Tundu Lissu: Hawa wanaoongoza Tanzania sasa hakuna aliyewachagua, ndio maana hawatetei Wananchi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,780
218,404
Akihutubia Umati wa wananchi huko Tabora , Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu anesema kwamba viongozi wanaoongoza Tanzania kwa sasa hawawatetei wananchi kwa vile hawakupigiwa kura.

Akizungumza kwa kujiamini huku akitoa mifano kadhaa iliyo hai mbele ya Mwenyekiti wake Mbowe na Mbele ya umati wa Wananchi wa Tabora, Lissu amedai kwamba kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na ule wa madiwani, Wabunge na wa Rais 2020, hakuna kura yoyote aliyopiga mwananchi iliyotoa kiongozi. Wote mnaowaona walipita bila kupingwa au walitangazwa tu.

Lissu amedai kwamba hata ukimuuliza Dr. Samia leo atutajie idadi ya kura za Urais ambazo yeye na Magufuli walipata 2020 hawezi kuzitaja kwa sababu hakuna mahali popote zilipoandikwa.

Amesisitiza kwamba Viongozi ambao hamkuwachagua hawawezi kuwa na uchungu na nyinyi, ndio maana hawawatetei na wanawatwanga tozo za kufa na kupona.

Toa Maoni yako.
 
Akihutubia Umati wa wananchi huko Tabora , Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu anesema kwamba viongozi wanaoongoza Tanzania kwa sasa hawawatetei wananchi kwa vile hawakupigiwa kura .

Akizungumza kwa kujiamini huku akitoa mifano kadhaa iliyo hai mbele ya Mwenyekiti wake Mbowe na Mbele ya umati wa Wananchi wa Tabora , Lissu amedai kwamba kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 , na ule wa madiwani , Wabunge na wa Rais 2020 , hakuna hakuna kura yoyote aliyopiga mwananchi iliyotoa kiongozo , wote mnaowaona walitangazwa tu .

Lissu amedai kwamba hata ukimuuliza Dr Samia leo atutajie idadi ya kura za Urais ambazo yeye na Magufuli walipata 2020 hawezi kuzitaja kwa sababu hakuna mahali popote zilipoandikwa .

Amesisitiza kwamba Viongozi ambao hamkuwachagua hawawezi kuwa na uchungu na nyinyi , ndio maana hawawatetei na wanawatwanga tozo za kufa na kupona .

Toa Maoni yako
Mia mia kama asemavyo figganigga
 
Kushindwa ni matokeo yanayoumiza sana na kukabiliana na kushindwa hususani kwa mtu mweusi mara nyingi huwa ni ngumu sana kuliko kwa wenzetu. Lissu anasumbuliwa na kutokukubali kushindwa na maumivu yanayoambatana na hiyo Hali.

Hata kama kuna hiyo Imani inayoaminiwa sana na upinzani ya kuibiwa kura Lissu alipata 13% ya kura zote ,idadi ambayo ukweli tu usemwe asingeweza kushinda.

Uongo huu CCM wanatakiwa kuutolea majibu kwa kuelezea mchakato mzima wa upigaji kura ili aumbuke na uongo wake.
 
Hayo matokeo umeyatoa wapi ikiwa hayakuandikwa popote ?
 
Akihutubia Umati wa wananchi huko Tabora , Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu anesema kwamba viongozi wanaoongoza Tanzania kwa sasa hawawatetei wananchi kwa vile hawakupigiwa kura .

Akizungumza kwa kujiamini huku akitoa mifano kadhaa iliyo hai mbele ya Mwenyekiti wake Mbowe na Mbele ya umati wa Wananchi wa Tabora , Lissu amedai kwamba kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 , na ule wa madiwani , Wabunge na wa Rais 2020 , hakuna kura yoyote aliyopiga mwananchi iliyotoa kiongozi , wote mnaowaona walipita bila kupingwa au walitangazwa tu .

Lissu amedai kwamba hata ukimuuliza Dr Samia leo atutajie idadi ya kura za Urais ambazo yeye na Magufuli walipata 2020 hawezi kuzitaja kwa sababu hakuna mahali popote zilipoandikwa .

Amesisitiza kwamba Viongozi ambao hamkuwachagua hawawezi kuwa na uchungu na nyinyi , ndio maana hawawatetei na wanawatwanga tozo za kufa na kupona .

Toa Maoni yako
Ameyasema hayo mbele ya Mwenyekiti Mbowe!!!! Unataka kusema nini bwashee?? Alitaka ujumbe umpate mlamba asali?
 
Kushindwa ni matokeo yanayoumiza sana na kukabiliana na kushindwa hususani kwa mtu mweusi mara nyingi huwa ni ngumu sana kuliko kwa wenzetu. Lissu anasumbuliwa na kutokukubali kushindwa na maumivu yanayoambatana na hiyo Hali.

Hata kama kuna hiyo Imani inayoaminiwa sana na upinzani ya kuibiwa kura Lissu alipata 13% ya kura zote ,idadi ambayo ukweli tu usemwe asingeweza kushinda.

Uongo huu CCM wanatakiwa kuutolea majibu kwa kuelezea mchakato mzima wa upigaji kura ili aumbuke na uongo wake.
Wakiweza kueleza mchakato ulivyokuwa najitoa jf.
 
..kwanini mpaka Ccm wajibu?

..kwani wananchi hawajui kama waliwachagua au hawakuwachagua Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya, na Wakurugenzi?

..Au uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kura zilikuwaje? Si maelefu ya wana Ccm walipita bila kupingwa?

..Lissu akitoa tamko fulani inabidi uwe makini. Usikimbilie kumjibu au kumtukana.
 
Japo kuna watu hawapendi kuusikia huu ukweli, lakini ukweli ni lazima usemwe.

Anachokisema Lisu ndiyo ukweli wenyewe ambao kila mtanzania mwenye akili timamu anaujua, na hata Dunia nzima kwa wale wanaojishughulisha na kufahamu kinachoendelea kwa kila nchi, ndivyo inavyojulikana.

Tumeamua twende hivyo hivyo kwa sababu hakuna njia ya mkato. Lakini tysiendelee na hayo kuanzia mwakani baada ya Serikali za mitaa. Wananchi tunatakiwa kuwa wakali zaidi kwa atakayetaka kutufanya tuendelee kuishi gizani.
 
Back
Top Bottom