Tungekopa Ndege (Boeing, Airbus) tungefaidikaje?

Tungekopa Ndege (Boeing, Airbus) tungefaidikaje?

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,845
Reaction score
14,071
Habari za Asubuhi wadau!

Kwa wakazi wa Dar es Salaam poleni na mvua.

Nimeona taarifa ya Prof: Mussa Assad aliyewahi kuwa CAG wa Tanzania juu ya taarifa yake ya kupondea ununuaji wa ndege kwa Cash, binafsi ile habari imefikirisha sana na naomba wanazengo leo mnisaidie kwa maswali yangu machache ambayo nafikiri yatasaidia ata member wengine humu ndani kupata elimu ya kile tunachokipondea ama kukitetea.

Kwanza nikiri wazi kuwa mimi ni muumini kindakindaki wa Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

Maswali yangu ni haya hapa chini.

1. Tungeenda kukopa ndege zetu kwa wanaotengeneza ndege (Boeing/ Airbus/ Bomberdier) tungefaidika vipi zaidi ya tulivyozinunua kwa Cash?

2. Tungekodi Ndege kama ilivyokuwa zamani baada ya kuingia enzi za JK tukaingia ubia na Shirila la ndege la South Africa na mwisho wa siku tukabaki na madeni makubwa tukidaiwa na Shirika hilo kwa ATCL isingetucost?

Nafikiri maswali yangu aya machache yanajitosheleza kama ni bora kukopa au bora kukodi? Maana nimeona ata KQ imepata hasara zaidi ya Mabilioni ya Fedha japo wamekopa pia ndege zao.
 
Kwani kulikuwa kuna ulazima gani wa kununua hizo ndege? Wakati Magufuli anaingia madarakani, Precision na Fastjet walikuwa wanafanya vizuri sana kwenye soko la ndani!

Kwa nini tusingewekeza nguvu kubwa kuboresha/kujenga viwanja vingi vya ndege ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi? Tena ni kipindi hicho shirika letu la ATCL lilikuwa na ndege sijui mbili zile (mbovu mbovu) huku likiwa na wafanyakazi 200! Na hivyo kuifirisi tu nchi kwa kuwalipa wafanyakazi wasiofanya kazi!

Sasa mzee wako kwa kupenda sifa na kwa kutokupenda kushaurika au kujiridhisha kwanza, akakurupuka nakununua madege lukuki, likiwemo lile li Dreamliner! Ona sasa zinavyozalisha hasara!
 
Kwani kulikuwa kuna ulazima gani wa kununua hizo ndege? Wakati magufuli anaingia madarakani, Precision na fast jet walikuwa wanafanya vizuri sana kwenye soko la ndani!....
Umelielewa swali langu bwa shekhe?
 
Umelielewa swali langu bwa shekhe?
Mkuu point in kwamba kwa nchi yetu Tanzania ambayo bado in masikini kuanzisha mradi Wa ndege ni sawa na maskini Wa huko kigoma kulazimisha kutembelea v8 wakati hana uhakika Wa kula Milo mitatu kwa siku.

Kukopa isingetufaidisha.

Kukodisha isingetufaidisha.

Hapa issue ilikuwa kutengeneza mazingira rafiki ya kibiashara watu waje kuwekeza wenyewe nchini kwetu ,kw a safari za anga.

Over
 
Mkuu point in kwamba kwa nchi yetu Tanzania ambayo bado in masikini kuanzisha mradi Wa ndege ni sawa na maskini Wa huko kigoma kulazimisha kutembelea v8 wakati hana uhakika Wa kula Milo mitatu kwa siku...
Ok nashukuru kwa ufafanuzi wako.

Basi kwa namna hii kumbe hakuna haja ata kupondea kununua Ndege Cash bali hoja iwe hatukuoaswa kuwa ndege za ATCL kwa sasa.
 
Wewe kweli mataga, hujui kwamba mkopo unalipa kidogo kidogo, wakati huo huo maendeleo mengine yanaendelea kufanyika.

Kuliko unateketeza fedha nyingi kwa wakati mmoja huku maendeleo ya upande wa pili yanasimama.

Nimejibu swali.
 
Kwani kulikuwa kuna ulazima gani wa kununua hizo ndege? Wakati magufuli anaingia madarakani, Precision na fast jet walikuwa wanafanya vizuri sana kwenye soko la ndani!

Kwa nini tusingewekeza nguvu kubwa kuboresha/kujenga viwanja vingi vya ndege ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi? Tena ni kipindi hicho shirika letu la ATCL lilikuwa na ndege sijui mbili zile (mbovu mbovu) huku likiwa na wafanyakazi 200! Na hivyo kuifirisi tu nchi kwa kuwalipa wafanyakazi wasio fanya kazi!

Sasa mzee wako kwa kupenda sifa na kwa kutokupenda kushaurika au kujiridhisha kwanza, akakurupuka nakununua madege lukuki, likiwemo lile li dreamliner! Ona sasa zinavyo zalisha hasara!
CAG anasema hizo ndege hazitengenezeki na nje haziwezi kwenda.
 
Elewa na wewe Bashite, tungelipa kidogo kidogo na fedha zingine kuelekezwa kwenye elimu na afya
Good..!! Bajeti ya Wizara ya Afya unaifahamu? Kitu gani kilikwama mara baada ya ununuzi wa ndege nchini?
 
Wewe kweli mataga, hujui kwamba mkopo unalipa kidogo kidogo, wakati huo huo maendeleo mengine yanaendelea kufanyika.

Kuliko unateketeza fedha nyingi kwa wakati mmoja huku maendeleo ya upande wa pili yanasimama.

Nimejibu swali .
Sisi ni matajiiriiiiii
Tena mandege mengine tumenunua keeeshiiii
 
CAG anasema hizo ndege hazitengenezeki na nje haziwezi kwenda .
Nje zinaweza kwenda kwa baadhi ya mataifa, ukanda wa Asia hauna shida sana tofauti na ukanda wa Magharibi, madeni ya ATCL yapo Magharibi.
 
Wewe kweli mataga, hujui kwamba mkopo unalipa kidogo kidogo, wakati huo huo maendeleo mengine yanaendelea kufanyika.

Kuliko unateketeza fedha nyingi kwa wakati mmoja huku maendeleo ya upande wa pili yanasimama.

Nimejibu swali .
Kwanza ieleweke kwamba tungekuwa tumekopa yamkini tungekuwa na ndege moja mpaka leo hii.. pili ukikopa maana utalipa zaidi ya vile ulivyonunua cash na mwisho kabisa lini sehemu fulani ilikosa pesa yakuendesha mradi fulani kisa tu hizo hela zilienda kununulia ndege?
 
Back
Top Bottom