Taratibu Uzee na Nadhifu: Rubani wa ndege ya jet na rubani mkongwe wa airbus

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
TARATIBU,UZEE NA NADHIFU;RUBANI WA NDEGE YA JET NA RUBANI MKONGWE WA AIRBUS.

Leo 11:05hrs 17/07/2022

Ndege ya Airbus 380 ikiambaa juu ya bahari ya Atlantic,Ndege ya kivita Jet inatokea,rubani wa ndege ya kivita aina ya Jet anapunguza mwendo,anaambaa karibu kabisa na ndege ya Airbus,anachukua radio call anampigia rubani wa ndege ya Airbus,anamsalimia anamwambia "Airbus ni ndege inayoboa eeh!!?" Ebu angalia ndege yangu aina ya Jet,

Rubani wa ndege ya Jet anairusha kinyume nyume kama inaruka sarakasi,anapunguza mwendo anaachia milio fulani ya ndege ya kivita,anairusha juu umbali fulani ambao kiumbe kikiruka kinakosa hewa ya oksijeni,anaishusha chini kwa kuchumpa kama mtu anaruka kupiga mbizi majini,anairudisha tena juu hadi ubavuni mwa ndege ya Airbus ananyanyua radio call anampigia rubani wa Airbus,anamuuliza umeionaje hiyo,rubani wa ndege ya Airbus anamwambia "hiyo safi sana" nawe angalia hii,

Rubani wa ndege ya Jet akiwa nyumba pembeni ya ndege ya Airbus anaiangalia kwa dakika 15,lakini hakuna kinachofanyika,ndege ya Airbus iliendelea kurua speed ile ile katika mstari mnyoofu,baada ya dakika 15 rubani wa ndege ya Airbus ananyanyua radio call anamuuliza rubani wa ndege ya Jet,vipi umeionaje hiyo!? rubani wa ndege ya Jet anashangaa sijaona kitu,kwani nini umefanya!?

Rubani wa Airbus anacheka, anamwambia niliinuka nikanyoosha miguu yangu,niliacha ndege ikienda yenyewe nikatembea hadi mwisho wa korido ya ndege,nikaingia chooni,nikatoka nikaenda kupata kifungua kinywa na chocolate kidogo,halafu nimerudi,rubani wa ndege aina ya Jet akamwambia "heshima kwako mkuu wangu"

Funzo;-
Unapokuwa kijana,mpya kazini,damu inachemka kila kitu unakiona kipya na unataka kukifanya,lakini unapoendelea kukua na kufika umri wa Mwalimu wako utagundua kuwa vyote si chochote,cha muhimu ni faraja na amani ya moyo,dedication kwa Wakongwe wenzangu,msiogope ndege aina ya jet zilizotuzunguka,tuendelee kufurahia amani na faraja tunayoipata kwenye ndege yetu ya Airbus,Nawatakia jumapili njema.
 
Kama huna hang up yoyote kwenye masuala ya ujana na uzee huna haja ya kuji justify kwa vyovyote vile.
 
Back
Top Bottom