Kobello
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 9,286
- 9,051
kWANZA KABISA SI KWELI KUWA UNITARY GOVERNMENT HULETWA KINGUVU.Serikali Moja:Pale ambapo ushirikiano huu SIO WA HIARI bali wa kulazimishwa na mwenye nguvu dhidi ya taifa hafifu kama vile ilivyotokea katika uhusiano wa uingereza na Ireland ya kaskazini; Serikali inayozaliwa chini ya mfumo huu ni ile ya mfumo mmoja, na chini ya mfumo huu, nguvu zote za mamlaka zinawekwa chini ya serikali ya bwana mkubwa; Dhana hii inakwenda kinyume na Mkataba wa Muungano, 1964, na hakuna ushahidi wowote kwamba dhamira ya muungano wetu ilikuwa ni hiyo kwani hakuna msingi na ushahidi wowote wa kihistoria, kisheria na kikatiba kwamba hiyo ndio ilikuwa ni nia ya waasisi wetu wawili; Kumbuka, chini ya Mkataba wa Muungano, 1964, kuanzisha serikali moja Tanzania ni kinyume na mkataba wa kimataifa wa Tanganyika na Zanzibar ambazo zina mamlaka kamili, vinginevyo hii ni ni kutafuta kesi ambayo inaweza kupelekwa mahakama ya kimataifa;
Mkuu Kobello, je, Muungano wetu kwa Mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964 ulilenga serikali moja?
Chukulia mfano wa Czechoslovakia. Unitary governance inaweza kuletwa kwa makubaliano au hata kinguvu, so is the federal system.
Dhamira ya muungano wetu ni serikalki moja, hasa kwa upande wa Tanganyika (kidhamira).
Inabidi uisome Introductory note ya Articles of the union kuhusu undugu na Umoja wa waafrika. Halafu kipengele kinachofuata ni makubaliano ya Serikali hizo kuanzisha Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa chini ya Katiba ya Tanganyika. Kwa masharti kuwa, itaipa zanzibar bunge kushughulikia mambo ya znz. Je, kuna kipengele kilichosema kutakuwa na bunge la Tanganyika ambalo litashughulikia mambo ya Tanganyika? Kwa sababu kama walitaka serikali tatu, kungekuwa na provisions za Bunge la Tanganyika ambalo lipo separate na bunge la Jamhuri ya muungano. Ila hili naona huliulizii.
Ukiangalia mkataba wa Scotland na England una preambles ambazo zipo sawa na za kwetu, na kipengele cha kwanza kinafanana. Mwaka 1707 bunge la scotland liliungana na bunge la England na kukaa pamoja Westminister, ingawa baadae scotland ilianza ku-pull out.
Tanganyika ilikufa tarehe 25/4/1964. Kwa makusudi yetu tukiwa na nia ya kuwa na serikali moja baadae. La svyo, tungetaka bunge letu na mahakama zetu ziwe separate na za muungano.
Kuna mifano mingi ya unitary governments ambazo zina semi autonomous states kama nchi nyingi tu za ulaya ...Spain, na Barlosque, Greece na Athos mountains etc. na kuna Federations zenye completely autonomous states kama inner Mongolia na China.
Pia kuna Federations kama za Brazil ambapo Manispaa, state na federal governments zipo autonomous. Kuna nchi kama Tanzania ambapo Manispaa ina mamlaka na serikali kuu ina mamlaka.
Kwa hiyo jibu langu ni kuwa serikali shirikisho halikuwa lengo, la sivyo tungeainisha kwenye hati ya muungano uanzishwaji wa bunge la Tanganyika SEPARATE from bunge la muungano.