Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Hataweza Fanya lolote huyu mpuuzi,na kama anaamini kuwa atakuwa rais basi amepotea sana,
Kikubwa msiibe kura basi. Mwaka huu kura zinapigwa vituoni, tunazilinda na matokeo yote yanatangazwa vituoni. Ni ngazi zote udiwani, ubunge hadi uraisi.

Kama mlikuwa hamjui kuhusu nguvu ya umma, mwaka huu ndo mtaiona. Enough is enough!!
 
Mna ubavu huo.Anyway kama kweli atuletee uthibitisho.Hata hivyo ukweli ni kwamba kapewa na mabeberu.Na kama ni hivyo,atawalipaje?Narudia tena,hfai ataiuza nchi.
Akuletee uthibitisho wewe kama nani??? Tumemchangia watanzania kwa upendo wetu kama tulivyowachangia kina mbowe kwenye kesi mliyowafunga kidhalimu mahakamani kisutu na tukawatoa gerezani
 
Napenda sana Mh. saana Mwenyekiti wangu Magufuli apate tena nafasi kwa miaka 5 kumalizia ngwe yake.

Shauku yangu kubwa ni ili apate kumalizia miradi aliyoianzisha. Haijalishi amebana vipi watu, ila awamu ya pili anapaswa kulenga watu sio vitu na huku akimalizia projects zake.

ILA pia namkubali sana Lissu, uwepo wake ni muujiza unaoishi, na kawaida muujiza huwa hautokei tu kwa bahati mbaya, bali ipo sababu na kusudi.

Nimalizie kuwakumbusha wanaLumumba wenzangu kuwa MUNGU anaishi, anaamua, na yule aliyemridhia ndiye atakayepita.

Wakati wa Mungu unapofika, hakuna cha kuzuia lililo lake (Rejea Mhubiri 9:11).
Ndugu yaangu una imani nzuri kwa Mungu.
Nami nakwambia tulimwomba Mungu atupe rais wa namna hii ya Magufuli, naye Mungu akayakubali maombi yetu, tumempata.
Pia maendeleo ya watu yanapatikanaje bila kuwatengenezea njia ?
Na hizo njia ndo hizo mnazoziita maendeleo ya vitu!!
 
Safari hii ni bampa kwa bampa, mkifanya ule ujinga kama wa LUBUVA tunaingia barabarani ili tumtoe kwa nguvu huyo jemedari wenu kama LAURENT GBAGBO.
Mje kwa wingi barabarani ile muione CORONA HALISI inavyofanya kazi.
 
Maalim Seif angekuwa na moyo wa aina hii, Zanzibar kingekwisha eleweka tayari. Na ndio maana watawala walitaka ufe. Wanakujua vizuri.
Serikali wala haikuwahi kuwa na shida na karoho kake.
Huyo walipigana kanzu na wenzake kwenye madili yao.
 
Hiyo ndio Kauli ya Mh Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye uchaguzi mkuu mwezi October 2020. Ataingiza watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.

View attachment 1526711

My take: Ni mapema Sana kwa mgombea urais kutoa kauli Kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Anasema akiibiwa. Atashindwa ki halali kabisa. Ni mgombea mzuri, lkn timing yake ndo ina shida. Angesubiri magufuri amalize muda wake ili aje apambane na atakaye kuja. Kwa nini magufuri?

1. Amebana wizi kwenye madini, tumeibiwa sana kapunguza. Bado kwenye dhahabu, bado ndege zinabeba na kupeleka ulaya

2. Miradi ya maji, sasa angalau anafanya. Kuna watu wako ziwani lkn hawana maji miaka 60 ya uhuru, yeye anaendelea kuyasogeza.

3. Umeme wa stiglers gorge, itakuwa historia mpya. Lissu na akina zitto wanakubaliana kuwa tunaharibu mazingira. Magufuri miaka mitano ataitumia kumaliza mradi huo.

4. Sgr ni mradi wa magufuri, pia kufufua reli na bandari zilizokufa siku nyingi. Hii ndo heshima ambayo Kenya wanajiharishia sasa

5. Kuongeza mapato ya serikali hadi trillions of money. Ndiyo maana tumeingia nchi ya kipato cha kati.

6. Seriousness katika kutatua kero halimashauri. Magufuri hana mfano

7. Kufufua shirika la ndege

8. Taasisi za kifedha kukusanya ukwasi hadi kutamani kuwekeza nchi za kibepari kama kenya ni juhudi za magufuri.

9. Daraja la kigongo Lissu anaweza likata maana atakuja na vipaumbele vyake.

10. Upinzani wote waliingia kwenye mtego wa skendo za covid, kama siyo magufuri hata mimi nilimchukia lkn ameniprove wrong. Zito na akina mbowe wangekuwa wameifunga nchi kwa hekaya za corona. Magufuri ni visionary leader maana wote waliofunga wanalazimika kufuata njia za Tanzania.

Hayo machache na mengine ni sababu za Magufuri kupewa muda zaidi ayamalizie na atunyoshee hawa wakenya.

Anayo mabaya machache lkn hayapiti mazuri aliyoyafanya kwa miaka mitano. Tumpe muda magufuri
 
Utani kusema unampelekea mama yako mzazi mwanaume tena mbele za watu baada ya kupewa tu jogoo??? Tunatania kwenye dada zetu na watoto zetu sio mama zetu wazazi
Unaujua utani wa Wasukuma, Wazilaghembe nk.wewe?Acha kujifanya unajua kila kitu.
 
Hiyo ndio Kauli ya Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi October 2020.

Tundu Lissu amepitishwa na CHADEMA kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Lissu amenukuliwa akisema ataingiza Watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.


My Take: Ni mapema sana kwa Mgombea wa Urais kutoa kauli kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.

MKUU LISSU KASEMA IWAPO AKIIBIWA KURA sasa wewe unavosema eti MY TAKE: hata akishindwa kihalali ataawambia watu waingie barabarani ili kutimiza azma yake hiyo kauli umeitoa wapi au umemsikia wapi? Itendee haki dhamiri yako!!
 
Hawezi kisema hivyo:

Jamani chungeni kauli zenu, mgombea urais aaenze kwa kauli hiyo, tena ametoka Ulaya juzi si watu wataamini ametumwa?

Mnataka tusimpigie kura tu.

Hawezi, tena akionyesha dalili hiyo atapishana na gari la mshahara
 
Kama Lissu sio presidential material Magu anayeropoka kumpa mama yake mzazi mwanaume baada ya kupewa jogoo yeye ni nani??!
Ahaa,sawa.Hivi unafikiri nchi anapewa mtu yeyote.Kama unadhani ni hivyo you are wrong.Maalim Sefu kiko wapi,miaka nenda miaka rudi si anahangaika tu.
 
Hiyo ndio Kauli ya Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi October 2020.

Tundu Lissu amepitishwa na CHADEMA kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Lissu amenukuliwa akisema ataingiza Watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.


My Take: Ni mapema sana kwa Mgombea wa Urais kutoa kauli kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
mbona kaongea vizuri tu,majambazi wanaweweseka
 
AJE ATANGULIE YEYE AKUMBANE NA VIRUNGU VYA MAMBOSASA ARUDI TENA UBERJIJI KUJIUZA
Tundu kwanza ni muoga utafikiri mtoto wa kike.
Aliwahi kugoma kutoka mahakamani, kwamba kuna askari wanamsubiri akitoka wamkamate. Siku hiyo mpaka kubembelezwa rpc akatoka nae huku jamaa analia.
 
Acheni kumlisha maneno
Alisema hivi na Nukuu

"Mimi sio yule wa kusema namwachia Mungu"
Hata hii ina ukakasi kidogo
Maana kuna Mungu na Ibilisi
Sasa akijitoa kwa Mungu anasimamiwa na ibilisi?

Kupona kwake ni mkono wa Mungu

Hautaki tena? Asitakafullulilah

Amekuwa Goliath? Kwa hapo ametoa Helmet Daud apige jiwe sasa
 
Lisu ndo mjumbe sasa wa ku deal na Magufuli.

Na hizi ndo mbinu za wajumbe sasa. Ukiiba kura ni spana tu tunaingia road.

Unatoa hutoi
Na ID yako inatoa ruhusa kufanyiwa ufyonso, utafanyiwa siku hiyo ukipona unaenda kwa Gwajima
 
Mleta mada wewe ndo wale watu mnasikilizaga habari kwa mihemuko, Ni Wapi ulisikia TL akitamuka maneno hayo.
Nanukuu alichokisema; "Tuchague mgombea ambae atakuwa na uwezo pamoja na Utayari wa kuwaingiza wananchi barabarani pale itakapohitajika" TL.

Je Umeona kaongelea nafsi hapo au ndo unatumia makalio kuelewa.
Aaah. Inabidi sasa nisikilize mwenyewe.
Ni hivyo?
Amechaguliwa yeye kwahiyo
"Anatuingiza barabarani? Aingie mwenyewe.
 
Keki ya taifa inamanufaa kwa watanzania wote?, Hao unaowatete wamefanya Jambo gani la msingi kwa mwananchi,hatari ipo kwa wananchi kwa maneno aliyotamka sema tunachotaka ni maendeleo thabiti tu
Hakuna anayetetewa, msingi wa keki ya Taifa ni amani na utulivu.
Kwa maana hiyo watu wakiingia barabara ndio sululu ya kugawana keki ya Taifa?
Mifano iko mingi, kuna baddhi ya nchi waligawana hiyo keki sawa sawa lakini leo hii hakuna hata uma wala kisu cha kukatia Keki zaidi ya kuruhusu mirija ya mabeberu kufyonza rasilimali zao.
Maendeleo thabiti yapo ndio maana leo tuna uhuru wa kusema chochote kwa kadri tuwezavyo ili mradi tusivuke mipaka.
Kwa mfano hayo yasemwayo yakitokea nini faida kwako?
 
Back
Top Bottom