Iwapo mwaka ujao Sheikh Ponda akisema kama Waislam tumeamua kumpigia kura Rais Samia

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
Jun 26, 2014
543
682
Katika uchaguzi uliopita Sheikh Ponda allibukia kuiunga mkono CHADEMA na akatoa kuwa 'WAISLAM TUMEKUBALIANA KURA ZOTE ZA URAIS TUTAMPIGIA TUNDU LISSU'.

Kauli hii iliungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Waislam isipokuwa Bakwata ambao mkakati wao wamejiegemeza zaidi kwa CCM.

Bahati mbaya kwa CHADEMA wamekuwa ktk kampeni ya Okoa Bandari. Kampeni iliyowaongezea ushawishi wa wananchi kwa mikoa ya bara ambayo kimsingi hawajui manufaa ya kiuchumi yanayopatikana kwa wananchi, wakati huo huo imezidi kujipotezea ushawishi kwa mikoa ya mwambao wa habari ya hindi.

Dalili ya kukataliwa alionekana siku ya ufunguzi kule temeke.

Na katika hili Sheikh Ponda yuko upande wa fikra zilizo mioyoni mwa watu wa mwambao kuwa Mkataba usisitishwe bali yafanyiwe marekebisho.

Katika suala la uchaguzi Sheikh Ponda mara zote husisitiza kupiga kura ya Maslahi.
Kwa maana ya kupiga kura kwa mgombea aliyeonyesha kuwa na sera zenye maslahi kwa waislam.

Ktk hali hii mgombea aliyetanguliza maslahi ni Mama Samia.

Swali ni hili: Iwapo mchakato wa waislam unaoendelea wa kuwaunganisha viongozi wa kiislam na taasisi wanazoziongoza; wawe na kauli moja juu ya mgombea gani watakaemuunga mkono; ambae kimsingi ni Mama Samia.....

Swali ni je Bakwata Watapinga kweli kama walivyopinga 2020.

Ktk hali kama hii tunadhani ndoto ya CHADEMA kuchukua dola itakuwepo tena.


View: https://youtu.be/uF_HyFwGwNU?si=De0knfVJGFewTJBy
 
Mkataba ukaandikwe upya

Huu wa sasa jinsi ulivyo haufai.

Siasa ni kukamata hisia za watu.

Hali ilivyo ni kwamba jamii ya watu wa mwambao wanaamini "Shida ya viongozi wa CHADEMA hawataki mwarabu uwepo bandarini.
Screenshot_20230715-140230_Twitter.jpg
 
Hata chadema msimamo wao ni huu:


"Na katika hili Sheikh Ponda yuko upande wa fikra zilizo mioyoni mwa watu wa mwambao kuwa Mkataba usisitishwe bali yafanyiwe marekebisho"
Wengi wa viongozi na wanachama wa kawaida wanahisiwa; hawawataki kabisa waarabu. Na kwamba mkataba sio yafanyiwe marekebisho. Bali ufutwe usiwepo
 

Attachments

  • Screenshot_20230715-140230_Twitter.jpg
    Screenshot_20230715-140230_Twitter.jpg
    190.4 KB · Views: 1
Saa 100 amejichokea muacheni apumzike.....inajulikana wazi amechoka!! Nchi ngumuu hiiii
 
Samia kushinda ni 100% ila shekhe ponda hana haki ya kuwashikia watu kauli kila mtu ana chagua lake ....Binafsi siwezi kupigia kura chadema hata agombee niliyezaliwa nae tumbo kama chama ni chadema siwezi kumpigia kura.
 
Waarabu ni wajomba zetu, Sisi tunataka kuchanganya damu tuzae mashombe shombe.
Teh teh teh
Ukisema hivi unawachoma mioyo wagalatia manake wao akitajwa mwarabu ni wanaleta picha ya Ustadh kaenda kuposa mwana parokia.
Hatari sana
 
Inategemea kuna Wagalatia wangapi nchini!
Maswala ya kura ni siri sio za makundi unategemea mtu yupo kwenye shavu serikalini atapenda mfumo ubadilike? Au mimi nipo maisha yangu hayaeleweki nimehangaika kutafuta kazi nimekosa naona watoto wa vigogo wanapeana mashavu nitaipa kura ccm?
Kwahiyo hayo mambo ya dini na makundi ni ujinga tu kura kiuhalisia watu wanaangalia maslahi binafsi kwanza then ndio ya wengine
Hivi bakwata ulikuwa unawwqmbia kitu kwa magu au makonda?
 
Back
Top Bottom