Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,017
- 12,305
Moja ya kosa kubwa lililo fanyika Tanzania toka utawala wa awamu ya kwanza ni kushindwa kupambana na udini.
Kilichofanyika wakati wa Nyerere na sasa ni kupambana na udini kwa kutengeneza udini wa dini hizi mbili Ukristo na Uislam.
Sio kweli kuwa Tanzania hakuna udini kama katiba inavyosema. Tanzania kuna udini wa ukristo na uislam ulio sogezwa karibu zaidi na serikali.
Huwezi sema unapambana na udini kwa kutengeneza udini wa ukristo na uislam muda huo huo.
Ni wiki kadhaa zimepita nilihoji hapa kuhusu uhalali wa Rais kutoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la KKKT Moshi majibu niliyopata humu yalinisikitisha sana.
Watu wanazipenda sana dini zao kuliko kupenda matumizi ya akili katika kuchanganua mambo.
Moja ya madhara ya dini katika utawala ni kutumika kulitawala vyema tabaka tawaliwa, hapa ndio sehemu rahisi zaidi kutawala watu wako vyema. matumizi ya akili katika dini kwa watu yapo chini sana kuliko sehemu yoyote ile.
Samia akitoa pesa katika ujenzi wa nyumba zenu za ibada mnaona sawa tu wala hamjiulizi ila viongozi wa dini wakisema wanakubaliana na serikali mnachukizwa. Ni kipi hasa kinacho wachukiza ?
Mnashindwa kuchukizwa na Rais kuvunja vipengele vya katiba kwa kushiriki kutangaza dini fulani kinyume na katiba inavyosema ila kwa ukosefu wenu wa akili mnasema Rais anadumisha upendo baina ya Watanzania.
Hivi Watanzania mnajua maana ya serikali isiyo na dini kweli ?