Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!

Status
Not open for further replies.

Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,141
Points
1,500

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,141 1,500
tena ujue kufanya magwaride kama hayo ni lots of cash imetumika hapo....huu ni ufisadi mwingine unaotakiwa kupigwa marufuku,halafu wanalia lia nja njaa,pumbaf sana hawa!
 

Kalamu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2006
Messages
874
Points
0

Kalamu

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2006
874 0
Naona wengi mnatumia msamiati ambao siafiki. Mnasema serikali haina dini. Serikali ni KITU, na ni WATU tu ndio wenye uwezo wa kuwa na dini. Serikali inaweza ikawa ya dini, lakini kusema serikali haina au ina dini ni msamiati wenye makosa.

Serikali ya Saudi Arabia ni ya dini. Hatuwezi kusema ina dini. Haina utashi. Serikali ya Tanzania si ya dini yoyote. Hivyo ndivyo tunavyopenda. Lakini inatambua na kushirikiana na dini za Watanzania.

Kuna aliyesema hataki wanae walazimike kusikia kuhusu Mungu. Ili kutatua hilo, anataka wanetu walazimishwe kutosikia kuhusu Mungu! Kumuondoa Mungu kwenye Wimbo wa Taifa ni kulazimisha imani ya wale wasiomtaka Mungu iwe ndiyo imani inayotambulika na kitaifa!
But then you turn around and force your religion upon them? Either way, it doesn't fit!
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Messages
4,047
Points
2,000

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2007
4,047 2,000
Jamani iko hivi:

Serikali yetu haina dini, ila inaamini uwepo wa mungu, ndiyo maana mungu anatajwa hata katika wimbo wetu wa taifa. "kutokuwa na dini" does imply "kutokuwepo mungu", isipokuwa the vice-versa is true. Mimi ninavoelewa hata wapagan wanaamin kuwa kuna mungu, sema tu sasa issue inakuwa katika mode of worship wanayotumia inakuwa tofauti kidogo na ya wakristo, au dini zingine. Ni sawa tu kama ambavyo wahindu na wakristo au waislamu wanavyoweza kutofautiana katika namna yao ya kuabudu. Ni atheists tu ndiyo wanaoamini kama hakuna mungu.

Lakini sasa, tumnachagua viongozi kwa kutumia democracy, kwamba the majority becomes the winners.bila kujali dini, ni dhahiri kuwa zaidi ya 50% ya watanzania wanaamini uwepo wa mungu.

Je kuna sababu gani sasa ya msingi kuizuia serilkali yetu pia kuamini hilo? Kuna sababu zipi za msingi za kifanya serikali yetu isitoe support za sherehe za kidini iwapo inaamini uwepo wa mungu? Atheists ni wangapi watuambie sasa wanataka nini na serikali wanahitaji iwafanyie nini, na si kuanza kutaka kuvuruga uhusiano mzuri uliopo kati ya serikali na mungu pamoja na dini zingine.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati mwingine tunakuwa ma-radical muno kiasi kwamba hata pale ambapo srikali haina doa, tuanjitosa kwa nguvu zote kukikosoa. Nadhani tunakuwa muno "zaidi ya wapinzani"
kila la kheri
 

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
5,028
Points
1,500

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
5,028 1,500
Kwanini hii nyuzi isipelekwe kwenye mambo ya dini? Au kwa sababu inaconnection na siasa? Hata hivyo ni ukweli usiofichika kuwa wakristo ni kama mabwege wao wana ile ya "ukipigwa kofi kushoto geuza kulia". Kama watu mnaweza kukumbuka wakristo walikuwa na shule nyingi tu, serikali ikazitaifisha na kuzivuruga vuruga, wao wakasema hewala.

Ingawa si vizuri kusema ukiangalia serikali ya Mkapa mambo mengi yanayohusu waislamu alikuwa anaogopa kuyafanya, au alikuwa anafanya mambo mengine tofauti na utashi wake just because he of fear. Aliwahi kusemewa mbovu kwenye msikiti mmoja kule mbagala live radioni na hakujibu lolote.

Kuna mengi ya kuayaorodhesha lakini yote ni useless...............
 

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2006
Messages
2,368
Points
2,000

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2006
2,368 2,000
Pamoja na ukweli kwamba Serikali ya Tanzania si ya dini yoyote, viongozi wake wana dini zao. Kiongozi aliyelewa madaraka anaweza kutumia taasisi za serikali kwa shughuli za dini yake. Hilo ndilo limefanyika huko Zanzibar.

Vyombo vya ulinzi na usalama vinaweza kutumika kulinda amani wakati wa sherehe za kidini. Kwa maoni yangu, kutumia Jeshi la Tanzania kufanya gwaride wakati wa sherehe za kidini ni kutumia madaraka vibaya sana. Tushauriane kama kuna sheria imevunjwa kwa kufanya hivyo. Ni nani mwenye mamlaka ya kuamrisha Jeshi lifanye gwaride ya kusherehekea sikukuu ya kidini?
 

Tanzania 1

Senior Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
197
Points
0

Tanzania 1

Senior Member
Joined Oct 4, 2007
197 0
Jamani, Hakuna Mtu Asiyekuwa Na Dini, Km Kweli Tutafuata Tafsiri Halisi Ya "dini". Hao Wanaosemekana Hawana Dini, Basi Hizo Taratibu Zao Za Maisha Ndio Dini Zao.
 

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,777
Points
1,195

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,777 1,195
Jamani wenye fani ya sheria,
Saidieni tunataka huyu aliye vunja katiba ya nchi yetu kwa kutumia pesa ya walipa kodi kuandaa gwaride la 'Eid' awajibishwe ili liwe funzo kwa hawa wanao chezea sheria na katiba yetu!
 

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
3,367
Points
1,195

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
3,367 1,195
JAMANI IKO HIVI: SERIKALI YETU HAINA DINI, ILA INAAMINI UWEPO WA MUNGU, NDIYO MAANA MUNGU ANATAJWA HATA KATIKA WIMBO WETU WA TAIFA.

"KUTOKUWA NA DINI" DOES IMPLY "KUTOKUWEPO MUNGU", ISIPOKUWA THE VICE-VERSA IS TRUE. MIMI NINAVOELEWA HATA WAPAGAN WANAAMIN KUWA KUNA MUNGU, SEMA TU SASA ISSUE INAKUWA KATIKA MODE OF WORSHIP WANAYOTUMIA INAKUWA TOFAUTI KIDOGO NA YA WAKRISTO, AU DINI ZINGINE. NI SAWA TU KAMA AMBAVYO WAHINDU NA WAKRISTO AU WAISLAMU WANAVYOWEZA KUTOFAUTIANA KATIKA NAMNA YAO YA KUABUDU. NI ATHEISTS TU NDIYO WANAOAMINI KAMA HAKUNA MUNGU. LAKINI SASA, TUMNACHAGUA VIONFGOZI KWA KUTUMIA DEMOCRACY, KWAMBA THE MAJORITY BECOMES THE WINNERS.BILA KUJALI DINI, NI DHAHIRI KUWA ZAIDI YA 50% YA WATANZANIA WANAAMINI UWEPO WA MUNGU.

JE KUNA SABABU GANI SASA YA MSINGI KUIZUIA SERILKALI YETU PIA KUAMINI HILO? KUNA SABABU ZIPI ZA MSINGI ZA KIFANYA SERIKALI YETU ISITOE SUPPORT ZA SHEREHE ZA KIDINI IWAPO INAAMINI UWEPO WA MUNGU? ATHEISTS NI WANGAPI WATUAMBIE SASA WANATAKA NINI NA SERIKALI WANAHITAJI IWAFANYIE NINI, NA SI KUANZA KUTAKA KUVURUGA UHUSIANO MZURI ULIOPO KATI YA SERIKALI NA MUNGU PAMOJA NA DINI ZINGINE.

TATIZO NINALOLIONA NI KWAMBA WAKATI MWINGINE TUNAKUWA MA-RADICAL MUNO KIASI KWAMBA HATA PALE AMBAPO SRIKALI HAINA DOA, TUANJITOSA KWA NGUVU ZOTE KUKIKOSOA. NADHANI TUNAKUWA MUNO "ZAIDI YA WAPINZANI"
KILA LA KHERI
Makanyaga ..I salute your comments sir... Nimefanya kuhighlits tu! Yaani Bottom Line is ...

DINI NA MUNGU NI MAMBO MAWILI TOFAUTI KABISA. MUNGU HANA DINI NA UNAWEZA KUMUAMINI BILA KUPITIA DINI. NAFIKIRI KAMA SIKOSEI MUNGU HATAMBUI DINI YEYOTE KAMA SEREKALI YETU TUKUFU!
 

Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2006
Messages
1,329
Points
0

Chuma

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2006
1,329 0
Wengi hatujui tofauti kati ya mungu na DINI. matokeo yake kuna watu wanaamini wanaweza kuishi bila mungu au DINI...
Hili ni somo pana sana na hapa JF square hapatoshi labda tupeana assignemnt kila mmoja azifanye kujifunza zaid.

DINI-ni mfumo wowote wa maisha ambao mwanadam kaamua kuufuata. Hivyo kila mtu ana DINI. inawezekana tu dini hio haina jina rasmi as Ukristo au Uislam...kwa utaratibu huo u-socialism nao ni dini..na mifumo mingine ya ulimwengu
[wengi wameelewa vibaya maana ya dini kwa kuinasibisha na IMANI, na ndo maana wengi wamekuwa wakisema dini ni IMAN..oh upendo n so on]...
Mungu- Maana ya Mungu ni kitu chochote unachokitumikia. Ikiwa MATAMANIO ya NAFSI Yako unayatumikia basi hayo yatakuwa Mungu wako. Wengi wameinasibisha maana ya mungu na supernatural powers. Ikiwa mtu bosi wake anamtumikia basi yeye huyo ndie mungu wake...
 

Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2006
Messages
1,329
Points
0

Chuma

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2006
1,329 0
Kuhusu Gwaride la Karume, mie huwa siafiki kwanini vyombo vya serikali vitumike..lkn pia baadhi ya wachangiaji wamekuwa wakichanga mada makusudi kupotosha.
ZNZ na TGnyika zimeungana lkn kila moja ina Historia yake... na ndio maana Leo ZNZ mwezi wa ramadhan wana sheria za kutokula HOVYO ktk PUBLIC. pia sikukuuu zao za EID ni nyingi kuliko Tanganyika..
Serikali ya Bara au Muungano kwa muda mrefu imekuwa ikitumia FUNDS zake pia vibaya...Chunguzeni...
 

JC

Member
Joined
Dec 19, 2007
Messages
43
Points
0

JC

Member
Joined Dec 19, 2007
43 0
Wengi hatujui tofauti kati ya mungu na DINI. matokeo yake kuna watu wanaamini wanaweza kuishi bila mungu au DINI...
Hili ni somo pana sana na hapa JF square hapatoshi labda tupeana assignemnt kila mmoja azifanye kujifunza zaid.

DINI-ni mfumo wowote wa maisha ambao mwanadam kaamua kuufuata. Hivyo kila mtu ana DINI. inawezekana tu dini hio haina jina rasmi as Ukristo au Uislam...kwa utaratibu huo u-socialism nao ni dini..na mifumo mingine ya ulimwengu
[wengi wameelewa vibaya maana ya dini kwa kuinasibisha na IMANI, na ndo maana wengi wamekuwa wakisema dini ni IMAN..oh upendo n so on]...
Mungu- Maana ya Mungu ni kitu chochote unachokitumikia. Ikiwa MATAMANIO ya NAFSI Yako unayatumikia basi hayo yatakuwa Mungu wako. Wengi wameinasibisha maana ya mungu na supernatural powers. Ikiwa mtu bosi wake anamtumikia basi yeye huyo ndie mungu wake...
Wakati na soma reply zote Nilifikiri Azimio jipya amefanya uchambuzi wa kina na wakutosheleza ...But Umenielimisha zaidi..kuhusu swala la DINI,hapo sina tatizo kabisa. Shida yangu ipo kwenye maelezo yako kuhusu MUNGU.

Je ukimtumikia Shetani...Utalielezaji hili? Ni kiwa na maana kuwa Mwingine anamtumikia Mungu Na mwingine anamtumikia sheteni. Wote watakuwa wanamtumikia MUNGU?
 

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2007
Messages
461
Points
0

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2007
461 0
mhhhh kazi kweli kweli.

halafu basi kule ktk BARAZA LA EID jamaa wanakata milo ya nguvu,nasikia pesa zinatoka IKULU.halafu waalikwa wa pale wengi wao mawaziri,wabunge wakurugenzi etc,yaani weee acha tu.

mie nahisi mheshimiwa angefanya la maana kama siku za EID akawa anajumuika na wazee wasijiweza kama kule NYUMBA YA WAZEE SEBLENI au akausanya mayatima au hata akapeleka misaada pale hospitali ya mnazi mmoja,kuliko kuwaalika hao mawaziri wake.

then ile khutba anaweza hata kufanya LIVE akiwa IKULU.
 

Mwafrika

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2006
Messages
5,490
Points
0

Mwafrika

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2006
5,490 0
Ni kweli kuwa mambo mengi kenya yanafanyika kwa kuangalia majina na sehemu ya kuzaliwa kama ilivyo kawaida ya nchi nyingi za Afrika. Hili la uchaguzi unaokwisha ambao umeleta mzee kikongwe mwingine madarakani (miaka 76) na kinachoendelea sasa hivi ni lazima kifundishe mataifa mengine.

Kama vile kenya kulivyo na ukabila, siku za karibuni mambo mengi tanzania yanaangaliwa kwa misingi ya kidini. Majina ya watu (ya kiarabu VS ya kikristo) yanatumika sana siku hizi katika mambo mengi tu Tanzania. Nilisikitika sana kuambiwa kuwa hata mashuleni siku hizi chaguzi za viongozi wa wanafunzi pia ni kwa misingi ya kidini!

Badala ya kukaa tunatoa macho kuwapondea wakenya kwa kile ambacho kimefanyika, ni vyema sasa Tanzania pia tukaacha haya ya udini ambayo sasa hata yanagawanya waislam (shia dhidi ya sunni) na wakristo ( walokole dhidi ya wasiookoka).

Tusipoacha hili, tusubiri tena vizazi vingine vitatu ili kupata maendeleo yale tunayopigania kwa mama yetu afrika.
 

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Messages
8,570
Points
0

Game Theory

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2006
8,570 0
Ni kweli kuwa mambo mengi kenya yanafanyika kwa kuangalia majina na sehemu ya kuzaliwa kama ilivyo kawaida ya nchi nyingi za Afrika. Hili la uchaguzi unaokwisha ambao umeleta mzee kikongwe mwingine madarakani (miaka 76) na kinachoendelea sasa hivi ni lazima kifundishe mataifa mengine.

Kama vile kenya kulivyo na ukabila, siku za karibuni mambo mengi tanzania yanaangaliwa kwa misingi ya kidini. Majina ya watu (ya kiarabu VS ya kikristo) yanatumika sana siku hizi katika mambo mengi tu Tanzania. Nilisikitika sana kuambiwa kuwa hata mashuleni siku hizi chaguzi za viongozi wa wanafunzi pia ni kwa misingi ya kidini!

Badala ya kukaa tunatoa macho kuwapondea wakenya kwa kile ambacho kimefanyika, ni vyema sasa Tanzania pia tukaacha haya ya udini ambayo sasa hata yanagawanya waislam (shia dhidi ya sunni) na wakristo ( walokole dhidi ya wasiookoka).

Tusipoacha hili, tusubiri tena vizazi vingine vitatu ili kupata maendeleo yale tunayopigania kwa mama yetu afrika.


Tunaomba ushahidi kuwa TANZANIA kuna UDINI, na ulifikia vipi conclusion kuwa Tanzania kuna udini
 

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
17,527
Points
2,000

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
17,527 2,000
..tanzania kuna UDINI na UKABILA pia. rejea post inayohusu uteuzi wa Othman Rashidi kuhusu udini, na ile ya TRA kuhusu ukabila. specifically kuna chuki ya dhahiri dhidi ya wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro.
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,389,666
Members 527,997
Posts 34,031,439
Top