Kwani kulikuwa kuna ulazima gani wa kununua hizo ndege? Wakati magufuli anaingia madarakani, Precision na fast jet walikuwa wanafanya vizuri sana kwenye soko la ndani!
Kwa nini tusingewekeza nguvu kubwa kuboresha/kujenga viwanja vingi vya ndege ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi? Tena ni kipindi hicho shirika letu la ATCL lilikuwa na ndege sijui mbili zile (mbovu mbovu) huku likiwa na wafanyakazi 200! Na hivyo kuifirisi tu nchi kwa kuwalipa wafanyakazi wasio fanya kazi!
Sasa mzee wako kwa kupenda sifa na kwa kutokupenda kushaurika au kujiridhisha kwanza, akakurupuka nakununua madege lukuki, likiwemo lile li dreamliner! Ona sasa zinavyo zalisha hasara!