Ibambasi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2007
- 9,260
- 4,667
Kwa kuwa Katiba ya Tanzania ya 1977 inaniruhusu kutoa maoni yangu alimradi sivunji sheria, na kwa kuwa slogan/ motto/ kaulimbiu ya JF ni "where we dare to talk openly", basi napenda kusema haya yafuatayo.
Nimekuwa nafuatilia kwa kina mjadala wa Mahakama ya Kadhi na mambo ya udini kwa ujumla katika nchi yetu. Wengi wanadai kuwa Tanzania ni secular state, haina dini. Pia kuwa haipaswi kuchanganya dini na siasa katika utawala wa nchi kwani madhara yake yanafahamika.
Sawa, haya ni maoni na hoja za watu mbalimbali. Lakini mimi nataka kujua swala moja, wanasema Tanzania haina dini, je ni kwa nini katika orodha ya sikukuu zinazotambuliwa rasmi kiserikali kuna Idd, Krismas, Pasaka, etc? Hizi ninavyojua ni sherehe za zile dini zinazoitwa za "kweli",i.e Uislamu na Ukristo.
Na pia katika sherehe hizi, viongozi wa kitaifa hualikwa na kuhutubia as if wako katika shughuli za kitaifa. Sasa inakuwaje serikali ya Tanzania haiizitambui sherehe kama Diwali za wahindu au zile zetu sisi tunaoitwa "wapagani"?
Ni lini na ni wapi Serikali yetu hii imewahi kuingilia kati udhalilishaji wa dini yetu "wapagani" ambao kila siku tunatukanwa kuwa tunaabudu mashetani na hao wakristo na waislamu? Kuna mhubiri mmoja wa Kiislamu aliwahi kushtakiwa Mahakama Kuu aliposema Yesu si Mungu, na likawa zogo la kitaifa, lakini sijawahi kusikia serikali hii hii imeingilia kati kuhusu udhalilishaji wa wazi wa imani zetu za jadi na hao watu wa dini za "kweli".
Pili, viongozi wa kitaifa wanapowaita viongozi wa "dini" sijawahi kuona Mwanamalundi au Nyunguyamawe wakiwa pale Ikulu na ngozi na manyoya yao na singa zao mikononi zaidi ya kina Askofu fulani na Shehe fulani. Hii inaashiria nini kwa wale wanaodai kuwa Tanzania haina udini? Ina maana kina Mngungwa mwa Mnyenyelwa sio viongozi wa "dini"?
Tatu, katika "documents" zote za Kiserikali zinazohitaji sahihi au uthibitisho toka kwa viongozi wa dini sijawahi kuona cheo cha "mfumu" zaidi ya "padre", "imamu/sheikh", "mchungaji", na maneno kama hayo (rejea fomu za kuomba mikopo bodi ya elimu ya juu). Sasa kwa mtu kama mimi ninayeambiwa naabudu "mashetani" wapi serikali inanitambua katika hizo documents zake?
Nne, katika mijadala yote na makongamano ya kitaifa yanayohusisha viongozi wa dini nai lini kina sie tuliwahi kufuatwa na kuitwa? Je, kina Pengo watakubali kukaa meza moja na sisi tunaoabudu "mizimu" ili tujadiliane masuala ya Taifa letu?
Inavyoonekana, ukiongelea dini hapa Tanzania unamaanisha Uislamu na Ukristo. Hata huu mjadala wa Mahakama ya kadhi, wahusika wakuu wa malumbano ni hao hao. Sisi tukiamka kuchangia tuaambiwa "wapagani" na waabudu "mizimu" na "uchawi" hivyo hatuna "locus standi" ya kuongea!!
Ukweli ni kuwa Tanzania ni nchi ya dini "kuu" mbili, Uislamu na Ukristo. Ndo maana hata katika kufanya maamuzi mengi ya kitaifa wataitwa mashehe na mapadre/ wachungaji kuwakilisha upande wa kidini. Waislamu na wakristo wamefaidi rasilimali nyingi tu za nchi hii at the expense ya watu wa dini nyingine (mf. majengo ya TANESCO Morogoro kutumika kwa ajili ya chuo kikuu cha Kiislamu). Najua baadhi yenu humu mtaudhika na ukweli huu, kuwa nina "pepo" na kuwa "nishindwe na nilegee"!!!
Yapo mengi tu ya kuweza kuthibitisha kuwa nchi hii ni ya kidini na hizo dini zinafahamika.
Hivyo for any critical observer (ambaye ataweka upenzi wa kidini pembeni, Koba you get me?) ataniunga mkono kuhusu issue hii, unless aamue kufumba macho na kuita nyekundu kuwa nyeupe iliyopitiliza rangi!!!
NB:Kinachonisikitisha zaidi hizi dini "kuu" 2 ni za nje,sio zetu Waafrika na zimetumika katika maouvu yote ambayo historia ya dunia hii imeshuhudia: utumwa, ukoloni, ubepari, ukandamizaji, mauaji (kama ya wale wahindi wekundu kule Amerika ya kusini yaliyofanywa na wamisionari wa kikatoliki wa Kireno), vita vya kidini (crusades),n.k...
Tulimkosea nini Mungu sisi watu weusi?