Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,323
Sehemu ya Kwanza: Utangulizi
Mjadala wowote juu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa kawaida unahitaji maandalizi makubwa na pia umakini wa hali ya juu, hasa iwapo unalenga hoja zenye kuuboresha kwa njia ya kuondokana na kero mbalimbali zilizopo, badala ya kuuvunja. Iwapo kuna masuala ambayo baadhi yenu mtadhania nimeyasahau au kuyaacha, ni kwa sababu ni vigumu sana kuja na mada kuhusu muungano ambayo inajitosheleza. Pamoja na hayo yote, kuna mengi nimeyaacha kwa makusudi lakini kwa lengo la kuyajadili zaidi baadae; Vinginevyo naomba mniwie radhi kwa mapungufu yoyote ambayo yatajitokeza.
Kupitia nafasi yake kama Msemaji Mkuu wa Upinzani Bungeni (Ofisi Ya Makamu Wa Rais – MUUNGANO), katika kikao cha Bajeti cha Mwaka wa Fedha, 2012-2013, Tundu Lissu (MB), aliwasilisha maoni kuhusu mtazamo na msimamo wa kambi hiyo juu ya Muungano Wetu. Kwa wale waliopata fursa ya kuisikiliza hotuba ya Lissu kwa makini, wengi watakubaliana na mimi kwamba hotuba yake ilijaa YALIO MEMA kuliko YASIYO MEMA, sio tu kwa Muungano wetu, bali pia kwa taifa letu. Vile vile, hotuba ya Lissu ina dhamira njema na yenye manufaa, sio tu kwa kizazi cha sasa, bali pia kizazi cha baadae. Lakini kama kawaida yetu, nchini Tanzania, "POLITICS HAS BECOME SURPEME TO EVERYTHING", kwani hoja ya Lissu imepotoshwa;
Kwanza: JE, Madhumuni ya Muungano Baina ya Tanganyika na Zanzibar, kwa Mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, Yalikuwa Ni Yepi na ni Mfumo wa Serikali ngapi ndio uliokusudiwa chini ya Mkataba huu wa Mwaka 1964?
Pili: JE, Viongozi Wetu na Wananchi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo hii, Wana Nia ile ile Adhimu na Malengo Yale Yale Yaliyowekwa katika Utangulizi wa Mkataba wa Muungano, 1964?
Tatu: Ifikapo Mwaka 2014, Muungano Wetu Utakuwa Umetimiza Miaka 50; By Coincidence, Kipindi hicho hicho pia Tunategemea Kupata Katiba Yetu Mpya; Swali linalofuata ni, JE: Katika Kipindi Hiki Cha Miaka 50 Ya Muungano, tutakuwa tumefikia wapi katika Kufanikisha Madhumuni Kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964?
Nne: Je, makosa ambayo yanapelekea muungano wetu kuyumba yalijitokeza wapi, na tuchukue hatua gani kurekebisha makosa haya, na kurudisha matakwa na dhamira iliyowekwa wazi kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964?
BILA TANGANYIKA, TANZANIA HAIWEZEKANI. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
Nilipo RED
Waarabu tuna usemi unaonena. ''NI RAHISI SANA KUWADANGANYA WATU. LAKIN NI VIGUMU SANA KUWAAMBIA WATU KUWA WAMEDANGANYWA''
Na vile vile Mwimbaji mashuhuri wa Reggae Robbert Nesta Marley (mmarufu kama Bob Marley) kwenye wimbo wake wa "Redemption song" alisema YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOMETIMES BUT YOU CAN'T FOOL ALL THE PEOPLE ALL THE TIME"
Nikiwaambia waTanganyika Nyerere aliwadanganya sana na alisimamia kidete kuhakikisha HAMUWEZI KABISA KUUNDA Serikali ya TANGANYIKA pamoja na Znz kuwasaidia sana kuwaombea Serikali Hiyo katika mjadala wa kwanza kuhusu Muungano wenu.
tumeamua kuiga tabia ya "ujanja" wa mbuni wa kuzika kichwa mchangani, eti kukwepa janga. Labda tujikumbushe kidogo kwa hili.
Mdahalo wa kwanza juu ya mfumo na muundo wa Muungano ulianza kwa njia ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1983/84. Hapo, kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais Aboud Jumbe, na wale wa Serikali ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Nyerere, walikuwa na mitazamo tofauti inayokinzana juu ya Muungano.
Jumbe na timu yake walitaka Muungano uwe na Serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar (iliyopo sasa) na Serikali ya Muungano yenye kushughulikia mambo ya Muungano tu, ambayo yameainishwa katika Ibara ya 6(a) ya Katiba ya Muungano (Articles of Union) na kifungu cha 8 cha Sheria ya Muungano (Acts of Union) Namba 22 ya 1964, na hatimaye ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Jumbe alikwenda mbali zaidi kwa kuandaa Hati ya Maombi ya kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba juu ya muundo sahihi wa Muungano kwa kutumia ibara ya 125 ya Katiba.
Tofauti hizi kati yake na Mwalimu hazikwisha salama kwa Jumbe kuthubutu kukanyaga mahali "patakatifu" bila kuvua viatu. Jumbe alilazimishwa kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi kuanzia Urais wa Zanzibar, Umakamu wa Rais wa Muungano, na nafasi zote za kichama Januari, 1984.
Utata mwingine huu uliibuka tena kwa nguvu mpya zaidi wakati Wabunge 55 (maarufu kama G55) wa Bunge la Muungano, walipowasilisha bungeni mwaka 1993, hoja ya kutaka kuundwa/kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika kwa kukasirishwa na hatua ya Zanzibar kujiunga na OIC kama nchi huru nje ya Muungano, Desemba 1, 1992.
Ukweli, Bunge lilikuwa limekwisha kupitisha kwa kauli moja, Azimio la kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika Agosti 24, 1993 kwa maana ya kuwa na Serikali ya Muungano inayoundwa na Serikali hai zenye Mamlaka huru, za Tanganyika na Zanzibar, kama vile tu alivyotaka Rais Jumbe mwaka 1983.
Hata hivyo, Azimio hilo lilipigwa rungu zito na Mwalimu Nyerere na likavunjika.. Na kama ilivyokuwa kwa Jumbe, hapa napo mambo hayakuisha salama; safari hii Waziri Mkuu wa wakati ule, John Malecela (hongera kwa kutimiza miaka 75) na Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba, walipoteza nyadhifa zao kwa sababu ya ama kunyamazia au kuunga mkono hoja / Azimio la G 55.
Kifupi naweza kusema mumeamua kuiga tabia ya "ujanja" wa mbuni wa kuzika kichwa mchangani, eti kukwepa janga.
Hongera sana Tundu Lissu kwani wewe ni miongoni mwa wale aliosema Bob Marley 'you can't fool all the people all the time"