Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Ina maana nawewe ni kati ya watu wasiyo julikana?
Hapo mbona bado sana ngoja muda wa campaign aanze kuongelea mambo ya kuvunja muungano, kumwita Nyerere mtu wa ovyo na hadithi yake isiyoisha ya risasi kumi 16.

Jamaa ni narcissist he rates himself so highly wenzake wanaenda kwenye campaign kwa porojo za watawafanyia nini wananchi, yeye anakwenda na agenda ambayo anaifahamu mwenyewe.

Yaani kichwani kwake keshaanza kuchagua rangi ya pazia atazoweka Ikulu; ni swala la muda kabla ya watu kukubali huyu mtu anahitaji psychological intervention ajatulia bado kutokana na mkasa uliompata na wala hana sifa za high office.
 
Hiyo ndio Kauli ya Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi October 2020.

Tundu Lissu amepitishwa na CHADEMA kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Lissu amenukuliwa akisema ataingiza Watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.


My Take: Ni mapema sana kwa Mgombea wa Urais kutoa kauli kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Lini ccm waliwahi kushinda uchaguzi kihalali???
 
Nawazungumzia watanzania hawahawa ambao walilazimisha Mwalimu Nyerere ang'atuke mwaka 1985. Au unadhani alikuwa anataka kuachia madaraka ??? Soma historia ufahamu matukio ambayo yule Mzee alifanyiwa na watanzania kuanzia mwaka 1980-1985: Halafu ukiwa na ufahamu utatambua kwamba kama busara haitatumika basi tunaweza kuona ule ukurasa mwekundu unajirudi hapa nchini. Be vigilant my friend, Raisi Magufuli analivuruga Taifa.

Ubaya wa Afrika ni huu, tofauti kabisa na Ulaya ambako mapinduzi yalifanywa na wananchi huku kwetu huwa yanaanzishwa na maafisa wa vyombo vya usalama wakishirikiana na wanasiasa. Nimesoma vizuri siasa za mapinduzi duniani kama sehemu yangu ya masomo ya Chuo Kikuu,na nikafanya Case Study yangu Afrika.

Hivyo navyokwambia kwamba Tanzania iko pabaya sana namaanisha ninachokwambia maana dalili zote zinaonekana, na sifahamu kwanini wenzangu ambao ni wasomi na mko Serikalini au kwenye chama hamyaoni haya na hamna hata chembe ya woga. Tunaweza tukakaa hapa JF tukiandika Propaganda kuwatishia wananchi vifo lakini ukweli ni kwamba watu ambao wanaweza kulivuruga hili taifa na serikali wako huko huko serikalini (TISS, JWTZ na CCM).

Soma vizuri historia na uchambue mambo kwa hekima utafahamu kwamba Lissu is not a threat entirely but an agent of chaos or in other words A man who opens Pandora's box.
Hiki ndio nilikuwa nawaambia watu juzi.
 
Anasema akiibiwa. Atashindwa ki halali kabisa. Ni mgombea mzuri, lkn timing yake ndo ina shida. Angesubiri magufuri amalize muda wake ili aje apambane na atakaye kuja. Kwa nini magufuri?

1. Amebana wizi kwenye madini, tumeibiwa sana kapunguza. Bado kwenye dhahabu, bado ndege zinabeba na kupeleka ulaya

2. Miradi ya maji, sasa angalau anafanya. Kuna watu wako ziwani lkn hawana maji miaka 60 ya uhuru, yeye anaendelea kuyasogeza.

3. Umeme wa stiglers gorge, itakuwa historia mpya. Lissu na akina zitto wanakubaliana kuwa tunaharibu mazingira. Magufuri miaka mitano ataitumia kumaliza mradi huo.

4. Sgr ni mradi wa magufuri, pia kufufua reli na bandari zilizokufa siku nyingi. Hii ndo heshima ambayo Kenya wanajiharishia sasa

5. Kuongeza mapato ya serikali hadi trillions of money. Ndiyo maana tumeingia nchi ya kipato cha kati.

6. Seriousness katika kutatua kero halimashauri. Magufuri hana mfano

7. Kufufua shirika la ndege

8. Taasisi za kifedha kukusanya ukwasi hadi kutamani kuwekeza nchi za kibepari kama kenya ni juhudi za magufuri.

9. Daraja la kigongo Lissu anaweza likata maana atakuja na vipaumbele vyake.

10. Upinzani wote waliingia kwenye mtego wa skendo za covid, kama siyo magufuri hata mimi nilimchukia lkn ameniprove wrong. Zito na akina mbowe wangekuwa wameifunga nchi kwa hekaya za corona. Magufuri ni visionary leader maana wote waliofunga wanalazimika kufuata njia za Tanzania.

Hayo machache na mengine ni sababu za Magufuri kupewa muda zaidi ayamalizie na atunyoshee hawa wakenya.

Anayo mabaya machache lkn hayapiti mazuri aliyoyafanya kwa miaka mitano. Tumpe muda magufuri
Umenena vema sana mkuu nimekuelewa.
 
Hiyo ndio Kauli ya Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi October 2020.

Tundu Lissu amepitishwa na CHADEMA kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Lissu amenukuliwa akisema ataingiza Watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.


My Take: Ni mapema sana kwa Mgombea wa Urais kutoa kauli kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Amesema akiibiwa kura, siyo akishindwa - soma hiyo tweet vizuri
 
...Tanzania inapita katika kipindi kigumu kuliko wakati wowote ule. Kama hatutakuwa makini basi tutakuja kuikumbuka hii miaka kwa masikitiko sana huko mbeleni.
Tupo kwenye uchumi wa kati mkuu hicho kipindi kigumu ni kipi tena?...😂😂😂
 
MKUU LISSU KASEMA IWAPO AKIIBIWA KURA sasa wewe unavosema eti MY TAKE: hata akishindwa kihalali ataawambia watu waingie barabarani ili kutimiza azma yake hiyo kauli umeitoa wapi au umemsikia wapi? Itendee haki dhamiri yako!!
Kwani hilo neno MY TAKE wewe umelielewaje mkuu?
 
Hata Kama tukiweka tume ya namna gani na uchaguzi ukiwa huru kiasi gani akishindwa bado hato kubali kuwa kashindwa kwasababu tayari kesha weka dhana mbaya kuwa ataibiwa kura.

Yaani kwake yeye uchaguzi huru na haki ni ule tu ambao yeye atashinda Ila akishindwa tu basi uchaguzi huo si huru na haki kwake.
Hiyo sasa ni extreme! Tufanye haki alafu tuanzie hapo. Na pia mashaka ya wapinzani, wote tunajua msingi wake, hasa kama tulikuwepo Tanzania, hata wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa tu, wacha chaguzi zile za maisha ya Aquilina Aquline!
 
Back
Top Bottom