Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!

Status
Not open for further replies.

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
5,622
2,000
Samahani wandugu, hivi Kauli ya Serekali ya tanzania, Uganda na Rwanda kwenye uchaguzi wa Kenya ni Vipi??
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
Kithuku,

nakubaliana na maelezo yako kuhusu "wachaga." ni kweli kabisa kuwa wamegawanyika ktk jamii ndogo ndogo kama wamachame,wauru,warombo,wamarangu etc etc.

katika hoja ya ukabila TRA watu walifikia mpaka kuunda kabila "WAKILIMANJARO." hiyo yote ilikuwa katika jitihada zao kujenga hoja kwamba wenyeji wa Kilimanjaro ni wakabila, madhalimu, na maadui wa maendeleo ya Tanzania.

inawezekana serikali yetu haina UDINI au UKABILA, lakini mwenendo wa posting mbalimbali hapa, na facts on the ground, ni kwamba ktk jamii yetu kuna watu wana matatizo na waimani kwamba yamesababishwa na watu wa dini na makabila mengine.

hali hii inayojitokeza inawafumba macho watu kuona jinsi wanavyoweza kujisaidia au hata misaada wanayopewa.

mfano, malalamiko ya ujenzi wa barabara ya rombo-tarakea yalisubiri mpaka Waziri Mramba alipohamishiwa wizara ya ujenzi. Waziri Magufuli aliyeanzisha mradi huo hakulaumiwa. Sasa hivi waziri Chenge yupo huko kelele hazisikiki tena.

tumefika mahali watu wanaamini kwamba Tanzania nzima imedhulumiwa na maendeleo yamepelekwa kilimanjaro. kama hilo lingekuwa kweli, na kwa kuzingatia udogo wa mkoa huo naamini Kilimanjaro ingekuwa inameremera kama Ulaya.


Chuma,
harakati za uhuru hazikuwa ktk misingi ya kidini bali KITAIFA. hata kama mashekhe na maimanu walishiriki harakati hizo nina imani kwamba walifanya hivyo kwa kutokana na UZALENDO wao na siyo DINI yao.

Mwalimu alifunga Ramadhani na watu walimuombea duaa. Lakini Mwalimu huyohuyo alifanyiwa MATAMBIKO mbalimbali ili azma yetu ya kupata Uhuru ifanikiwe. harakati zile zilijumuisha watu wa dini na imani mbalimbali.

Waislamu wenyewe walishaukataa UDINI kwa kuwakemea Sheikh.Takadiri na Zuberi Mtemvu. Sasa sijui kwanini vijana Waislamu wa leo wanajaribu kuturudisha nyuma na kudai kwamba harakati zile zilikuwa za Kidini.

Ni kweli kabisa historia ya Uhuru/Tanu imepindishwa. Pia wako waliotoa mchango mkubwa ktk harakati zile lakini hawakupewa heshima yoyote. Hilo halikuishia kwa wanaharakati waumini wa Kiislamu peke yao.

Kwa kifupi Mwalimu hakupenda upinzani wowote ule wa kisiasa. Mwalimu hakujali kwamba wewe ni Mkatoliki mwenzake au Muislamu ktk "kushughulikia" wapinzani.

Umezungumzia rasilimali za umma. Hivi wenyeji wa Kilimanjaro siyo sehemu ya umma wa Watanzania?
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,512
2,000
August,
Nchi zote zimekaa kimya, conveniently. Utapongeza nini? Mauaji? Uchomaji moto wa majumba? Kibaki naye hajaonekana hadharani tangu aapishwe.
 

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,397
1,250
Kithuku: kwa ushuhuda wa hao mabosi waliyojisifu kuingiza ndugu zao huko makazini kwao ndio ukabila wenyewe huo ati!

Kosa moja ambalo tumelifanya TZ ni ku-surpress analysis yeyote ya mambo on the basis of tribes and religion. Hutakuta research zikijumuisha ethnic group kama one of the demographic factors. Matokeo yake hatuna evidence ya mambo mengi kuhusu ukabila zaidi ya hisia. Kwa hiyo hoja kwamba ukabila upo au haupo itabaki siku zote kuwa indicative rather than conclusive, and this is good and bad at the same time.
Kitila nakubaliana na wewe kabisa. Sasa hivi inajengeka neo-tribalism ambayo iko institutionalized, na hatari yake ni ya wazi kuliko udini. Wajua waafrika twashikamana na kabila zetu zaidi kuliko dini zetu? Asilimia kubwa tunafuata desturi na imani za makabila yetu sambamba na dini za kigeni, ni vigumu kumpata mtanzania aliyelikana kabisa kabila lake na kubaki na dini ya kigeni pekee. Inafaa sasa kuangalia pia influence of the tribe as a variable in individual decisions and choices, and my hypothesis is that the effect of the tribe, on the aggregate, far surpasses that of religion.

Athari za udini hata hivyo, kama udini nao utajisimika, ni mbaya kwa sababu ya external influences maana wenye dini watatafuta washirika wa nje, ambao hawa hakika watakuwa ni wanasiasa wagombanaji tu na wala si waenezaji imani! Ila kama nilivyosema awali, sijaona ushahidi wa wazi wa udini Tanzania, ila naona institutional neo-tribalism. Mbaya hii!
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,978
2,000
Wakati Kitabu cha UNTOLD STORY for Muslim Stuggle against British Colonialism in Tanganyika kinatoka kuna kijana mmoja alinunua copy 2, na alipopata taarifa kuwa Mwalim Nyerere anaumwa alikwenda Kumtembelea. Nyerere alipokiona kile kitabu baada ya kukisoma few pages akasema ALIYOYAANDIKA MOHD ni KWELI ila WATU HAWATAMWAMINI, yule kijana akamwachia copy moja mwalim. na Mwalim akaambiwa kuwa copy tayari zipo mtaani.

Myths again! Huyu kijana nani? Ni lazima mkali ambaye aliweza kuwa na access ya kirahisi kwa Mwalimu(RIP). Myth kama hizi ndiyo zinaendekeza udini. Kwani kulikuwa na haja gani kumuingiza Mwalimu(RIP) ili ku'legitimize' claims za kitabu? Kwani Mwalimu (RIP) alikuwa pekee yake kwenye struggle? Na jee, hao waislamu (nakiri sijasoma kitabu hiki) wali'struggle' kama waislamu against colonialism au kama watanganyika? Kama wali'struggle' kama waislamu walikusudia nini baada ya kuushinda ukoloni? Taifa la kiislamu? Tusiwapandikizie udini wale waliotufikisha hapa tulipo. Tukitaka kubomoa yale waliyotuachia tufanye hivyo bila kupindisha michango yao. Ni wengi tuu ambao hawakupewa credit kwenye vita ile. Ndivyo historia ilivyo. Mchango wa wanawake na watu weusi katika independence struggle ya wamarekani umeanza kutambulika hivi karibuni. Mchango wa watu wasio wazungu katika kumng'oa Hitler hivyo hivyo. Turudie upya historia yetu lakini tuwe wakweli. Tusijenge hoja kufit context ya sasa hivi. Hatutakuwa tunatenda haki. Mawazo kama haya ndiyo yanayowafanya waKikuyu kuona wao ndio wastahili kutawala Kenya kutokana na vita ya Majimaji. Na washona vilevile Zimbabwe dhidi ya wamatabele. Msitupeleke huko.
 

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,605
2,000
Nilikaa Katika Kijiji Kimoja Hukolindi,kule Watakupiga Na Kukuloga Ukila Nguruwe Lakini Ukileta Pombe Hasa Bia Pale Wanakupa Kiwanja Ili Ujenge Baa.mnaona Matatizo Yetu Haya
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,978
2,000
Nilikaa Katika Kijiji Kimoja Hukolindi,kule Watakupiga Na Kukuloga Ukila Nguruwe Lakini Ukileta Pombe Hasa Bia Pale Wanakupa Kiwanja Ili Ujenge Baa.mnaona Matatizo Yetu Haya
Mimi sioni tatizo. Ndiyo uniqueness yetu. Hatukuwa extremists wakati ule. Tulichukuwa dini zote hizi, tukazi'interpret' kwa mazingira yetu. Mzee wa kanisa ana wake kibao! Wakristu kwenda kufagia na kutambika makaburini. Waislamu kukukaribisha pombe. Mkristo kula daku wakati wa Ramadhani.Waislamu kuimbisha pambio kwenye misiba. Ndivyo tulivyokuwa. Yote yalifanyika na hakuna aliyeona ubaya. Ni sisi wa siku hizi ndiyo tunataka kuleta matatizo.
 

Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,607
1,500
To this point i don't see the facts of the arguments. Tanzania never experienced udini before, if you real want to see how udini look like, then try Lebanon.
 

FDR Jr

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
249
0
dhambi ya kubagua ni kama dhambi ya kula nyama ya mtu; huwa haikomi. Ukimshabagua huyu inabidi utafute mwingine wa kumbagua hadi mwisho unaanza kubagua watu wa nyumba yako mwenyewe!
Yeye aliyeyatamka haya pia aliandamwa na dhambi hiyo mpaka pale alipochukuliwa na mungu,hakuwa mdini wala mkabila bali hakuwa tayari kufungumana na wale wote aliotofutiana nao kisera au msimamo, ni dhambi iliyoiletea umaskini mkubwa Tanzania.

Mungu ampe rehema na amsamehe dhambi zake kwani kwa kutueleza haya yote ktk siku zake za mwisho duniani alimaanisha kukiri udhaifu wake kama binadamu na kutubu kwa mungu wake na sisi ndugu zake.
Mwalimu pumzika kwa Amani
 

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,329
0
JOKAKUU- Kimsingi waislam walimkumbusha Mwalim Dhuluma alizokuwa anazifanya dhidi ya waislam. Walimkumbusha kuwa matunda ya UHURU ni yetu sote si watu FULANI. Nukta za Takadiri ni kusisitiza kuwa Muslims waliweza kumtenga mwislam mwenzao kwa lengo lao la awali likuwa TANGANYIKA HURU..
SOON Baada ya UHURU Mwalim alifanya makubwa kudidimiza maendeleo ya waislam...Vijana wa KIISLAM wa sasa na wazamani lengo lao ni kuikumbusha Jamii ya Tanganyika HURU kuwa TULILETA UHURU ili kuondoa DHULUMA dhidi ya MKOLONi ambae alikaaa in FAVOR of Christians.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,978
2,000
Vijana wa KIISLAM wa sasa na wazamani lengo lao ni kuikumbusha Jamii ya Tanganyika HURU kuwa TULILETA UHURU ili kuondoa DHULUMA dhidi ya MKOLONi ambae alikaaa in FAVOR of Christians.
Myths, insinuations etc. etc. Unataka kutuambia ni waislamu peke yao waliopigania uhuru maana wakristu walikuwa wanafaidika nao? Unataka kutuambia kuwa ukoloni uliwekwa ili kuwalinda wakristo? Na hao waarabu waliotuuza kama mboga walikuwa wakristu? Hao waliotuhasi na kutuweka kwenye harem zao walikuwa wakristu? Udini, udini usio na msingi!
 

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,329
0
Fundi...waislam hawakuwa na lengo la dola la kiislam..hilo ni kosa la JINAI kwasasa na hata wakati ule wa Mkoloni...
TUKUBALI KUWA SASA KTK TANGANYIKA HURU DHULUMA YA AINA YOYOTE HAITOZAA MATUNDA MEMA KWA YOYOTE. Wislam wasikae kudhulum wakristo na Wakristo wasidhulum waislam...What is going on now...christian wachache walipo ktk MAMLAKA wanaona NCHI hii wao wana HAKI nayo kuliko wengine...na hapa ndipo kwenye Tatizo...IWEJE HAKIMU WA MOROGORO ASEME KUWA ALIETUNGA QURAN ASHITAWE? anapata wapi ujasiri HUU?...KIHISTORIA TANGANYIKA hapakuwa na vita yoyote ya UDINI, AMANI imekuwa moja ya TABIA ZETU...IELEWEKE WAISLAM HAWATAKI UPENDELEO KAMA ULE WANAOPEWA WANAWAKE...WANATAKA FAIR PLAY KILA MTU APEWE HAKI ZAKE...
 

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,329
0
Fundi kasome kitabu..UKUMBI hautoshi...Mwandishi kaeleza kila mkoa nani alikuwepo ktk struggling za UHURU...Hatusemi waislam peke yao ndio waliopigania Uhuru...ila waislam walikuwa FRONTIERS kwa wakati kwani MFUMO wa UKOLONI wao Uliwaathiri zaidi kulino wengine...
UTUMWA ni mada pana...hapa si mahala pake...
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,978
2,000
Careless words. Huwezi kuwahukumu wakristo wote kwa mapendo ya mpuuzi mmoja. Kuna waislamu wangapi ambao nao wametamka maneno ya ovyo? Mara ngapi tumewasikia wakitangaza fatwa, kudai mtu anastahili achinjwe n.k. kwa vile hawakubaliani na aliyoyatenda? Napo tuseme waislamu WOTE wana nia mbaya na wakristo? Umesahau mbwa Immigration aliyehukumiwa kifo na hakimu? Wapuuzi wako pande zote na hakuna dini yenye monopoly kwenye hili. Kutumia vitendo vya hawa wachache kuhalalisha imani kuwa wote wanachukia upande mwingine ndivyo wenzetu walivyofikia walipofika. Kwenye uzembe uliofanyika kuhusu mahujaji, watu kutoka dini hizi mbili walihusika. Kwa jinsi unavyoongea itaonekana kama vile ilikuwa ni conspiracy ya Vatican kumtumia David. Tuwe waangalifu tunaporusha hizi accusations. Mhukumu mtu na siyo dini yake.
 

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,329
0
Sahaman Fundi..Issue ya Mahujaji ni ingine huko UZEMBE PLUS... NO UDINI ni UZEMBE KAMA ilivyo sehem zingine.
Pia si kweli kuwa Kiongozi wa Mahujaji alisema MTU achinje media wame-exagrate...nimesoma ile ripoti ya ATC na nimeongea na muhusika kwanza alishangaa...so fanya tafiti kaka.
Pia sikusema wakristo wote, nimesema wale wachache waliopata MAMLAKA.soma vizuri acha jazba...
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,978
2,000
Fundi kasome kitabu..UKUMBI hautoshi...Mwandishi kaeleza kila mkoa nani alikuwepo ktk struggling za UHURU...Hatusemi waislam peke yao ndio waliopigania Uhuru...ila waislam walikuwa FRONTIERS kwa wakati kwani MFUMO wa UKOLONI wao Uliwaathiri zaidi kulino wengine...
UTUMWA ni mada pana...hapa si mahala pake...
Kwa mtazamo huo, wazanaki wanastahili heshima ya pekee kwa vile Nyerere alitoka kwao? Hata nikikisoma haitasaidia kitu kwa maana ni maneno ya mtu mmoja. Waislam walishiriki kwenye mapambano, wakristu walishiriki na wasio na dini pia. Wote hawa wanastahili kuenziwa bila MMOJA wao kudai yeye ndiye aliyestahili sifa zaidi. Hauwezi kutumia dini kuhukumu ukoloni na kukataa kuangalia utumwa ambao hadi sasa unaendelea Mauritania, Sudan n.k. Saudi Arabia waliondoa utumwa mwaka 1959. Mimi sitaki kuingia huku maana naamini wote hawa walimwona mtu mweusi kuwa sub-human na ndivyo walivyohalalisha dhuluma dhidi yetu. Kamsome Frantz Fanon ndugu yangu.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,978
2,000
Sahaman Fundi..Issue ya Mahujaji ni ingine huko UZEMBE PLUS... NO UDINI ni UZEMBE KAMA ilivyo sehem zingine.
Pia si kweli kuwa Kiongozi wa Mahujaji alisema MTU achinje media wame-exagrate...nimesoma ile ripoti ya ATC na nimeongea na muhusika kwanza alishangaa...so fanya tafiti kaka.
Pia sikusema wakristo wote, nimesema wale wachache waliopata MAMLAKA.soma vizuri acha jazba...
Kwa vile wamehusika waislamu imekuwa uzembe mtupu? Angekuwa David peke yake ungeiangalia hivyo? Matamshi kuwa kuna mtu( na sio kiongozi wa mahujaji) alidai mtu achinjwe yalikuwa kwenye ripoti na siyo kunukuu kutoka kwa media.Chuma, kama nilivyosema, careless words zina matatizo yake. Ulitumia kigezo cha hawa wachache kuwa wakristo kuwahukumu. hapo ndipo kwenye tatizo. Ungewahukumu kama wazembe tuu bila kuingiza udini nisingekuwa na tatizo. Mimi naogopa masuala yote yenye kiharufu cha udini na ukabila na nina amini ni wajibu wetu wote kukemea pale yanapojitokeza.
 

Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,140
1,500
naamini matatizo mengi ya afrika yataisha kama katiba zetu zitalinda na kuheshimu liberty ya mtu as individual,ukabila/udini unaanza pale mtu anapoona anaonewa na kuanza kutafuta ile sense of belonging ambayo ndio inazaa ukabila au udini ....katiba nzuri inayofocus uhuru na haki za mtu binafsi itafanya tusahau hayo mambo ya ukabila na udini
 

Tom

JF-Expert Member
May 14, 2007
472
0
Si udini wala ukabila bali ni kukata tamaa na maisha. Watu hukata tamaa pale wanapofanya kazi kwa bidii lakini bila kupata matunda mazuri ya kazi zao tokana na uongozi mbaya ama pale wanapojua kuwa hata watoto wao hawatakua na future yeyote. Vurugu na mauaji yanayotokea Kenya ni njia tu ya kutafuta mchawi ni nani.

Yanayotokea Kenya, TZ pia yanaweza tokea ili mradi tu itokee kundi la wakereketwa walio tayari kulipa chochote kwa ajili ya haki yao. TZ tuna wakereketwa wa CCM, lakini CCM imekua ikishinda uchaguzi na ndio maana inaonekana TZ pana amani. CCM wasiporebisha UFISADI wao wategemee wakereketwa wapinzani kuongezeka, na hapo ndio itakua kivumbi. Na kama itakuwa CHADEMA basi moto utalipuka zaidi.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,978
2,000
Naomba nijisahihishe. Soko la watumwa lilipigwa marufuku mwaka 1962. Wakati sisi tunasherehekea uhuru kuna wenzetu walikuwa wanapigwa mnada Saudi Arabia!
 
Status
Not open for further replies.
Top Bottom