Kobello,
Naomba nianze na hili:
…PIA, neno Tanzania lilianza kutumika tangu, 1964 ....try to find out.
Unaposema lilianza kutumika, una maana kisheria au kisiasa?
Hoja yako ina elements aidha za spin au kutoelewa mantiki nzima ya hoja yangu kuhusu JINA TANZANIA;
Jina Tanzania lilizaliwa na Mkataba wa Jamhuri ya Muungano, 1964, lakini chini ya Makubaliano kwamba ndani ya mtoto Tanzania, wazazi wake Tanganyika na Zanzibar wataendelea kuwepo na kuwa na mamlaka kamili NDANI YA JAMHURI MOJA, kwa masuala nje ya yale ‘11' ambayo ndio yalikubaliwa yawe ya muungano;
Hoja ya msingi hapa kuhusu jina Tanzania ambayo ningependa uelewe ni kwamba – sikatai kuhusu kuzaliwa kwa jina Tanzania 1964, kwani hii ni kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964; Ninachopinga mimi ni matumizi ya Jina hili huko baadae KISHERIA; Kwa mfano, Mwaka 1967, kupitia Sheria namba 24 ya Bunge la JMT (ambalo tayari nimeshajadili kwamba halikuwa halali Per articles of the Union, 1964), bunge hili chini ya sheria hii ikalifuta JINA TANGANYIKA, na sasa Tanganyika nayo ikaitwa TANZANIA, huku Zanzibar likibakia kuwa lile lile ZANZIBAR; Hii nadhani ni kwa sababu ilikuwa weird kwa rais wa JMT kuendelea pia kuwa rais wa entiry called Tanyanyika, especially nje ya utaratibu uliokubaliwa chini ya Mkatab wa Muungano;
Ilipofika Mwaka 1977, jina na Zanzibar Nalo likaanza kuchezewa chezewa, kwani Katiba ile ikaita Zanzibar sasa kama TANZANIA ZANZIBAR, huku Tanganyika nayo ambayo mwaka 1967 iligeuzwa kuwa Tanzania, ilionekana inaelea kwa kiini macho, hivyo Katiba ya 1977 ikabadili tena jina hili na kuitwa TANZANIA BARA; Kwahiyo, tofauti na makubaliano ya Mkataba wa Muungano ambao ulilenga Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Katiba ya JMT 1977, sasa ikautambua Muungano ule kwamba ni wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani;
Naomba uelewe hapa kwamba hata ukija na sheria gani katika hoja zako, bado haialalishi na wala haibadilishi kwamba nguzo kuu ya Muungano imebakia kuwa Mkataba wa Muungano, 1964, sio kwa sababu ilikusudiwa hivyo, bali ulichakachuliwa, hivyo mambo yote yaliyofuata yanakuwa batili na yanakosa nguvu za kisheria ndani ya JMT;
Huwa mara nyingi unazungumzia kuwa na mjadala wa kisheria, na unacholeta huku ni kifungu cha saba kuhusu commission na constituent assembly..... Are you serious?
Kujadili kitu kisheria ni kujadili sheria ndiyo maana nikakwambia Articles of the Union siyo sheria mpaka iwe ratified.
Nimejaribu sana kulitolea maelezo hili, lakini nadhani sasa maelezo yangu ya bandiko namba ‘144' litakuelewesha vizuri zaidi hoja yangu ya msingi ambayo ni kwamba – hakuna anayebisha kuhusu umuhimu wa Articles of the Union kuwa ratified, suala la msingi hapa ni kwamba – kilichoingizwa kweney sheria ya muungano, 1964 to ratify Mkataba wa Muungano, 1964, kilikuwa sicho kilichokubaliwa ndani ya Mkataba wa muungano; Kwahiyo utaendelea kuizungumzia sheria hii mpaka kesho, lakini ukipata muda nenda katika sehemu yoyote ya kisheria nchini Tanzania kaulizie kama Sheria ile ina nguvu yoyote; Haina nguvu kwa sababu ilikwenda kinyume na Mkataba wa Muungano, na hii ni moja ya sababu kwanini mkataba wetu una mgogoro mkubwa wa Kikatiba; Bandiko langu namba 144 litakusaidia uelewe hoja yangu vyema zaidi;
Na kwenye ratification, unatakiwa uexplain maana ya terms utazoona zinaweza kuleta utata. Hizo terms zimekuwa defined na nguvu ya presidential decrees zimeelezewa kwenye "Union of Tanganyika and Zanzibar Act,1964" na "Union of Zanzibar and Tanganyika Law,1964".
Nimefanya hivyo kwenye bandiko langu namba 144 ukurasa wa nane wa uzi huu;
Kwa hiyo kama unataka kuzungumza kisheria ungebase zaidi kwenye hizo acts, lakini kisiasa umeamua ku-base kwenye articles of the Union na kuzitafsiri kwa maoni yako au malengo yako ya kisiasa.
Rejea bandiko langu namba 144, utaona kwamba mim sipigi siasa kama wewe juu ya hili Kobello, nazungumzia suala hili kisheria;
Kama wewe kweli unataka kulizungumzia hili swala kisheria , let's do it! Sijui kwanini unanibambikizia mimi usiasa wakati posts zako nyingi zipo kingonjera zaidi. Kwa mfano, mahesabu yako ya synergy, your metaphorical explanation ya baba, mama na mtoto ... I mean C'mon dude!
Unaanza hasira, rejea bandiko namba 144; vinginevyo mimi sipo hapa to win arguments but to find the truth, na kama ni suala la ushindi, naweza kukupa ushindi tukamaliza mjadala baina yangu mimi na wewe;
Kuhusu ushahidi, nimekupa preambles na article ya mkataba kati ya Scotland na England,1707 ambao unafana na mkataba wetu wa 1964. Ambapo bunge la scotland liliunganishwa na la England, na Crown ya Scotland ikaunganishwa na England kuwa kitu kimoja. Yaani executive na Legislature were united into one!! sasa hiyo siyo serikali moja? Na through time wamebadilisha na sasa wanataka separate powers.
Hili ndio tatizo, kwani hata Mwalimu alisema kwamba aliiga mfumo wa UK ambao ni unitary, only kukimbilia mfumo wa US ambao ni federal baada ya ujio wa vyama vingi ili kuokoa CCM isipate aibu, kwani katiba ya 1977 ya JMT ilidhania CCM itakuwa chama pekee cha siasa Tanzania; Muungano wetu una elements za Unitary na Federal, wakati Mkataba wa Muungano ulidhamiria uwe Federal; Hata hii element ya federal imekuja ingizwa baadae na Tume ya Bomani iliyopewa kazi ya kusaidia okoa aibu ya CCM kuweza ushinda Bara, lakini kushindwa Zanzibar;
Na hoja yako kuhusu serikali moja ni bira uachane nayo kwani haikudhamiriwa kuwa serikali moja chini ya mkataba wa muungano, 1964; lakini muhimu zaidi pia ni kwamba, SERA YA CHAMA CHA MAPINDUZI NI SERIKALI MBILI; Serikali moja sasa inatoka wapi?
Pia umegoma kabisa kujibu hoja zangu kwamba Mfumo wa Serikali uliodhamiriwa ndani ya mkataba, 1964 ulikuwa ni shirikishi; katika bando langu la huko nyuma, ninakuelezea aina kuu tatu za ushirikiano wa mataifa, na katika kila mfumo, nikajadili na kumalizia kwa swali kwako, lakini haujajibu maswali mawili yaliyobakia, hasa juu ya mfumo shirikishi, ulijibu swali kuhusu serikali moja, huku ukikimbia swali juu ya mfumo wa matangamano ya serikali ya majimbo; Sikuona sababu ya msingi ya kujibu hoja yako kuhusu serikali moja kwani ilitakiwa ujibu maswali yote ili tufananishe yote uliyoyasema na kile kilichopo katika Mkataba wa muungano, 1964;
Wewe hujaleta ushahidi wowote wa kisheria zaidi ya kusema Zanzibar hawakupewa Constituent assembli na kulikuwa hakuna commission within one year ... are you serious? Au sijakuelewa?
Iwapo bandiko langu namba 144 halikuridhishi, nifahamishe, na naomba uwe specific;
Ndiyo maana nikakwambia kuwa, ukisoma kwa undani, tena nilibold utaona kuwa formation of constituency assembly na hiyo commission dependende on Agreement between Karume na Nyerere.
Hakuna ukweli katika hili; it will remain a fact kwamba ibara ya ‘7' ya Mkataba wa Muungano, 1964, ndio ilikuwa iwe mwanzo wa safari yetu kuelekea kupata mkataba wenye uhalali na nguvu kisheria ndani ya nchi, lakini kwa vile ibara hii ilikiukwa, hakuna mwanasheria wa masuala ya katiba leo hii atakubaliana na wewe kwamba Muungano wetu una uhalali wa sheria za ndani ya nchi;
Sasa unadhani karume alitishiwa bunduki? Au alirogwa ndiyo maana hawakuulizia hiyo commission? Au waliagree kutoitisha hiyo assembly?
Whatever the case, hii haithibitishi uonevu au armtwisting ya aina yeyote, kwa sababu walikuwa na uwezo wa kudai hilo baraza
Hayo ni maneno yako wewe binafsi, vinginevyo mimi maneno yangu juu ya hili yapo kwenye bandiko namba 144, ukipata muda wa kusoma utaelewa nini kilichotokea; Vile vile rejea hoja yangu kuhusu ukiukwaji wa ibara ya
tatu na ile ya
saba ya mkataba wa muungano, 1964; Vinginevyo change la macho lilitokea katika ile Sheria ya Muungano, 1964, na ukisoma bandiko namba 144, utaelewa nina maana gani;
Kuhusu reversability of my last sentence .... mhm!!, so whats up with this federation or three (now you say two) government noise, lets go our own way then.
I have never advocated for serikali mbili, nilichosema ni kwamba SERA YA CCM NI SERIKALI MBILI, na itapigania hili mpaka kifo chake; Mimi kuvaa shati la kijani haina maana kwamba ninakubaliana na Sera hii; Mimi naunga mkono Muungano wa SERIKALI TATU, na nilishaeleza kwanini, nikianzia na utiifu wangu kwa Mkataba wa Muungano, 1964, kuliko Katiba ya JMT, 1977 – kuhusu JMT; Na nitaendelea kuwa na msimamo huu hadi pale Tanganyika itakapozaliwa, au nitakapo aga dunia;
TOFAUTISHA BAINA YA NIA/LENGO NA MATOKEO. Naweza kuexplin kisheria,
Unaweza ukampa mtu shilingi mia ili akakuletee paspoti kutoka uhamiaji.
Bahati mbaya huyo mtu alikuwa ni afisa uhamiaji.
Akafungua mashtaka kuwa umemhonga ili upate paspoti.
Ukamwambia judge kuwa nia yako siyo kumuhonga, bali kupata paspoti bila wewe kwenda uhamiaji.
Ukato mfano wa mtu aliyekwisha wahi kufanya hivyo na akapata pasipoti kihalali.
Jaji ataangalia nia yako, as oppossed to evidence iliyopo na maneno ya mshtaki na jinsi alivyounganisha na wewe kumpa shilingi mia.
Nia yako, kisheria itaoverride connection ya sheria na ushahidi.
Sijakuelewa hapa, na actually, nilidhania nime quote bandiko la mtu mwingine toka mada nyingine; Vinginevyo kama ni suala la ushahidi, mimi na wewe sio mahakimu, na hakuna verdict bado, na hiyo sio kazi yangu, wala kazi yako, vinginevyo, kinachoendelea ni mjadala TO SEEK THE TRUTH NOT TO WIN ARGUMENT;
Vinginevyo naomba nikurejeshe kwenye maudhui na madhumuni yangu kuja na mada hii, hasa kwa kutumia majibu yale yale niliyompa mimi ni baba; nilimjibu hivi:
Imenichukua miezi kama miwili kujiandaa na mada hii; Hii ni kwa sababu, siku zote nilikuwa nachukulia kero za muungano kwa mtazamo wa kisiasa zaidi; Lakini baada ya Lissu, ambae ni Mwanasheria by profession, kutoa hotuba yake Bungeni Mwezi Juni, 2012, na kutumia neno ‘kiini macho', hii ilikuwa ni wake up call kwangu kwamba pengine mgogoro huu utaeleweka zaidi iwapo utaangaliwa kisheria zaidi kuliko kisiasa; Hivyo nikaamua kujifanyia utafiti wangu wa hapa na pale taratibu, na niliporidhika na facts nilizopata, nikaja na mada hii, chini ya title inayolenga kuendeleza neno "kiini macho", ili kuipa longevity hoja ya Lissu ambayo nadhani ilikuwa ni muhimu sana lakini ikafa upesi sana;
Kama umekuwa unanisoma, hasa katika majibu yangu kwa washiriki wengine humu, najaribu sana kukwepa matumizi ya siasa katika kujenga hoja, na badala yake kujaribu kutumia zaidi hoja za kisheria, ingawa mimi sio mwanasheria; Nina amini kwamba, kuangalia mkataba huu kisheria ndio njia pekee ya kuelewa kiini macho hiki kipo wapi, lakini pia ndio njia pekee ya kuirudisha Tanganyika yetu, kwani haikufa kwa SIASA bali kwa SHERIA, kwa mujibu wa sheria ya bunge namba 24, 1967, na kupewa jina jipya la TANZANIA;
Kwahiyo mimibaba, maudhui yangu ndio hayo – kudadisi mgogoro uliopo kwa mtazamo wa kisheria zaidi, kwa imani kwamba tutaweza kuelewa chanzo cha mgogoro, lakini pia jinsi ya kuutatua mgogoro huu, ikiwa ni pamoja na kuifufua Tanganyika yetu;