Aliyeozeshwa mtoto ahukumiwa miaka 30 Jela

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe tarehe 16 Februari 2024 imemhukumu mshtakiwa GIVEN MICHAEL NZUNDA (24) Mkulima, mkazi wa Shilanga kutumikia Kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la Kubaka.

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 15, 2023 maeneo ya Shilanga, Kata ya Ihanda Tarafa ya Vwawa ambapo alituhumiwa kuozeshwa mtoto mwenye umri wa miaka 14 na kuishi nae kama mke na mume jambo ambalo ni kosa kisheria.
 
Huyo bwana mdogo mikosi imemuandama tayari.

Matendo hayo yapo sana katika jamii yetu, hasa kwa wasichana wanaoishia shule ya msingi, huozeshwa kwa makubaliano ya wazazi.

Sijasikia maneno matatu muhimu: 'kutoroshwa', 'mwanafunzi' na 'kubaka', badala yake naona tu 'kuozeshwa'.

Kwani sheria ya ndoa ya '71 ya Tz inayotumika sasa hivi inasemaje kuhusu umri wa msichana wa kuolewa?

Naiona njia ya rufaa ya kumtoa ipo upande wake akipata wanasheria wazuri.
.
 
Huu nao ni upuuzi mwingiine wa police na mahakama, zetu.
Unamfunga mwanaume aliyeoa binti wa miaka 14,

Lakini wazazi wa binti na shehe aliyeozesha hiyo ndoa wapo uraiani.
 
Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe tarehe 16 Februari 2024 imemhukumu mshtakiwa GIVEN MICHAEL NZUNDA (24) Mkulima, mkazi wa Shilanga kutumikia Kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la Kubaka.

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 15, 2023 maeneo ya Shilanga, Kata ya Ihanda Tarafa ya Vwawa ambapo alituhumiwa kuozeshwa mtoto mwenye umri wa miaka 14 na kuishi nae kama mke na mume jambo ambalo ni kosa kisheria.
TAARIFA NJEMA SANA HII
KIJANA KARIBU URAIANI 2039
 
Mambo ya hovyo kabisa, kesi gani hiyo ya kijinga namna hiyo.

Kaozeshwa, wazi wameridhia shida iko wapi? Au bint alilazimishwa?
 
Kama binti hasomi na tayari katiba ya nchi inampa mtu mamlaka ya joa binti wa umri huo ikiwa ameridhia mwenyewe pasipo shuruti, jamaa ameonewa sana
 
Huu nao ni upuuzi mwingiine wa police na mahakama, zetu.
Unamfunga mwanaume aliyeoa binti wa miaka 14,

Lakini wazazi wa binti na shehe aliyeozesha hiyo ndoa wapo uraiani.
Ulikuwa hujui kuoa mtoto ni kosa kisheria? Wewe unachukuliaje mtoto wa miaka 14 kuolewa?
 
Back
Top Bottom