama wanavyofanya wazaire labda tuhuma za udini zitapungua, lakini wataibuka wa kupekua majina ya kina "Mwakabima", "Masawe", "Rutachungululwa", na tuhuma za ukabila zitaibuliwa. Kumbe tunahitaji kwanza sura ya kitaifa kabla ya hizi dini, kabila nk, ambayo hakika itahitaji vizazi na vizazi kuijenga.

Na hao tunaowatuhumu ati wameteuliwa kwa "udini" unakuta wala hawashiki hizo dini! Maana JK angekuwa anateua mawaziri au mabosi wengine kiislamu, ningetegemea atafute ushauri wa mashehe, ili ateue waislamu "safi", kwa msingi wa dini, lakini hatujaona ushahidi wa namna hiyo.

Naishia hapa kwa leo.
 

Kitila Mkumbo

Verified Member
Joined
Feb 25, 2006
Messages
3,348
Points
1,250

Kitila Mkumbo

Verified Member
Joined Feb 25, 2006
3,348 1,250
Kithuku: kwa ushuhuda wa hao mabosi waliyojisifu kuingiza ndugu zao huko makazini kwao ndio ukabila wenyewe huo ati!

Kosa moja ambalo tumelifanya TZ ni ku-surpress analysis yeyote ya mambo on the basis of tribes and religion. Hutakuta research zikijumuisha ethnic group kama one of the demographic factors. Matokeo yake hatuna evidence ya mambo mengi kuhusu ukabila zaidi ya hisia. Kwa hiyo hoja kwamba ukabila upo au haupo itabaki siku zote kuwa indicative rather than conclusive, and this is good and bad at the same time.
 

Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2006
Messages
1,329
Points
0

Chuma

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2006
1,329 0
Kithuku umejitahidi kuelezea...Dhana ya ukabila either hujaielewa au hukusoma posts za watu huko nyuma.
Wachaga washa-move kutoka general ukabila na upo ktk Level ya umajimbo...they are on the Highest LEVEL...mfano leo wazaramo wakaanza ukabila, then ukishakuwa mkubwa watamove another step ya kusema yule ni ni kisarawe, yule wa mkuranga, or yule wa bagamoyo..or yule wa kibaha etc...na Hio ni STEPS tu...pia wanaweza ku-move huko na kwenda ktk KOO(Familia zaid)...ah ile koo ya akina MUSHI or ile...Waarabu nao wanahio...Naweza sema walofanikiwa zaid Wazungu ila nao wapo ktk UTAIFA..hapa nakusudia zaidi dhuluma au upendeleo ambayo mtu anaifanya kupendelea watu wa aina FULANI...
Ktk NCHI yetu Tanzania muhim Resource tutumie sote. HIvi vyama vya kikabila vimejaa sana VYUONI. KITHUKU ilibidi uweke wazi watu hao ulioshiriki vikao vyao pale MLIMANI ni wa KABILA GANI..ili tuupige vita..
Binafsi sichukui mtu kupeleka maendeleo kwao,its right lakin asitumie RASILIMALI za Ummah au kudhulumu wengine...
Kuhusu UDINi ushaaaauri wa Kitila juu ya UTAFITI ni kitu MUHIMU..labda kithuku nenda ukasome kitabu kilichoandika na padri Sivalon Juu ya KANISA na SIASA Tanzania.
Wakati Kitabu cha UNTOLD STORY for Muslim Stuggle against British Colonialism in Tanganyika kinatoka kuna kijana mmoja alinunua copy 2, na alipopata taarifa kuwa Mwalim Nyerere anaumwa alikwenda Kumtembelea. Nyerere alipokiona kile kitabu baada ya kukisoma few pages akasema ALIYOYAANDIKA MOHD ni KWELI ila WATU HAWATAMWAMINI, yule kijana akamwachia copy moja mwalim. na Mwalim akaambiwa kuwa copy tayari zipo mtaani.
Kundi la vijana wa Mwalim akina Prof Haroub Othman, Generali Ulimwengu na wengineo nao walimfuata MWALIM juu ya hichi kitabu, wao walimuomba mwalim ajibu, Mwalim aliwaambia yeye uwezo wa kuandika sasa haupo ila atakuwa anajibu na wao watakuwa wanaandika, Bahati Mbaya HALI ya MWALIM ilikuwa inazidi kuwa mbaya hadi UMAUTI wake ulipofika....
Issue za Mwembechai issue dhahir juu ya UDINI..etc

UDINI, UKABILA HAVITOKWISHA KAMA UTAMADUNI WA KUMWAMBIA DHALIMU/FISADI AACHE KUUNDELEZA UKABILA AU UDINI WAKE...
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,391,228
Members 528,385
Posts 34,076,486
Top