Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Joka Kuu

Jina halisi la muungano lilikuwa ni Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama ni jina la nchi basi ni hili. Lakini nia ilikuwa ni kuipoteza Tanganyika au jina Tanganyika lisitumike basi ndio uchakachuaji ulipoanza wa kubadilisha jina. Mazingaombwe na ukiini macho ulianza tokea alfajiri.

The name Tanzania derives from the names of the two states, Tanganyika and Zanzibar, that united in 1964 to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, which later the same year was renamed the United Republic of Tanzania Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia

Tanganyika na Zanzibar zilikoma vipi kuwa dola au nusu dola wakati ziliungana kwa mambo 11 tu? Na mengine Tanganyika ilitakiwa kujifanyia kivyake na pia Zanzibar kujifanyia kivyake yale mambo ambayo si ya muungano.

Umeridhika na Tanzania yako bila ya kusikia mzazi mmoja wa Tanzania kutajwa tajwa?

Wewe unasherehekea uhuru wa Tanzania bara? au uhuru wa Tanganyika?.

Nonda,

Asante sana kwa hoja zako zinazodidi kufunua watu kuhusu hiki kiini macho ingawa naona kama kazi hii ni kubwa sana, ni karibia na kugeuza mtu imani yake ya dini;

Ningependa ku-share mawazo ya mdau mwenzetu - barubaru ambae alitoa hoja inayoendana sana na hoja yako. Ingawa kuna sehemu hajatumia lugha ya kistaarabu kwetu watanganyika lakini kuna mambo muhimu ya kuyatilia maanani katika hoja yake.

Waarabu tuna usemi unaonena. ''NI RAHISI SANA KUWADANGANYA WATU. LAKIN NI VIGUMU SANA KUWAAMBIA WATU KUWA WAMEDANGANYWA''

Na vile vile Mwimbaji mashuhuri wa Reggae Robbert Nesta Marley (mmarufu kama Bob Marley) kwenye wimbo wake wa "Redemption song" alisema YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOMETIMES BUT YOU CAN'T FOOL ALL THE PEOPLE ALL THE TIME"

Nikiwaambia waTanganyika Nyerere aliwadanganya sana na alisimamia kidete kuhakikisha HAMUWEZI KABISA KUUNDA Serikali ya TANGANYIKA pamoja na Znz kuwasaidia sana kuwaombea Serikali Hiyo katika mjadala wa kwanza kuhusu Muungano wenu.

tumeamua kuiga tabia ya "ujanja" wa mbuni wa kuzika kichwa mchangani, eti kukwepa janga. Labda tujikumbushe kidogo kwa hili.

Mdahalo wa kwanza juu ya mfumo na muundo wa Muungano ulianza kwa njia ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1983/84. Hapo, kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais Aboud Jumbe, na wale wa Serikali ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Nyerere, walikuwa na mitazamo tofauti inayokinzana juu ya Muungano.

Jumbe na timu yake walitaka Muungano uwe na Serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar (iliyopo sasa) na Serikali ya Muungano yenye kushughulikia mambo ya Muungano tu, ambayo yameainishwa katika Ibara ya 6(a) ya Katiba ya Muungano (Articles of Union) na kifungu cha 8 cha Sheria ya Muungano (Acts of Union) Namba 22 ya 1964, na hatimaye ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Jumbe alikwenda mbali zaidi kwa kuandaa Hati ya Maombi ya kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba juu ya muundo sahihi wa Muungano kwa kutumia ibara ya 125 ya Katiba.

Tofauti hizi kati yake na Mwalimu hazikwisha salama kwa Jumbe kuthubutu kukanyaga mahali "patakatifu" bila kuvua viatu. Jumbe alilazimishwa kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi kuanzia Urais wa Zanzibar, Umakamu wa Rais wa Muungano, na nafasi zote za kichama Januari, 1984.
 
VII) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.
Mchambuzi, muungano wetu kiukweli ulishaharibika kabla hata ya mwaka 1977,kwasababu kipengele hicho kilianisha kuwa mkataba huo utathibitishwa kwa kutungiwa sheria na bunge la Tanganyika na baraza la mapinduzi la jamuhuri ya watu wa Zanzibar,hilo halikutokea kwasababu sheria ilitungwa na bunge la Tanganyika bila ya kulishirikisha baraza la mapinduzi kwenye utunzi.Walichofanya wao(baraza la mapinduzi) ni kuthibitisha tu,sasa sijui tatizo hapo lilikuwa wapi?Maybe ni kwasababu kulikuwa hakuna utawala wa kisheria huko Zanzibar ambapo Karume ndiye alikuwa msemaji wa mwisho?

Kwa mfano kipengele hicho hapo chini...

Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri:-
b) Masharti yatakayowekwa kwa amri ya Rais wa Zanzibar juu ya sheria yoyote inayohusu jambo lolote lililotajwa kwenye ibara ya (iv), na kufuta sheria yoyote inayolingana Zanzibar.

Hicho kipengele b kinamaanisha kuwa Karume alikuwa na nguvu ya kuweka masharti kudhibiti sheria yoyote ile kwa kutumia amri.Kwahiyo hatakama sheria ya mkataba ilisema baraza la wawakilishi lishirikishwe,bado Karume angekuwa na uwezo wa kusema lolote kupingana na maamuzi yoyote ya baraza hilo la mapinduzi .
 
Joka Kuu

Jina halisi la muungano lilikuwa ni Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama ni jina la nchi basi ni hili. Lakini nia ilikuwa ni kuipoteza Tanganyika au jina Tanganyika lisitumike basi ndio uchakachuaji ulipoanza wa kubadilisha jina. Mazingaombwe na ukiini macho ulianza tokea alfajiri.

The name Tanzania derives from the names of the two states, Tanganyika and Zanzibar, that united in 1964 to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, which later the same year was renamed the United Republic of Tanzania Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia

Tanganyika na Zanzibar zilikoma vipi kuwa dola au nusu dola wakati ziliungana kwa mambo 11 tu? Na mengine Tanganyika ilitakiwa kujifanyia kivyake na pia Zanzibar kujifanyia kivyake yale mambo ambayo si ya muungano.

Umeridhika na Tanzania yako bila ya kusikia mzazi mmoja wa Tanzania kutajwa tajwa?

Wewe unasherehekea uhuru wa Tanzania bara? au uhuru wa Tanganyika?


Hata mifano uliyoitoa ya jumuia, nchi wanachama wa jumuia hupoteza ndio baadhi ya powers lakini haifanyi kuwa nchi hizo zisiwe dola. Chukua mfano wa EU, soma histoia yake.

Nonda,

..United Republic of Tanganyika na Zanzibar maana yake dola ni mbili zimeungana na kuwa dola moja -- chini ya Raisi na Amiri Jeshi Mkuu mmoja.

..dola yoyote ile ikichukua yale mambo 11 original ya muungano na kuyakabidhi kwa mamlaka nyingine basi dola hiyo itakuwa imefikia kikomo.

..kwa maana nyingine dola za Tanganyika na Zanzibar zilikufa pale zilipoyakabidhi yale mamlaka 11 kwa dola mpya iliyoitwa United Republic of Tanganyika and Zanzibar, ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuwa United Republic of Tanzania.

..ushahidi mwingine ni kile kitendo cha Tanganyika na Zanzibar kubadilisha uanachama wao wa ktk UN na kuchukua uanachama mpya kwa jina moja, TANZANIA.

..hata nchi marafiki ziliacha kuzitambua Tanganyika na Zanzibar na badala yake kuanza kuitambua dola mpya TANZANIA.

..mwisho, mahakama ya rufaa ya TANZANIA ilitoa hukumu kuunga mkono hoja iliyotolewa na mawakili wa chama cha CUF kwamba huwezi kutenda kosa la uhaini kwa Zanzibar, kwasababu Zanzibar siyo nchi/dola.

..usijaribu kufananisha Tanzania[muungano wa Tanganyika na Zanzibar] na Jumuiya ya nchi za Ulaya. Hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa. Ungekuwa sahihi kama ungefananisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya nchi za Ulaya.

NB:

..Hakuna haki, usawa, kuheshimiana, na kuthaminiana, ndani ya muungano wetu. Kwa msingi huo nadhani ni bora muungano uvunjwe, na Tanganyika irudi.
 
Mchambuzi, muungano wetu kiukweli ulishaharibika kabla hata ya mwaka 1977,kwasababu kipengele hicho kilianisha kuwa mkataba huo utathibitishwa kwa kutungiwa sheria na bunge la Tanganyika na baraza la mapinduzi la jamuhuri ya watu wa Zanzibar,hilo halikutokea kwasababu sheria ilitungwa na bunge la Tanganyika bila ya kulishirikisha baraza la mapinduzi kwenye utunzi.Walichofanya wao(baraza la mapinduzi) ni kuthibitisha tu,sasa sijui tatizo hapo lilikuwa wapi?Maybe ni kwasababu kulikuwa hakuna utawala wa kisheria huko Zanzibar ambapo Karume ndiye alikuwa msemaji wa mwisho?

Mkuu jmushi1,

Nakubaliana na hoja yako ya msingi, na natumaini kobello anakusoma pia; Nakubaliana na wewe kwamba Muungano ulishaingia doa way before 1977, hasa pale sharti muhimu la kwanza la kuzidi kuujenga muungano uwe bora na rasmi lilipokiukwa, na hii ni ile ibara ya saba ya Mkataba wa Muungano inayouhusu uteuzi wa tume ya katiba kukusanya maoni ya pande zote mbili ili hatimaye Katiba mpya ya JMT yenye kukidhi maslahi ya pande zote mbili, itakapozaliwa; Badala ya hili kufanyika, Bunge la JMT baada ya lile sharti ya kipindi cha mpito ku-expire, huku tume ya katiba ikiwa bado ni hadithi tu, bunge hili likajitengenezea sheria ambayo ikaja kupitisha katiba ya muda, 1965, ambayo ndio ikaja tengeneza mamlaka ya serikali ya JMT na ya nchi shirikishi, huku ikiahirisha kwa mujibu wa sheria, tena INDEFINITELY, ibara ya saba ya Mkataba wa Muungano - kuhusu kuundwa kwa tume ya katiba yenye uwakilishi wa pande zote mbili za muungano;

Kuhusu karume, na maamuzi yaliyotokea, historia inatueleza kwamba - wakati katiba ya muda, 1965 inaanzishwa, JMT ilikuwa na vyama viwili vya siasa; Nina swali la uzushi hapa je:

Ina maana kabla ya ndoa ya TANU na ASP, Tanzania ilikuwa ni nchi ya vyama vingi i.e. TANU na ASP?

Ama kweli mazingaombwe ya muungano hayaishi; anyways, back to my point - Kulikuwa na ASP na TANU as of 1965. Lakini katiba ya muda (1965) ilipochapishwa, tayari ilikuwa katika nyongeza ya kwanza ya TANU; Uamuzi huu ulifanywa bila ya kupata idhini yoyote kutoka Zanzibar; Ebu tutazame kidogo katiba ya muda ya 1965:

Kipengele cha 3(2) cha katiba hii kinasema hivi:

["Mpaka hapo TANU itakapoungana na ASP na kufanya chama kimoja cha siasa, chama hicho kwa Tanganyika kitakuwa TANU na na kwa Zanzibar kitakuwa ASP;" ]

Kitendo cha katiba ya TANU kutiwa katika Katiba ya nchi (1965) maana iliyo wazi ni kwamba - nia ilikuwa ni kuleta dhana kwamba kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa Katiba ya muda ya 1965, basi kanuni za TANU na katiba yake zitakuwa zimefanywa kuwa ni sehemu ya sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; TANU walifanikisha walicholeng, hasa kutafuta supremacy ya ku-dominate maamuzi yanayohusiana na muungano; Kwahiyo kwa hili, tusimlaumu Karume bali TANU; na tabia hii ya kushika hatamu ilikuwa kuwa sealed and made official kwenye katiba ya 1977 ambapo sasa Katiba ya CCM became supreme hata kwa katiba ya nchi;

Nikirejea kwenye hoja yangu ya awali hapo juu kuhusu TANU na katiba ya muda, 1965, ebu tutumie muda kidogo kumtafsiri Pius Msekwa katika kitabu chake cha Towards Party Supremacy (1977):

["Halmashauri Kuu ya TANU imekuwa siku zote ni kiungo muhimu cha uunganishi; Vyombo vitatu vya Chama ni Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu...Lakini Halmashauri Kuu ndio yenye nguvu za Chama; Pale KATIBA ya CHAMA ilipofanywa kuwa KATIBA YA NCHI, Chama hapo kikawa kimejijengea UHALALI WA KATIBA; Moja katika nguzo kuu katika utawala wa kisasa ni kuwa na chama kikubwa ama kiwe kimehodhi au la; kwa sababu muendesho wa siasa za kisasa hautakuwa rahisi pale panapokosekama jamii iliyoungwa pamoja KATIKA MFUMO WA CHAMA; Lakini pamoja na nafasi kubwa inayochukua CHAMA katika maendesho ya kisiasa na kiserikali, mara nyingi huwa panakosekana nguvu za kisheria, hadhi na dhamana ya chama, ikiwa ni pamoja na wale walio madarakani; Katika hali hii, basi kwa KUIFANYA TANU KUWA NA UHAI WA KIKATIBA, KATIBA YA MUDA YA JAMHURI YA MUUNGANO IMEWEKA HISTORIA KWA KUANZISHA DHANA MPYA, HASA KATIKA MTIZAMO WA KISHERIA;"]

Nadhani mpaka hapa tunaona jinsi gani Mkataba wa Muungano, 1964, ulivyokiukwa,na tunaona wa kulaumiwa ni nani; Tunaweza ona kwa uwazi kabisa madhara ya hili kwa Zanzibar yalikuwa ni nini;
 
Nonda,

..Hakuna haki, usawa, kuheshimiana, na kuthaminiana, ndani ya muungano wetu. Kwa msingi huo nadhani ni bora muungano uvunjwe, na Tanganyika irudi.

Mkuu Joka Kuu,

Tupo sawa lakini hatupo sawa; usawa wetu ni TANGANYIKA irudi, na katika hili ningependa kusikia mawazo yako: Kwa vile Jina Tanganyika liliuliwa na chombo batili i.e. suala la ku deal na majina na nchi za Tanganyika na Zanzibar halikuwa ni suala la Muungano per articles of the union, 1964, bali hili lilikuwa ni suala la kila nchi wanachama wa muungano; Lakini bado JMT kupitia bunge lake, sheria no 24 ya Mwaka 1967, Rais akapewa madaraka ya kuzika Jina Tanganyika, kwa mujibu wa sheria; Je, Tanganyika itafufuka kwa mujibu wa sheria ya bunge la JMT lililo ua Tanganyika, kinyume na articles of the Union, au Bunge la Tanganyika (ambalo) halipo, kama Articles zinavyosema i.e. kwamba masuala ya majina haya na maana yake sio suala la muungano;

Kwa zanzibar ni rahisi hata wao kubadili jina lao liwe Kilwa, Tukuyu etc, kwani nguzo ya muungano bado leo hii ni Mkataba wa Muungano, na ndugu zetu wa zanzibari wao wana bunge lao ambalo wanaweza ku deal na masuala yasiyo ya muungano, kwa mfano kubadil jina la nchi yao; Sijui kama umenielewa mkuu, na kama umenielewa naomba unipe mawazo yako juu ya jinsi gani tutaweza kurudisha Tanganyika, given kiini macho na kizungu mkuti hiki nilichojadili hapa; tofauti na ndugu zetu wazanzibari, bunge letu lina wajumbe kutoka Zanzibar, kwahiyo hatuna chombo cha kurudisha Tanganyika kisheria per articles of the union, 1964;

Kuhusu mimi na wewe kutofautiana ni katika tu suala zima la kutupilia mbali muungano; mimi nina amini bado kwamba tunaweze kuuokoa lakini iwapo TANU/CCM watakubali kwamba imechangia sana kuvuruga muungano huu, kuliko inavyotaka tuamini kwamba wameujenga; TANU/CCM waliunda,lakini hawakuujenga na badala yake wanazidi kuubomoa kwa kung'ang'ania serikali mbili, towards moja, kinyume kabisa na mkataba wa muungano, 1964; tutengenezeni jamani mazingira ya vizazi vyetu hata mwaka 5000 ndio waje waamue kama muungano uwe wa serikali moja, mbili, tatu n.k, na njia pekee ya kufanua hivyo ni kwa kurudia mkataba wa muungano, 1964, na kuwa na serikali tatu ili kuondoa migogoro iliyopo, na mwaka 3000 huko, vitukuu vyetu waje kufanya maamuzi ya kuboresha zaidi; vinginevyo hii tabia ya kuharakisha mambo ili tuache legacy tukiwa hai haitatupelekea popote; Rome wasnt built in a day;

Achana na hii hoja yangu ya mwisho katika majibu yangu juu ya tofauti zetu hizi ndogo, naomba tu kupata maoni yako ukiwa na muda kuhusu hoja yangu ile ya kwanza i.e the meand towards the return of our BELOVED TANGANYIKA;
 
Mchambuzi,

..kiini cha matatizo ya muungano ni wetu ni ama kuuwawa kwa serikali ya Tanganyika, au kuendelea kuwepo kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar.

..sasa ukitaka kuokoa huu muungano unapaswa kuifufua serikali ya Tanganyika, na kuunda mfumo wa shirikisho, au kuifuta serikali ya mapinduzi Zanzibar, na kuunda Jamhuri moja.

..kwa upande wangu mimi nadhani wenzetu wa Zanzibar hawataki muungano. they have already moved on. katika mazingira hayo, hakuna haja ya kuwabembeleza wala kuwalazimisha na masuala ya muungano.

..tunachotakiwa kukifanya ni kutumia BUSARA na USTAHAMILIVU wakati tunavunja muungano wetu.
 
Mchambuzi,

..kiini cha matatizo ya muungano ni wetu ni ama kuuwawa kwa serikali ya Tanganyika, au kuendelea kuwepo kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar.

..sasa ukitaka kuokoa huu muungano unapaswa kuifufua serikali ya Tanganyika, na kuunda mfumo wa shirikisho, au kuifuta serikali ya mapinduzi Zanzibar, na kuunda Jamhuri moja.

..kwa upande wangu mimi nadhani wenzetu wa Zanzibar hawataki muungano. they have already moved on. katika mazingira hayo, hakuna haja ya kuwabembeleza wala kuwalazimisha na masuala ya muungano.

..tunachotakiwa kukifanya ni kutumia BUSARA na USTAHAMILIVU wakati tunavunja muungano wetu.

Nimekusoma mkuu,
Lakini ningependa kujua mawazo yako juu ya jinsi gani tunaweza kuuvunja - kisheria;
 
kweli itabaki kuwa kweli hata kama kweli hiyo inatoka kwa kinywa cha adui yako!

Serikali tatu zitaongeza mzigo kwa wananchi na itashawishi kuvunja muungano!

Wazanzibari au watanganyika wenye mawazo ya kujitenga hawatabaki salama kamwe.

Sisi ni watanzania chonde chonde tusichague uasi bali mshikamano.
 


Serikali tatu zitaongeza mzigo kwa wananchi na itashawishi kuvunja muungano!

Unatumia vigezo gani katika ku prove hoja hii kuhusu mzigo? Je, una mtazamo gani juu ya hoja ifuatayo: Serikali ya JMT ina watoto wawili wa kuwalea na haitaki kuwapa uhuru ili wao wakachume kivyao na walete michango kwa mzazi ili aendelee kuwasimamia, hoja hii unaoinaje? Hoja yako kuhusu mzigo kwa walia kodi, ni hoja maarufu sana miongoni mwa wanasiasa wa CCM wanao jaribu kufuta dhana ya serikali tatu vichwani mwa wananchi kwani serikali tatu ni Kifo cha CCM kwani iliua Tanganyika kwa mujibu wa sheria ya bunge namba 24, 1967; Vile vile ujio wa Tanganyika ina maana hata Rais mpya wa tanganyika hatokuwa na mamlaka kama ile ya marais waliomtangulia; HATOKULA BATA KISAWA SAWA; Vinginevyo, hoja ya mzigo kwa walipa kodi inawaingia kweli wananchi wakati its full of fallacy;
Wazanzibari au watanganyika wenye mawazo ya kujitenga hawatabaki salama kamwe.

Hii ni hoja nyingine ambayo ingawa ina mashiko, lakini inajenga dhana ya HOFU katika kujaribu kutatua mgogoro ambao chanzo chake ni wazi - Sheria Mama ya Muungano ilikiukwa, period; badala ya kuishi na hofu hii, na kuja kurithisha vitukuu wetu hofu hii hii, na mgogoro huu huu, kwa sababu za kibinafsi tu, hasa madaraka, tuanze ku sensitive UMMA wa pande zote mbili kwamba tulikosea hapa na pale, sasa tunarudi kurekebisha tatizo; isitoshe, nguzo ya muungano itaendele kuwa Mkataba wa Muungano, 1964, na kupitia elimu tosha, wananchi wataelewa vizuri; tatizo pengine ni kwamba CCM itakuwa katika hali mbaya sana kisiasa iwapo itakiri wazi wazi kwamba kuna makosa yalifanyika;


Sisi ni watanzania chonde chonde tusichague uasi bali mshikamano.
Iwapo unautaka muungano bado, basi kudai Tanganyika sio kuasi, bali ni kuwa mwaminifu kwa Mkataba wa Muungano, 1964;
 
Serikali ya Muungano uisemayo ya baba mwenye watoto wawili haipo! Iliyopo ni Serikali mfano wa Baba aliyeungana na Mama, na Akazaliwa mtoto(Tanzania), Baada ya kuzaliwa mtoto, Baba akafariki, mama akaendelea kuishi, Utakubaliana nami kuwa baba aliendelea kuishi kupitia mtoto kwa maana mtoto (Tanzania) ni matokeo ya baba na mama, Huwezi kumrudisha baba kuwa hai kwa kumuua mtoto ndudu yangu!

1+1=2 Ndio maana waliamua kuipoteza Tanganyika na kuiacha Zanzibar kwa sababu always aliye mdogo au dhaifu kupewa upendeleo maalum ni kawaida ili acjihic kuonewa.

Kama unaunganisha watu wawili katika ndoa ya Kikristo, 1+1=1 kwa maana wawili hawa wanakuwa wamoja, Tanganyika haijapotea Ndugu yangu bali imeboreshwa na kuchukua sura mpya yenye mtazamo wa kujitambua sababu Tanzania haitokani na matokeo na maamuzi ya wakoloni! Tubaki na Serikali mbili, Tujadili mambo yote yaletayo mgogoro na Tutaafikiana. Baada ya hapo tuelekee Serikali moja.

Serikali Tatu ni mzigo kwa Wananchi, Tutalazimika kutozwa kodi zaidi ili kuzihudumia Serikali hizi, Itafika muda tutachoka na kufikiria kuchangia Serikali ya Afrika Mashariki yenye nchi nyingi zaidi kuliko Muungano wa nchi Mbili pekee na suluhu itakuwa ni kuuvunja. Muungano wetu ni wa pekee, unafanana na United Kingdom.

Wazo la Kuvunja muungano ili tuunde Serikali Tatu ingekuwa na mashiko kama kusingekuwapo na EAC, Muungano wetu Ndugu umeunganisha watu kwa miaka 46 sasa hivyo kuuvunja lazima uanzishe migogoro mikubwa na uasi, Mnaweza jaribu vunja muungano lakini hamtaweza kuhimili kishindo cha kuwaondoa Wazanzibari walio Bara na kuwaondoa Watanganyika walio Zanzibari wenye ardhi,ndugu na familia, Nyerere aliona mbali ndo maana alisema dhambi ya Uasi itawahukumu sababu alishajua baada ya muda mrefu kupita hatwezi tena kutengana.


Ahsante kwa hoja nzuri iliyo na mashiko lakini utakubaliana nami kuwa humu JF watu wamekaa ki ushabiki zaidi wa kisiasa wakisahau kuwa wanaweza kuishi bila C.C.M, C.D.M au CUF lakini Hawawezi kuishi bila Mama yao mzazi (TANZANIA).
 
Ndamo Emmanuel,

Asante sana kwa mchango wako; Nitakurudia baadae hasa juu ya hoja yako kwamba Serikali Tatu itakuwa ni gharama kwa walipa kodi; Huu ni upotoshwaji uliopitiliza ambao wanasiasa wanautumia sana kutisha wananchi bila sababu yoyote; Kuna wadau wengine humu wana hofia hilo pia - suala la Tanganyika kuwa mzigo kwa walipa kodi, mfano kobello na wengine; Nitakuja na hoja yangu baadae nikiamka kwanini mfumo wa sasa ni mzigo kwa walipa kodi kuliko mfumo wa serikali tatu; nitakuja na facts, sio porojo ambazo ndio hutawala hoja kwamba Tanganyika itakuwa ni mzigo kwa mlipa kodi; Tuwaambie wananchi ukweli juu ya hili, na nitafafanua zaidi nikiamka salama kesho;
 
Mkuu Mchambuzi,
Labda nitakuwa nimedandia treni kwa mbele naomba radhi ikiwa ni hivyo.
Muungano una matatizo tena makubwa, nashukuru nilianza kuliona hili wakati nilipohoji kwanini twende Zanzibar kwa Passport? Hapo ndipo nilianza kufuatilia muungano na nashukuru kuwa yote yanayoongelewa na akina Lisu niliyaona mapema sana, tena mengine hayakusemwa.

Kwanza nieleze kuwa sikubaliani na dhana ya kuwa wazanzibar wanauelewa mkubwa kuliko sisi. nina sababu za kusema hivyo.

Pili, ninaona tunazungumzia serikali 3, mkataba n.k.
Kuna maswali muhimu tunayotakiwa tuyajibu kwanza kabla ya kufikiri twende wapi

1. Kwanini watu wanadhani tunahitaji muungano wa nchi mbili.
2. Kwanini watu wanadhani tunahitaji serikali 3 au mkataba.
3. Kwanini watu hawazungumzii kuvunja muungano

Ahsante
 
Mchambuzi safi sana,
Unajua! kila siku nilikuwa najiuliza MUUNGANO HUU NI WA NAMNA GANI? yaani (ni wa MTU na MTU au ni wa NCHI na NCHI?) Jibu nimeshapata Asante sana Mchambuzi kwa kuchambua hii Mada.
 
Sehemu ya Kwanza: Utangulizi


Kuna jambo moja linanishangaza. Pamoja na umuhimu wa hotuba ya Lissu aliyoitoa Bungeni, hotuba hii haipo kwenye Hansard ya Bunge. Kwa kweli this is both - Very Unusual and Very Wrong; Lakini kukosekana kwa hotuba hii kwenye Hansard haiwezi kutuwekea kikwazo sisi wananchi kuendeleza mjadala ule huku uraiani kwa nia ya kujenga, na sio kubomoa, na kwa maslahi ya taifa letu, hasa vizazi vya baadae; Sidhani kama kuna yoyote miongoni mwetu ambaye ana nia ya kuachia watoto na wajukuu zake taifa lililojaa migogoro; Kuzuia mjadala huu au kuhofia kujadili hoja hii, ni mwanzo wa maandalizi ya kuachia vizazi vyetu vya baadae MGOGORO mkubwa sana;

Nilibahatika kunukuu baadhi ya maeneo muhimu kutoka katika hotuba ya Tundu Lissu kupitia TBC1. Kwa kifupi, Lissu alikuwa ana ‘challenge’ hoja ya Serikali iliyotolewa na Waziri husika wa muungano kuhusu ya hali ya muungano wetu, miaka 48 baadae [1964-2012]. Waziri huyo alizungumza mengi ikiwa ni pamoja na haya yafuatayo:

[“…Katika Kipindi hicho muungano wetu umekuwa na mafanikio katika maeneo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa…muungano wetu ndio nguzo kuu ya umoja na amani…”]

Katika sehemu ya majibu yake juu ya hoja hii ya Serikali, pamoja na mambo mengine, TUNDU LISSU alitamka yafuatayo:

[“…hata hivyo mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri aliliambia bunge lako tukufu kwamba, licha ya mafanikio hayo, zipo changamoto katika kumaliza vikwazo vinavyokwamisha shughuli za muungano. Mheshimiwa Spika, Waziri hakuzitaja Changamoto hizo.”]

“…Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu ni namna gani maoni ya wale wanaotaka kiini macho hiki cha Muungano kiishe yatashughulikiwa na Tume ambayo imepewa jukumu kisheria la kukihifadhi na kukidumisha kiini macho hicho? Ni kipi kitakachoizuia Tume ya Warioba kupuuza maoni ya watu hao kwa hoja kwamba Sheria inaielekeza Tume kuratibu na kukusanya maoni na kutoa mapendekezo ya kuhifadhi na kudumisha Muungano?”]

Kiini macho anachozungumzia Tundu Lissu ni Serikali Ya Tanganyika kupotea KIMAZINGAOMBWE, kinyume na makubaliano yaliyomo ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964, pamoja na athari zake kwa taifa kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa, Mazingaombwe haya ndio chanzo cha mgogoro wa muungano wetu huku hisia tofauti zikizidi kujengeka miongoni mwa wananchi wa pande zote mbili za muungano, kila upande ukiamini kwamba mfumo wa sasa wa Muungano hauwatendei haki. Tutaliona hili kwa undani baadae katika mjadala.

Suala la kwanza. Ni jadi kwa viongozi wengi wa CCM (sio wote), kuwa na misimamo inayo unga mkono mfumo wa sasa wa muungano wetu – yani mfumo wa Serikali Mbili, huku wengine wakiwa na mtazamo wa serikali moja; Wengi ya viongozi hawa huwa na mtazamo kwamba, madai ya Serikali ya Tanganyika hayana nia Njema kwa muungano wetu na taifa letu kwa ujumla; Kuna sehemu kubwa sana ya UMMA ambayo inanunua kauli hizi. Ni muhimu UMMA ukaelewa kwanini viongozi wengi huwa na mtazamo huo. Sababu kuu ni Viapo wanavyokuwa baada ya kuteuliwa KUSHIKA DHAMANA ZA UMMA. Viongozi wetu huapa hivi:

“Mimi ...................bin........ ..........naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba nitaahifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ewe mwenyenzi mungu nisaidie.”

Ni muhimu kwa kiongozi yoyote anayeteuliwa kushika cheo kama DHAMANA, kwani kinyume chake ni kujiweka hatarini kupoteza madaraka; Lakini viongozi wengi hujisahau kwamba vyeo hivi sio lolote zaidi ya Dhamana, na wenye mamlaka ya juu kabisa na nchi yetu ni UMMA wa Tanzania, Sio VIONGOZI. Tukirejea kwenye hoja ya msingi katika hili, viongozi hawa hawana jinsi bali kuunga mkono muungano wetu kama ulivyo, vinginevyo kufanya kinyume ‘is to contravene with the cocountry’s Constitution, 1977’, hivyo kujiweka pabaya na madaraka/vyeo walivyonavyo.

Sehemu ya Kwanza ya Katiba yetu inazungumzia: Jamhuri ya Muungano na Watu, na inatamka hivi:

1. Tanzania ni nchi Moja na Ni Jamhuri ya Muungano.

2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Kwa maana hii, tusitegemee kiongozi yoyote aliyekula kiapo cha “kuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano, na kuhifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, aje na msimamo tofauti au aunge mkono hoja ya kudai Tanganyika.

Ukitizama kwa makini maneno haya yaliyomo ndani ya Katiba Ya JMT (1977), licha ya Tanzania kuwa mtoto wa Tanganyika na Zanzibar, nchi ya ‘Tanganyika’ haipo, na badala yake, mzazi huyu wa Tanzania amepewa jina la ‘Tanzania Bara’; Hiki ni kiini macho cha hali ya juu; Tangia lini mzazi anapewa jina tofauti baada ya kuzaa mtoto? Suala lingine muhimu zaidi hapa ni kwamba, HUU NI UCHAKACHUAJI na ni KINYUME NA MKATABA WA MUUNGANO, 1964.


Suala la Pili. Tofauti na viongozi hawa, raia wengine wanapozaliwa, hawali kiapo cha kulinda katiba, muungano….; Vile vile kabla ya kupewa pasi zeti za kusafiria kama watanzania, hakuna kiapo tunachokula; tunapoajiriwa katika sekta sekta binafsi n.k, vile vile hakuna kiapo tunachokula; tunapoamua kuwa wajasiriamali na kupokea usajili wa makampuni yetu kule BRELA au kupokea mbalimbali zinazo turuhusu leseni kuendesha biashara zetu n.k, hatuli kiapo kama cha hawa wakubwa. Sasa iwaje tuogope kujadili muungano kama nia yetu ni kuuboresha? So Let the People Speak. Isitoshe, hatima ya nchi yetu ya Tanzania pamoja na Muungano wetu, ipo mikononi mwa UMMA, sio Viongozi hawa wanaokula viapo, kwani UMMA ndio wenye mamlaka ya mwisho katika taifa letu. Na haki ya raia kutoa mawazo yao ni kwa mujibu wa Katiba (1977);

Suala la Tatu. Kwa Mtazamo wangu, Mtanzania yeyote mwenye nia njema na muungano wetu ni lazima kwanza awe Mwaminifu Kwa Mkataba wa Muungano, 1964, badala ya kuwa Mwaminifu kwa Katiba ya JMT, 1977; Hii ni kwa sababu, Katiba ya JMT, 1997, haina mema na muungano wetu, kwani Katiba hii mbovu ndio chanzo kikubwa cha mgogoro ulipo sasa; Tutalijadili hili kwa kina baadae, hasa jinsi gani Katiba ya JMT, 1977, ilivyouchakachua Mkataba wa Muungano, 1964.

Kama tutakavyoona, Mkataba wa Muungano, 1964, ulikuwa na nia ni njema kabisa – ya kuunganisha watu wa Tanganyika na Zanzibar, huku kila taifa likiwa huru na kujiamulia mambo yake yasiyo ya muungano; Badala yake, kilichokuja kutokea baadae ni mazingaombwe na uchakachuaji ambayo ulifanya tupoteze nchi ya Tanganyika, ambae ni Mmoja ya Wazazi wa Tanzania, na mzazi huyu kupewa jina jipya la “Tanzania Bara”, mara tu alipojifungua mtoto wake “Tanzania”, huku mzazi mwenza “Zanzibar”, nae akipewa jina jipya “Tanzania Visiwani”, lakini kwa kuogopa kumchakachua zaidi, akaachiwa awe na majina mawili – yani Zanzibar na Tanzania Visiwani, huku uchakachuaji juu yake ukiendelea kwa njia ya kuongeza orodha ya masuala ya muungano, Kinyume na Mkataba wa Muungano, 1964;

Suala la nne, ni kuhusu arrangement ya Katiba ya Tanzania, 1977. Shivji analiweka hili kwa lugha rahisi zaidi kueleweka pale anaposema kwamba: “The underbelly of Tanzania’s constitutional arrangement is and has been the union or Zanzibar.”

Kwa bahati mbaya sana, msimamo wa ndugu zetu wazanzibari juu ya muungano umekuwa unapotoshwa, na kuwekwa completely out of context. Je ni kwa madhumuni gani? Ni vigumu kuelewa; Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba throughout, ndugu zetu wazanzibari wamekuwa na tatizo moja tu kuhusu muungano, na hili sio jingine bali “Loss of Their Autonomy”. Kwa sababu tusizozijua, hoja yao hii ambayo ni LEGIT kabisa, hasa kwa kufuatana na Makubaliano chini ya Mkataba wa Muungano, 1964, msimamo wao umekuwa ‘politicized’, na kupelekea ujenzi wa chuki kubwa baina ya ndugu hawa wawili – wazanzibari na watanganyika; Imekuwa jadi kwa baadhi ya watu kuwashutumu ndugu zetu wazanzibari kwamba misimamo yao juu ya Muungano wetu una msukumo wa kidini; huu ni upotoshwaji wa hali ya juu; Ukweli ni kwamba - throughout, Wazanzibari wamekuwa na nia njema kabisa na Muungano, lakini kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, ambapo Serikali Tatu was envisaged;

Ningependa kusema kitu kimoja at this juncture:

Kwa sababu kadhaa, ndugu zetu wazanzibari wamekuwa ni waelewa zaidi juu ya kiini macho cha muungano kuliko wengi wetu wa upande wa bara; Mbaya zaidi ni kwamba, badala ya sisi kujikita katika kuelewa tatizo la msingi lipo wapi, hasa jinsi gani Katiba ya JMT 1977 ilivyofanya mazingaombwe na kuchakachua Mkataba wa Muungano, 1964, na badala ya na sisi kuwaiga na kudai Tanganyika yetu, kitu ambacho wao throughout wamependelea kiwepo, badala yake tunaelezeka juhudi zetu kubwa sana to fight the wrong enemy i.e. kuwakosoa ndugu zetu wa Zanzibar juu ya madai yao, badala ya kuwaelewa na kuwaiga;

Wengi wetu tunajenga hoja potofu kwamba wazanzibari wanafaidika zaidi na muungano, au wanatunyonya; hii hoja sio sahihi kwa sababu – kama ni kweli Bara tunanyonywa na muungano huu, basi ni kwa sababu ya makosa yetu wenyewe ya Kukiuka Mkataba wa muungano, 1964, kupitia katiba ya JMT, 1977; Isitoshe – iwapo mtoto wako haumpi ‘autonomy’ au haumfundishi maisha ya kujitegemea, kwanini sasa uanze kumgeuka na kumuona kwamba ni mzigo kwako? Ni dhahiri kwamba, iwapo wangepewa Autonomy kwa Mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, Zanzibar ingeweza kabisa kujitegemea; Kinyume chake, baada ya Muungano, serikali ya Muungano ikaanza taratibu kunyakua mambo mbalimbali na kuyatumbukiza kama nyongeza ya masuala ya muungano, kinyume kabisa na Mkataba wa Muungano, 1964; Leo hii tunaposema ndugu zetu wazanzibari ni mzigo, hii ni dhambi kubwa sana kwetu watu wabara;

Pia wengi tunasahau kwamba, Zanzibar ilijiunga na Tanganyika miezi minne na nusu tu baada ya kufanikisha Mapinduzi yake mwaka 1964 yaliyotokomeza Utawala wa Kisultani; Ikumbukwe pia kwamba, katika kipindi hiki cha miezi minne na nusu Ya UHURU Wao [DECEMBER 10[SUP]th[/SUP] 1963 – APRIL 26[SUP]th [/SUP]1964], Zanzibar waliamua kukaa kimya kabisa na kutokimbilia kujiingiza katika Mikataba yoyote au makubaliano yoyote ngazi ya Kimataifa; kwa maana nyingine, hawakutaka kuwa signatories wa suala lolote ngazi ya kimataifa mpaka pale watakapojipanga; Mkataba wao wa kwanza ukawa ni ule wa Muungano na Tanganyika na hatimaye kujikuta kwamba, mengi ambayo Tanganyika walikuwa wamesha establish position yake kimataifa, yakageuka kuwa binding kwa Zanzibar pia; Lakini kwa ajabu, wengi wetu suala hili tunalipuuza;

Ni muhimu tukaelewa pia kwamba - tofauti na nchi zilizokuwa jirani yake (Zanzibar), yani Tanganyika, Kenya na Uganda ambazo uhuru wao ulipatikana kwenye Board Rooms za Lancaster Hall huko London, huku wahusika wakiwa wamevaa suti na kunywa wine na kahawa katika mijadala, ndugu zetu wa Zanzibar hali ilikuwa ni tofauti; Wao uhuru wao ulipatikana “in the streets”, kupitia mtutu wa bunduki; The bottom line hapa ni kwamba, mtazamo wa baadhi ya watu wa “Tanzania bara” kwamba eti Wazanzibari wanatulalia, umejaa upotoshwaji mkubwa sana.

Suala la Tano na la mwisho kujadili katika sehemu hii, ni kwamba – Kama wapo watanzania wenye ujasiri wa kumkosoa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, basi ni wachache sana; Wale wenye uoga juu ya hilo wanasahau kwamba Nyerere alikuwa ni binadamu kama wao; Mimi ni muumini mkubwa sana wa Falsafa ya Mwalimu, including suala la Muungano wetu, lakini nina amini kwamba kuna baadhi ya maeneo ambayo Mwalimu kama binadamu, aliyakosea, licha ya yeye kuwa na nia njema kwa taifa letu, hasa ikizingatiwa kwamba “Nyerere Did Not PROFIT From Politics”; Makosa ya Mwalimu juu ya muungano yalikuwa na yanaendelea kuwepo kwenye “MFUMO”, sio kwenye NIA; Nyerere alikuwa was a ‘True Panafrianist’, na kuna wakati alikuwa yupo tayari hata kuifanya Afrika ya Mashariki iwe ni nchi moja baada ya uhuru na kabla ya muungano na Zanzibar, kwa nia nzuri kabisa; Kwahiyo when it comes to suala la Muungano na Mwalimu, “The END” Was Justified, But Not The “MEANS”; Wasiwasi wa Mwalimu juu ya hatima ya Muungano iwapo Tanganyika itarudi, upo LEGIT; lakini tutaendelea kukaa na hofu hii mpaka lini, hasa ikizingatiwa kwamba Mgogoro wa muungano wetu unatokana na Ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano, 1964?

Machafuko yote yaliyojitokeza Zanzibar miaka ya nyuma, na ambayo yanaendelea leo chini kwa chini, chanzo chake ni mgogoro wa Kikatiba unaotokana na Katiba ya JMT, 1977, kuchakachua Mkataba wa Muungano, 1964. Kwa mtazamo wangu, mgogoro huu wa kikatiba Poses More Threat to our Peace and Tranquility kuliko ujio wa Tanganyika; Isitoshe, hata Tanganyika ikizaliwa, nchi yetu ya Tanzania itabakia kuwa ile ile, hasa mipaka na mahusiano ya watu wake; Kitachobadilika kitakuwa ni Mfumo tu wa Serikali; Hivyo mimi sioni busara kwa Watanzania kufanya maamuzi KIHOFU HOFU na kuacha mgogoro huu ubakie kama ulivyo; Tutakuwa ni wabinafsi sana iwapo tutarithisha vizazi vyetu vyaa baadea hali hii hii ya HOFU hii lakini pia MGOGORO huu huu, ambao kiini chake ni Ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano, 1964. Hivi kweli, Vizazi Vya Baadae Vitafikiria Sisi Tulikuwa ni Watu wa Namna Gani?




BILA TANGANYIKA, TANZANIA HAIWEZEKANI. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
Bila Tanganyika hakuna Tanzania, Suburini muone moto wake. Wajinga wanasema ni manno ya uchochezi, Lakini dhuluma hii haitapita hivi hivi.
 
3. Kwanini watu hawazungumzii kuvunja muungano

Ahsante

Nguruvi3 Tanzania tumekuwa watu wa ajabu kwa kutokutaka kuzizungumzia issues head on kwa sababu ya mazoea. Nakuunga mkono kwenye swali lako la tatu.

Tunakubaliana kwa ushahidi kuwa huu muungano haukushirikisha wananchi wa pande zote. Kwa vile taratibu za muungano zilipitia bungeni sisi tuwaombe wawakilishi wetu, au wawakilishi wapeleke mswaada wa kuvunja muungano. Halafu watuulize kama tunataka muungano na wa aina gani.

Nilikataa kuchangia maswali 4 ya mchambuzi huko juu kwa vile yana misingi ya kuutaka muungano bila kuuvunja uliopo. Nilitoa sababu moja tu kuwa muungano ulikuwa na bado ni wa watawala kwenye mgongo wa udugu. Sasa sisi baadhi ya ndugu tunataka uvunjwe ili tuunde wetu kwa maafikiano si kwa matakwa ya watawala.
 
Serikali Tatu ni mzigo kwa Wananchi, Tutalazimika kutozwa kodi zaidi ili kuzihudumia Serikali hizi, Itafika muda tutachoka na kufikiria kuchangia Serikali ya Afrika Mashariki yenye nchi nyingi zaidi kuliko Muungano wa nchi Mbili pekee na suluhu itakuwa ni kuuvunja. Muungano wetu ni wa pekee, unafanana na United Kingdom.

Wazo la Kuvunja muungano ili tuunde Serikali Tatu ingekuwa na mashiko kama kusingekuwapo na EAC, Muungano wetu Ndugu umeunganisha watu kwa miaka 46 sasa hivyo kuuvunja lazima uanzishe migogoro mikubwa na uasi, Mnaweza jaribu vunja muungano lakini hamtaweza kuhimili kishindo cha kuwaondoa Wazanzibari walio Bara na kuwaondoa Watanganyika walio Zanzibari wenye ardhi,ndugu na familia, Nyerere aliona mbali ndo maana alisema dhambi ya Uasi itawahukumu sababu alishajua baada ya muda mrefu kupita hatwezi tena kutengana.


Ahsante kwa hoja nzuri iliyo na mashiko lakini utakubaliana nami kuwa humu JF watu wamekaa ki ushabiki zaidi wa kisiasa wakisahau kuwa wanaweza kuishi bila C.C.M, C.D.M au CUF lakini Hawawezi kuishi bila Mama yao mzazi (TANZANIA).


Kwa nini unawawekea watu maneno mdomoni?

Hakuna ushabiki wa siasa hapa unapotaka yajadiliwe matatizo yaliyopo ya muungano unakiri kuwa hali ya muungano si shwari. Si shwari kwa sababu wanaolazimishwa kuungana hawaoni mwanga mwisho wa tundu.

Mwenzangu umechangia kishabiki pia, maana ni maagizo ya CCM kuwa katiba mpya izingatie aina ya muungano uliopo. Mimi nasisitiza tuvunje muungano, tusiwe na muungano mpaka hapo tutakapouhitaji hivi sasa hatuuhitaji. Kujilinganisha na UK ni utumwa wa fikra.

Unapozungumzia gharama za serikali tatu kwani tuliunganishwa kupunguza gharama? Tuvunje muungano ili tusiwe na hizo gharama basi. Tutakapoweza kugharamia tutaona muungano gani utatufaa.
 
Mkuu Kobello,

Nianze na hoja yako kwamba hauoni tatizo kwa CCM ku hijack the entire project kwa sababu ilikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo; Nianze na maswali hapa: Mamlaka hiyo CCM ilipewa na nani? Je, CCM alikuwa superior to articles of the Union? Naomba upitie vizuri Articles of the Union Section 2 to 6 ili uone jinsi gani Mkataba wa Muungano, 1964, ambao literally ilikuwa ni sheria mama, ulianza kuchakachuliwa; Unajengaje hoja kuhalalisha kilichofanywa na CCM? Naomba niulize tena, huo uhalali/mamlaka unayosema CCM ilikuwa nayo, ilipewa na nani? Kama unakubali kwamba Mkataba wa Muungano ulikuwa ndio sheria mama, kwanini katika mkataba ule hatuoni neno CCM, ASP, TANu, wala lolote kuhusiana na maamuzi ya kisiasa? Mambo haya hayakuwa ya muungano, yalikuwa yawe chini ya nchi shirikishi, per articles of the union 1964;Au labda uniambie kwamba aliyekuwa ana type ule mkataba aliyasahahu hayo kwa bahati mbaya!
Sikubaliani na wewe kuwa Articles of the Union zilikuwa ndiyo sheria mama.
Sheria mama ya republic yeyote ni katiba, ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa ni katiba ya Tanganyika ya mwaka 1962.Articles of the union, siyo sheria ni makubaliano tu ambayo yanabidi yapitishwe kisheria na bunge la Tanganyika na Baraza la mapinduzi na yalikuwa ratified chini ya "Union of Tanganyika and Zanzibar act, 1964 (nitakuja kukumbushia baadae).
Na makubaliano hayo hayakuwa baina ya nchi shirikishi bali baina ya marais wa nchi shirikishi. Katiba ya mwaka 1965 (interim) sehemu ya kwanza kifungu cha tatu ibara ya kwanza mpaka tatu zimeestablish one party rule na ibara ya pili imeeleza haswa kuwa TANU na ASP zitaungana.
Mwaka 1975 shughuli zote za siasa zilikuwa chini ya TANU. Namaanisha bunge mpaka rais. Na kwa kuwa rais alipewa mamlaka ya kutoa decree yeyote kuhusu muungano na kwa kuwa executive organ ipo chini ya chama ambacho kilikuja kuwa CCM, basi CCM ilipata haki kisheria ya kutoa decree kuhusu muungano.
Kubali tu kwamba kinyume na Sheria Mama ilivyoagiza i.e. Mkataba wa Muungano, 1964, CCM iliamua kuingia jikoni kwa nguvu na hapo ndipo mchafuko wa muungano ulipoanza; na tusiwazingizie wenzetu wa zanzibar, TANU ilikuwa inatafuta njia ya kujipatia uhalali wa maamuzi juu ya muungano kwa muda, na ikagundua kwamba njia pekee ni kujiunga na ASP ili kuifunika, kisha kuanza kufanya maamuzi ya muungano kutokea Dodoma; baada ya CCM kuamua kuingia jikoni, kinyume na sheria mama, wakateuliwa wajumbe kutoka CCM-NEC ambao hawa waliundiwa kamati ya kuangalia wafanye mambo gani ili kufanikisha azma yao ya kuzidi kukiuka Article of the union na kuwa na aina ya muungano ambao bara ingeupende; In the end, kamati maalum ya chama ikachukua nafasi ya Tume ya Katiba na bunge likachukua nafasi ya baraza la kutunga sheria, kinyume na utaratibu uliokubaliwa ndani ya Articles of the Union, 1964; Yet unasema CCM ilifanya haya kwa uhalali? kwa kweli hizi ni siasa tu Kobello, sio reflection ya uhalisia wa mambo;
Mkuu, tangu mwaka 1965 ilijulikana kuwa hivi vyama vitaungana,, hata Kenya, Zaire kulikuwa na chama kimoja. Huo ulikuwa ndiyo mfumo wa kiuongozi na labda ni ujinga wetu, hata kura ya maoni kuhusu vyama vingi, watanzania walitaka chama kimoja. Najua unataka kuiweka CCM ile kama ilivyo hii, lakini utakuwa hujawatendea haki baadhi ya wazee wetu.
Watanganyika tuliingia miguu miwili kwa kuheshimu maamuzi ya JKN, hata kungekuwa na refferrendum wakati huo nina uhakika walikuwa wanataka nchi moja ingawa tulikuwa tukiingia na passport Unguja.

Kuhusu zanzibar kuwa na autonomy kutokana na kuwa na legislature, executive na court system yao, ni lazima ukumbuke kwamba haya hayakuja kirahisi, kwani kwa muda mrefu yalikuwa yanaendeshwa kwa kiini macho; ukitaka nifafanue ntafanya hivyo, lakini nadhani unaelewa jinsi gani zanzibar imevipigania hivi over time, halikuwa ni suala la moja kwa moja na rahisi kama unavyotaka tuamini;
Nani aliwazuia? Na tangu walipokuwa nazo, unaweza kunionyesha statistically uchumi au jamii ilivyoendelea?

Tukiwa bado kwenye hili la autonomy, pia nimependa ulivyoweka numerali ya 22 kama ndio matters of the union; kama unakumbuka vizuri au kama umesoma vizuri mkataba wa Muungano, 1964, kulikuwa na masuala 11 tu yaliyokubaliwa, na yaliyobakia ilikuwa yafuate baada ya katiba mpya kuja, vinginevyo katika kipindi kile cha mpito ambacho maximum kiliwekwa kuwa mwaka mmoja, juhudi kubwa zilikuwa zielekezwe katika uteuzi wa tume ya katiba na baraza la kutunga sheria; cha ajabu ni kwamba, badala yake, mwaka 1965, katiba ile ikawa ya muda, na ikazidi kuchakachua masuala yaliyokuwa yanaipa zanzibar autonomy yake na kuyaweka kwenye muungano, kinyume na makubaliano ya awali ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964;
Mkuu usiangalie Articles of the Union, angalia Act of the union na hapo kwenye nyekundu angalia kwenye definitions uone what it meant by "Interim period" (nazungumzia union act,1964). Articles ni makubaliano na ACT ni sheria ... kwa hiyo let's base our discussions on tha Union act,1964.Unaexaggerate hilo sualka la mwaka mmoja.

Na majibu yako kuhusu serikali ya Tanganyika nilitegemea yatajaa Siasa kuliko kitu kingine; umeelezea vyema complications zilizopo, ambazo kwangu mimi its a myth na nimeelezea kwa undani sana katika majibu yangu kwako awali uliponiuliza, je mfumo wa federation - ya serikali tatu una faida gani kiuchumi, kijamii na kisiasa? Majibu yangu yale bado yanasimama hata hapa kujibu hoja yako inayopinga shirikisho;
Mkuu nadhani wewe ndiyo upo kisiasa zaidi, kilawama zaidi. Tofauti na kizazi chetu, watanganyika walikuwa na umoja, na decisions nyingi za viongozi wao zilikuwa na ridhaa just because kulikuwa na heshima na level ya elimu na upataji habari ambao ulitawaliwa na propaganda uliipa consent serikali.





Ukubwa wa Tanganyika na udogo wa Zanzibar unapimwa na nini, land mass? Population? GDP? Whats the righ way kupima ukubwa wa nchi? Mimi nina amini kwamba ni vyema tupime ukubwa wa Zanzibar by Potential GDP
Sidhani kama upo sahihi,hata kama tutakuwa na federation, population ndiyo hutumika. Hasa kama tutakuwa na one man, one vote.

Naamini kwamba, given rasilimali walizonazo Zanzibar – utalii, mafuta na gesi, more autonomy to Zanzibar itapelekea taifa hili kuwa kubwa sana kiuchumi, pengine kufanana na Tanganyika kama sio kukaribiana na Tanganyika;
Upo kisiasa zaidi.Mafuta na gesi ipi?
Itabidi upresent facts, nakubaliana na wewe kuwa unaamini, ila sidhani kama hili ni jukwaa lake.
 
mimi sishangai hoja zenye nguvu zinajibiwa na hoja legelege hata bungeni tumezoea kuona hata mwanasheria anadiriki kupotosha uma na ni hodari kwa kutumia mifano ambayo si pahali pake "kazi ya kichwa ni kufikiria na sio kufuga nywele" ili tu kuuaminisha uma na kuilinda serikali kazi ambayo hatukumtuma pale bungeni ila majibu tunayo 2015"
 
Nonda,

..United Republic of Tanganyika na Zanzibar maana yake dola ni mbili zimeungana na kuwa dola moja -- chini ya Raisi na Amiri Jeshi Mkuu mmoja.

Kama ni hivyo, kwa nini orodha ya mambo ya muungano imekuwa ikiongezeka?

Pia kwa nini dola moja ina serikali mbili? Au ni uhusiano upi uliopo baina ya serikali ya muungano na serikali ya Zanzibar?

Pia kwa nini mamlaka ya serikali ya Tanganyika kwa mambo ambayo si ya muungano yamekasimiwa kwa serikali ya Muungano? Je hii sio sawa na kuitia serikali ya Tanganyika mafichoni, isionekane wakati taasisi zake kwa mambo yasiyo ya muungano zipo na zinaonekana? kwa mfano, mahakama ya rufaa tu ndio jambo la muungano lakini mahakama nyengine zote ni mahakama za Tanganyika. Wizara ya Afya. Wizara ya kilimo, utalii, miundo mbinu, michezo nk.
..dola yoyote ile ikichukua yale mambo 11 original ya muungano na kuyakabidhi kwa mamlaka nyingine basi dola hiyo itakuwa imefikia kikomo.
Hapa nitofautiane nawe kidogo. EU (na sio EEC) unasema ni jumuia. Foreign policy sasa linaamuliwa katika jumuia hii na hivyo nchi wanachama wa EU hazijasita kuwa dola ingawaje wamesalimisha baadhi ya powers zao Brussels, makao makuu ya EU. Pia wamo katika mchakato wa kuwa na Katiba ya EU ambayo inakataliwa kupitia kura katika nchi wanachama.

Kilichofanyika katika mkataba wa Muungano ni kukabidhi baadhi ya mamlaka kwa taasisi ya pamoja na kubakisha baadhi ya mamlaka katika serikali za pande husika.

Kama tutakubaliana na maelezo yako basi hakukuwa na sababu ya kuongeza mambo ya muungano baada ya yale 11.Kuongeza mambo ya muungano maana yake ni kuchukua mamlaka zaidi kutoka katika serikali zilizounda muungano na kuweka mamlaka hayo kwa dola ,ambayo wewe unasema ni moja na ambayo tayari iko kamili kwa vile mamlaka ya dola zile mbili yalifikia ukomo. Kama zile dola mbili hazikuwa tena na mamlaka ya kidola kwa nini serikali ya muungano ikwapue mamlaka yaliyobaki kutoka kwa serikali mbili hizo?
Kwa nini inafanya hivyo? Na kwa manufaa gani?

..kwa maana nyingine dola za Tanganyika na Zanzibar zilikufa pale zilipoyakabidhi yale mamlaka 11 kwa dola mpya iliyoitwa United Republic of Tanganyika and Zanzibar, ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuwa United Republic of Tanzania.

Joka Kuu
Dola ya Tanganyika haikukabidhi(surrender) mamlaka yake yote kwa serikali ya muungano, ndio maana msemo wa kukasimu(delegate) mamlaka yake unatumika. Pia Zanzibar haitoa mamlaka yake yote kwa Muungano, ilibakisha baadhi.
Na kama kiini macho cha kukasimisha madaraka ya Tanganyika kwa serikali ya muungano hakikufanyika ni wazi zingekuwepo serikali tatu. Serikali ya Tanganyika(mambo yasiyo ya muungano) Serikali ya muungano(mambo ya muungano) na serikali ya Zanzibar( mambo yasiyo ya muungano).

Nchi mbili zinapoungana na kuwa Nchi moja mifumo ya kawaida ya miundo ya Katiba ni miwili: Muungano wa Serikali Moja, au Shirikisho la serikali Tatu. Kwa mfumo wa kwanza kila nchi itafuta serikali yake na nchi mpya inayolizaliwa itakuwa ni nchi moja yenye Serikali moja. Katika mfumo wa pili kila nchi itajivua madaraka ambayo yatashikwa na serikali ya shirikisho na itakuwa na serikali ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yaliyobaki.

Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha Serikali ya Shirikisho; uk 10-11 link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)


..ushahidi mwingine ni kile kitendo cha Tanganyika na Zanzibar kubadilisha uanachama wao wa ktk UN na kuchukua uanachama mpya kwa jina moja, TANZANIA.

Hilo nalo lilifanyika kinyemela kama ilivyofanyika kubadilisha jina la nchi kutoka Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa Tanzania. Na baada ya ukimya wa miaka 48 sasa Zanzibar wanataka kiti chao UN.

Ukiini macho huu hautaki darubini, Joka Kuu. Kila sehemu ambayo ilisomeka Tanganyika,ilibadilishwa kuwa Tanzania. Kuanzia kutoka katiba ya Tanganyika kupata ya Muungano na mengine yote.

Unafikiri kulikuwa na umuhimu wa kubadili jina la asili/awali la Jamhuri ya muungano na hivyo kulipoteza jina Tanganyika?

..hata nchi marafiki ziliacha kuzitambua Tanganyika na Zanzibar na badala yake kuanza kuitambua dola mpya TANZANIA.

Ni kutokana na kulazimishwa na pia usisahau ushawishi wa nchi za US na UK katika kuundwa kwa muungano wa Nyerere na Karume.

Kama unataka kujua kuwa nchi za mataifa hazikuisahau Zanzibar fuatilia vipi wameibana serikali ya muungano na vipi wameshiriki katika kuleta miafaka baada ya migogoro iliyotokana na CCM kung'ang'ania madaraka huko Zanzibar kila baada ya uchaguzi mkuu.
..mwisho, mahakama ya rufaa ya TANZANIA ilitoa hukumu kuunga mkono hoja iliyotolewa na mawakili wa chama cha CUF kwamba huwezi kutenda kosa la uhaini kwa Zanzibar, kwasababu Zanzibar siyo nchi/dola.

Hukumu ile imeishusha hadhi mahakama ambayo uwepo wake pia umetokana na uchakachuaji kama alivyoelezea Mchambuzi.( au Lissu?). Ukiitafsiri hukumu ile ni kuwa Mahakama ilisema kuwa Zanzibar ni mkoa , wilaya au serikali ya Zanzibar ina hadhi ya serikali ya mtaa/wilaya/mkoa. Kama mahakimu hawakuwa waoga wangesema hadharani hadhi ya serikali ya Zanzibar si zaidi ya serikali ya mtaa au vipi?. Unafiki ndio unaongeza utata wa muungano huu.
..usijaribu kufananisha Tanzania[muungano wa Tanganyika na Zanzibar] na Jumuiya ya nchi za Ulaya. Hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa. Ungekuwa sahihi kama ungefananisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya nchi za Ulaya.

Joka kuu
EU sasa imeshapita hatua ambazo iko Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wameshafikia hatua ya kutaka kuwa na katiba ya EU.
Nafikiri kosa ambalo sisi tunafanya ni kusema Tanzania ni nchi moja, dola moja(kuelekea serikali moja?). Tanzania si nchi moja bali ni muungano wa nchi mbili, tena kwa mambo 11 tu.
NB:

..Hakuna haki, usawa, kuheshimiana, na kuthaminiana, ndani ya muungano wetu. Kwa msingi huo nadhani ni bora muungano uvunjwe, na Tanganyika irudi.


Aliyekiuka mkataba wa muungano ndie ambaye anapaswa kubeba lawama ya ukiini macho/mazingaombwe haya. (Mwalimu na CCM).Mchambuzi ameataja kwa uwazi huku kukiwa na vitisho anapata kutokana na kuweka unafiki pembeni.
Tanganyika itarudi tukitaka irudi lakini kwa umma wetu wa wadanganyika ulivyo inaonekana tunapenda kuziba macho ili kiza kitawale wakati jua la kiangazi la saa 6 mchana linawaka.
Wadanganyika kwa pamoja na kwa amani tunaweza kuirudisha Tanganyika na kumaliza mazingaombwe ya muungano. Wazanzibari wameshatuonesha njia. Tudai Tanganyika yetu.
 
Mchambuzi,

..kiini cha matatizo ya muungano ni wetu ni ama kuuwawa kwa serikali ya Tanganyika, au kuendelea kuwepo kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Kwa maoni yangu, kiini cha matatizo ni kuificha/ kukasimisha madaraka ya serikali ya Tanganyika kwa serikali ya muungano. Serikali ya muungano inapaswa iseme imechoka kubeba majukumu/mamlaka ya Tanganyika na hivyo Irudishe yale mamlaka yaliyokasimiwa kwa serikali husika. It is so simple. Serikali ya Tanganyika haikuuawa imefanyiwa mazingaombwe tu.

Kuendelea kuwepo kwa serikali ya Zanzibar ni tatizo kwa wale wanaotaka nchi moja, dola moja, taifa moja na serikali moja. Lakini kwa wale wanaotaka muungano wenye tija kwa wabia/wanachama wake basi uwepo wa serikali ya Zanzibar ni kielelezo tu cha muungano kwa vile itabaki kushughulikia yale mambo ambayo si ya muungano.Sifikiri kama Zanzibar ingekuwa ni nchi kubwa kama Kenya au Uganda tungependelea kuwa na serikali moja tu ya muungano na dola moja, taifa moja. Au tungependa kuungana na Kenya na kuwa dola moja na serikali moja? Kama jibu ni hapana. Kwa nini tupendelee kuwa na serikali moja , dola moja na Zanzibar tu?

Kumbuka hakuna nchi huru inayopenda kupoteza mamlaka yake, hasa baada ya kuipigania mamlaka hiyo kwa kumwaga damu.


..sasa ukitaka kuokoa huu muungano unapaswa kuifufua serikali ya Tanganyika, na kuunda mfumo wa shirikisho, au kuifuta serikali ya mapinduzi Zanzibar, na kuunda Jamhuri moja.
Ukiondoa ukiini macho(kukasimisha madaraka ya Tanganyika kwa serikali ya muungano) basi unapata mfumo wa shirikisho. Mfumo wa shirikisho utatoa nafasi kwa nchi nyengine pia kujiunga.
Hivi sisi wadanganyika huwa tunajiuliza kwa nini baada ya miaka 48 muungano wetu wa "mshikamano, amani na utulivu" hakuna nchi nyengine iliyosogeza pua yake kunusa manukato(perfume) ya mazingaombwe yetu. Kama utasema zilitokea kwa nini basi hazikujiunga nasi?

..kwa upande wangu mimi nadhani wenzetu wa Zanzibar hawataki muungano. they have already moved on. katika mazingira hayo, hakuna haja ya kuwabembeleza wala kuwalazimisha na masuala ya muungano.

Zanzibar kwa bahati nzuri wameshaweka msimamo wao hadharani, wanataka muungano kama wa EU. Si saula la kubembeleza bali na sisi wadanganyika kuweka hadharani msimamo wetu. Tunataka muungano? Wa aina ipi?
Ujanja ujanja ,usanii, kushindwa kutatua kero za muungano kumetufikisha hapa tulipo leo.

Wakati viongozi wa Zanzibar wanapanda kwenye viriri, kwenye makongomano,warsha wanasema misimamo yao. Wadanyanyika wachache tupo JF kuzunguka mbuyu badala ya kusema tunataka muungano au hatuuutaki. Na wa mfumo,muundo upi. kama tunataka tuirudisha serikali ya Tanganyika au hatutaki.
..tunachotakiwa kukifanya ni kutumia BUSARA na USTAHAMILIVU wakati tunavunja muungano wetu.
Kwa miaka 48 hivyo vitu, BUSARA na USTAHAMILIVU kwa upande wetu ndio vimekosekana. Kila mjadala wa muungano unapoibuka tunaubinya na kuufananisha na uhaini.
Kada za uongozi ziko kimya nafikiri ni busara kwa wananchi sasa kumfunga paka kengele!
Mchambuzi amenza hapa na tuunge mkono ukweli na uwazi. Katika kipindi cha wiki moja tu habari itasambaa vipembe vyote vya Tanganyika(Tz bara?) na watawala wataelewa kuwa wadanganyika wameshaamka na wanataka ukomo wa mazingaombwe/uchakachuaji wa mkataba wa muungano.

Uchaguzi na uamuzi utakuwa ni wao kuwa na busara na ustahamilivu au kutumia mbinu zile zile za kuficha taka taka chini ya zulia.
 
Back
Top Bottom